PAROKIA YA MTONGANI


PAROKIA YA MTAKATIFU NICHOLAUS (KUNDUCHI) MTONGANI

Tumsifu Yesu Kristu

YAH: TAARIFA FUPI YA PAROKIA YA MTAKATIFU NICHOLAUS KUNDUCHI MTONGANI.2018

Parokia yetu ya Mt Nicholaus Kunduchi Mtongani ilizaliwa mnamo tarehe 5/12/1999 ikiwa na vigango 5, yaani Kigango cha Bahari Beach, Salasala, Mbezi Beach St Gaspari, Bikira Maria Mama wa Huruma, na Dominico. Na badaye tulianzisha kigango cha Kilongawima ( Mt Kizito). Vigango vyote hivi kwa sasa vemeshakuwa parokia kamili na hivyo hatuna kigango kwa sasa.

Parokia yetu ya Mtakatifu Nicholaus Kunduchi Mtongani

  • Ina waumini  wapatao 2200, kutoka familia zipatazo 440
  • Idadi ya jumuiya ndogo ndogo ni 17 ambazo zimegawanyika katika Kanda 5
  • Vyama vya Kitume Hai ngazi ya Parokia vipo 9 vikiwamo; WAWATA; UWAKA; VIWAWA; SHIKWAKA, UTOTO Mtakatifu; Aloisi Gozaga, Karismatiki Katoliki; Neo Katekuminato; Legio Maria na Moyo Mtakatifu wa Yesu

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kufikia August 2018, parokia yetu ilipata mafanikio yafuatayo:    

  • Ubatizo:
    Idadi ya waliopata sakramenti ya Ubatizo -  93 kati yao watoto ni 82 na watu wazima ni 11
  • Ndoa:
    Idadi ya waliopata sakramenti ya Ndoa ? 40. Katika ndoa hizi jumla ya ndoa 27 zilifungwa kwa pamoja siku ya sikukuu ya somo wa Parokia Mt. Nicholaus
  • Komunyo ya Kwanza:
    Idadi ya waliopata komunyo ya Kwanza - 76
  • Kipaimara:
    Idadi ya watakaopata Kipaimara  - 48
  • Miaka 150 ya Uinjilishaji:
    Katika Kuadhimisha mwaka wa Jubilee ya miaka 150 ya Uinjishaji Tanzania, parokia yetu imefanya maadhimisho haya kwa kufanya Ibada ya kusimika Msalaba, Kusimika Neno la Mungu, kuwasha Mshumaa katika kila familia . Mpaka sasa tumekamilisha kanda zote 5 yaani Jumuiya 17, ambapo tumefanikiwa kutembelea na kusali pamoja katika familia zote.
 

Mafanikio Mengineyo

Tunamshukuru Mungu kwa kutujalia Neema za kuweza kuwa na:

  1. Kipaimara na Komunyo kila mwaka
  2. Idadi ya Ndoa zinazofungwa kuongezeka mwaka hadi mwaka
  3. JNNN na Vyama vya Kitume kuendelea kuwa  hai
  4. Kupatikana kwa kiwanja cha Bahai kwa ajili ya miradi ya kiuchumi.
  5. Ujenzi wa Kanisa jipya.

  Changamoto

  • Waamini wapangaji ? Hivyo waaamini kuwa wa vipindi vifupi vifupi katika Parokia
  • Kuwepo kwa waumini wanaoishi bila kuwa na sakramenti ya ndoa
  • Parokia kutokuwa na kigango
  • Parokia kuzungukwa na madhehebu tofauti tofauti
  • Changamoto za Kimapato kwa Waamini wengi ? Hii inapunguza kasi ya miradi ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa Kanisa Unaondelea
  • Parokia kutokuwa na shirika la kulea wasichana baada ya Utoto Mtakatifu

  Matarajio

  • Kuanzishwa kwa shirika la Bikira Maria kwa ajili ya kuendelea kulea watoto wa kike baada ya Utoto Mtakatifu. Shirika hili linategemewa kuzinduliwa rasmi katika kilele cha maadhimisho a sherehe za Mt Nicholaus somo wa Parokia wetu mwezi wa Desemba
  • Kuendelea kufunga ndoa za jumla ili kupunguza tatito la uchumba sugu. 

