DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA LUHANGA
MAMBO YA JUMLA YA PAROKIA
Jina la parokia ni mtakatifu yohane mbatizaji luhanga
-Msimamizi wa parokia ni mtakatifu yohane mbatizaji
- Jina halifanani na parokia nyingine za jimbo la Dar es salaam
Mahali parokia ilipo ni Wilaya ya Ubungo kata ya Mabibo Farasi.
Parokia ilitangazwa rasmi 20 january 2013
Parokia ipo katika dekania ya Ubungo
Idadi ya waumini katika parokia Mpaka kufikia 2016 ilikua ni kati ya waumini 7500 na imepatikana kwa njia ya sense iliyofanyika 2016 kwa waumini kujaza fomu maalumu.kwa sasa kuna waumini Zaidi ya 7500.Sensa nyingine inatarajiwa kufanyika 2018
Jumuiya zilikuwa (25) lakini kutokana na watu wengi kuhamia jumuiya hizo zimefikia 47.
Parokia ina kigango kimoja kinachofahamika kwa jina la mt Peter Feba. Na kipo Mabibo na kina kanda,Jumuiya 16.
Parokia ina idadi ya jumuiya 65 na zinatumia majina ya watakatifu.
Kila jumuiya ina kaya kati ya 20-25
Jumuiya zinasali mara moja kila siku ya jumamosi kuanzia saa 12:30 kwa kufuata mwongozo wa jumuiya ndogo ndogo toka Jimboni
Kanda husali mara moja kila baada ya mwezi mmoja mwisho wa mwezi.
Maudhuri kwa jumla katika JNNK ni ya wastani, na maudhurio huwekwa katika kumbukumbu.
Viongozi wa kamati tendaji wana utaratibu wa kuzitembelea jumuiya JNNK , Kanda na pia misa zinasomwa.
Kanda JNNK hua zinaadhimisha Misa takatifu za somo wa jumuiya na kanda kwa kuomba kibali kutoka hierakia.
Uongozi wa jumuiya umekamilika na pale ambapo inapotokea kuna mapungufu yanajazwa mara moja kwa kuitisha uchaguzi mdogo.
Uongozi wa Halmashauri ya walei parokia hukutana kila baada ya miezi miwili, na kwa kanda ni baada ya miezi mitatu.
Huduma za kiroho na jamii hutolewa katika JNNK/Kanda na mitaa kama ifuatavyo.
a) Misa za somo wa jumuiya
b) Huduma za kutembelea wagonjwa na kuwapa sacrament
c) Ujazaji fomu kwaajili ya maombi ya sakramenti kama Ubatizo, Komunio ,kipaimara, na huduma zingine zitolewazo na kanisa.
d) Kutembelea waumini na kuhimiza juu ya kufanyika sacrament mbalimbali pamoja na kuhimiza kuondokana na uchumba sugu.
Changa moto kubwa zilizopo ni maudhurio madogo kwa waumini kwenye Jumuiya , Mikutano,na hata semina.
Pia kuna mwamko mdogo katika utoaji michango inayohusu kanisa
Changamoto nyingine ni michango kuwa mingi kanisani.
UONGOZI
Kamati tendaji ipo na imekamilika kikatiba
Kamati tendaji ya parokia hukutana mara moja kila mwezi siku za jumamosi na kikao kinachukua muda wa masaa mawili kujadili .Baba paroko ni mshiriki katika kikao hicho.
Vikao vya dharura hufanyika pale vinapo hitajika.
Halmashauri ya walei ya parokia inaundwa na viongozi watano wa kila jumuiya pamoja na wenyeviti wa vyama vya kitume na inakutana mara moja kila baada ya miezi mitatu.
Agenda na taarifa za vikao zinapatikana kwa wakati na zinatunzwa.
Parokia haijawa na ofisi za halmashauri ya walei ya parokia, lakini mipango ipo ya kuwa na ofisi na vitendea kazi vya ofisi vipo baadhi, lakini computer inatumika ni ya ofisi ya paroko.
Njia za mawasiliano kwa wajumbe wa kamati tendaji pamoja na halmashauri ya walei ni :
Kwa njia ya barua pepe(yaani E mail) simu,Whats aap, lakini zaidi ya hapo ni kwa matangazo kanisani.
Anuani ya barua pepe yaani E mail ya parokia ipo.
Zipo kamati ndogo ndogo za kikatiba na zimekamilika,
kamati hizo hua zinakutana mara mara.
Zipo kamati zingine Ambazo sio za kikatiba na zinaripoti kwa kamati tendaji ya parokia, kamati hizi ni kama zifuatazo:
a) Kamati ya ujenzi
b) Kamati ya uhamasishaji.
Kamati zote za kikatiba na zisizo za kikatiba zinaripoti kwa kamati tendaji ya paarokia
kamati hizi hazina mwingiliano lakini kuna wakati zinashirikiana
Dira malengo na mikakati ya parokia
- DIra ; Dira ya Parokia ni kuwajenga waumini kiroho hasa wale wwanaoonyesha kukata tamaa ikiwa ni pamoja na kuwatembelea
- Malengo;Kuendeleza mipango ya parokia kama ujenzi wa kanisa la kudumu la kigango cha MT Peter Feba kilichopo mabibo na kumaliza jingo la vijana.
- Mikakati ya parokia; Mikakati ya parokia inaendana na
utekelezaji wa malengo ya mikutano halmashauri ya walei itakapo pangwa
na parokia.
Ipo kalenda ya matukio ya mwaka ya kiparokia amabayo imetengenezwa kwa ushirikishwaji wauminiWaamini wanaarifiwa mipango ya parokia kwa kupitia maatangazo kanisani , pia kupitia JNNK kupita halmashauri ya walei ya parokia au viongozi kutembelea jumuiya na kueleza jambo husika.
VYAMA MASHIRIKA NA JUMUIYA ZA KITUME (VMJ)
Vipo vyama vya kitume 13na vikundi 3
Vyama hivi vina wachama wa wastani vinakidhi mahitaji ya parokia
Vyama na vikundi vya kitume vinafanya kazi kulingana na katiba ya halmashauri ya walei ya jimbo.na vyama vyote hivi viko hai
Vyama hivi havina ofisi parokiani, lakini vinalelewa na vipo chini ya paroko.
Wasimamizi wake wamegawanyika katika makundi, yaani Makatekista, Masista na kamati tendaji ya parokia.
VMJ vinatoa taarifa na repoti pamoja na ya fedha mara kwa mara kwa uongozi wa parokia
Na pia vinajitegemea na viko chini ya uangalizi wa parokia
Vyama vina ushirikiano mzuri katika dekania na katika ngazi ya jimbo
VMJ haina mambo maaalumu ambayo yanaweza kuigwa na parokia nyingine yote ni ya kawaida sana. Kama vile kuuza maadili katika jamii has kwa vijana.
SEMINA MBALIMBALI KATIKA UENDELEVU WA IMANI, UONGOZI NA UTEGEMEZAJI
Ziko semina ambazo zimeshafanyika kuanzia ngazi ya JNNK, VMJ na hadi Parokia
Mafungo na semina mbalimbali ziinaendelea kuandaliwa kutokana na ratiba ya parokia.
Vyama vya kituume vina ongozwa na ratiba yake maalumu.
Viongozi wa kamati tendaji wamefanyiwa semina .
Semina za kiroho zinafanyika kwa kalenda ya parokia
Hali ya Imani kwa ujumla inaridhisha, na inatakiwa kuendelezwa kwa nguvu, lakini katika kipindi cha huruma ya Mungu Viongozi na hiarakia wameweza kuhamasisha waumini waliokuwa na ndoa , Ndoa thelathini na tano zimeweza kufanikishwa.
Kimsingi hali ya utoaji parokiani ni ya wastani na kiasi inaridhisha.
Hali kadhalika utoaji wa zaka kama amri ya kanisa upo kwa kiwango cha chini.
Parikia inatoa michango ya jimbo kamili kama inavyo paswa
FEDHA NA MIPANGO
Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa jimbo
Mapato na matumizi ya parokia yanajulikana kwa waumini na yanatolewa taarifa.
Matoleo ya kila dominika yanatangazwa kwa waumini kila dominika inayofuata na kubandikwa kwenye mbao za matangazo ya kanisa.
Fedha zote zinazokusanywa hupelekwa benki kwa wakati
ULINZI NA USALAMA
Hali ya ulinzi na usalama parokiani ni ya kuridhisha, na ulinzi unafanywa na kampuni binafsi
MAENDELEO YA KIUCHUMI
Parokia ina miradi miwili
Shule ya chekechea
Na shule ya sekondari ya miaka miwili yaani Qt
Kwa sasa Parokia ipo katika ujenzi wa kigango cha Mt Peter Feba mabibo na jengo la vijana la parokia , na hali ni nzuri na waumini wanahamasishwa kuendelea kutoa michango yao.
Lakini pia ipo mipango ya kuwaendeleza waumini kiuchumi
a) Ipo saccos ya parokia waumini wanahamasishwa wajiunge
b) Mpango mwingine ni jingo la vijana na watoto wa utoto mt
c) Malengo mengine ni kuwa na vyarahani ili kuwaendeleza vijana
MAMBO YA JUMLA
Parokiia haina mgogoro wowote wa kimipaka
Kwa sasa parokia haina mipango yeyote ya kuwaendeleza waumini wake kiuchumi isipokuwa kwa kadiri parokia inavyokuwa itafanya juu chini mipango hiyo iwepo
Idadi ya mapadre inatosheleza
Parokia ina wanasemiri 11 kwa ujumla katika seminari mbalimbali
Hakuna waumini waliojiunga na utawa katika parokia yetu
Maandiko kuhusu historia ya parokia picha waamini na picha za miradi zipo baadhi na zinaaendelea kufanyiwa kazi.
Mwisho tunawashukuru kwa ushirikiano wenu.