PAROKIA YA SEGEREA


Msimamizi wake ni roho mtakatifu, hiyo inajulikana kwa jina la parokia ya Roho mtakatifu

KIJIOGRAFIA
Parokia ipo katika kata ya segerea , kwa upande wa kaskazini inapakana na parokia ya makoka, na kwa upande wa kaskazini mashariki inapakana na kimanga, lakini kwa upande wa mashariki inapakana na parokia ya tabata,  na upande wa kusini ni parokia ya kipawa, magharibi ni parokia ya kinyerezi

IDADI YA WAUMINI
Parokia inaidadi ya waumini wapatao 7,906 ambayo ilitokana na sense iliyo fanyika 2014 Ambapo kina baba walikuwa 1251,  na wakinamama walikuwa 1364 ,Vijana na watoto 4069, wasaidizi wa familia walio wakatoliki 1222,wasidizi wa familia waprotestant 369, waislamu 203, na wa[pagani 3
Parokia haina vigango
Parokia ya Roho mtakatifu inatumia majina ya kanda
Parokia inakanda 16 na wastani wa jumuiya ndogo ndogo 5 kwa kanda.
Jumuiya na kanda zimegawanyika kulingana na jiografia mahali na jinsi ambavyo wanaweza kusaidiana, na mipaka ni barabara  na au mikondondo ya maji
Uongozi wake umepatikana kwa njia ya uchaguzi kwa kadiri ya katiba ya halmashauri ya walei taifa.
Uongozi umekamilika upande wa kamati tendaji  za JNNK na kanda isipokuwaa VJM ndipo kuna baadhi ya nafasi bado ziko wazi
Jumuiya zote zinatumia majina ya watakatifu, Majina yote ya kanda ni ya mapapa watakatifu
Parokia ina jumla ya JNNK 88 , na kila jumuiya ina wastani wa kaya 15-20
JNNK zote zinatumia majina ya watakatifu
Kanda husali mara moja kwa mwezi, kwa upande wa JNNK sala za jumuiya hufanyika kila siku za jumamosi
Mwongozo unaotumika ni ule wa utaratibu wa sala za jumuiya.
Mauhudhurio kwenye jumuiya ni ya wastani na kumbukumbu zinahifadhiwa kwenye daftari

USHIRIKI
Ushiriki upande wa kina baba na vijana ni wa kusuasua
Jumuiya na kanda huadhimisha misa kuwakumbuka watakatifu na somo wamajina ya kanda na jumuiya zao.
Uongozi umekamilika kwa kanda zote yaani kuanzia kamati tendaji za kanda na VJM
Kwa upande wa JNNK ni upande wa kamati tendaji tu uongozi ndio umekamilika
Jitihada za kukabiliana na mapungufu hayo ni  viongozi kutumikia  Zaidi ya nafasi moja ya utume.
Halmashauri za JNNK/kanda hukutana mara moja kwa mwezi  haswa pale panapokuwa na uhitaji, viongozi  husika huomba uwakilishi wa kiongozi wa kamati ya utendaji ya halmashauri ya walei  parokia.

HUDUMA ZA KIROHO
Matendo ya huruma kama vile kuwatembelea wagonjwa na kuwapa misaada mbalimbali ya vyakula ,mavazi na malazi
Pia zinapohitajika huduma za kiuinjilishaji au semina maalumu za kiroho hutolewa kwenye kanda na jumuiya NNK kwa kushirikiana na  kamati ya mafundisho ya dini parokiani.
Pia kunachangamoto moja ya waumini kutokuelewa umuhimu wa kushiriki vikao na sala za JNNK
Baadhi ya waumini kutokua na makazi ya kudumu kwenye JNNK

SEHEMU YA UONGOZI
Kamati tendaji ya parokia ipo na imekamilioka
Kamati tendaji hukutana kila mwezi ,muda wa saa moja jioni siku ya ijumaa au siku ambayo itaonekana haiingiliani na majukumu mengine
Halmashauri ya walei parokia inaundwa na kamati tendaji za kanda  zenye wajumbe watano(5) na kufanya jumla ya wajumbe (80), yaani wenyeviti, na VJM ngazi ya parokia
Jumuiya vyama vya kitume  na mashirika  ni kama ifuatavyo;
UWAKA, WAWATA, VIWAWA, NEOKATEKUMINATO, charismatic, Wasekulari, Legio maria, Utoto mtakatifu, ministrant
Halmashauri ya walei parokia hukutana mara nne kwa mwaka siku ya jumapili kufuatana na kalenda
Agenda taarifa zote hupatikana kwa wakati , na ripoti zote hutunzwa kwenye mafaili kwa katibu na kwa njia za kielectonia
Vitendea kazi vipo kama vile computer , desk, printer, na vifaa vingine vya ofisi.


NJIA ZA MAWASILIANO ZINAZOTUMIKA
>    Matangazo ya siku ya dominika ,
>    Whatsaap groups
>    Ujumbe mfupi kwenye group
>    Mawasiliano ya simu
>    Kupitia kwenye tovuti ya Parokia ambayo ni www.segereacatholic.org
>    Barua pepe (E mail)

Kamati ndogondogo za kikatiba
I.    Kamti ya malezi ya kifamilia
II.    Kamati ya mipango , uchumi na fedha
III.    Kamati ya liturjia na ibada
IV.    Kamati ya elimu ya dini ,mafundisho ya kanisa na theolojia.
V.    Kamti ya haki na Amani

Kamati zote za kikatiba wenyeviti wake ni kwa kadiri ya katiba ya halmashauri ya walei taifa. Wajumbe wengine huteuliwa na kamati tendaji ya paarokia kwa kushirikiana na baba paroko
Kamati zisizo za kikatiba zilizoko katika parokia ni kama zifuatazo
1)    Kamati ya afya
2)    Kamati ya ulinzi na usalama. Inaratibu shughuli zote za ulinzi wa wamini , kanisa , mapadre, watawa na wote waliopo ndani ya kanisa.
3)    Kamati ya ardhi. Inaratibu maswala yote yanayohusu ardhi na mipaka yake
4)    Kamati ya shule. Kuratibu shughuli zote za shule, kufuatilia vibali vya shule na
5)    Kutoa ushauri juu ya uendashaji wa parokia.
6)    Kamati ya ujenzi . kusimamia shughuli zote za ujenzi ukarabati wa majengo na  miradi ya ujenzi parokiani.

Kamati zote huripoti kwa kamati tendaji ya parokia, na hakuna mwingiliano wa shughuli za kiutendaji sababu kila kamati ina mwongozo katika kusimamia utekelezaji wa majukumu yake
Ipo kalenda ya parokia ambayo inaonyesha matukio mbalimbali ya parokia vyama vya kitume.
Kamati tendaji ya parokia huitisha kikao cha halmashauri ya walei ya parokia  yenye wajumbe 92, kujadili kwa uwazi mapendekezo ya kamati tendaji bajeti na mipango ya mwaka baada ya majadiliano na mapendekezo ya taarifa mbalimbali kupelekwa parokiani kwa wanajumuiya.
Mukhtasari wa makubaliano ya kikao cha halmashauri ya walei parokia huelezwa kwa waumini wakati wa matangazo kwenye dominika  inayofuata. Taarifa hiyo hutolewa na mwenyekiti wa parokia

SEHEMU C: VYAMA, MASHIRIKA NA JUMUIYA ZA KITUME (VMJ)
Katika parokia , vyama , mashirika na jumuiya `za kitume vipo kama ifuatavyo;
UWAKA, WAWATA, VIWAWA, NEOKATEKUMINATO, KARISMATIKI, WASEKULARI, VIFRA, Utoto mtakatifu, MINISTRANT, LEGIO MARIA, USHUJAA WA EMAKULATA, MOYO MTAKATIFU WA YESU NA SHIKWAKA
Vyama hivi vina wanachama wa kutosha na vinakidhi mahitaji ya parokia
Vyama vyote vimekua vikifanya kazi kwa kadiri ya katiba ya halmashauri ya walei.
Uhai wake ni mzuri lakini mwamko wa waamini kujiunga na VMJ ni mdogo
Kwa sasa VMJ haina ofisi isipokuwa VIWAWA
VMJ vyote vipo chini ya usimamizi wa kamati tendaji ya Parokia
Taarifa zote za fedha na mambo mengineyo hutolewa ka kamati tendaji ya parokia na kwa baba paroko
Ushiriki wa VMJ kwenye majukumu ya dekania na jimbo ni mazuri

