DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA MARIA DEMATTIAS



HISTORIA YA PAROKIA YA MT. MARIA DE MATTIAS-MIVUMONI
Parokia ya Mt. Maria De Mattias-Mivumoni iko katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam na katika Dekania ya Mt.
Gaspar del Bufalo. Parokia hii iko katika Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni. Parokia hii inaendeshwa na Mapadre wa Jimbo.
Historia ya Parokia ya Mt. Maria De Mattias inaanzia pale ambapo Halmashauri ya Walei ya Kigango cha Mt.
Fransisko Xaveri - Wazo Hill (Kwa sasa Parokia ya Mt. Benedikto Abate- Wazo Hill) ilipokabidhi uangalizi wa eneo hili la kanisa kwa Kanda ya Mt. Inyasi wa Loyola zikiwa na Jumuiya mbili za Mt. Inyasi wa Loyola na Mt. Martha mwezi Mei 2005. Wakati huo kulikuwa na hofu ya uvamizi wa viwanja kwani maeneo yalikuwa ni mapya na hivyo ramani ya eneo haikuwa ikifahamika vizuri. Jumuiya hizo mbili ziliendelea kuhudumia eneo hili kwa kufanya usafi, kupanda miti na kulinda mipaka kwa kushirikiana na Jumuiya nyingine zilizozaliwa baadaye. Mbali na shughuli hizo za uangalizi, sala za jumuiya, misa (zikiwemo za ubatizo na ndoa) na hata shughuli nyingine za kiroho zilifanyika katika eneo hili bila kuwa na jengo la kanisa.
Kutokana na umuhimu wa malezi ya kikristo kwa watoto na mafundisho mengine ya dini, mnamo mwezi Januari 2009 waamini waliamua kwa pamoja kujenga kibanda kidogo cha muda ambacho kingetumika kufundishia watoto mafundisho ya dini ifikapo mwezi Mei 2009. Hata hivyo, kwa sababu mbalimbali, ujenzi huo haukuweza kuanza hadi ilipofika mwezi Desemba 2009. Wakati huo, wazo liliibuka la kuwa na jengo dogo la kanisa badala ya kibanda cha kufundishia watoto.
Ujenzi wa jengo dogo la Kanisa ulianza rasmi mwezi Januari 2010 na ilipofika Aprili 2010 jengo lenye uwezo wa kukaa waamini 200 lilikuwa limefikia hatua ya kuwa na paa na hivyo kuruhusu ibada ya kwanza ya Pasaka kufanyika bila sakafu. Ujenzi wa jengo la Kanisa ulipitia hatua mbalimbali za usanifu na ramani ili kuendana na raslimali fedha zilizotakiwa kufanikisha kazi hii. Ujenzi huu uligharimu zaidi ya Shilingi Millioni Hamsini za Kitanzania (50,000,000.00), kiasi ambacho kinajumuisha michango ya fedha taslimu, vifaa vya ujenzi na nguvu kazi (gharama nyingine nyingi hazikuweza kukadiriwa kwa kuwa zilikuwa ni majitoleo kwa njia ya nguvu kazi, punguzo la bei ya vifaa n.k.). Ujenzi ulifanyika kwa kushirikisha jumuiya zote na ulihusisha kujenga sakristia, ofisi, vyoo, kuweka nguzo za uzio, kununua vifaa mbalimbali mfano viti, meza, kabati n.k.
Baada ya ujenzi kukamilika kwa asilimia kubwa, kanisa lilipata hadhi ya kuitwa kigango. Hivyo uzinduzi rasmi ulifanyika tarehe 29 Agosti 2010 na Baba Padre Felix Mushobozi, Katibu wa Shirika la Damu Takatifu ya Yesu Duniani chini ya uongozi wa Parokia ya Damu Takatifu ya Yesu Tegeta na Baba Paroko akiwa Padre Richard Tiganya. Ili kuweza kuendelea na majukumu mbalimbali ya kigango wajumbe wa Kamati Tendaji na baadhi wa vyama vya Kitume ngazi ya Parokia na Kamati ya Ujenzi waliteuliwa, kusimikwa na kuanza kazi rasmi wakati wa misa hiyo ya uzinduzi. Mara baada ya uzinduzi Padre Josephat Msuya alichukua nafasi ya Paroko baada ya Padre Richard Tiganya kuhitajika masomoni ulaya ya muda mrefu. Wakati huo, Kigango kilikuwa na jumla ya jumuiya nane ambazo ni Mt. Inyasi wa Loyola, Mt. Martha, Mt. Rita wa Kashia, Mt. Monika, Mt. Katarina wa Siena, Mt. Ambrose, Mt. Lusia na Mt. Thomas Mtume.
Hapo awali kabla ya Parokia, Kigango kiliwekwa chini ya Mt. Monika kama Msimamizi Somo wake. Baadaye ilionekana ni muhimu kubadilisha Msimamizi Somo wa Kigango ili kuondokana na mkanganyiko ambao ulikuwa unatokana na jina la Mtakatifu huyo kutumiwa na baadhi ya Parokia na Vigango vingine vya Jimbo. Kutokana na maelekezo kutoka kwa Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, kuanzia tarehe 28 Agosti, 2013 Kigango kiliwekwa rasmi chini ya Mt. Maria De Mattias kama Msimamizi Somo wake hadi sasa.
Ziara iliyofanyika kigangoni mnamo Januari 2014 na Mhashamu Baba Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Eusebius Nzigilwa pamoja na mambo mengine ilikuwa na lengo la kutathmini maendeleo ya jumla na vigezo vya kuwezesha Kigango kuwa parokia. Kigezo kimojawapo katika tathmini hiyo ilikuwa uwepo wa nyumba ya mapadre. Baada ya ziara hiyo kanisa lilipata hadhi ya kuitwa Parokia terehe 7 Julai 2014 na kukabidhiwa kwa utume wa Mapadre wa jimbo na Padre Edwin Epimack Kigomba ndiye Paroko wa kwanza hadi sasa na Msaidizi wake alikuwa Padre Paul Sabuni Mboje.
Makabidhiano rasmi ya Parokia yalifanyika mwezi Agosti 2014 na Padre Novatus Mbaula, Mkurugenzi wa Msimbazi Centre.Wakati huo, Parokia ilikuwa na jumla ya jumuiya 13. Baada ya kutangazwa Parokia, Kigango cha Mt. Benedikto Abate –Wazo Hill kilikabidhiwa chini ya uongozi wa Parokia ya Mt. Maria De Mattias kikiwa na jumuiya 23 hivyo kufanya jumla ya jumuiya kufikia 36. Baadae jumuiya 22 ziliongezeka; 13 kutoka Mt. Benedikto Abate-Wazo na 9 kutoka Mt. Maria De Mattias-Mivumoni hivyo kufikia jumuiya 58. Hata hivyo, baada ya Parokia Teule ya Mt. Benedikto Abate –Wazo kutangazwa Parokia kamili Julai 2016, Parokia ya Mt. Maria De Mattias –Mivumoni ilibaki na jumuiya 22 na ziliendelea kuongezeka.
Parokia ya Mt. Maria De Mattias –Mivumoni ina jumla ya waamini 2,618 ambapo watoto ni 970, Vijana 337 Akina baba 562 na akina mama 645 kulingana na taarifa ya 2018. Kwa sasa Parokia inafamilia 678 na Jumuiya Ndogondogo za Kikristo 30 nazo ni Jumuiya ya Mt. Inyasi wa Loyola, Jumuiya ya Mt. Martha, Jumuiya ya Mt. Rita wa Kashia, Jumuiya ya Mt. Monika, Jumuiya ya Mt. Katarina wa Siena, Jumuiya ya Mt. Ambrose, Jumuiya ya Mt. Thomas Mtume, Jumuiya ya Mt. Lusia, Jumuiya ya Mt. Gaspare del Bufalo, Jumuiya ya Mt. Kizito, Jumuiya ya Mt. Augustino, Jumuiya ya Mt. Anna, Jumuiya ya Mt. Margareta Maria Alakok, Jumuiya ya Mt. Yohane Paulo II, Jumuiya ya Mt. Teresia wa Mtoto Yesu, Jumuiya ya Mt. Yohane wa XXIII, Jumuiya ya Mt. Josephine Bakhita, Jumuiya ya Mt. Anthony wa Padua, Jumuiya ya Mt. Marko Mwinjili, Jumuiya ya Mt. Luka Mwinjili, Jumuiya ya Mt. Yosefu Mfanyakazi, Jumuiya ya Mt. Maria Goreti, Jumuiya ya Mt. Marcelino, Jumuiya ya Mt.Veronica, Jumuiya ya Mt. Joakimu, Jumuiya ya Mt. Yohane Bosco, Jumuiya ya Mt. Petro, Jumuiya ya Familia Takatifu, Jumuiya ya Mt. Mikael Malaika Mkuu na Jumuiya ya Mt. Yuda Tadei.
Takwimu za sakramenti kuanzia 2010 hadi Juni 2018
Mwaka | Ubatizo-Watoto | Komunio | Kipaimara | Ndoa | Ubatizo Watu Wazima | Wakristo waliopokelewa ukatoliki |
2010 | 24 | 0 | 0 | 6 | 1 | 0 |
2011 | 47 | 17 | 21 | 8 | 3 | 0 |
2012 | 55 | 39 | 23 | 10 | 10 | 0 |
2013 | 75 | 29 | 32 | 5 | 5 | 0 |
2014 | 34 | 36 | 34 | 5 | 6 | 5 |
2015 | 95 | 25 | 19 | 6 | 48 | 5 |
2016 | 93 | 81 | 86 | 23 | 9 | 3 |
2017 | 66 | 106 | 82 | 15 | 12 | 4 |
2018 | 55 | 83 | 63 | 12 | 6 | 11 |
Vyama vya Kitume vilivyopo katika Parokia ni pamoja na WAWATA (562), UWAKA (485), Vijana (226), Utoto Mtakatifu (562), Moyo Mtakatifu wa Yesu (7), Legio Maria (8), Wadiministranti (36), Shikwaka (86) (Kwaya ya Mt. Maria De Mattias, Kwaya ya Mt. Yohane Paulo II, Kwaya ya Kristo Mfalme) na Kwaya ya Watoto.
Uongozi wa Halmashauri Walei ya Parokia kuanzia 2012 hadi 2018
Mwaka 2012 hadi 2015
Na. | Jina | Wadhifa |
1. | Ndg. Cosmas Mwaisobwa | Mwenyekiti |
2. | Ndg. Chrysanthus Chenga | Makamu M/kiti |
3. | Ndg. Adelaide Sallema | Katibu |
4. | Ndg. Andrew Peter | K/Msaidizi |
5. | Ndg. Mary Mwapili | M/Hazina |
Mwaka 2015 hadi 2018
Na. | Jina | Wadhifa |
1. | Ndg. Chrysanthus Chenga | Mwenyekiti |
2. | Ndg. Zephrine Galeba | Makamu M/kiti |
3. | Ndg. Adelaide Sallema | Katibu |
4. | Ndg. Andrew Peter | K/Msaidizi |
5. | Ndg. Mary Mwapili | M/Hazina |
Ee Mtakatifu Maria De Mattias, mtangazaji na mtume hodari wa Damu Takatifu ya Yesu. Uliyetumia maisha yako yote kwa kuvuta roho za watu kwenye chemchemi ya neema inayotoka moyoni mwa Yesu Msulubiwa. Unijalie moto wa mapendo kama ule uliogusa moyo wako na bidii kwa wokovu wa watu, uliokuwa lengo kuu na la pekee la maisha yako. Amina.
Mt Maria De Mattias …….Utuombee….x3
UJENZI WA JENGO KUBWA LA KANISA
Wazo la ujenzi wa jengo kubwa la Kanisa lilitokana na tathmini ya ongezeko la idadi ya waamini wa Mivumoni. Hivyo, mawazo, majadiliano na mikakati ilianza kufanywa na ilipofika Novemba 2013 michoro na ramani ya kanisa vilipatikana.
Mnamo 17 Novemba 2014 Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam alibariki msingi wa jengo la kanisa na ilipofika Februari 2015 ujenzi wa jengo kubwa la Kanisa ulianza rasmi kwa muda wa miaka mitatu. Makadirio ya gharama za ujenzi wa Kanisa ni takribani Shilingi za kitanzania bilioni 1.
Kazi ya ujenzi wa Kanisa imekuwa ikisimamiwa na Kamati ya Ujenzi iliyoteuliwa tangu mwaka 2014 na kupewa majukumu. Wajumbe wa Kamati ni kama ifuatavyo:
Na. | Jina | Wadhifa |
1. | Ndg. Andrew Peter | Mwenyekiti |
2. | Ndg. Prosper Manyele | Makamu M/kiti |
3. | Ndg. Gaudensia Simwanza | Katibu |
4. | Ndg. Deusdedith Magala | K/Msaidizi |
5. | Ndg. Jane Moshy | M/Hazina |
Jiwe la msingi la jengo la Kanisa liliwekwa rasmi tarehe 5 Julai 2015 na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaamwakati maendeleo ya ujenzi yakiwa kwenye hatua ya kuweka dari. Jengo hili lina ukubwa wa kuingia waumini 1200 kwa mara moja.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliyetujalia neema na baraka zake hadi tumefikia hatua ya kubariki Kanisa na kutabaruku Altare mnamo mwezi Februari 2018. Tunamshukuru sana Mungu kwani moyo ya Waumini wa Parokia hii wa kujitoa kwa Kanisa ni mzuri bila kujali jinsia au rika. Waumini kwa Parokia ya Mt. Maria De Mattias wameshiriki kikamilifu katika shughuli zote za maendeleo kuanzia ujenzi wa Kanisa dogo (sasa ukumbi wa Parokia), ujenzi wa nyumba ya Mapadre, Kanisa kubwa, Grotto, maliwato ya kisasa na katika majukumu mengine ya kikanisa. Tunaomba umoja na mshikamano huu wa kuiendeleza kazi ya Mungu hapa duniani iendelee bila kusita ili tuweze kukamilisha majukumu mengine yajayo na hasa uwekaji wa mabenchi kanisani. Tunazidi kuomba Neema na Baraka za Mungu na tukaongozwe na neno lake kutoka Hagai 1: 7-8.
SALA YA KUOMBEA UJENZI KATIKA PAROKIA YA MT. MARIA DE MATTIAS
Ee Mungu Baba Mwenyezi, Wanaparokia wa Mt. Maria De Mattias tunakushukuru kwa neema na mapaji unayotujalia. Tunakuja kwako jinsi tulivyo kwa unyeyekevu mkubwa tukiomba msaada wako. Bila msaada wako Mungu wetu sisi hatuwezi kitu. Ujenzi wa Kanisa hili si kwa nguvu zetu wenyewe bali ni kwa uwezo wako Mungu unatuwezesha. Tunakusihi Baba wa Milele utukinge sisi watoto wako dhidi ya hila zozote mbaya zinazopingana na juhudiza ujenzi tunazoendelea nazo. Uwabariki wote wanaojitoa kwa uchaji wa kiMungu katika ujenzi kwa namna mbalimbali. Uwazidishie ari ya kujitoa zaidi tukikumbuka kuwa nafsi zetu, sisi wenyewe na vyote tulivyo navyo ni mali yako Bwana. Hivyo, hatuna budi kuvirudisha kwako. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana Wetu anayeishi na kutawala daima na milele. Amina.
Mt. Maria De Mattias….Utuombee
Mt. Gaspar del Bufalo….Utuombee
Watakatifu wote wa Mungu…Mtuombee.
PAROKIA YA MT MAARIA DE MATTIAS –MIVUMONI
Jina la Parokia ni mt Maria De Mattias- Mivumoni
Mtakatifu msimamizi wake ni Maria De Mattias
Jina hili haliingiliani na parokia zingine za jimbo la dar es salaam
Parokia ya Mt Maria De Mattiias ipo katoka jimbo kuu la Dar es salaam,Wilaya ya kinondoni
Parokia ina patikana mivumoni ambapo kwa upnde wa mashariki imepakana na parokia ya salasala, kwa upande wa magharibi ni Parokia ya Boko, na kwa upande wa kaskazini ni Paarokia ya Benedict wa Abate Wazo na kwa upande wa kusini ni paroki ya Madale
Parokia hii ipo katika Dekania ya Ya Mt Gaspar De Bufalo
Parokia ina idadi ya waumini wapatao 2200 ambayo imepatikana mwaka 2017 kwa kupitia taarifa za utekelezaji kutoka katika kila jumuiya ambapo upatikanaji wake ni sense.
Sensa ya mwisho kufanyika ilikuwa 2017
Na ilifanyika kwa kujaza fomu maalumu za sense. Na sense nyingine itafanyika pale itakapo bidi
Kwa sasa parokia haina kigango
Shughulil za kikanda zinafanyika lakini hazipo (officially),rasmi
Uongozi wake pia haujakamilika.
Parokia inajumla ya jumuiya 27
Kila jumuiya ina wastani wa kaya 15-20. ziko baadhi ambazo zina kaya nyingi na mchakato wa kuzigawa uko mbioni.
