DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA MADALE
MAMBO YA JUMLA YA PAROKIA
Jina la parokia ya Madale
-Msimamizi wa parokia NI BIKIRA MARIA MALKIA WA AMANI.
- Jina halifanani na parokia nyingine za jimbo la Dar es salaam
Mahali parokia ilipo ni madale
Parokia ilitangazwa rasmi 20 january 2013
Kijiografia Parokia inapakana na parokia ya maria dematias mivumoni.
Parokia ipo katika dekania ya mt gaspary Dar es salaam.
Idadi ya waumini katika parokia Mpaka kufikia 2013 ilikua ni kati ya waumini 1734 na imepatikana kwa njia ya sense iliyofanyika 2013 kwa waumini kujaza fomu maalumu.kwa sasa kuna waumini Zaidi ya 3760 kutokana na sense ya mpaka kuishia 2017
Jumuiya zilikuwa (25) lakini kutokana na watu wengi kuhamia jumuiya hizo zimefikia 47.
Parokia ina vigango viwili na kanda zipo tano
Kila jumuiya ina kaya kati ya 20-25
Jumuiya zinasali mara moja kila siku ya jumamosi kuanzia saa 12:30 kwa kufuata mwongozo wa jumuiya ndogo ndogo toka Jimboni
Kanda hua wanasali mara moja kila baada ya miezi miwili
Maudhuri kwa jumla katika JNNK ni ya wastani, na maudhurio huwekwa katika kumbukumbu.
Upo pia utaratibuwa kuzitembelea jumuiya NNK , Kanda na pia misa zinasomwa.
Kanada JNNK hua zinaadhimisha Misa takatifu za somo wa jumuiya na kanda kila baada ya mwaka mmoja.
Uongozi wa jumuiya umekamilika na pale ambapo inapotokea kuna mapungufu yanajazwa mara moja kwa kuitisha uchaguzi mdogo.
Halmashauri ya walei ya parokia /kanda hukutana mara chache
Huduma za kiroho na jamii hufanywa na jumuiya , hii ni pamoja na huduma za masakramenti kwa wanajumuiya mfano;Ndoa, mpako wa wagonjwwa, kipaimara, na pia matendo ya huruma kwa kutembelea wagonjwa na wenye shida mbali mbali.
Changa moto kubwa ni maudhurio ya waumini katika sala na matukio au matendo ya huruma yanapofanyika , lakini changamoto nyingine kubwa ni maudhurio duni ya wanaume na vijana
UONGOZI
Kamati tendaji ipo na imekamilika kikatiba
Kamati tendaji ya parokia hukutana mara moja kila mwezi siku za jumamosi na kikao kinachukua muda wa saa moja kujadili .Baba paroko ni mshiriki katika kikao hicho.
Halmashauri ya walei ya parokia inaundwa na viongozi watano wa kila jumuiya pamoja na wenyeviti wa vyama vya kitume na inakutana mara moja kila baada ya miezi miwili.
Agenda na taarifa za vikao zinapatikana kwa wakati na zinatunwa.
Parikia haijawa na ofisi za halmashauri ya walei ya parokia , lakini mipango ipo ya kuwa na ofisi na vitendea kazi,ofisi inaandaliwa na itakamilika hivi karibuni
Njia za mawasiliano kwa wajumbe wa kamati rendaji pamoja na halmashauri ya walei ni :
Kwa njia ya barua pepe(yaani E mail) simu,Whats aap, lakini zaidi ya hapo ni kwa matangazo kanisani.
Anuani ya barua pepe yaani E mail ya parokia ni changanyikeniutatumtakatifu@gmail.com
Zipo kamati ndogo ndogo za kikatiba na zimekamilika,
kamati hizo hua zinakutana mara mara.
Zipo kamati zingine Ambazo sio za kikatiba na zinaripoti kwa kamati tendaji ya parokia, kamati hizi ni kama zifuatazo:
a) Kamati ya ujenzi
b) Kamati ya ulinzi na usalama
Ipo kalenda ya matukio ya mwaka ya kiparokia amabayo imetengenezwa kwa ushirikishwaji waumini
Waamini wanaarifiwa mipango ya parokia kwa kupitia maatangazo kanisani , pia kupitia JNNK kupita halmashauri ya walei ya parokia
VYAMA MASHIRIKA NA JUMUIYA ZA KITUME (VMJ)
Vipo vyama vya kitume 12 kama ifuatavyo
1. WAWATA,
2. UWAKA
3. VIWAWA,
4. Utoto mtakatifu
5. Shikwaka
6. MOYO MT WA YESU
7. MINISTANTS
8. KARISMATIKI KATOLIKI
9. REGIO MARIA
Vyama hivi havina watumishi wa kutosha na havikidhi mahitaji ya parokia
Vyama na vikundi vya kitume vinafanya kazi kulingana na katiba ya halmashauri ya walei ya jimbo.na vyama vyote hivi viko hai
Vyama hivi havina ofisi parokiani, lakini vinalelewa na vipo chini ya uongozi wa parokia
VMJ vinatoa taarifa na repoti pamoja na ya fedha mara kwa mara kwa uongozi wa parokia
Na pia vinajitegemea na viko chini ya uangalizi wa parokia
Vyama vina ushirikiano mzuri katika dekania na katika ngazi ya jimbo
VMJ havijafanya mambo maaalumu ambayo yanwweza kuigwa na parokia nyingine
SEMINA MBALIMBALI KATIKA UENDELEVU WA IMANI, UONGOZI NA UTEGEMEZAJI
Kuna semina za kijumiuiya ambazo zimeshafanyika ,lakini kwa sasa mipango inaandaliwa ili semina nyingine ziweze kufanyika
*Kamati ya walei parokia ilishapatiwa semina ya uongozi na mgurugenzi wa utume wa walei jimbo , lakini bado semina zingine zinahitajika kwaajili ya jumuiya.
Semina za kiroho hazijaanza kufanyika bado
Hali ya Imani kwa ujumla inaridhisha, na inatakiwa kuendelezwa kwa nguvu
Kimsingi hali ya utoaji parokiani pia si nzuri bali inaridhisha.
Hali kadhalika utoaji wa zaka kama amri ya kanisa haziridhishi.
Parikia inatoa michango ya jimbo kamili kama inavyo paswa
FEDHA NA MIPANGO
Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa jimbo
Mapato na matumizi ya parokia yanajulikana kwa waumini na yanatolewa taarifa mara nne kwa mwaka
Matoleo ya kila dominika yanatangazwa kwa waumini kila dominika inayofuata
Fedha zote zinazokusanywa hupelekwa benki kwa wakati
ULINZI NA USALAMA
Hali ya ulinzi na usalama parokiani ni ya kuridhisha, na ulinzi unafanywa na kampuni binafsi
MAENDELEO YA KIUCHUMI
Parokia haijawa na miradi yake kwa sasa
Kwa sasa kuna mipango ya uendelezaji wa ujenzi wa NYUMBA YA MAPADRE kuweka miundo mbinu na kujenga fensi
Pia kwwa upande wa kanisa zipo shughuli za kuweka tiles, kupaka ranga , kuweka milango n.k
Lakini pia ipo mipango ya baadae ya
a) kujenga ofisi za parokia
b) Kufungua mradi wa duka
c) Kutafuta shirika litakalo anzisha shule ya awali katika eneo la parokia kama mradi wa parokia
d) Kununua thamani za ofisi pamoja na nyumba ya mapadre
MAMBO YA JUMLA
*Parokiia haina mgogoro wowote wa kimipaka
Kwa sasa parokia haina mipango yeyote ya kuwaendeleza waumini wake kiuchumi isipokuwa kwa kadiri parokia inavyokuwa itafanya juu chini mipango hiyo iwepo
Idadi ya mapadre na watawa hawatoshelezi
Parokia haina wanasemiari kwa ujumla
Ipo pia historia ya parokia pindi itakapohitajika