DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA BUGURUNI
HISTORIA YA PAROKIA YA BUGURUNI TOKEA KIGANGO HADI KUWA PAROKIA 1956-2012
PAROKIA YA MT STEFANO
Parokia hii ipo katika Jimbo kuu la dar es salaam. Upande wa mashariki inapakana na Bungoni na Sharifu Shamba, na upande wa Magharibi inapakana na Parokia ya Vingunguti na Tabata, Mpaka wake ni reli iendayo ubungo. Kaskazini inapakana na Parokia ya Tabata na Kigogo ambapo mpaka wake ni mto Msimbazi. Kusini inapakana na reli ya kati iendayo Bara
KUUNDWA KWA KIGANGO
Eneo kilipoundwa kigango Kilimilikiwa na Mzee Masudi. Mnamo mwaka 1956 Walegio maria kutoka Parokia ya Msimbazi walifika katika eneo hilo na kuwakusanya waumini waliokaa katika maeneo hayo ili waweze kusali pamoja , na walikusanyika kwa mzee Petro Joseph Mlongwa .1958 Mzee Mzozimi Mkude na wenzake walibatizwa baada ya kupata mafundisho , na baada ya hapo walianza kusali kwa Mzee Kiliani Matongo aliyekuwa anakaa maeneo hayo lilipo jengwa kanisa na kisha waliamia kwa mzee Zozimi Mkude kwa siku ya jumatatu na jumapili walienda Parokiani msimbazi.
Mnamo mwaka 1959 Kigango cha Buguruni kilianzishwa rasmi kwa juhudi za wana Legio maria waliokuwa wanatembelea nyumba hadi nyumba .1962 Walegio Maria walihamasisha kusali na kujenga kigango cha miti.
Mzee Mzozima Mkude kwa upendo wake mkubwa aliamua kutoa eneo lake bure bila malipo yeyote, na bati zilizoezekwa zilitoka Parokia ya msimbazi.
Na viongozi wa kwanza walikuwa :
a) Mwenyekiti John Mbena,
b) Katibu Victor Kunambi
c) Mweka hazina Zozimi Mkude
d) Rymond Martini kama Mjumbe
e) Kiliani Martini Mjumbe pia.
Baadhi ya wana Legio maria wa Buguruni waliruhusiwa kussali na wenyeji wao kwa sharti la kuto kugonga kengele.
Mwaka 1963 Mzee Zozima na wenzake walikubaliana kutafuta taruma za reli wakalifunga nakuanza kugonga kengele kwa mara ya kwanza kwa nia ya kukutana kusali. Walipata upinzani mkubwa kutoka kwa wenyeji lakini waliendelea kugonga na kusema wanamwomba Mungu kama wao wanavyo kutana na yanayofanyika ni ya Mungu.
UUNDAJI WA JUMUIYA
1972 Kazi iliyo fuata ilikuwa ni uundaji wa jumuiya , Na jumuiya ya kwanza kuundwa ilikuwa ya Mt Stefano. Jumuiya hiyo iliitwa Mt Stefano kwasababu ya upinzani walioupata wa kurushiwa mawe wakati wa kusali. Na jumuiya nyingine zilizoundwa ni :Mt Yohana ,Mt joseph, Mt Paulo, Mt Vicenti, Mt Monika, Mt Teresia, Mt Brigita, Mt Bikira Maria, Mt Yuda Thadei. Jumuiya kumi na saba ziliundwa chini ya Mwenyekiti Mzee Charles Ezekieli Nguvumali.
Jumuiya ya Mt Petro ilibadilishwa jina na kuwa jumuiya ya Mt Filipo, na Mt Stefano likawa jina wa somo wa Kigango.
Walegio Maria walienda Tabata na kufungua jumuiya Tabata kisiwani na baadae jumuiya hiyo ikakua na kupata kigango cha tabata , na sasa ndio parokia ya Kristo mfalme. Hivyo msingi wa Parokia ya Tabata ni Kigango cha Buguruni.
