DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA BAHARI BEACH
Jina la Parokia ni BAHARI BEACH
-Msimamizi wa Parokia MTAKATIFU ANDREA MTUME
- Jina halifanani na Parokia nyingine za jimbo la Dar es salaam
Parokia ilitangazwa rasmi 2012
Kijiografia Parokia ipo Bahari Beach Wilaya ya kinondoni
Parokia inapatikana katika dekania ya Mt Gaspary de Buffalo
idadi ya waumini katika parokia Mpaka kufikia 2012 ilikua ni kati ya waumini 700 na imepatikana kwa njia ya sense iliyofanyika 2012 kwa waumini kujaza fomu maalumu
Sensa ya mwisho ni 2012 na nyingine itafanyika 2017
Parokia haina vigango .
Ziko JNNK 12
Kila jumuiya ina kaya kati ya 20-25
Jumuiya zinasali mara moja kila siku ya jumamosi kuanzia saa 12:30 kwa kufuata mwongozo wa jumuiya ndogo ndogo toka Jimboni
Maudhuri kwa jumla katika JNNK ni ya wastani, na maudhurio huwekwa katika kumbukumbu.
Upo pia utaratibuwa kuzitembelea jumuiya NNK , Kanda na pia misa zinasomwa.
Kanada JNNK hua zinaadhimisha Misa takatifu za somo wa jumuiya na kanda kila baada ya mwaka mmoja.
Uongozi wa jumuiya umekamilika na pale ambapo inapotokea kuna mapungufu yanajazwa mara moja kwa kuitisha uchaguzi mdogo.
Halmashauri ya walei ya parokia /kanda hukutana mara chache
Huduma za kiroho na jamii ni pamaoja matendo ya huruma kwa kutembelea wagonjwa na wenye shida mbali mbali.
Maudhurio katika sala na matukio au matendo ya huruma ni changamoto kubwa
UONGOZI
Kamati tendaji ipo na imekamilika kikatiba
Kamati tendaji ya parokia hukutana mara moja kila mwezi siku za jumapili baada ya misa ya pili, muda saa moja .Baba paroko ni mshiriki katika kikao hicho.
Halmashauri ya walei ya parokia inaundwa na viongozi watano wa kila jumuiya pamoja na wenyeviti wa vyama vya kitume na inakutana mara moja kila baada ya miezi miwili.
Agenda na taarifa za vikao zinapatikana kwa wakati na zinatunwa.
Parikia ina ofisi za halmashauri ya walei ya parokia na ina vitendea kazi.
Njia za mawasiliano kwa wajumbe wa kamati Tendaji pamoja na Halmashauri ya Walei ni :
Kwa njia ya barua pepe(yaani E mail) simu,Whats aap, lakini zaidi ya hapo ni kwa matangazo kanisani.
Zipo kamati ndogo ndogo za kikatiba na zimekamilika,
kamati hizo hua zinakutana mara mara.
Zipo kamati zingine ambazo sio za kikatiba na zinaripoti kwa kamati tendaji ya parokia, kamati hizi ni kama zifuatazo:
a) Kamati ya mavuno
b) Kamati ya ujenzi
c) Kamati ya maendeleo
kamati hizi zimetengenezwa kwa ushirikishwaji waumini
Waamini wanaarifiwa mipango ya parokia kwa kupitia maatangazo kanisani , pia kupitia JNNK kupita halmashauri ya walei ya parokia
VYAMA MASHIRIKA NA JUMUIYA ZA KITUME (VMJ)
Vipo vyama vya kitume 7 kama ifuatavyo
1. WAWATA,
2. UWAKA
3. VIWAWA,
4. Utoto mtakatifu
5. Shikwaka
6. MOYO MT WA YESU
7. Watumikizi wa altare
Vyama hivi vina watumishi wa kutosha baadhi ya Parokia
Vyama na vikundi vya kitume vinafanya kazi kulingana na katiba ya halmashauri ya walei ya jimbo na vyama vyote hivi viko hai
Vyama hivi havina ofisi parokiani, lakini vinalelewa na vipo chini ya uongozi wa parokia
VMJ vinatoa taarifa na repoti pamoja na ya fedha mara kwa mara kwa uongozi wa parokia
Na pia vinajitegemea na viko chini ya uangalizi wa parokia
Vyama vina ushirikiano mzuri katika dekania na katika ngazi ya jimbo
VMJ havijafanya mambo yeyote mapya ambayo yanaweza kuigwa na parokia nyingine
SEMINA MBALIMBALI KATIKA UENDELEVU WA IMANI, UONGOZI NA UTEGEMEZAJI
Kuna semina za kijumiuiya ambazo zimeshafanyika ,lakini kwa sasa mipango inaandaliwa ili semina nyingine ziweze kufanyika
Kamati tendaji parokia ilishapatiwa semina ya uongozi jimboni lakini bado semina zingine zinahitajika kwaajili ya Halmashauri ya walei parokia
Semina za kiroho hazijaanza kufanyika bado
Hali ya Imani kwa ujumla inaridhisha, na inatakiwa kuendelezwa kwa nguvu
Kimsingi hali ya utoaji parokiani ni ya wastani.
Hali kadhalika utoaji wa zaka kama amri ya kanisa ni wa wastani.
Parikia inatoa michango ya jimbo kamili kama inavyo paswa
FEDHA NA MIPANGO
Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa Jimbo
Mapato na matumizi ya parokia yanajulikana kwa waumini na yanatolewa taarifa kila baada ya miezi mitatu kwa mwaka
Matoleo ya kila dominika yanatangazwa kwa waumini kila dominika inayofuata
Fedha zote zinazokusanywa hupelekwa benki kwa wakati
ULINZI NA USALAMA
Hali ya ulinzi na usalama parokiani ni ya kuridhisha, na ulinzi unafanywa na kampuni binafsi
MAENDELEO YA KIUCHUMI
Parokia haijawa na miradi yake kwa sasa
Kwa sasa kuna mipango ya ujenzi wa kanisa
MAMBO YA JUMLA
Parokia haina mgogoro wowote wa kimipaka
Kwa sasa parokia haina mipango yeyote ya kuwaendeleza waumini wake kiuchumi
Idadi ya mapadre na watawa inatosheleza.
Idadi ya wanafunzi wa seminari kutoka parokia hii ni wawili (2)
Parokia haina waumini waliojiunga na utawa kwa sasa.
Ipo pia historia ya parokia pindi itakapohitajika inayoeleza juuu ya waumini, mapadre, picha za sasa na za zamani na mairadi iliyokuwepo sasa.