Yako mambo ambayo parokia zingine zina paswa kuiga nazo ni;
>    Kuandaa wiki za neema angalau mara mbili kwa mwaka haswa wakati wa kwaresma na wakati wa majilio
>    Kuratibu na kuendesha semina mbalimbali za kiroho
>    Kuendesha mafungo ya aina mbalimbali kwa waumini kwa nyakati mbalimbali hapa parokiani na je ya parokia
>    Kuongoza semina za malezi na makuzi ya kiroho kwa waamini wanao penda kujifunza neno la mungu.
>    Uwaka kutegemeza utume wa wadada wadogo wa shirika la mt Fransisco mbagala ambapo kwa miaka kadhaa parokia imekuwa ikishika nafasi ya kwanza kijimbo
>    Viwawa kuandaa kongamano la ajira kila mwaka
>    Kutegemeza uinjilishaji kupitia vyombo vya habari kama vile radio maria na radio tumaini ambapo kw 2017 parokia imekuwa ya kwanza kitaifa katika kutegemeza radio maria kwenye mbio za mama Maria(Mariathon)
>    Uchangiaji wa kituo cha hija pugu ambapo katika 2017 parokia imekua ya kwanza kijimbo

SEHEMU D: SEMINA MBALIMBALI KATIKA UENDELEVU WA IMANI
                                   UONGOZI NA UTENDAJI
Parokia huendesha semina na mafungo kulingana na kalenda ya liturjia, mfano kipindi cha kwaresma parokia huandaa  semina maalumu kwaajili ya waumini na utolewa kila ijumaa baada ya ibada ya njia ya msalaba kwa msaada wa mapadre.
Zipo semina pia kwaajili ya jumuiya na kanda kadiri ya mahitaji. Inahusisha pia kushiriki mafungo na semina kwa siku moja kwenye gloto ya parokia.
Upo utaratibu wa kuwapatia viongozi  na semina inayotolewa pia  kwaajili ya waumini wote.
Yako mahitaji ya semina kwa waumini kwaajili ya utoaji zaka na matoleo mbalimbali
Semina za kiroho na tegemeza kanisa zinafanyika parokiani
Semina za halmashauri ya walei ni nne kwa mwaka
Hali ya Imani katika parokia inatia moyo ijapokuwa kuna changamoto zake nyingi hii ni pamoja na waumini kuhama imani na kurudi, na pindi mtu huyo anapo rudi hajui afanye nini.
Changamoto nyingine ni watu kuhama makazi na kuhamia maeneo mengine.

SEHEMU E: MATOLEO MBALIMBALI
-Hali mya utoaji sio mbaya na sio nzuri kwa kila ibada makusanyo yanafika 2 ml, na kwa matoleo ya pili kwa shughuli za kimaendeleo mapato yanayo kusanywa ni kati ya sh/ 700,000 hado 900,000. Lakini kulingana na idadi ya waumini na mwonekano kungekuwa na uwezekano wa kukusanya hata 5ml hadi 7ml kama kila mwana segerea angetoa matoleo
-Utoaji wa zaka sio mbaya , kwa mwaka 2014 peke yake tuliweza kukusanya matoleo ya zaka sh/ 135ml, 2017 zimekusanywa 117 ml, lakini 2016 zilipatikana 197 ml ikiwa ni ongezeko la 68% ukilinganisha na 2015 sababu kubwa ilikuwa ni uhamasishaji.
-Mwaka 2016 zilikusanywa 30m kwa harambe ambazo zote zilipelekwa jimboni
Taarifa za mapato na matumizi hutolewa mara moja kila mwaka, na mapato ya kila dominika husomwa kila dominika inayofuata kwa waumini wote kila baada ya miezi mitatu.
-Matoleo yote hupelekwa banki na waumini kupitia jumuiya yao

SHEMU F: ULINZI NA USALAMA
Hali ya ulinzi na usalama ni nzuri,  iwe wakati wa misa na siku zingine
Ulinzi unatoka kampuni ya VOLUMETRIC DATA SECURITY makao yake makuu ni segerea

SEHEMU G; MAENDELEO YA KIUCHUMI
•    Kuna mradi mmoja tu, shule ya Anthony wa padua
•    Upo pia mpango wa ujenzi wa ukumbi wa parokia
•    Upo pia mpango wa ujenzi wa shule ya msingi ya mtakatifu Anthony wa padua na gharama kutokana na faida ya shule
•    Kuna eneo pia ambalo limenunuliwa kwa ajili ya miradi ya parokia itakavyo amuliwa baadae
•    Pia 2017 imenunuliwa nyumba kwajili ya masister ambayo ni ya waalimu wa shule ya mt Anthony wa padua

MAMBO YA JUMLA
-kuna mgogorowa kimipaka kati ya parokia ya segerea na parokia ya makoka lakini unafanyiwa kazi na askofu mkuu wa jimbo
-Parokia inahudumiwa na mapadre watatu wa shirika la ndugu wa Fransisko Wakovenchuari na kwa sasa wanatosheleza.
Idadi ya watawa pia inatosheleza, na kwa upande wa waseminary wako 11, na wote wapo seminari ndogo katika vidato tofauti tofauti. Waumini waliojiunga na utawa ni sita na mabruda wawili na masister wanne
DIRA YA HALMASHAURI YA WALEI PAROKIA
Halmashauri ya walei parokia itakua ndio kiini cha ushauri kwa hierakia ya parokia , kanda , na jumuiya ili kuyatakatifuza malimwengu na kuwapeleka waamini wa parokia ya segerea mbinguni

LENGO LA HALMASHAURI YA WALEI PAROKIA
Lengo ni kuongoza, kusimamia, na kuratibu maazimio mbalimbali yanayotolewa na hierakia, halmashauri ya walei parokia, Kanda,Jumuiya na vyama vya kitume ili kuifanya parokia kudumisha udugu, upendo na Amani kwa waamini wa parokia ya segerea

MALENGO YA KIUTENDAJI
Ili kufikia malengo yake yafuatayo kutekelezwa
•    Kujenga uwezo wa viongozi  wa halmashauri ya walei parokia, jumuiya na vyama vya kitume kwa kutoa semina na mafungo.
•    Kuunda kamati ndogo ndogo za kikatiba na zisizo za kikatiba ambazo zitafanya kazi bila mwingiliano
•    Kusimamia utekelezaji wa maazimio na maelekezo yatakayotolewa na jimbo
•    Kusimamia kufuata na kuweka taratibu zote za fedha kadiri zinavyo idhinishwa na jimbo kuu la dar es salaam
•    Kubuni na kutekeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi katika parokia zilizo ainishwa na kupitishwa na halmashauri ya walei parokia
•    Kutekeleza na kuweka mawasiliano yalio bora kwa kushirikiana na hierakia juu ya ulinzi wa kanisa na maeneo ya kuabudia kwa usalama na Amani

MIKAKATI YA KIUTENDAJI KUANZIA 2016-2019
Njia zifuatazo kutumika

KIROHO
1.    Kujenga uwezo wa kiimani kwa viongozi na waumini kwa njia ya semina na mafungo
2.    Ziara za kichungaji katika familia, jumuiya na kanda zote za parokia
3.    Kuimarisha JNNK kiuongozi na kiimani ili ziweze kutekeleza majukumu yao kadiri ya maelekezo kutoka ngazi mbalimbali

UTENDAJI
I.    Kuwepo uwazi na uwajibikaji kwa vitendo katika kutekeleza majukumu.
II.    Kusimama na kuimarisha vyama vya kitume parokiani na kuwezeshwa uanzishwaji wa VMJ vingine
III.    Kusimamia vyanzo vya mapato vyote vya kanisa kwa kuratibu na kuhakikisha mapato yanatumika ipasavyo kwa nia na lengo lililokusudiwa
IV.    Kusimamia maazimio na malengo yatolewayo na jimbo na dekania yanatekelezwa.
V.    Kulinda na kufuatilia mali za kanisa  ili zisipotee na maeneo ya kanisa yabaki salama

JE UNATAFUTA

PAROKIA?

Upate majibu yako haraka zaidi
Ramani ya Parokia
Hakuna ramani kwa sasa...
Kuhusu Kanisa Katoliki

Ofisi ya Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam inapatikana makao makuu ya Jimbo,
Kanisa la St. Joseph, barabara ya Sokoine na Manseld street.

P.O Box 167, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 762 024 199
Email: mawasiliano@waleijimbodaresalaam.org
            darwaleijimbo@yahoo.com
Web: www.waleijimbodaresalaam.org

Kwa Habari kemkem za Kanisa jiunge nasi

Andika email yako hapo juu, na upokee taarifa za H/walei

Copyright © 2025. All Rights reserved by H/Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam