PAROKIA YA MT. BENEDICTO WA ABATE


      PAAROKIA YA WAZO
Jina la msimamizi wake ni MT BENEDICTO WA ABATE
Parokia ilizaliwa 2016
Kijiografia parokia ya mt Benedicto wa Abate inapatikana wazo karibu kabisa na kiwanda cha Saruji (Tanzania Portland cement company), kwa upande wa mashariki inapakana kabisa na parokia ya Maria De Mattias na upande wa kaskazini imepakana na parokia ya damu takatifu ya yesu tegeta
Idadi ya waumini katika Parokia nzima ya mt Benedicto wa abate ni kati ya waumini 3,200. Parokia ina wakina mama wengi zaidi kwa 30% ,wakina baba 23%, watoto 29% na vijana 18%
Halmashauri ya walei ya parokia ndio imekuwa na jukumu la kusimamia ustawi wa parokia kiroho, kiimani na kimaendeleo

HALI YA UONGOZI.
Kamati tendaji ipo na imekamilika.
Uongozi umeundwa na halmashauri ya walei ya parokia ,kamati tendaji ya parokia,wenyeviti vyama vya kitume ngazi ya parokia.
 Aidha ,parokia imekuwa na kamati tendaji za jumuiya za kanda katika jumuiya zake zote 50 .
Kwa ujumla parokia inaidadi ya Jumuiya ndogo ndogo kati ya 50.
Na  kanda zilizopo ni 8 na zinatumia majina ya watakatifu.
Viongozi wake wamechaguliwa kwa mujibu wa katiba ya halmashauri ya walei jimbo.

KIROHO
Hali ya masakramenti
Hali ya sakramenti katika parokia inaendelea kuimarika miongoni mwa waumini, Idadi ya wanaoitikia kufunga ndoa ni kubwa sana , kwa mfano kwa kipindi cha mwaka 2017 peke yake Ndoa zilizofungwwa ni 11, waumini waliobatizwa ni 31 na waliopokea kipaimara ni 13

ULINZI NA USALAMA
Hali ya ulinzi na usalama kwa sasa inaridhisha , walinzi wanaotumika ni kutoka kampuni binafsi ambao hulinda mali na muda watu wanapo abudu

HALI YA MICHANGO
Inahusu Zaidi majitoleo ya waumini yaani michango mbalimbali hususani ile ya mavuno na pentekoste
Pentekoste
Hali ya michango ni ya wastani, na michango yote inawakilishwa jimboni kwa kadiri ya maelekezo ya jimbo.
Tegemeza jimbo
Michango ya kutegemeza jimbo inachangwa na kuwasilishwa kwa wakati jimboni. Kiasi cha sh 11,000,000 zilichangwa 2017 na uhamasishaji Zaidi unaendelea .

MAFANIKIO
Uimarishaji wa Imani miongoni mwa waumini
Ziara ya wadada wadogo Mbagala, uwaka walishiriki kikamilifu ziara ya wadada wadogo mbagala, na katika ziara hiyo UWAWKA waliwakilisha kiasi cha sh 5,000,000/=
WAWATA, VIWAWA  na utoto mtakatifu kwa upande mwingine wameshiriki katika ziara na hija mbalimbali kulingana na ratiba ya jimbo kuu.
Pia kumekuwa na zoezi la kutembelea waumini nyumba kwa nyumba na kuzungumuza nao juu ya mambo ya kiimani, kutembele wagonjwa na kufanya maombezi majuumbani kwao na pia kuwapa sakramenti stahiki.
Maendeleo ya kimiundombinu
     Ujenzi wa vyoo vya parokia.
Ujenzi wa vyoo vya parokia umeisha kwa asilimia 90%, hii ni katika kipindi cha 2017 pekee.
     Ujenzi wa kituo cha katekisi
Parokia imejenga kituo cha katekisi ili kusogeza huduma za kirohi na mafundisho ya watoto wanaotoka jumuiya zilizopo maeneo ya karibu na parokia.
     Ujenzi wa ukuta
Parokia imeanza kufanya ujenzi wa ukuta kuzunguka eneo la parokia ili kuimarisha ulinzi katika maeneo ya parokia na waumini wakati wa ibada, pia kuweka ulinzi katika mali za parokia , maandalizi yako vizuri kwaajili ya kuanza kufanya kazi.

CHANGAMOTO
1.    Uimbali kutoka jumuiya hadi jumuiya kwa baadhi ya jumuiya za maeneo ya tegeta
2.    Ongezeko kubwa la waumini katika misa zote tatu siku ya jumapili ambapo wengine hukosa mahali pa kuketi
3.    Mauhudhurio hafifu hususani kwa wanaume na vijana
4.    Majitoleo hafifu hususani shughuli za maendeleo hasa ujenzi
5.    Ulipaji hafifu wa zaka kama amri ya kanisa.
6.    Kutowajibika ipasavyo kwa viongozi wa jumuiya katika jumuiya zao

MIPANGO YA PAROKIA YA BAADAE
Mipango ya kiimani
Kutembelea kila familia katika parokia
Kutoa semina ili kuimarisha Imani na kuamsha hari katika majitoleo na kusali miongoni mwa waumini
Kuimarisha ulinzi na usalama wa maeneo ya parokia wakati wa ibada na  misa nyakati za usiku.
Kubuni vitega uchumi ngazi ya parokia na vyama vya kitume.

Mipango ya kimaendeleo
>    Kujenga ukuta kuzunguka kanisa
>    Kununua gari la parokia(4wd)
>    Kupata michoro ya ramani mpya ya kanisa .
>    Kuanza ujenzi wa kanisa la parokia
        

JE UNATAFUTA

PAROKIA?

Upate majibu yako haraka zaidi
Ramani ya Parokia
Hakuna ramani kwa sasa...
Kuhusu Kanisa Katoliki

Ofisi ya Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam inapatikana makao makuu ya Jimbo,
Kanisa la St. Joseph, barabara ya Sokoine na Manseld street.

P.O Box 167, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 762 024 199
Email: mawasiliano@waleijimbodaresalaam.org
            darwaleijimbo@yahoo.com
Web: www.waleijimbodaresalaam.org

Kwa Habari kemkem za Kanisa jiunge nasi

Andika email yako hapo juu, na upokee taarifa za H/walei

Copyright © 2025. All Rights reserved by H/Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam