DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA SALASALA
HISTORIA YA PAROKIA YA SALASALA
Historia ya kigango cha Mt Augustino Salasala inaanzia mwaka 1992 wakati ambapo jumapili moja ya kila mwezi Padre alifika nyumbani kwa mzee Antoni au kwa mama Suzane Thomasi kusoma misa.
Kadiri siku zilivyo songa waumini walianza kupungua mpaka ikafikia jumapili moja Padri alifika na kukuta waumini sita tu (6).Upungufu huu wa washiriki katika Misa na kumkatisha tamaana padre aliamua kusitisha safari zake za jumapili moja alizo jipangia kila mwezi. Hii ilikuwwa katika kipindi cha mwaka huo huo wa 1992.
Huduma za naman hiyo zilirudiwa tena mwaka 1994 mpaka 1996 ndipo zilipo fifia tena kwa mara ya pili.
Tarehe 8 october 1997 kwa mwaliko wa mlegio (Mama modesta Luoga) aliyehamia Salasala kutokea magomeni Walaegio na Wakarismatiki kutoka Tegeta walikuja kuhamasisha uanzishwaji wa jumuiya ya Mt Josephine bakhita. Siku hiyo ya kwanza walikusanyika pia Walegio 10 waliokuwa wakazi wa salasala, na mkusanyiko huo ulihusisha waumini 19.
Jumuiya hiyo iliendelea toka siku hiyo chini ya uongozi wa Yotham Kanga akiwa ndio Mwenyekiti, Katibu Modesta Luoga, katibu Msaidizi Ludoviki Milulu na mtunza hazina akiwa Agustino Lucas na katekista George Salenge.
Jumuiya hii ilianza tena kupata huduma ya Padre mara moja kwa mwezi, lakini siku ya jumatano na siku ya jumapili wanajumuiya haawa waliendelea kukutana kwa Suzana Thomas na kuendesha ibada ya Misa bila Padre wakiongozwa na George Ssalenge.
Tarehe 15 Aprili jumuiya iliazimisha sherehe ya ubatizo wa watu wakubwa 25 na watoto 23, pamoja na ndoa 6 na ibada hii iliongozwa na Padre Fr Dominico Atieri kutoka parokia ya Tegeta pale pale mbele ya nyumba ya suzana Thomas chini ya miti. Baada ya padre Dominico kuona wingi wa washiriki hao alitamka mara moja kuwa tokea siku hiyo mkusanyiko huo wa wakrosto wa salasala si jumuiya tena bali ni Kigango
Baada ya tangazo hilo waumini walikutana tena na kufikiria namna ya kupata eneo la kujenga maahali maalumu kwaajili y ibada ya kigango, lakini kutokana na kutokua na uwezo wa kujenga jengo kama hilo waumini walipeleka maombi kwa Paroko kupata msaada wa kununua kiwanja . Ombi hilo lilikubaliwa na uwwanja ukapatikana mwezi wa julai kwwa gharama ya shilingi milioni mbili na laki tano, eneo lenyewe ni hili ambapo kanisa limejengwa kwas asa.
Mara baada y kiwanja kupatikana waumini walikusanyika tar 1 agosti kusafisha eneo la kiwanja na kufikia 9 agost kanisa la makuti lilianza kujengwa, Ujenzi huo uliongozwa na Marehemu Michael Maumba eneo ambalo kwas asa linapangwa magari.
Wakati huo huo uongozi wa kigango ulikua chini ya Mama Luoga akisaidiwa na George Mkude, Alex Bonga akiwa katibu, Katibu msaidizi akiwa Mr Ludovick Mililu, Agustino Lucas akiwa kama mtunza hazina na katekisa mr Protas Mateo.
Mwezi septemba kwa msaada wa wafadhili uliopatikana kwa juhudi za shirika la damu takatifu ya Yesu,
Ujenzi wa jumba hili kubwa la kanisa ulianza na waumini walishiriki katika kusomba Mchanga , kokoto , kuchota maji na kumwaga jamvi. Kufikia mwezi wa sita mwaka 1999 kanisa lilikuwa limeshaezekwa na ibada ziliamia kanisa jipya ambapo hapakuwa na kiti hata kimoja na kipindi hicho vilikuwa vina okotwa vipande vya matofali na kukaliwa kama viti. Lakini tokea hapo polepole mabenchi yalijazwa na kanisa kupambwa kufikia hali hii tuliyo nayo sasa.
Katika maendeleo haya mwaka 2003 ulikuja ugeni ambaye ni Baba Muadhama kardinali Polycarp Pengo wakati akitembele vigango kadhaa wa kadha vya parokia ya Mtongani, siku hiyo risala ya parokia ombi lilikuwa limetolewa kwake kuangalia uwezekano wa kuruhusu vigango vya parokia ya mtongani viwe Parokia ombi ambalo alilikubali.
Miezi michache baadae mapadre wa shirika la Roho matakatifu walianza kulihudumia kanisa hili la kigango cha salasala .
Mwezi januari 2004 zilikuwepo tetesi z aza uwezekano wa salasala kuhamishiwa moja kwa moja shirika la Roho Mtakaatifu na hivyo uwezekano wa kuwa Parokia, leo hii sio tetesi tena kigango cha Salasala kimehamia shirika la Roho Mtakatifu na kubeba hali ya uparokia.
Hiyo ndio historia ya kigango cha Salasala ambacho tarehe 25/07/2004 kimehamishwa rasmi katika Shirika la Roho Mtakatifu.
Parokia ya Mt. Agustino ni moja katika zao la Parokia ya Tegeta (Damu takatifu ya Yesu) kigango kilianza october 1997. Kabla yake waumini walikuwa wanasali katika Kigango cha Mtongani ambacho pia kilikua chini ya Parokia ya Damu takatifu ya yesu Tegeta. Baadae Fr Dominico wa Shirika la Damu takatifu ya Yesu aliwauliza waumini wake kama wangependa kusali na kuwa chini ya Tegeta au Mtongani, na walipendekeza kusali Tegeta.
Jumuiya iliyokuwepo kwa wakati huo ilikuwa moja tu ya Mt Josephine Bakhita, na walisali chini ya mti Nyumbani kwa marehemu Suzane, na baadae walipata eneo jingine walilokuwa wakilitumia kusali na hatimaye kanisa lilijengwa kwa nguvu za waumini. Ndipo 2004 ikawa Parokia chini ya Mapadre wa Holy Ghost.
Ni mojawapo ya Parokia 101 za Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. Parokia hii pia ni miongoni mwa Parokia 17 zinazounda Dekania ya Mt. Gaspar de Bufalo. Parokia hii ilizinduliwa tarehe 15 Agosti, 2004 ikiwa na vigango viwili (Agustino na Dominico) na ilikuwa na jumuiya 10 zenye jumla ya waamini wapatao 1700.
Kutokana na ushirikiano mzuri kati ya Jimbo, Shirika la Roho Mtakatifu ambalo mapadre wake ndio wanaohudumu Parokia hii, Uongozi wa Halmashauri ya Walei na waamini, Parokia imekua ikikua kiimani mwaka hadi mwaka ambapo mwaka 2007 Parokia ilifanikisha Kigango cha Mt. Dominico na kuwa Parokia kamili. Kutokana na waamini kuendelea kukua kiimani, Parokia nayo imeendelea kukua na mpaka sasa inahudumia Vigango vitano (Agustino, Ambrosi, Cecilia na Mt. Theresia na Kanda J), jumuiya Ndogondogo 104 kutoka jumuiya 10 zilizokuwepo mwaka 2004. Jumuiya hizi zinaunda Kanda 20 zenye wastani wa jumuiya 5 kila moja. Kwa sasa Parokia inakadiriwa kuwa na waamini 8,900 kwa takwimu za mwezi Januari, 2018.
