Liturujia ya Kanisa Katoliki
LITURUJIA YA KANISA KATOLIKI
MAANA YA LITURUJIA
1. Maana ya liturujia
Neno liturujia linatokana na neno la kigiriki ‘Leitourgia” neno hilo limeundwa na maneno mawili. La kwanza ni laos likiwa na maana ya watu- taifa, na la pili ni ergon likiwa na maana ya kazi au huduma –Kufanya tendo
Hivyo neno liturUjia lilitumika kumaanisha kazi inayofanywa hadharani au tendo linalofanywa hadharani kwamanufaa ya umma au ya taifa mfano;
- Kazi zifanywazo na watu kwa faida ya wenyewe kama vile; (kuchimba kisima , kujenga shule n.k)
- Kazi zifanywazo na mtu mmoja kwa kwa faida ya jumuiya nzima hasa kwa mfano ;( katika uwanja wa elimu, maburudisho na hata ulinzi).
- Kazai zifanywazo na watu kwa bwana wao
Lakini Biblia ya Kigiriki ilitumia neno liturujia kumaanisha: Kumtukuza Mungu, Kwa ujumla ni mambo ya ibada
Tunaweza kusema liturjia ni wajibu wa umma au huduma kwa taifa inayofanywa na raia, ni kazi ya watu wote au huduma kwa niaba /kwa manufaa ya taifa.
2. Katika biblia huduma –huduma ni liturujia
a. Katika agano la kale
Tafsiri yay a Biblia ya kigiriki iitwayo Septuagiinta inatumia liturjia kwajili ya utumishi wa umma wa Hekalu, Kut 39:1 Utaona kutumika ni Liturujia. (Tafsiri ya Kiswahili haitumii neno liturujia) Bali inatumika kueleza kazi za dini za makuhani, Kama vile kazi ya huduma ya hekaluni na hii tunaweza kuipata katika kitabu cha Yoel 1:9, 2:17
b. Katika agano Jipya
Ni adhimisho la ibada ya Kimungu Lk 1:23 -Makuhani (mf. Zakaria, Walawi na huduma yao)
Na pia ni tangazo la injili tunaweza kuona kupitia Mdo 13:2, Rum 15:16
Hali kadhalika ni Mapendo kwa Matendo Rum 15 27.
Sadaka ya Kristo.
Katika luka 1:23,’ Ikawa siku za huduma yake zilipo Timia akaenda nyumbani kwake “Katika Waebrania 8:6. Lakini sasa amepata huduma iliyo Bora Zaidi kwa kadiri alivyo mjumbe wa Agano lililo bora na lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora “Kuhani mkuu wa sheria Mpya amepata Liturujia ilio bora kwani ni aina bora ya utumishi kuliko ule wa hekalu.
3. Liturujia katika kanisa
Soma sacrosanctum Concilium namba 7. Tuna soma hivi, “Kumbe kwa haki liturujia inatazamwa kama utekelezaji wa kazi ya kikuhani ya yesu Kristu katika liturujia kwa ishara zinazoonekana, Huonyesha na kutendeka katika kutakatiifuza kwake wanadamu na kila ishara ikiwa na maana yake ya kipekee.Katika liturujia Ibada halisi za hadharani huadhimishwa na mwili wa fumbo wa yesu kristu Hili ni tendo takatiiifu kupita yote.
Matumizi ya Liturujia katika kanisa lina maana ya huduma au utumishi rasmi wa kanisa wa hadhara. Hivyo basi:
Liturujia ni kazi ya ukuhani wa Yesu Kristu.
Kazi ya Kristo –kwa njia ya Liturujia , Kristu Mkombozi wetu na kuhani Mkuu huendeleza katika kanisa lake pamoja nalo na kwa njia yake , kazi ya ukombozi wetu.
Kazi ya kanisa. Katika liturujia kanisa huadhimisha hasa fumbo la Pasaka ambalo kwalo kristo alikamilisha kazi ya wokovu wetu. Hivyo, Kanisa la Mungu lashiriki katika kazi ya Mungu.