    Dr, Richard T. Njau.
    Mwenyekiti,
    Halmashauri ya Walei,
    Kunduchi Mtongani.       
    Mtakatifu msimamizi wa parokia ni Mt Nicholaus wa Myra/Bari



Jina hili haliingiliani na Parokia zingine za jimbo kuu la dar es salaam

Parokia hii ilizaliwa 1999

Mahali parokia ilipo kijiografia

Parokia ya Mt Nicholaus ipo katika wilaya ya kinondoni , jimbo kuu la dar es salaam

Kwa upande wa mashariki imepakana na Bahari ya hindi

Upande wa magharibi imepakana na barabaara iendayo Bagamoyo/Parokia ya mt Augustino salasala

Upande wa kaskazini imepakana na parokia ya damu azizi ya yesu Tegeta

Kusini imepakana na parokia teule ya mt kizito Kilonga wima.

Parokia ya mt Nicholaus ipo katika dekania ya Mt Gaspar the Bufalo.

Idadi ya waumini ni kati ya 4000 ambayo imepatikana kutokana na sense iliyofanyika 2012

Ilifanyika kwa njia ya kuandaa na kutoa fomu maalumu za sense kwa kila familia katika jumuiya.

Kwa sasa parokia haina vigango, baada ya kigango kilichokuwepo kufanywa kuwa parokia teule  tarehe 06 january 2017

Parokia ina kanda ambazo ziliundwa  mwaka 2016,

Kwa ujumla zipo kanda 5ambazo zimeundwa kwa kuunganisha jumuiya jirani kijiografia .

Idadi ya jumuiya katika kanda zimetofautiana, kanda nyingine zimeundwa  na jumuiya tatu tu isipo kuwa kanda moja ambayo imeundwa na jumuiya tano (5)

Uongozi wake umepatikana kwa kwa viongozi kuchaguliwa kwa kura na kwa mujibu wa katiba na umekamilika

Jumuiya zinatumia majina ya watakatifu, isipokuwa kanda bado hazijachagua watakatifu wasimamizi

Kuna jumla ya jumuiya NNK 17 katika parokia .na kila jumuiya inawastani wa kaya 15-30

JNNK zinasali pamoja siku ya jumamosi saa 12:30 asubuhi. Na utaratibu wa kanda umeanza 2015. Utaratibu wa kusali pamoja bado haujawekwa.

Utaratibu wa kusali ni kadiri ya mwongozo wa jumuiya au sala za jumuiya.

Maudhurio kwa ujumla katika mikutano ya jumuiya ni ya wastani na yanaarekodiwa.Wakina baba na vijana ndio wanaoonyesha ulegevu katika ushiriki ukilinganisha na wakina mama.

Jumuiya hufanyika kwa kufuata utaratubu wa nyumba kwa nyumba na hivyo kubaini walegevu.

Mara nyingi familia  na JNNK hutembelewa na viongozi /mapadre na katika matukio mbali mbali ikiwa ni pamoja na maandalizi ya misa za familia/jumuiya na ibada za kuhamasisha mavuno

Jumuiya huwa zina utaratibu wa kuadhimisha misa wa somo wake kila mwaka,

Uongozi katika JNNK/kanda umekamilika na hauna mapungufu yeyote

Uongozi Halmaashauri wa JNNK hukutana kila baada ya miezi mitatu

Huduma za kiroho zitolewazo ni kamazifuatazo:
    Sakrament kwa wagonjwa
    Misaada kwa wahitaji
    Ushauri kwa walegevu katika Imani
    Ushauri na upatanisho hasa kwa wanandoa

Ujazaji fomu kwaajili ya kuomba huduma za sakramenti kama ekarist takatifu, ubtizo,kipaimara ndoa n.k

Changamoto katika kuzihudumia jumuiya NNK/Kanda /mitaa.
    Maudhurio hafifu kwenye mikutano na ibada mbalimbali.
    Baadhi ya waumini kubabaika na madhehebu ya kilokole
    Ugumu katika utoaji katika kulitegemeza kanisa.
    Kujali Zaidi mafundisho ya dunia kuliko mafundisho ya kiroho

Uongozi
Kamati tendaji ipo na imekamilika ingawa wajumbe wawili wanatoka katika parokia teule ya mt kizito mpaka taarifa hii inaandikwa.
Hivi karibuni uongozi utachaguliwa.
Kamati tendaji hukutana mara moja kwa mwezi na haswa siku za ijumaa ya mwisho wa mwezi, baba paroko anashiriki katika kikiao hicho na au kutoa ruhusa ya kukutana.
Vikao vya dharura hufanyika kila vinapohitajika.

