DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA MBAGALA KUU
PAROKIA YA MT GABRIEL MALAIKA MKUU MBAGALA KUU.
Jina la Parokia ni mt Gabriel Malaika Mkuu.Halifanani na jina la paroia zingine
Parokia inapatikana Mbagala kuu Wilaya ya temeke, na ipo katika Dekania ya Kigamboni.
Parokia ilitangazwa rasmi kuwa kigango 7/7/2016.
Parokia ina jumla ya jumuiya 22, na mitaa sita.
Kwa sasa Parokia ina idadi ya waumini wapatao 2400, na imepatikana kwa kujaza fomu maalumu za sense kupitia kila jumuiya, Sensa ya mwisho ilifanyika mwaka 2016 kwa kujaza fomu zilizo andaliwa na parokia.
Parokia haina kigango kwa sasa.
Kila jumuiya ina kaya kati ya 15-20 na maboresho hayahitajiki kwa sasa.
Jumuiya zinakutana na kusali pamoja siku ya jumamosi kuanzia sa 12:00 asubuhi hadi saa 7:00 Asubuhi.
Mahudhurio ni ya wastani na yanarekodiwa kijumuiya.
KIROHO
Mwamko wa kiroho kwa waumini umeongezeka kwa kasi sana , Hii ikichangiwa na upatikanaji wa huduma za kiroho kwa ukaribu Zaidi ikiwemo sakramenti ya kitubio, Ubatizo , Ndoa, Ekarist Takatifu, Mpako wa wagonjwa kipaimara n.k pamoja na utaratibu mzuri wa sala.
VYAMA VYA KITUME
Kazi y a uimaarishaji vyama vya kitume inafanyika na inaendelea kufanyika, kwa sasa vipo vyama vya kitume kama vifuatavyo;
Uwaka, Wawata, Utoto mt, Watumishi wa Altare, Viwawa, Moyo mt wa Yesu ,Kway ya mt Padre Pio, Kwaya ya mt Yohane na kwaya ya Shirikisho.
MAENDELEO
Pamoja na maendeleo ya kiroho , Parokia imepiga hatua y kimiundo mbinu tangia itangazwe kuwa parokia hapo 2016.
1. Imeweza kujenga na kukamilisha ofisi ya Paroko na makatekista.
2. Ujenzi wa uzio /ukuta upande mmoja wa kanisa.
3. Ukarabati wa kanisa kwa kubadilisha mwonekano wa altare, Ukarabati wa vyoo, Ujenzi wa Tabernakulo, Upakaji rangi wa kanisa ndani na nje pamoja na sakrestia.
4. Kuendeleza ujenzi wa nyumba ya Mapadre ambao uko katika hatua za mwisho.
SEMINA
Semina mbalimbali zimefanyika kuhusu utoaji na zinaendelea
Parokia iliweza kutoa pia semina ya viongozi kwa viongozi wote wa parokia, semina ilihusu Zaidi (a) Uongozi (b) Wajibu wa kiongozi (c) Kujitoa na utoaji (D) Katiba pamoja na vikao vyenye Tija, semina iliyo ongozwa na Halmashauri ya walei jimbo kuu la Dar es salaam ikiongozwa na mwenyekiti Mzee Silo.
Elimu ya dini na mafundisho hutolewa kila jumapili kwa watoto ambao hawajafikia umri wa kuanza mafundisho.
Kamati ya liturjia hutoa elimu ya maadili kabla au mwisho wwa ibada kwa siku za jumapili.
MIPANGO YA BAADAE
> Kumaliza nyumba ya mapadre
> Kupima eneo la kanisa na kuandaa master plan
> Ujenzi wa Groto ya mama Bikira Maria, Choo cha waumini na ukumbi wa mikuitano
> Upanuzi wa kanisa ili kuwezesha waumini kusali kwa utulivu.
> Kuendeleza uzio wa kanisa ili kuendeleza eneo lililo baki
> Kuendelea kutoa huduma za kiroho na kiofisi kwa karibu Zaidi
> Kununua jenereta kukabililanan na tatizo la umeme.
> Kuongeza nguo za misa na vitambaa vya altare kadiri ya mpango kazi wa kamati