Parokia imeweza kupiga hatua kubwa katika maendeleo ya kiroho (kiimani) na kijamii. Hali hii inadhihirishwa kutokana na kuongezeka kwa takwimu za waamini wanaopata sakramenti mbalimbali kila mwaka kama ifuatavyo:-
MWAKA | UBATIZO | KOMUNIO | KIPAIMARA | NDOA |
2004 | 47 | 3 | 1 | 4 |
2005 | 338 | 82 | 100 | 51 |
2006 | 419 | 120 | 107 | 38 |
2007 | 235 | 149 | 137 | 39 |
2008 | 197 | 117 | 120 | 21 |
2009 | 138 | 127 | 100 | 12 |
2010 | 238 | 206 | 154 | 26 |
2011 | 97 | 166 | 36 | 13 |
2012 | 169 | 158 | 131 | 14 |
2013 | 126 | 123 | 125 | 33 |
2014 | 625 | 229 | 204 | 39 |
2015 | 323 | 117 | 43 | 30 |
2016 | 653 | 256 | 211 | 40 |
Jan- Juni, 2017 | 126 | - | - | 36 |
JUMLA | 3731 | 1853 | 1469 | 396 |
Ni matumaini yetu kuwa kwa baraka za Mwenyezi Mungu tutaendelea kushikamana ili idadi hii izidi kuongezeka kwa ajili ya ustawi wa kanisa la Mungu.
Ustawi wa kanisa mahalia umeendelea kukua. Parokia imeendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Kwa kifupi tumefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ununuzi wa maeneo ya ujenzi- Parokiani na Vigangoni ukiwemo ununuzi wa eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kigango cha Jumuiya zinazounda Kanda J kwa waamini ambao awali walikuwa wanasali Parokia ya Damu Takatifu- Tegeta; ujenzi wa kanisa lipo katika hatua ya finishing. Ununuzi wa shamba kiasi cha ekari 100 huko Bagamoyo Pwani kama kitega uchumi na pia ujenzi wa maduka kama mradi wa kanisa. Aidha, kwa sasa tuna mradi wa Ujenzi wa Kanisa letu jipya ambao unaendelea vizuri na tupo katika finishing.
CHANGAMOTO
Penye mafanikio hapakosi changamoto, Pamoja na mafanikio hayo tunakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo mwamko mdogo wa waamini katika kutekeleza masuala mbalimbali kuhusiana na maendeleo ya kiroho na pia maendeleo ya kijamii. Aidha, kuna ushiriki usio ridhisha katika misa za katikati ya wiki, ushiriki hafifu katika vyama vya kitume na pia kasi ndogo ya utoaji katika kuchangia michango mbalimbali ya kanisa ikiwemo sadaka, zaka na shukrani kama mavuno.
Ili kukabiliana na changamoto hizo, Parokia imeanza na utaratibu wa kuimarisha jumuiya ndogondogo kwa kugawa jumuiya kwa idadi ya familia kumi hadi kumi na tano ili kurahisisha huduma na kuhakikisha angalao kila mwanajumuiya katika kila kaya anafikiwa.
Aidha, kwa kushirikiana na uongozi wa Hierakia tumeanza kufikisha huduma za kiuchungaji katika ngazi ya Jumuiya kwa lengo la kuwaweka waamini karibu. Hatua hii imesaidia sana kubainisha changamoto zinazowakabili waamini mmoja mmoja na hivyo kutusaidia kubuni mbinu za kukabiliana nazo kwa lengo la kuinua ari na imani za waamini, zoezi hili linaendelea na tunaamini litaleta mafanikiao makubwa.
Hatua nyingine ni pamoja na kuwasaidia wakristu kuondokana na baadhi ya vikwazo zikiwemo sakramenti za ndoa kwa kurahisisha upatikanaji wa sakramenti hizo hususan kuwaondolea gharama zilizokuwepo awali.
Tumeanza kuona mafanikio kwani idadi ya waamini waliojiandikisha kwa kufunga ndoa katika kipindi cha miaka hii miwili ni kikubwa cha kuridhisha ukilinganisha na miaka ya nyuma kama takwimu zinavyoonesha.
Aidha, tuna mpango kabambe wa kuhamasisha waamini kupitia semina na makongamano mbalimbali kwa lengo la kuinjilisha na kuinua ari ya imani. Tutaendelea kuimarisha uongozi wa Kanda na kuhakikisha kuwa viongozi wanatembelea wanajumuia ili kufahamu changamoto zinazowakabili na kusaidiana na wanajumuia pamoja na Hierakia kuzitatua.
MWENYEKITI
HALMASHAURI WALEI – PAROKIA
PAROKIA YA MT. AGUSTINO-SALA SALA
25 JUNI, 2018
PAROKIA YA MTAKATIFU AGUSTINO SALASALA
Mtakatifu msimamizi wa parokia ni Mt Agustino
Jina la parokia halilingani na parokia zingine za jimbo la dar es salaam
MAHALI PAROKIA ILIPO KIJIOGRAFIA
Kijiografia Parokia ipo wilaya ya kinondoni kata ya Wazo eneo la Salasala, parokia ya salasala ni mojawapo ya parokia iliopo katika dekania yam t Gaspar De Bufalo
Idadi ya waumini katika parokia ya Mt Agustino ya salasala inakadiriwa kufikia 8,500, na idadi ya waumini imepatikana kwa sense iliyofanyika mwanzoni mwa kila mwaka, Na sense ya mwisho kufanyika ni 2017
Parokia ina vigango viwili ambavyo ni Mt Cecilia Kinzudi na kikango cha Ambrose Kilima hewa. Pia zipo juhudi za kuanzishwa kikango kingine kinachoundwa na Jumuiya za kandda A
Majina yanayotumika ni ya kanda i.e kanda A, B, C….J.
Katika parokia kuna kanda 13 ambazo zimegawanyika kulingana na mazingira ya kimakazi na barabara
Zipo jumuiya NNK 98. Jumuiya hizo zinatumia majina ya watakatifu lakini kanda zinatumia Alfabeti
Kila jumuiya ina wastani wa kaya 15-20
JNNK zinasali pamoja kila jumamosi saa 12:30 asuubuhi.
Kanda husali pamoja angalau mara moja kila mwisho wa mwezi kwa kutumia kitabu cha mwongozo wa sala.
Maudhurio kwa ujumla katika kanda na JNNK ni ya wastani na yanarekodiwa
Viongozi wa kamati tendaji ya parokia wanao utaratibu wa kutembelea vigango, kanda na jumuiya
Aidha katika, Katika misa za somo wa jumuiya na maisa za kanda kunakuwapo pia na utaratibu wa ushiriki
a. Jumuiya na kanda huadhimisha Misa za somo waJumuiya na kanda. Na kanda huadhimisha misa kila wanapo hitaji.
b. Uongozi katika JNNK /Kanda na vigango umekamilika na hakuna mapungufu yeyote
Uongozi halmashauri ya walei ya parokia hukutana kila baada ya miezi miwili. Kanda ni kila baada ya miezi mitatu
HUDUMA ZA KIROHO
Huduma zingine za kijamii/kiriho zinazotolewa katika JNNK/kanda na mtaa ni kama zifuatazo:
a. Huduma za kutembelea wagonjwa na kuwapa sacrament
b. Misa za somo wa jumuiya
c. Huduma ya ushauri na upatanisho has kwa wanandoa
d. Kutembelea wachumba sugu na kuwahamasisha kufunga ndoa
e. Ujaaji fomu kwaajili ya kuomba sakramenti. Mfano ubatizo, kumunio ya kwanza na kipaimara, ndoa pamoja na huduma ya mazishi
Zipo changamoto mbalimbali katika kuzihudumia JNNK/kanda na mitaa.
• Mahudhhurio hafifu .
• Mwamko mdogo hususani katika utoaji wa zaka
UONGOZI
Kamati tendaji ipo na imekamilika kikatiba.
Kamati tendaji hukutana mara mija kwwa mwezi. Mara nyingi Zaidi ni siku ya jumapili baada ya misa baba
paroko akiwa mshiriki mkubwa katika kikao
Vikao vya dharura vinafanyika pale ambapo vinahitajika.
Halmashauri ya walei ya paarokia inaundwa na wajumbe wafuatao:
• Wajumbe watano wa kamati tendaji ya parokia,
• Wajumbe watano wa kamati za tendaji za vigango (Ambrose na Cecilia)
• Wenyeviti 13 wanaounda kanda parokia.
• Wenyeviti wa vyama vya kitume ngazi ya parokia na paroko.
Agenda na taarifa za vikao zinapatikana kwa wakati na zinatunzwa kama kumbukumbu.
Pia kuna ofisi ya halmashauri ya walei parokia na inavitendea kazi ambavyo vinakidhi mahitaji
Njia za mawasiliano zilizopo ni pamoja na hizi zifuatazo:
- Barua pepe yaani E mail
- Whatsaap Group
- Simu na Baarua
- Njia za matangazo kanisani siku za dominika na siku zingine
Parokia ina kamati ndogo ndogo za kikatiba za halmashauri ya walei, wajumbe wake wapo na wamekamilika
Pia kuna kamati ndogo isiyo ya kikatiba yaani kamati ya Ujenzi ambayo hukutana kutimiza majukumu ya ujenzi Wa kanisa.
Kamati ndogo ndogo za kikatiba zinaripoti kwwa kamati tendaji ya parokia
Kamati hizi zinafanya kazi kwa umakinifu na kuwasiliana lakini hazina mwingiliano
Parokia ina kalenda ya mwaka ya matukio ya kiparokia ambayo imetengenezwa kwwa kupitia ushirikiano wa
kamati ndogondogo na vyama vya kitume
Njia zinazotumika kuwaambia waumini mipango ya parokia ni kwa kupitia
-halmashauri ya walei ya parokia
-Njia ya matangazo ya siku za dominika
-Viongozi kutembelea JNNK
VYAMA MASHIRIKA NA JUMUIYA ZA KITUME
-Katika parokia vipo VMJ kumi na mbili
-Wanchama waliopo katika vyama hivi ni wa wastani, na vingi vinajitahidi kukidhi mahitaji ya parokia
-Vyama na vikundi vya kitume vinafanya kazi kulingana na katiba ya halmashauri ya walei na vinatimiza wito wa kitume
Kwa ujumla VMJ havina ofisi parokiani lakini hupewa fursa ya kufanya mikutano yao katika kumbi za parokia, aidha katika jingo jipya la kanisa VMJ vitakuwwa na ofisi katika kutekeleza majukumu yao.
VMJ vinatoa taarifa na ripoti (pamoja na ya fedha) mara kwa mara katika uongozi wa parokia.
Ushirikiano na ushiriki wa VMJ za parokia katika shughuli dekani na jimbo uko vizuri.
Semina mbalimbali katika uendelevu wa Imani ,uongozi na utegemezi
Semina mbalimbali huandaliwa katika ngazi ya parokia i.e
A. -Semina za uongozi katika kanisa
-Semina za utoaji.
B. Kwa vyama vya kitume viongozi wa vyama hivyo wanakuwa na ratiba maalumu
Uongozi wa parokia kamati tendaji ya parokia na halmashauri ya walei ya parokia wamepatiwwa semina ya uongozi katika kanisa . na pia swala semina ni swala endelevu
Hali ya mwamko katika parokia ni mzuri. Na katika kipindi cha miaka miwili zimetolewa sakramenti nyingi ukilinganisha na miaka ya nyuma, aidha hali ya kujitoa imeongezeka sana nah ii imeashiria hali ya kiimani kukua
Utoaji wa zaka kama amri ya kanisa ni mzuri
Parokia pia inatoa michango ya jimbo kama inavyo paswa kwa wakati.
Fedha na mipango
Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa jimbo
Mapato na matumizi ya parokia yanajulikana kwa waumini, na taarifa hutolewa mara nne kwa mwaka
Matoleo ya kila dominika hutangazwa kila baaa ya dominika inayofuata
Fedha zote zinapelekwa banki kwa wakati.
Ulinzi na usalama
Hali ya ulinzi na usalama parokiani ni nzuri
Walilnzi wanaotumika ni kutoka kampuni binafsi.
Maendeleo ya kiuchumi
Parokia ina mradi mmoja wa duka mbele ya kanisa
Parokia pia ipo kwenye mradi wa ujenzi wwa kanisa kubwa la kisasa, waumini wengi wamehamasishwa na wamehamasika vilivyo kwa ujenzi huo, hali kadhalika parokia ipo katika hatua za awali kujenga jingo la muda kanda Alitakalo tumika kama outstation, kazi hii inatarajiwa pia kufanyika kanda Jbaaada ya parokia kununua eneo litakalotumika kujenga kigango siku za baadae