Kamati ya halmashauri ya walei parokia inaundwa na watu wafuatao:
a.    Kamati tendaji ya parokia
b.    Wenyeviti na makatibu wa kila Kanda (kwa kanda zote tano)
c.    Wenyeviti wa vyama vya kitume ngazi ya parokia ambao ni UWAKA, WAWATA, SHIKWAKA, MOYO MT WA YESU,VIWAWA, KARISMATIKI KATOLIKI

Mikutano ya halmashauri ya Walei ya  Parokia hukutana mara nnekwaw mwaka siku za jumapili baada ya misa ya pili.

Agenda na taarifa za vikao hupatikana kwa wakati na vinatunzwa
Kwa ujumala ofisi ya halmashauri ya walei Parokia inayo ofisi kwaajili ya kuendeshea shughuli zake na ambayo pia inatumiwa na makatekista, ofisi hiyo in; computer  na Printers mbili, meza pamoja na kabati za kutunzia nyaraka

Njia za mawasiliano kwa wajumbe wa kamati tendaji pamoja na halmashauri ya walei ni pamoja na
     Simu
     Barua pepe yaani E mail
     Ujumbe mfupi wa maneno SMS
     Makundi ya whatsaap
     Na pia njia ya matangazo kanisani.

Barua pepe au E mail ya parokia ni mtnikolous@gmail .com

Kamati
Zipo kamati ndogo ndogo za kikatiba na wajumbe wake wamechaguliwa kwa mujibu wwa katiba ya halmashauri ya walei, na pia kamati hizo zimekamilika

Parokia ina kamati zisizo za kikatiba zilizoundwa kusimamaia malengo mbalimbali ya kiparokia, kamati hizo ni kama zifuatazo:

  • Kamati ya ujenzi. Kazi yake kubwa ni kuratibu na kusimamia  shughuli zote katika parokia ,ukarabati wa majengo na miundo mbinu katika parokia. Mfano ni shughuli za ujenzi wa kanisa zinazoendelea.
  • Kamati ya ardhi ( Kamati ya shamba la parokia ) Kusimamia uendelezaji wa shamba la parokia  lililokoko kisarawe
  • Kamati ya ulinzi na usalama. Kazi yak e kubwa ni kusimamia shughuli zinazohusu ulinzi na usalama katika eneo la parokia au kanisa kwa ujumla

Kamati zote za kikatiba na zisizo za kikatiba zinaripoti kwenye kamati tendaji ya parokia ambayo huandaa nyaraka kwaajili ya taarifa kwenye hallmashauri ya parokia
Pia kamati hizi zinafanya kazi pasipo muingiliano na kamati zingine.

Mpaka sasa parokia haijawa na kalenda yake ya matukio ya kiparokia , matukio mengi  hufuata kalenda ya kiliturjia na mwongozo kutoka jimboni.

Njia zinazotumika kuwaarifu wwaumini wote juu ya mipando ya parokia ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za kanisa ni kama zifuatazo:
a.    Mikautano ya halmashauri ya walei parokia , viongozi kutoka katika jumuiya ndogo ndogo huelekezwa na kupewa taarifa mbalimbali juuu ya majukuimu yanayohitajika kutekelezwa ili waweze kuwafikishia  wanajumuiya.
b.    Njia ya matangaazo ya siku ya dominika
c.    Viongozi kuongea na waumini kanisani pamoja na
d.    Viongozi kutembelea jumuiya na kuwaeleza jambo husika.

Vyama mashirika na jumuiya za kitume

Katika parokia VMJ vipo, navyo ni :UWAKA, WAWAT, UTOTO MT,MOYO MT WA YESU,UMTUME, KARISMATIKI KATOLIKI, ALOIS GONZAGA NA REGIO MARIA

Wanachama waliopo katika baadhi ya vyama ni wakutosha na hivyo vyama vinajitahidi kukidhi mahitaji ya parokia.

Vyama na vikundi vya kitume vinafanya kazi kulingana na katiba ya halmashauri ya walei

Uhai wa VMJ
Uhai wa VMJ upo, vy ama vyote hushiriki matukio ya kiparokia , Dekania na jimbo

Vyama hivi haavina ofisi parokiani ijapo kwamba vimeruhusiwa kuendesha shughuli zake parokiani kama vile kufanya mikutano yao kaatika kumbi mblimbali za parokia

Baadhhi ya vyama vinawalezi parokiani kama vila utoto mt, VIWAWA, na SHIKWAKA, vikundi vivi pia vina bajeti ya kila mwaka ili viweze kujiendesha.

VMJ vinatoa taarifa na ripoti ( pamoja nay a fedha) mara kwwa mara karika uongozi wa paarokia.

Ushirikiano na ushiriki wa VMJ za parokia katika shughuli za dekania na jimbo uko vizuri

Semina mbalimbali katika uendelezi wa Imani, uongozi na utegemezaji

Semina mbalimbali huandaliwa katika ngazi ya parokia wakishirikiana VMJ

Ratiba ya semina imeandaliwa.

kamati tendaji ya halmashauriya walei ya parokia wameshapatiwa semina jimboni, nab ado semina zinaonekana kuendelea kuhitajika hasa zinazohusu uongozi katika kanisa , kwa viongozi JNNK na halmashauri kwa ujumla kwani viongozi wengine ni kwa mara ya kwanza ndio wameanza kuongoza.

Inapobidi parokia huleta wawezeshaji kutoka sehemu mbalimbali au wahubiri makhususi wakati wa misa kwa masuala kama ya kulitegemeza kanisa , mafungo, mikutano ,warsha  n.k

Hali ya Imani katika parokia kwa ujumla ni nzuri na inaridhisha, hata hivyo bado zinahitajika semina mbalimbali za kuimarisha waumini kiroho.
Swala la utoaji

Swala la utoaji kwa ujumla sio baya, waumini wanaonekana kujitoa lakini pia wakihamasishwa katika swala la utoaji wanatoa Zaidi.

Utoaji zaka kama amri ya kanisa bado uko chini
Parokia inatoa michango kamili ya jimbo kama inavyo amriwa.

Fedha na mipango
Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa jimbo
Taarifa juu ya mapato na matumizi hutolewa mara mbili kwa mwaka na hujulikana kwa waumini
Matoleo ya kila dominika hutangazwa kwa waumini kila inayofuata na fedha zote hupelekwa benki kwa wakati.

Hali ya ulinzi na usalama kwa ujumla ni nzuri, na walinzi wanaotumika ni kutoka kampuni binafsi

Maendeleo ya kiuchumi
Hakuna mradi wowote kwa sasa.
Mkakati uliopo kwa sasa ni ujenzi wa kanisa la kisasa la parokia na pia ujenzi wa kibanda cha walinzi

Mambo ya jumla
Parokia imeunda chama cha kuweka na kukopa SACCOS, KUMPAHO ambacho kinawasaidia waumini kujiendeleza kiuchumi na kiafya.
Idadi ya mapadre inatosheleza lakini kwa upande wa watawa wanahitajika Zaidi kwaajili ya kufundisha mashuleni
Parokia ina vijana idadi ya wanafunzi wanne walioko seminary za jimbo .




JE UNATAFUTA

PAROKIA?

Upate majibu yako haraka zaidi
Ramani ya Parokia
Hakuna ramani kwa sasa...
Kuhusu Kanisa Katoliki

Ofisi ya Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam inapatikana makao makuu ya Jimbo,
Kanisa la St. Joseph, barabara ya Sokoine na Manseld street.

P.O Box 167, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 762 024 199
Email: mawasiliano@waleijimbodaresalaam.org
            darwaleijimbo@yahoo.com
Web: www.waleijimbodaresalaam.org

Kwa Habari kemkem za Kanisa jiunge nasi

Andika email yako hapo juu, na upokee taarifa za H/walei

Copyright © 2025. All Rights reserved by H/Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam