DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA MAGOMENI
Parokia inaitwa Watakatifu mashahidi wa Uganda magomeni. Ilizaliwa 1965
Mahali kijiografia ilipo ni magomeni Makuti, wilaya ya kinondoni,mipaka yake kwa upande mashariki ni mto msimbazi, magharibi ni bonde la Tandale kabla ya kufika kituo cha tandale kwa tumbo, kaskazini ni bonde la mto mkwajuni na kusini bonde la mto kigogo.
Parokia ipo katika dekania ya Mt. Petro ambayo imeundwa na Parokia zifuatazo:
- Parokia ya Mt. Petro
- Parokia ya Mikocheni
- Parokia ya Mwenge
- Parokia ya sinza
- Parokia ya mwananyamala
- Parokia ya Hananasif
- Parokia ya Kawe
- Parokia ya Magomeni
- Parokia ya makongo juu
- Parokia ya kijitonyama
Parokia hii inaundwa na idadi ya waumini 400 kutokana na sensa iliyofanyika mwaka 2017. Parokia ya Magomeni haina Vigango.
Parokia ya magomeni inaundwa na kanda 9.
Kanda zinatumia majina ya watakatifu Mashahidi wa Uganda.
Jumuiya ndogo ndogo zipo 31 zenye idadi ya kaya 10 hadi 20 kwa kila jumuiya.
Jumuiya zinatumia Majina ya Watakatifu.
Jumuiya zina kutana kila wiki kwa kusali pamoja, lakini kikanda zinakutana mara moja kwa mwezi kutokana na mwongozo wa jimbo.
Mpango wa kuwatembelea waumini katika JNNK na Kanda unafanywa na Kamati Tendaji ya Parokia.
Jumuiya na kanda Huadhimisha Sikukuu wa somo wao pale wakati husika unapo wadia.
JNNK zina viongozi ambao huchaguliwa kwa kupigiwa kura kwa mujibu wa katiba.
Na kwa ujumla uongozi umekamilika. Pale mapungufu yanapotokea Kamati Tendaji huitisha uchaguzi mdogo ili kuziba nafasi iliyowazi.
Huduma zitolewazo katika JNNK na Kanda ni kama zifuatazo;
Kutembelea Wagonjwa, Kubariki nyumba, Kuadhimisha Misa wa somo wa Jumuiya na kusaidiana katika maisha ya kawaida.
Changamoto.
Waumini wengi katika JNNK na Kanda wanaishi katika nyumba za kupanga, na walio wengi wanapanga katika nyumba za waamini wa madhehebu na dini nyingine.
Uongozi
Kamati Tendaji ipo na imekamilika
Kamati Tendaji ya Parokia Hukutana kila Mwezi, Vikao huchukua saa moja Hadi masaa mawili, Baba paroko anashiriki katika vikao.
Halmashauri ya walei ya parokia inaundwa na wajumbe ambao ni viongozi watano kutoka kila jumuiya, Kamati tendaji ya Parokia na Wenyeviti kutoka Vyama vya kitume.
Agenda na taarifa zi vikao zinapatikana kwa wakati na vinatunzwa.
Ofisi ya Halmashauri ya Walei baado haijakuwepo rasmi lakini vitendea kazi vipo kuwezesha shughuli kuendelea.
Njia za mawasiliano zinazotumika ni kama;
Barua pepe E mail, Whats’aap groups, Siimu , Barua, Ubao wa matangazo n.k
Parokia haijawa na barua pepe bado
Zipo kamati mbali mbali zilizo za kikatiba na zisizo za kikatiba.
a. Kamati ya kikatiba ya Halmashauri ya Walei ipo na imekamilika
b. kamati zisizo za kikatiba zilizoundwa katika Parokia ni kama zifuatazo
Kamati ya ulinzi ,Kamati ya afya, Kamati ya hija na kamati ya sherehe na matukio.
Kamati ndogo ndogo za kikatiba na zisizo za kikatiba zote zina ripoti kwa kamati Tendaji.
Dira ,malengo na mikakati ya parokia
- Kuhamasisha waumini kushiriki sacrament mbali mbali za kanisa
- Kujenga familia bora na takatifu
- Kuhamasisha vijana kujiunga na VJM
- Waumini kujiunga na vikundi vya kujikwamua kiuchumi
- Ujenzi wa mnara mpya wa kengele
- Upanuzi wan a ukarabati wa nyumba ya Mapadre
Kalenda ya matukio ya mwaka ya kiparokia inaandaliwa.
Njia zinazotumika kuwaarifu waumini wote mipango ya parokia ni kwa kupitia:
matangazo kanisani , vikao na viongozi JNNK, whatsaap groups, Mawasiliano ya simu .
VYAMA MASHIRIKA NA JUMUIYA ZA KITUME (VMJ)
Vipo VMJ 13 katika parokia.
VMJ vina wanacha wa kutosha
Vyama na vikundi vya kitume vinafanya kazi kulingana na Katiba ya Halmashauri ya Wale na Vinatimiza wito wao.
Uhai wa VMJ Parokiani ni wa kawaida
Baadhi ya VMJ vina ofisi Paarokiani mfano Wawata.Vilivyo baki havina lakini hufanya kazi zao maeneo ya parokia.
Vyama hivi mlezi wake ni Paroko, Paroko Msaidizi na Kamati Tendaji.
VMJ vinatoa taarifa na ripoti pamoja nay a fedha mara kwa mara katika Uongozi wa Parokia.
Hamna chagamoto zozote katika VMJ ambazo zinawez kuhatarisha Imani Katoliki.
Ushirikiano wa VMJ za Parokia katika shughuli za kidekania na Jimbo uko vizuri.
Mambo ya kujivunia yaliyofanywa na VMJ za parokia zipasavyo kuigwa na Parokia zingine ni kama
a. Kama tamasha la vyama vya Kitume
b. Mabonanza na michezo mbalimbali.
c. Mikesha ya sala na maombi.
SEMINA MBALIMBALI KATIKA UENDELEVU WA IMANI, UONGOZI NA UTEGEMEZAJI.
Ziko semina mbalimbali na mafungo yaliyoandaliwa ki JNNK, Kanda au Kiparokia ni
Semina za za uongozi, Elimu ya Biblia, Semina za ndoa na Malezi
Semina za Kiroho na tegemeza kanisa zinafanyika Paarokiani na zimepangwa kulingana na ratiba .
Hali ya Imani kwa ujumla ni nzuri na imepangwa kuendelezwa kwa nguvu zote.
Kuhusu Utoaji, Hali ya utoaji kimsingi ni Nzuri nay a kutia moyo.
Hali kadhalika utoaji wa zaka ni mzuri kama amri ya kanisa. Ipo kamati maalumu inayoratibu zoezi la zaka.
Parokia inatoa michango kamili ya jimbo kama inavyo elekezwa.
FEDHA NA MIPANGO
Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa Jimbo.
Mapato na matumizi ya Parokia yanajulikana kwa waumini na inatolewa taarifa mara moja kwa mwaka.
Matoleo ya kila dominika yanatangazwa kwa waumini kila dominika ifuatayo, na pia inabandikwa katika mbao za matangazo.
Fedha zote hupelekwa benki.
ULINZI NA USALAMA.
Hali ya ulinzi na usalama parokiani inaridhisha.
Parokia inatumia walinzi wwa kampuni na hali ya usalama iko vizuri.
MAENDELEO YA KIUCHUMI.
Miradi inayoendeshwa na Parokia kwa sasa ni;
Ukumbi wa wazi, Shule ya ufundi na chekechea, Maduka ya parokia.
Ujenzi wa upanuzi nyumba ya Mapadre unaende vizuri kwa michango ya waumini.
MAMBO YA JUMLA
Hakuna migogoro yeyote ya kimipaka na parokia nyingine au jamii.
Katika kuwaendeleza waumini kiuchumi, Parokia imeandaa mazingira mazuri kwa wwaumini kutumia SACCOS ya hapa parokiani na kujiunga na vikundi vidogo vidogo vya VIKOBA hapa Parokiani..
Kipo kitabu cha Historia ya Parokia kilichoandaliwa.