-Mpaka kufikia wakati huu jumuiya zilizopo ni
.
-Idadi ya waumini ni kati ya
-Zipo kanda
UJENZI WA KIGANGO
Kati ya miaka 1980 hadi 1990 jengo la kigango lilianza kuchoka na waumini walihamasishana kujenga kigango kwa kujitolea kama vile kufyatua matofali, kina mama kuchota maji. Ujenzi ulifanywa na Mzee Rafaeli Otieno, Mzee Benedict Kimoko, Petetr Msomba na wengine.
Wako wengine walio jitoa pia kwa namna zao, kwa mfano , Pd Zakayo alitoa mitumba na kuwaaambia waumini wauze ili pesa itakayo patikana iingie katika ujenzi, na katika hilo ziliweza kupatikana kiasi cha shilingi 460 na zilikuwa fedha nyingi kwa wakati huo.
Sambamba na kipindi hichoJumuiya zingine zilianzishwa na kuongeza idadi ya jumuiya zingine ambazo ni Mt Sophia, Mt Petro, Mt Anna , Mt S/Kirene, Mt Antoni wa Padua na Mt Veronika.
UFUNGUZI WA CHEKECHEA 1973
Shule ya chekechea ilifunguliwa 1973 chini ya Mwalimu Victor Kunambi na Zozimi Mkude , Waliweza kuwafundisha watoto wote wakristo na waislamu isipokuwwa wakristo walikuwa na somo la ziada kuhusu Dini. Kutokana na ongezeko kubwa la watoto, wazazi walikaa na Mwenyekiti wa Chama cha wazazi wa wilaya wakati huo Bw Ibrahimu Raha au Mzee Jongo 1076 na kuamua kuhamisha shule ya msingi , Hivyo msingi wa shule y buguruni moto ni kigango cha Buguruni.
Wa legio Maria walienda Vingunguti Miembeni na hapo walimkuta mzee mnyamwezi aitwaye Emanueli ambaye pamoja na dada yake walizungukia watu nyumba kwa nyumba na walifanikiwa kufungua kigango cha miti mwa 1983. Mahali hapo ndipo parokia ya Vingunguti ilipo kwa sasa. Kwa hivy msingi wa parokia ya Vingunguti ni kigango cha Buguruni.
UBATIZO NA NDOA
Kazi kubwa ya kufungua jumuiya , Ubatizo na kuhamasisha watu kufunga ndoa pia ziliendelea.
Kuanzia tarehe 30/11/2003 palianza kusomwa misa moja kila dominika , na 29/ 02 /2004 misa mbili zilianza kusomwa kiila dominika.
UZINDUZI WA VYAMA NA VIKUNDI VYA KITUME
Tar 09/ 05/2005kulikuwa na uzinduzi wa chama cha kitume cha WAWATA , na pia kuna vyama vingine vya kitume ambavyo vilizinduliwa navyo, vyama hivyo ni ;
Utoto mtakatifu, Viwawa, Uwaka , Karismatiki, Legio Maria, Utume wa Fatima, Kwaya(shikwaka), Mt Stefano, Familia takatifu na Upendo wa Moyo mt wa Yesu
UJENZI WA PAROKIA.
Tare 19/02/1999 kulifanyika mkutano wa waumini wote na kuamua kujenga kigango kingine cha pili . wakati waumini wakijiandaa kujenga kigango kingine . 28/08/2000 Paroko wa wakati huo Pd Ambrosi Mosha aliitisha kikao cha viongozi na kuazimia kujenga Parokia na sio kigango, na waumini waliupokea uamuzi huo kwa furaha kubwa. Pd Switbert Masao alipewa Jukumu la kusimamia ujenzi na baadae alikabidhiwa Pd Mathew Masawe ambaye alisimamia shughuli hiyo nzima ya ujenzi kwa sehemu kubwa akishirikiana na kamati ya ujenzi iliyoongozwa na;
Mzee Jordani Mapunda ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti, Deusdedit Maiga kwa upande mwingine akiwa ndio katibu ,Flaviani Magali kama Katibu Msaidizi ,Frediriki Temba Mweka Hazina.
Wengine ni Fortunatus Magina , John Tibrus Asenga, Mr and Mrs Kagaya, Bonifasi Mpaze , Imelda Wakasenyi, Flowingi ngongola,Dr Vicent Tarimo, Bernadeta Mugaya, Dr Josefu Shitundu, John Mayo, Vicent Mayo Rymond Munishi na Salome Mahundi.
Manamo mwaka 2005/09/18, Askofu Method Kilaini alibariki eneo la kanisa. Na tarehe 05/09/2006 Mkataba wa ujenzi ulisainiwa kati ya kampuni iitwayo KOLILA CONSTRACTION na ujenzi kuanza chini ya usimamizi wa ndugu E .Masika
Kazi ya ujenzi ilianza mnamo tarehe 13/09/2006 kwa kuanza kuchimba msingi kwaajili ya ujenzi wa kanisa kuanza. Kazi ya ujenzi iliendelea ikienda sambamba na upanuzi wa eneo la kanisa ambapo nyumba kadhaa zilinunuliwa kwa ushirikiano na waumini wakiongozwa na Padre Mathew Masawe, Pd castor Ngowi Na Pd Floriani.
10/06/2007 Maandamano ya Ekarist Takatifu yalifanyika kwa mara ya kwanza kwenda shule ya msingi Buguruni Moto na maandamano hayo yamekuwa yakiendelea kila mwaka wakati wa sikukuu ya Ekarist Takatifu.
Tarehe 16/09/2007 Ndipo waumini walipoanza kusali ndani ya kanisa kwa mara ya kwanza.
CHANGAMOTO ZILIZOPO KWA SASA
Eneo la kanisa bado limezungukwa na wenyeje ambao kwa namna moja au nyingine sio wakristo wa Roma na tena kwa asilimia kubwa ambayo imepelekea kuwapo kwa changamoto nyingi za kiimani.
Hali kadhalika miundo mbinu bado haijakaa vizuri kwa kadiri inavyo takikana na inahitaji upanuzi wa maeneo ili kukidhi mahitaji , lakini hata hivyo bado changa moto ni kubwa kuweza kuongeza maeneo kwani maeneo hayo bado ni nyumba za watu na wengi wao hawajawa tayari kuhama katika maeneo yao.Hata hivyo juhudi bado zina fanyika kuwashawishi wenyeji.
Waumini wengi ni watu wa kipato cha chini na walio wengi wakiwa wamepanga chumba kimoja kimoja wakichangamana na wenyeji ambao pia wengi wao ni waislamu na madhehebu mengine , hivyo hata uendeshaji wa jumuiya ni mgumu ukilinganisha na maeneo mengine
Wakristo wengi ni wapangaji katika nyumba hivyo huingia na kutoka hivyo baadhi ya jumuiya hazija simama kikamilifu.
Swala la utoaji si baya ukilinganisha na asili ya watu waliopo lakini kwa upande mwingine maendeleo ya kanisa yanasonga mbele.
MIPANGO ILIYOPO KWA SASA 2018, 2019
.
Mipango iliyopo kwa sasa ni kuongeza maeneo kuweza kukidhi mahitaji ya Parokia kwa ujumla ikiwa ni Pamoja na eneo la Barabara ya kutokea, Eneo la maegesho ya magari , na eneo jipya ambapo nyumba ya mapadre itajengwa baada ya iliyopo kwa sasa kubomolewa na kuhamishiwa eneo jingine.
Kuweka miundombinu mingine ya kiulinzi kama CCTV kamera , kuweka Peving Blocks kuzunguka eneo la kanisa , Kuandaa maeneo ya kujenga ofisi mpya na yenye hadhi inayokidhi viwango kwaajili ya baba Paroko, kamati tendaji na vyama vya kitume pale inapobidi kuwa nayo kama eneo litatosheleza.