Katika hali zote, Liturujia ni swala la huduma kwa Mungu na kwa watu.
Kwa hivyo kila adhimisho la Liturujia kwakuka ni tendo la yesu kristo kuhani na mwili wake , ndilo kanisa , na ni tendo takatifu kupita yote na hakuna tendo jingine la kanisa linalofanana nalo kwa manufaa na kwa kiwango kile kile kwa daraja la ile ile (SC 7)
4. Liturujia
Ni tendo la hadhara la Kristu mzima kabisa katika kanisa lake ambapo waamini hufanya ibada ya hadhara ya kumsifu na kumtukuza Mungu Baba wakiwa wameunganika na kichwa Yesu Kristo.
5. Nia ya liturujia
Liturujia ni chanzo au chemchem sifa ya milele ya maji yaliyo hai ambapo inabidi kuchota bure zawadi ya Mungu. Mababa wa Mtaguso wa pili wa Vatikani wanaeleza nia ya liturujia inayowekwa katika kazi ya wokovu kuwa ni kwaajili ya:
- Tendo la shukrani la kumsifu Mungu/Masifu kwa Baba
- Kumbukumbu ya sadaka ya Kristu na ya mwili wake
- Na utakaso wa mwanadamu kwa uwepo wa Kristo na neno lake na roho wake.
6. Asili ya Liturujia ya Kanisa.
Mungu Baba: ametuumba.Ndio asili ya Liturujia. Lengo la Liturjia ni utukufu kwa Mungu .Maisha ya Binadamu lazima yaelekezwe kumjua Muumba wake, Agano kati ya Mungu na mwanadamu ni kati ya Pande zisizo sawa:Mungu awezaye yote na ni Binadamu anaye mtegemea Mungu kabisa .Udogo huu wa binadamu mbele za Mungu huonyeshwa kwa namna binadamu anavyo takiwwa kujinyenyekeza mbele za Mungu kwa kumsifu ,kumwomba n.k
7. Maana ya sakramenti katika adhimisho la Ekarist takatifu.
Lugha ya zamani ya kanisa ilikuwa Kigiriki. Walipokuwa wakiadhimisha ubatizo na kipaimara. Walikuwa wakisema kuwa ni Mysterion yaani fumbo .9yaani kitu kilichofichika) walipokuja kulitafsiri neno hilo la Kigiriki katika kilatini wakasema kuwa ni Mysterum. Lakini watu walipata shida kuelewa neno hili kwa sababu halikuwa rahisi kwao, Ndipo wakatafsiri kwa kutumianeno la pili la Sakramentum, Ambalo linatumika kwa katika Kiswahili kama Sakramenti alama inayoonekana. Katika Kiswahili Maysterium inatafsiriwa Kama fumbo na sakramenti inatafsiriwa kama SakramentiSakrament ni ishara inayoonekana ambayo ndani yake kuna Fumbola wokovu (Mysterium), Ndio maana tunapo adhimisha Sakramenti tunasema tunaadhimisha mafumbo ya wokovu.
8. Mambo muhimu katika kuadhimisha Sakramenti
Sakramenti huadhimishwa katika Imani kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Katika kuadhimisha sacrament kuna mambo muhimu yanayo hitajika. Materia –Ishara na Forma- Maneno na mhudumu. Materia ni kitu kinachotakiwa kutumika ili kuadhimisha hiyo sakramenti, mfano maji kwaajili ya Ubatizo, Forma ni maneno yanayotamkwa wakati wa kuaadhimisha hiyo Sakramenti. Mfano; X nakubatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Muhudumu ni yule anaeadhimisha Sakramenti kwa jina la kanisa na kwa mamlaka ya kanisa.
9. Sakramaneti ya Ekaristi
Sakramenti ya Ekaristi ni chemchem na kilele cha maisha yote ya kikristo (K.K.K 1324 ) Kushiriki Ekaristi ndio kiwango cha Juu cha Kuungana na kristo katika tendo la kumwabudu Mungu Baba . Sakramenti hii huitwa majina mbalimbali yanayotokana na jinsi ilivyo adhimishwa katika mwendo wa karne. Neno Ekaristi la maanisha kutoa shukrani kwa mungu” Hivyo Ekarist ni ni tendo la Shukrani kwa Mungu. Yesu anatoa Shukrani Kwa Mungu kwa kukamilisha kazi aliyo pewa, Huitwa pia karamu ya bwana ambayo yajieleza kwa kumega mkate, yaitwa ukumbusho wa Mateso ya bwana na vilevile yaitwa komunyo. Kwa sababu katika kuupokea Mwili na Damu yake tunaungana naye nakuwa mwili mmoja. Adhimisho lake linaitwa misa takatifu. Materia ni Mate na Divai iliyo changanywa na maji.
10. Anayeadhimisha Liturujia –Misa takatifu
Ni Taifa lolote la Mungu –Mwili wa Fumbo wa yesu Kristo – Mwadhimishaji wa kwanza ni waumini waliokusanyika pamoja na kanisa. Kila mtu huchukua nafasi katika adhimisho hili kadiri ya hali yake. na mtendaji mkuu ni Kristo na kanisa ambalo linaonekana kwa njia ya waumini , Hivyo adhimisho ni tendo la Liturujia la kanisa zima . Adhimisho la liturujia ni sherehe (Celebration)
11. Maeneo muhimu katika adhimisho
Fumbo – utatu mtakatifu katika Historia ya wokovu
Ibada-sababu ya kipasaka. Tukio la pasaka katika adhimisho. Ibada ni ni kuishi tukio au tendo la Pasaka –Kumbukumbu.
Uwepo wa Kristo- Fumbo linalo adhimishwa katika Ibada ni lazima liwe hai na liwe ni maisha halisi.
12. Tabia
Tendo la kukutana katika kundi acclesia.
Kuitwa taifa la Mungu limekusanywa kwa jina la Baba, la mwana na la Roho Mtakatifu.
Kufanya Shere-Adhimisho la Ekarist ni sherehe, nitendo la shukrani linalofanywa kwa Mungu
13. Mwenendo wa adhimisho la Ekaristi Takatifu.
Liturujia ya Neno (masomo ya Agano la kale na Agano Jipya).
Kusoma Neno-Homilia, na maombi yake.
Liturujia ya Ekaristi –kuleta mkate, na Matoleo, Kushukuru konsekrasio na Komunyo
Matayarisho ya Vipaji –Kuviweka altareni
Utangulizi (Prefatio)-Shukrani za kanisa Kwa Mungu Baba-Uumbaji Duniani –Mbinguni
Anaphora (sala ya Ekarist) sala ya shukrani na sala ya wakfu (consecration)- Epikles –Kumwomba roho Mtakatifu Pamoja na maneno ya Yesu –Kilele cha mageuzo.
Anamnes- kumbukumbu ya mateso, ufufuko na kurudi kwake katika utukufu
Maombi –Umoja wa kanisa zima –Yanagusa sehemu mbalimbali
Komunyo- Baba yetu Sala ya Bwana na kumega Mkate.
14. Fumbo la Pasaka
Kiini cha adhimisho la liturujia ni fumbo la Pasaka ya kristo Kufa na kufufuka. Katika adhimisho la Liturujia Kristo ndiye anayetenda.
1. Kristo yupo katika Neno lake
2. Kristo yupo katika Muhudumu-Kasisi –Padre.
3. Kristo yupo katika hadhara ya waumini-katika kanisa linalosali na kuimba
4. Kristo yupo katika ekaristi takatifu (sakramenti zote saba)
15. Vitabu vya Liturujia (misa takatifu)
Kitabu cha masomo ya Misa takatifu-the Lectionary (lectionaries) Ni kitabu chenye masomo yanayosomwa wakati wa Misa takatifu.
Misale (Misale Romanum) Ni kitabu chenye sala na kanuni mbalimbali (Rublics) Zinazotumika kwa adhimisho la missa takatifu.
Pontificale (Kitabu chenye maadhimisho yanayoongozwa na Askofu (kwenye Ushemasisho, Upadrisho, Uaskofusho na kutabaruku kanisa)
Rituale –Ni kitabu cha sala na maelekezo muhimu kwaajili ya kuadhimisha Sakramenti na Visakramenti, mazishi, maandamano na maadhimisho mengine.
16. Mwaka wa Liturujia-Adhimisho la fumbo la Kristo
Mwaka wa liturujia ni mzunguko wa kila siku mwaka wa kalenda ya Liturujia ambapo kanisa huadhimisha matukio makubwa ya historia ya wokovu, toka umwilisho na kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo, mateso , kufa na kufufuka kwake na mpaka siku ya zawadi ya Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste. Mwishoni mwa mwaka Liturujia Hutafakari kwa matumaini kurudi kwake Bwana .Mwaka wa liturujia umewekwa kwa mzunguko mzunguko wa makundi ya mwaka A,B na C. Hivyo kuna masomo yanayosomwa mwaka A,B na C na masomo haya yamekuwa na lengo Fulani.
17. Injili inasomwa kwa mtiririko huu.
1. Mwaka A-Injili kadiri ya Mathayo
2. Mwaka B-Injili kadiri ya Marko.
3. Mawka C- Injili kadiri ya Luka.
4. Injili ya Yihana haina mwaka maalumu isipo kuwa husomwa katika miaka yote mitataukwa matukio, Na injili hii husomwa Zaidi wakati wa mateso ya Bwwana.
18. Mpangilio wa mwaka wa liturujia
- Majilio
- Kipindi cha kuzaliwa bwana
- Kipindi cha mwaka baada ya tokeo la Bwana
- Kwaresma
- Siku tatu kuu za Pasaka (triduo Pasquale). Kitvu vha maadhimisho yote ya mwaka ya Liturujia kimeundwa na siku tatu kuu za pasaka fumbo. Mateso, Kufa,na kufufuka kwa Yesu Kristo amabapo ni mwaka wa kiliturujia . Siku tatu kuu za pasaka za mateso na ufufuo wa bwana zinag’aa kama ukamilifu wa mwaka wote wa liturujia.
- Kipindi cha Pasaka mpaka pentekoste, Kipindi cha mwaka baada ya
pentekoste. Kipindi cha mwaka cha liturujia kina majuma 33 au 34. Ni
maadhimisho ya historia ya wokovu ambapo dominika ni pasaka ya wiki.
19. Sherehe.
Sherehe zinatazamwa Kama siku muhimu katika mwaka wa kanisa. Maadhimisho yake huanzia na masifu ya kwanza ya jioni siku inayotangulia. Baadhi ya sherehe zina misa yake ya kasha ambayo amabayo inaadhimishwa jioni kabla ya siku ya sherehe. Na masomo ni maalumu ya sherehe
20. Sikukuu
Huadhimishwa siku yenyewe, hazina masifu ya kwanza ya jioni .sikukuu za bwana zinazoangukia siku ya dominika ya mwaka au kipindi cha noeli nazo huchukua nafasi ya Dominika.
21. Kumbukumbu
Ni za lazima au za hiari .Hizo huingizwa katika adhimisho la siku ya juma kadiri ya kanuni zilizowekwa katika katiba kuu za misale ya kirumi na ya kiliturujia ya vipindi. Kumbukumbu za lazima zinazotokea siku za juma wakati wa kwaresma zaweza kuadhimishwa tu kama kumbukumbu za hiari. Iwapo katika siku moja zinatokea kumbukumbu Zaidi ya moja, ni moja tu yaweza kufanyika.
22. Jumamosi
Jumamosi za kawaida Kama hakuna kumbukumbu ya lazima inaruhusiwa kufanya kumbukumbu ya hiari ya Bikira Maria.
23. Sheria muhimu za liturujia (Fundamental Principles of Liturgy)
Sheria zinazoongoza liturujia (Guiding Principles)
a. Liturujia ni utekelezaji wa kazi ya kikuhani ya Yesu Kristo (SC 7),
Na ni teologia iliyo katika mtindo wa sala, kiini chake ni fumbo la Pasaka, kila tendo la kiliturujia tufanyalo ni ushiriki wetu katika fumbo la pasaka la kristo.
b. Lioturujia ni kilele cha chemchem cha shughuli zote za kanisa (SC 7,10),
Lengo la klazi za kitume ni kuwakusanya wabatizwa wote wamtukuze Mungu katika kanisa, washiriki sadaka na kuila karamu ya Bwana .Liturujia huwasukuma waamini walio lishwa kwa Sakramenti za kipasaka ‘’ kuishi katika umoja wa utakatifu’’
c. Liturujia hutaka ushiriki kamili (SEC 14)
Kama kanisa anatamani Sana waamini wote waongozwe katika kuyashiriki maadhimisho ya kiliturujia kwa utimilifu, kwwa ufahamu na utendaji.
d. Liturujia hutambulisha kanisa (SC 14)
Katika adhimisho la kiliturujia ambapo, AskofuMapadre na Walei wamekusanyika kuzunguka Altare moja, katika umoja wa ala, hapa sur ya kanisa inaonekana wazi wazi.
e. Liturujia yataka Unity (Umoja) na si “Uniformity”(SC 37)
Zamain kulikuwa na usemi: Roma lakuta, causa finite. Hilo halieleweki hivyo siku hizi kikubwa watu wamsifu Mungu kadiri ya desturi zao.
f. Liturujia yahitaji “ Mapokeo mema”
Liturujia inasehemu mbili muhimu, Isiyo onekana, isiyobadilika, ya milele na inayoonekana, inayoweza kubadilika na ya kibinadamu. Yaliyowekwa na Yesu kristo mwenyewe na hakika leo hii hatubadili. Mf .Alama za mkate na divai.
Sheria zinazosaidia utendaji (Operational Principle)
g. Liturujia yataka lugha inayoeleweka.
Kilatini kilikua na faida kwani popote utakapokuwapo, utaweza kushiriki misa vizuri, ila hakikuwa kinaeleweka na wengi , ili kuwe na ushiriki kamili kwa mafumbo hayo ya kimungu lazima tuelewe kile tusemacho . Jibu sahihi ni kwamba, Liturujia ifanyike katika lugha ambayo inaeleweka na watu wa mahali hapo.
h. Liturujia yadai kujulikana kwa neno la Mungu
Biblia ni muhimu sana katika Liturujia , kwa sasbabu kutokana na hayo tunapata sala, masomo, zaburi, mahubiri, n.k. Aidha maandiko matakatifu ndiyo yanayotusaidia kuelewa maana ya sakramenti , Visakramenti na hata Baraka.
i. Liturujia yataka kujulikana (SC 44-46)
Watu wafundishwe kujua liturujia ili washiriki vizuri .Katekesi ya Liturujia ni muhimu sana kujulikana.
j. Liturujia huendana na Muziki (SC 112-121)
Mt. Agustino allisema anayeimba vizuri ,husali mara mbili .Muziki mtakatifu huzidi kuwa mtakatifu pale uunganikapo na tendo la liturujia, kwa sababu utafanya sala kuwa tamu Zaidi na hasa kuonyesha umoja wa moyo , pia utaleta heshima Zaidi katika maadhimisho matakatifu
UTARATIBU WA LITURUJIA MAJIMBONI
Kwavile liturujia ni tendo la kanisa zima, linahitaji kuratiibishwa ili maadhimisho hayo yasaidie kukuza Imani ya wanakanisa. Kwa lengo la kulilea jimbo kiliturujia, kila askofu mahalia awe na kamati ya liturujia (SC 41, 42). Hiyo itahusika na Madhehebu, Muziki mtakatifu na mahali pa kuabudia na vifaa vyake. (SC 44-46).
Kazai ya kamati ni kuratibu liturujia jimboni.
Wajumbe wake lazima wawe:
a. Wapende kujielimisha katika liturujia.
Kuna hati nyingi zitolewaza na kanisa juu ya liturujia. Wafanye bidii ya kujisome na kufahamu yasemwayo humo.
b. Wawe na jicho linaloona na sikio linalosikia.
Wanakamati wwafungue macho na masikio ili kuona na kusikia jinsi liturujia yetu inaavyo adhimishwa. Pale ambapo inakwenda Kwa kadiri ya miongozo, tunawapongeza na kuwatia moyo waendelee. Pale ambapo kuna shida watafute namna iliyo bora ya kurekebisha ili watu wamtukuze Mungu kwwa kufanya vizuri kiliturujia.
KAMATI YA LITURUJIA JIMBO
Kamati ya liturujia jimbo yafaa iwe na wajumbe wapatao 20 ambao watatengeneza idara ndogo ndogo zitakazo shughulikia mambo maalumu kama zitakavyo tumwa na kamati. Ifuatayo ni orodha ya mapendekezo ya idara hizo ndogo ndogo na majukumu yake.
a. Idara ya ibada
Kutoa semina juu ya maadhimisho pamoja na alama za Liturujia kwa wadau wa liturujia jimboni. Mapadre, watawa, Walei, Kwaya, Makatekista na vyama vya kitume.
Ufuatiliaji wa maamuzi ya kamati ya liturujia jimbo.
Kufuatilia uundwaji wa kamati ya liturujia maparokiani.
Kuhakikisha kuwe na vifaa mbalimbali vinavyo hitajika katika liturujia , mf; Vitabu (vitabu vya misa, masomo, kalenda, chetezo, misalaba, n.k)
Kupanga utaratibu wa namna ya kuendesha jumuiya ndogo ndogo za kikristo.
Kufuatilia madhimishi ya kiliturujia kuona kama yanaenda kadiri ya miongozo mf:
Kwaya na kucheza/Kwaya na matendo ya kiliturujia.
Heshiima mbali mbali kwa kanisa, mf; namamna ya kutembea, kukaa n.k.
b. Idara ya muziki mtakatifu.
Kupitia nyimbo ambazo zinatungwa kila sikuna kuzihakiki na kisha kutoa kibali cha nyimbo zile zitakazoimbwa jimboni.
c. Idara ya Sanaa takatifu na na mapambo
Kueleza maana ya Sanaa takatifu na nafasi ya mapambo katika maadhimisho mbalimbali.
Kutoa miongozo na namna ya kujenga makanisa n.k
d. Idara ya tafsiri na Matini
Kutunga sala Kwa mahitaji mbali mbali.
Kurekebisha kutafsiri ya matini mbalimbali.
Kuendeleza kutunza vitabu vilivyo tayarishwa.
Reference (vitabu vya rejea)
Amigu, T., Maswali Wanayobandikwa Wakatoliki.Peramiho Printing Press, Peramiho, 2007.
Paulines Publications, Katekisimu ya Kanisa katoliki.Paulines Publications Africa, Nairobi, 1999.
Pd Kaluwa Y., Jifunze liturujia ya Misa Takatifu.Moccony Printing Press Publications, Dar es Salaam, 2017
Pd kangalawe J., Liturujia ya Misa Takatifu.Idara ya Liturujia, Dar es Salaam, 2014.
Martimort, A.G., The church at Prayer Vol I, Principles of the Liturgy. The liturujical Press, collegevill Minesota
- Matukio
- Juinge na Kanisa
- Neno kuu la mwaka 2018
- Kalenda ya matukio 2018
- Ramani ya Tovuti
- Biblia Mtandaoni na zaidi
- Liturujia ya Kanisa Katoliki
- Mkate wa siku ya LeoLorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore Ut enim ad minim magna aliqua”2 kor 2:16