JNNK na Kanda zinasali pamoja . JNNK zinasali pamoja kila jumamosi kuanzi saa 12:30 na zina tumia kati ya saa moja na nusu.
Sala ni kwa kupitia kitabu cha mwongozo wa sala
Maudhurio katika jumuiya kwa ujumla ni ya wastani na yanaarekodiwa. Hali kadhalika uhamasishaji unafanyika pia ili mwamko uwepo wa kusali.
Mara nyingi JNNK zinatembelewa na padre karika matukio mbalimbali pamoja na huduma kwa wagonjwa
Hali kadhalika Jumuiya hua zinaadhimisha siku wa somo wake kila inapofikia siku na wakati husika.
Uongozi katika JNNK umekamilika na hauna mapungufu.
Uongozi halmashauri ya walei Parokia hukutana kila mara na inapobidi kila mwezi
Huduma za kiroho
Huduma za kiroho zitolewazo katika JNNK na kanda ni kama zifuatazo:
-Sakramenti kwa wagonjwa,hali kaadhalika kupaeleka mahitaji kwa wagonjwa, ushauri na upatanisho hassa kwa wanandoa.
-Sakrament ya ubatizo , kipaimara na komunio zinatolewa kwa wale wanao stahili kupokea.
-Kufanya matendo ya huruma kwa wahitaji ,kuendesha misa takatifu katika shughuli za maziko na kujaza fomu za kuomba misa.
Changamoto
Maudhurio machache kwenye ibada, semina, mikutano, na vikao mbalimbali, haswa kwa wakina baba na vijana.
Waumini wengi hawajui maana ya utoaji katika kanisa
Uchumba wa muda mrefu
Waumini baadhi kukimbilia kwenye makanisa mengine
Kamati tendaji ipo na imekamilika
Kamati tendaji hukutana mara moja kwa wiki na maranyingine ni siku ya jumapili baada ya misa na baba paroko anapewa taarifa na anashirikishwa. Vikao vya dharura hufanyika pale vinapo hitajika
Hamalamashauri ya walei ya parokia inaundwa na Kamati tendaji ya parokia , Viongozi watano kutoka kila JNNK, Wenyeviti vyama vya kitume,
Agenda na ripoti za vikao hupatikana kw wwakaati na vinatunzwa.
Parokia inayo ofisi ya Halmashauri ya walei na inavitendea kazi vinavyo kidhi.
Njia zinazotumika kwa mawasiliano kwa wajumbe wa halmashauri ya walei pamoja na kamati tendaji ni kama zifuatazo;Barua pepe yaani (E mail), What up Group, Simu, Barua na matangazo ya kanisani.
Kamati
Katika parokia kuna kamati ndogo ndogo za kikatiba na zimekamilika. Na pia
Zipo kamati zisizo za kikatiba ambazo ni ;Kamati ya ujenzi, na inakutana kala inapo hitajika kufanya hivyo, Kazi yake ni kuratiibu shughuli na kusimamia shughuli zote za ujenzi na ukarabati ndani ya parokia.
Kamati zote hizo za kikatiba na zisizo za kikatiba zinaripoti kwa kamati tendaji ya parokia
Kamati hizi zinzfanya kazi kwa umakinifu na mawasiliano lakini hazina muingiliano.
Ziko dira malengo na mikakati ya parokia
Parokia ina kalenda ya matukio ya mwaka ili kuiwezesha kuwa na mipangilio bora, na imeandaliwa kwa kushirikisha waumini.
Njia zinazotumika kuwaarifu waumini mipango ya parokia kwa ushiriki kamilifu ni ;
> Mikutano ya halmashauriya walei parokia.
> Njia ya matangazo siku za dominika
> Viongozi kuongea na waumini kanisani
> Viongozi kutembelea jumuiya na kueleza jambo husika
> Kupitia kamati ndogo ndogo.
Vyama mashhirika na jumuiya za kitume (VMJ)
Vyama mashirika na jumuiya za kitume katika Parokia yam aria De Mattias vipo (8).
Wanachama waliopo katika vyama hivi ni wa wastani, na waumini bado wwanaendele kujiunga.
Na Vingi vinajitahidi kukidhi mahitaji ya Parokia.
Vipo vyama na vikundi vya kitume ambavyo navyo vinafanya kazi kulingana na katiba ya halmashauri ya walei na viatimiza vizuri wito wao wa kitume.
Vyama mashirika na jumuiya za kitume vina shiriki vizuri matukio ya Kiparokia ,dekania na jimbo.
VMJ havina ofisi maalum Parokiani lakini huruhusiwa kufanya mikutano na sala zao katika ukumbi wa parokia na baadhi ya ofisi zilizopo.
Baadhi ya vyama vimewekewa utaratibu maalumu wa kuvichangia mfano utoto mt na Viwawa, lakini baadhi wanamifukoyao ya kujiwezesha kwenye matukio
VMJ vunatoa taarifa pamoja nay a fedha mara kwa mara katika uongozi wa parokia
Hakuna changamoto zozote katika VMJ zinazohatarisha Imani katoliki ,Amani na utulivu katika parokia
Ushirikiano wa ushiriki wa VMJ za parokia katika shughuli za dekania na jimbo uko Vizuri
Mamabo yaliyofanya n VMJ za parokia zipasavyo kuigwa na parokia nyingine ni –Waumini kuchangia ujenzi wa Groto Pugu Kupanda mlima kilimanjaaro, ziara za vyama na uchangaiaji wa shughuli za maendeleo eneo husika mfano ;visiga seminary, Mabagala kwa masister wadogo, uinjilishaji vijana na tumaini media.
Semina mabalimbali katika uendelevu wa Imani , uongozi na utegemezaji
Semina mbalimbali huandaliwa katika ngazi ya parokia mfano ;utoaji, Imani na pia ratiba ya semina imeandaliwa
Kamati tendaji imepatiwa semina kupitia jimbo bado halmashauri ya walei parokia , lakini semina zinahitajika zaidikwa kufundisha ,kukumbusha na msisitizo ili kuboresha kamati husika.
Halli ya Imani katika parokia ni nzuri Semina na mafundisho ya dini nay a kuimaarisha Imani yanahitajika Zaidi.
Utoaji kwa ujumla ni mzuri na unaridhisha kwani waumini wanajitoa Zaidi kulingana na vipato vyao
Waumini wanahamasishwa kila siku kuhusu swala la utoaji wa zaka kila jumapili na hata kaatika ngazi ya jumuiya.
Parokia inatoa michango kamili ya jimbao kwa kadiri inavyoelekezwa.
Fedha na mipango.
Mpango wa fedha unaotumika si ule wa jimbo.
Taarifa za mapato na matumizi hutolewa kwenye vikao vya halmashauri ya walei parokia na vikao vya jumuiyana pindi waumini wanapo hitaji kujuwa husomewa kanisani.
Matoleo ya kila dominika hutangazwa kwa wwaumini kila dominika inayofuata.
Fedha yote hupelekwa benki kwa wakati
Ulinzi na usalama
Hali ya ulinzi na usalama parokiani iko vizuri, lakini bado liko swala la uimarishaji Zaidi kuhusu ulinzi kutokana na shughuli mbalimbali za ujenzi ambazo zinaendelea.swwala hilo pia limefikiriwa katika mpangoo mkakati wa parokia.
Na walinzi wanaotumika ni walinzi binafsi.
Maendeleo ya kiuchumi
Kwa sasa hakuna mradi wowote unaoendeshwa na parokia kwani parokia iko katika hatua za awali za kujijenga ;(jengo la kanisa , vifaa vya ibada , huduma za kiroho, maliwato, ofisi, nyumba ya mapadre finishing, landscaping n.k.)
Parokia ipo katika ukamilishaji wa jengo kubwa la kanisa pamoja na ujenzi wa maliwato ya kisasa, waumini wengi wamehamasishwa na wakahamasika kwa ujenzi huo.
Mambo ya jumla
Hakuna mgogoro wa kimipaka kwa sasa katika parokia
Mipango ya kuwaendeleza waumini kiuchumi haipo kwa sasa lakini ipo kwa mipango ya baadae
Idadi ya mapadre haitoshelezi na hakuna watawa kwa sasa
Parokia haina wafunzi wa seminari kwa sasa na hata mtawa pia.
Mwisho
Yapo maandiko ya parokia kuhusu historia ya parokia , mapadre wwaumini na picha za sasa na za zamani , ambapo maandiko yanapatikana kaatika mfumo wa taarifa na risala , upo pia utaratibu wa kuandika kijarida /booklet ambayo itaonyesha matukio yote ya wakati wa kukabidhiwa kiwanja cha kanisa na paarokia ya jirani ya mt Benedicto wa Abate 2005