PAROKIA YA ANANASIF


Jina la msimamizi wa parokia ni mtakatifu Hananasif na haiingiliani na parokia nyingine

Mahali Parokia ilipo kijiografia ni kinondoni Hananasif, na inapakana na parokia ya Mwananyamala upande wa kaskazini, upande wa magharibi ni parokia ya magomeni, na upande wa kusini inapakana na parokia ya St Imakulata na upande wa mashariki inapakana na parokia ya St peters

Parokia ya Mt Hananasifu iko katika dekania ya St Peter’s

Idadi ya waumini katika Parokia ya Mt Hananasif ni kati ya waumini 3050 na imepatikana kwa njia ya sense iliyofanyika 2016

Sensa ilifanyika kwa kupitia JNNK

Parokia haina kigango

Parokia inakanda 7 na jumuiya 24, na viongozi wake wanachaguliwa kulingana na katiba ya jimbo, Kanda pamoja na JNNK wanatumia majina ya watakatifu

Kila jumuiya ina kaya kati ya 15-20

Jumuiya zinasali mara moja kila siku ya jumamosi kuanzia saa 12:30 kwa kufuata mwongozo wa jumuiya ndogo ndogo.

Kuhusu maudhuri kwa jumla katika JNNK, wakina mama wanajitahidi, lakini kuna changamoto kwa upande wa akina baba.

Maudhurio yanarekodiwa hutunzwa katika kumbukumbu.

Upo pia utaratibu wa kuzitembelea jumuiya JNNK na Kanda. Misa takatifu za somo wa JNNK na Kanda huadhimishwa kila baada ya mwaka mmoja.

Uongozi wa jumuiya umekamilika na pale ambapo inapotokea kuna mapungufu yanajazwa mara moja kwa kuitisha uchaguzi mdogo.

Halmashauri ya walei ya parokia /kanda hukutana mara moja kwa mwezi

Mapadre wanawatembele wagonjwa na kuwapa huduma za kiroho wahitaji, na wahitaji wanahudumiwa mara moja kila wiki, huduma ya afya na macho hutolewa kila baada ya miezi mitatu.

Mahudhurio hafifu hasa kwa akina baba, vijana pamoja uchumba sugu, madawa ya kulevya pamoja na ukosefu wa ajira ni changamoto kubwa katika utoaji huduma katika JNNK

UONGOZI
Kamati tendaji ipo na imekamilika kikatiba

Kamati tendaji ya parokia hukutana mara moja kila mwezi majira ya jioni na kikao kinachukua muda wa saa moja kujadili .Baba paroko ni mshiriki katika kikao hicho.

Halmashauri ya walei ya parokia inaundwa na viongozi watano wa kila jumuiya pamoja na wenyeviti wa vyama vya kitume na inakutana mara mbili kwa mwaka siku ya juumapili.

Agenda na taarifa za vikao zinapatikana kwa wakati na zinatunzwa.

Parokia haijawa na ofisi za Halmashauri ya Walei ya Parokia , lakini mipango inaundwa ili kuwa na ofisi na vitendea kazi

Njia za mawasiliano kwa wajumbe wa kamati rendaji pamoja na halmashauri ya walei ni :

Kwa njia ya barua na simu

Kwa ujjumla barua pepe yaani E mail ya parokia hamna kwa sasa.

Zipo kamati ndogo ndogo za kikatiba na zimekamilika, na kamati hizo hua zinakutana mara moja kwa mwezi

Zipo kamati zingine Ambazo sio za kikatiba na zinaripoti kwa kamati tendaji ya parokia, kamati hizi ni kama zifuatazo:
a.    Kamati ya afya
b.    Kamati ya maafa
c.    kamaati ya ibada
d.    kamati ya maendeleo

Ipo kalenda ya matukio ya mwaka ya kiparokia ambayo imetengenezwa kwa ushirikishwaji waumini

Waamini wanaarifiwa mipango ya parokia kwa kupitia matangazo kanisani, pia kupitia JNNK kupita halmashauri ya walei ya parokia

VYAMA MASHIRIKA NA JUMUIYA ZA KITUME (VMJ)
Vpo vyama vya kitume 12 kama ifuatavyo
1.    Moyo mtakatifu wa yesu
2.    NEO KATEKUMINATO
3.    WAWATA,
4.    UWAKA
5.    VIWAWA,
6.    Utoto mtakatifu
7.    Shikwaka
8.    Mt Anna
9.    Watumishi wa altare

Vyama hivi vina watumishi wa kutosha na vinakidhi mahitaji ya parokia

Vyama na vikundi vya kitume vinafanya kazi kulingana na katiba ya halmashauri ya walei ya jimbo.na vyama vyote hivi viko hai

Vyama hivi havina ofisi parokiani, lakini vinalelewa na vipo chini ya uongozi wa parokia

VMJ vinatoa taarifa na repoti pamoja na ya fedha mara kwa mara kwa uongozi wa parokia

VMJ vinajitegemea lakini viko chini ya uangalizi wa parokia

Vyama vina ushirikiano mzuri katika dekania na katika ngazi ya jimbo

Mambo ya kujifunza katika parokia hii ni jinsi ambavyo kwaya zinavyo injilisha

SEMINA MBALIMBALI KATIKA UENDELEVU WA IMANI, UONGOZI NA UTEGEMEZAJI
Semina mbali mbali zinaandaliwa na kufanyika hapa parokiani zikiwemo semina za ndoa ,semina za vijana ,utoaji na uongozi

Semina zingine ni zile ambazo zinatolewa kwa viongozi mfano ni semina ya viongozi iliyofanyika st joseph na masimbazi centre na bado semina za namna hiyo zinahitajika ili kuimarisha uwezo w kiutendaji kwa viongozi.

Zipo semina za kiroho ambazo zinafanyika parokiani , ambapo viongozi wa kiroho huwatembele JNNK mara kwa mara na kusoma misa pamoja na kuhamasisha  waumini.

Hali ya Imani kwa ujumla inaridhisha

Kimsingi hali ya utoaji parokiani pia ni nzuri

Hali kadhalika utoaji wa zaka kama amri ya kanisa pia ni mzuri

Parikia inatoa michango ya jimbo kamili kama inavyo paswa

FEDHA NA MIPANGO
Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa jimbo

Mapato na matumizi ya parokia yanajulikana kwa waumini na yanatolewa taarifa na hii inatolewa mara moja kwa mwaka

Matoleo ya kila dominika yanatangazwa kwa waumini kila dominika inayofuata

Fedha zote zinazokusanywa hupelekwa benki kwa wakati

ULINZI NA USALAMA
Hali ya ulinzi na usalama parokiani ni ya kuridhisha, na ulinzi unafanywa na kampuni binafsi

MAENDELEO YA KIUCHUMI
Kuna ujenzi wa jengo la kitega uchumi, na pia kuna mradi wa shamba wa hekari 13.5 uliopo kijiji cha karakaza kibaha kwa matiasi

MAMBO YA JUMLA
Parokia inaendesha SACCOs ili kuwaendeleza waumini wake. Pia kuna shule ya ushonaji na chekechea. Hali kadhalika semina mbalimbali zinaendeshwa juu ya ujasiriamali katika kutoa mbinu mbalimbali za kibiashara

Idadi ya mapadre kwa sasa inatosha

Parokia imetoa idadi ya wanafunzi watano waliojiunga na seminary.

Waumini ambao wamejiunga na utawa kutoka parokia ya hananasif ni watano

Ipo pia historia ya parokia pindi itakapohitajika

JE UNATAFUTA

PAROKIA?

Upate majibu yako haraka zaidi
Ramani ya Parokia
Hakuna ramani kwa sasa...
Kuhusu Kanisa Katoliki

Ofisi ya Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam inapatikana makao makuu ya Jimbo,
Kanisa la St. Joseph, barabara ya Sokoine na Manseld street.

P.O Box 167, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 762 024 199
Email: mawasiliano@waleijimbodaresalaam.org
            darwaleijimbo@yahoo.com
Web: www.waleijimbodaresalaam.org

Kwa Habari kemkem za Kanisa jiunge nasi

Andika email yako hapo juu, na upokee taarifa za H/walei

Copyright © 2025. All Rights reserved by H/Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam