PAROKIA YA MAKUBURI


PAROKIA YA MWENYEHERI ANWARITE, MAKUBURI

Utangulizi.
Parokia ya Mwenyeheri Anwarite, Makuburi ilianza kama Kigango chini ya  Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Manzese. Msimamizi na Mwombezi wetu ni Mwenyeheri Sista Maria Clementina Anwarite. Siku ya kumbukumbu yake ni tarehe 1 Desemba kila mwaka. Mapadre wa wakati huo walikuwa chini ya Shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers).

Uanzilishi wa Kigango.
Mwaka 1986, jitihada za kutafuta kiwanja cha kujenga Kanisa la Kigango zilifanyika chini ya Paroko wa Parokia ya Manzese, Padre Gerald Chebanon. Baada ya yeye kuondoka ziliendelezwa na Padre Jean-Francois Galtier, Maparoko wasaidizi Padre George Smith na Padre Raymund Echeveria, wakishirikiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei Parokia ya Manzese ndugu Gislar K. Zullu. Katika jitihada hizo tunamshukuru Mungu, kwani Halmashauri ya Jiji ilitupa kiwanja bila malipo yoyote, na baadaye tuliongeza eneo la Kanisa kwa kununua nyumba za majirani.

Uzinduzi wa Kigango.
Tarehe 18/08/1988, Kigango cha Makuburi kilizinduliwa kwa ibada ya misa Takatifu iliyoadhimishwa na Paroko wa Parokia ya Manzese Padre Jean-Francois Galtier. Kigango cha Makuburi kiliendelea kuwa chini ya Parokia ya Manzese kwa miaka 9 (1988-1997).

Parokia Teule.
Tarehe 16/05/1997, Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Baba Mwadhama Polycarp Kardinal Pengo alikiteua Kigango cha Mwenyeheri Anwarite, Makuburi kuwa Parokia Teule ya Makuburi.

Uzinduzi wa Parokia.
Tarehe 02/08/1997,  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alizindua rasmi Parokia ya Mwenyeheri Anwarite Makuburi katika adhimisho la Misa Takatifu, na alimsimika Padre Gerald Derksen kuwa Paroko, na Paroko msaidizi alikuwa Padre Brian Mkude.

Upanuzi wa Kanisa.
Jiwe la msingi la Kanisa liliwekwa rasmi na aliyekuwa Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Mhashamu Baba Askofu Mkuu Francisco Javier Lozzana katika adhimisho la misa takatifu tarehe 01/05/1998. Ujenzi ulikamilika na jiwe la ufunguzi wa Kanisa liliwekwa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo tarehe 12/12/1998.

Parokia ilipo (Jiografia):-
Kata ya Makuburi, wilaya ya Ubungo katika mkoa wa Dar es Salaam.
Katika Dekania ya Ubungo.
Inapakana   na   shule   za   msingi   Mabibo/Makuburi  na  Export  Processing Zone Authority (EPZA).
Parokia yetu inapakana na:-

  • Parokia  ya  Msewe upande wa Kaskazini,  Parokia  ya Kibangu upande  wa  Kaskazini
    Magharibi, Parokia ya  Makoka upande wa Magharibi,   Parokia  ya   Kimanga  upande      
    wa   Kusini  Magharibi,   Parokia  ya  Manzese   upande  wa   Mashariki,   Parokia    ya 
    Luhanga upande wa Kusini Mashariki, Parokia ya Tabata  Kisiwani  upande wa Kusini.
        

Maparoko waliohudumu kuanzia mwaka 1997 hadi sasa 2018.
Padre Gerald Derksen                                     - 1997 - 2006
Padre Nicolaus Pesambili Masamba           - 2006 - 2010
Padre Faustine Mlelwa                                   - 2010 - 2012
Padre Jovin Bakekera                                     - 2012 - hadi sasa 2018

Maparoko wasaidizi waliohudumu kuanzia mwaka 1997 hadi sasa 2018.
Padre Brian Mkude                                       - 1997 - 2000
Padre Ireneus Mbahurila                             - 1999 - 2003
Padre George Sayi                                        - 2000 - 2006
Padre Sixtus Kimaro                                    - 2003 - 2003
Padre Romuald Mukandara                        - 2004 - 2005
Padre Nicolaus Pessambili Masamba      - 2006 - 2006
Padre Gallen Mvungi                                    - 2007 - 2011
Padre James Mweyunge                             - 2009 - 2010
Padre Christian Likoko                                 - 2010 - 2011
Padre Joseph Mapunda                               - 2011 - 2015
Padre Joseph Kazikunema                          - 2015 - 2016
Padre Paschal Kamugisha                          -  2016 - hadi sasa 2018

Kamati tendaji ya Halmashauri ya Walei Kigango cha Makuburi 1988-1997

  • Mwenyekiti            - Ndugu Gislar K. Zullu
  • Makamu Mwenyekiti     - Ndugu Stanslaus S. Kazimoto (Marehemu)
  • Katibu                - Ndugu Peter Felix
  • Katibu Msaidizi       - Katekista John Mwalyenga

Kamati tendaji ya Halmashauri ya Walei Parokia ya Makuburi 1998 - 2001

  • Mwenyekiti                       - Ndugu Gislar K. Zullu
  • Makamu Mwenyekiti      - Ndugu Adrian Mpande (Marehemu)
  • Katibu                               - Ndugu Monica Changamike
  • Katibu Msaidizi               - Ndugu Casmir Massawe
  • Mhazini                            - Ndugu Roman Kavishe (Marehemu)

Kamati tendaji ya Halmashauri ya Walei Parokia ya Makuburi 2001 - 2003

  • Mwenyekiti             - Ndugu Bruno Hinju
  • Makamu Mwenyekiti      - Ndugu Humphrey Lyimo
  • Katibu                 - Ndugu Monica Changamike
  • Katibu Msaidizi        - Ndugu Casmir Massawe
  • Mhazini                - Ndugu Boniface Lesso


Kamati tendaji ya Halmashauri ya Walei Parokia ya Makuburi 2003 - 2006

  • Mwenyekiti             - Ndugu January Kisanko (Marehemu) / Ndugu Lucas Mushi
  • Makamu Mwenyekiti      - Ndugu Edwin Mikongoti / Ndugu Herman Sichalwe (Marehemu)
  • Katibu                 - Ndugu Monica Changamike / Ndugu Buberwa
  • Katibu Msaidizi        - Ndugu Lucian Kikoti
  • Mhazini                - Ndugu Boniface Lesso

Kamati tendaji ya Halmashauri ya Walei Parokia ya Makuburi 2006 - 2009

  • Mwenyekiti             - Ndugu Fortunatus Nzota (Marehemu)
  • Makamu Mwenyekiti      - Ndugu Peter Felix
  • Katibu                 - Ndugu Wilhelmina Malima
  • Katibu Msaidizi        - Ndugu Agino Safari
  • Mhazini                - Ndugu Bonitas Mwaleni


Kamati tendaji ya Halmashauri ya Walei Parokia ya Makuburi 2006 - 2009

  • Mwenyekiti             - Ndugu Fortunatus Nzota (Marehemu)
  • Makamu Mwenyekiti      - Ndugu Peter Felix
  • Katibu                 - Ndugu Wilhelmina Malima
  • Katibu Msaidizi        - Ndugu Agino Safari
  • Mhazini                - Ndugu Bonitas Mwaleni

Kamati tendaji ya Halmashauri ya Walei Parokia ya Makuburi 2010 - 2013

  • Mwenyekiti             - Ndugu Jackson S. Mtoka
  • Makamu Mwenyekiti      - Ndugu Prudence Mgobe
  • Katibu                 - Ndugu John C. Mgaka
  • Katibu Msaidizi        - Ndugu Arodia Ndena
  • Mhazini                - Ndugu Vedastus Namwata


Kamati tendaji ya Halmashauri ya Walei Parokia ya Makuburi 2013 - 2016

  • Mwenyekiti             - Ndugu Jackson S. Mtoka
  • Makamu Mwenyekiti      - Ndugu Herman Sichalwe (Marehemu) / Ndugu Mary J. Kimaro
  • Katibu                 - Ndugu John C. Mgaka
  • Katibu Msaidizi        - Ndugu Felista Sengerere
  • Mhazini                - Ndugu Vedastus Namwata


Kamati tendaji ya Halmashauri ya Walei Parokia ya Makuburi 2016 - mpaka sasa 2018

  • Mwenyekiti             - Ndugu Mary J. Kimaro
  • Makamu Mwenyekiti      - Ndugu Johanes Rwezaula
  • Katibu                 - Ndugu Bernard Mukasa
  • Katibu Msaidizi        - Ndugu Felista Sengerere
  • Mhazini                - Ndugu Vedastus Namwata


Watawa wa kike.
Toka mwaka 1997 mpaka sasa Parokia yetu inahudumiwa na Masista wa Shirika la Bikira Maria Malkia wa Mitume wa Jimbo la Mbeya.

Vigango.
Kwa sasa Parokia haina Kigango, lakini iliwahi kuwa na vigango 7 navyo ni:-

1. Kigango cha Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni - Ubungo Kibangu, tayari ni Parokia tangu mwaka 2000.

2. Kigango cha Mt. Theresia wa Mtoto Yesu - Nzasa, kilihamishiwa Parokia ya Kibangu, tayari ni Parokia tangu mwaka 2015.

3. Kigango cha Mt. Gaudensi - Makoka,  tayari ni Parokia tangu mwaka 2010.

4. Kigango cha Bonyokwa, kwa sasa ni Kigango cha Parokia ya Mt. Gaudens, Makoka.

5. Kigango cha Mt. Monica - Kilungule, kilihamishiwa Parokia ya Kibangu, tayari ni Parokia tangu mwaka 2011.

6. Kigango cha Mt. Yohana Mbatizaji - Luhanga, tayari ni Parokia tangu mwaka 2005.

7. Kigango cha Mt. Padre Pio - Tabata Kisiwani, tayari ni Parokia tangu 2016.

MUUNDO WA UTAWALA WA PAROKIA.

- PAROKO / PAROKO MSAIDIZI

- WATENDAJI
   MAKATEKISTA
   WAAJIRIWA / WAHUDUMU


- WASHAURI
   KAMATI TENDAJI YA HALMASHAURI YA WALEI PAROKIA
   HALMASHAURI YA WALEI PAROKIA

Muundo wa Parokia.
Parokia ina jumla ya kanda 10 nazo ni:-

  1.  Mt. Yohane Paulo XIII - Papa, Relini.
  2. Mt. Anyesi, Mandela.
  3. Mt. Ritha wa Kashia, Ubungo Kisiwani.
  4. Mt. Yohane Mtume na Mwinjili, Ubungo Maziwa.
  5. Mt. Yohane Paulo II - Papa, Makuburi.
  6. Mt. Gregory Mkuu - Papa, Gereji.
  7. Mt. Katarina wa Siena, Mikongeni.
  8. Mt. Theresa wa Kalkutta, Jeshini.
  9. Mt. Mathayo Mtume na Mwinjili, Redio
  10. Mt. Leo Mkuu - Papa, Maji.



Parokia ina jumla ya Jumuiya ndogondo za Kikristo 73.

Parokia ina jumla ya waamini 6,100, kulingana na sensa ya mwaka 2017.

  • Wanawake     - 1,765
  • Wanaume      - 2,014
  • Watoto            - 2,771
    Jumla             - 6,100

Vyama, Mashirika na Jumuiya za Kitume vipo 11.

  • Moyo Mtakatifu wa Yesu.
  • Shirika la Utoto Mtakatifu wa Yesu.
  • Legio Maria
  • Vincent De Paul
  • CPT (Christian Proffesionals of Tanzania)
  • WAWATA (Wanawake Katoliki)
  • UWAKA (Wanaume Katoliki)
  • VIWAWA (Vijana Katoliki)
  • SHIKWAKA   ( Shirikisho  la  Kwaya: -   Mt.  Kizito,   Mwenyeheri   Anwarite  na
       Mt. Cecilia )
  • Kolping
  • Karismatiki Katoliki


Ratiba za Misa.
Dominika kuna Ibada za Misa 4:-
Misa ya 1 inaanza saa 12:00 asubuhi.
Misa ya 2 inaanza saa 1:30 asubuhi.
Misa ya 3 inaanza saa 3:20 asubuhi.
Misa ya 4 inaanza saa 5:00 asubuhi.

Misa za kila siku katika juma:-
Jumatatu - Ijumaa, misa zinaanza saa 12:30-1:00 asubuhi.

Jumamosi misa inaanza saa 1:00-1:30 asubuhi.

Alhamisi misa inaanza saa 10:30-11:00 Jioni.

Kuabudu Ekaristi Takatifu.
Ni kila Alhamisi, inaanza saa 11:00-12:00 jioni.

Ratiba ya Sakramenti ya kitubio.
Jumatatu-Ijumaa, kila baada ya Misa ya juma.
Jumamosi, baada ya Misa ya ndoa.

Sakramenti nyingine.
Zinatolewa kama kawaida kulingana na uhitaji wa waamini.

Saa za Ofisi.
Jumatatu-Ijumaa kuanzia saa 2:00-6:30 mchana - saa 9:00-12:00 jioni.
                                              
Jumamosi kuanzia saa 2:00-6:00 mchana.
Jumatano ofisi zinafungwa.

Huduma za kiroho.
Waamini wanashiriki Misa Takatifu katika Jumuiya ndogondogo za Kikristo na kanda.
Waamini wanapata mafundisho ya Sakramenti mbalimbali.
Waamini wanashiriki maisha ya sala katika Jumuiya ndogondogo za Kikristo.
Waamini wanashiriki Misa Takatifu siku za juma na Dominika.
Waamini wanashiriki Ibada mbalimbali hapa Parokiani (Kuabudu Ekaristi Takatifu, kusali Rozari, n.k.)
Waamini wanashiriki semina  na mafungo mbalimbali.
Waamini wamejiunga kwenye Vyama, Mashirika na Jumuiya za Kitume ili kukuza Imani.
Wanaparokia wanashiriki Hija mbalimbali.
Kutembelea wagonjwa na wazee wanaoshindwa kufika Parokiani.
Timu ya Uinjilishaji inatembelea jumuiya na kanda zote ili kukuza imani.

Huduma za kimwili.
CHEMA (Chuo cha Elimu ya Maisha): Shule hii inatoa elimu ya msingi kwa mpango wa MEMKWA kwa watoto/vijana walioshindwa kujiunga na elimu ya msingi wakiwa na umri mdogo na ambao wanaishi katika mazingira magumu (wahitaji). Inapokea vijana wa jinsia zote, madhehebu yote na dini zote.
Kupitia Parokia, wanaparokia waliohitaji bima ya afya wanazo kadi za bima ya afya kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
VICOBA kwa wakina mama.

Tunda la Kanisa.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupatia Padre Denis Ananias Wigira,ambaye ni  mzawa wa Parokia hii.

Changamoto.
Eneo dogo la Parokia yetu, hivyo tuko kwenye mkakati wa kununua nyumba za majirani ili kuongeza eneo.
Wanaparokia wengi ni wapangaji, hivyo ni ngumu kuwa na idadi kamili ya wanaparokia na kila mara tunafanya uchaguzi mdogo kuziba nafasi za viongozi wanapohama.

Hitimisho.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa mema yote aliyotujalia mpaka tumefika hapa tulipo na tunamuomba azidi kutujalia ili tusonge mbele zaidi kulijenga Kanisa lake. Mwenyeheri Anwarite msimamizi na mwombezi wetu utuombee.

          

JE UNATAFUTA

PAROKIA?

Upate majibu yako haraka zaidi
Ramani ya Parokia
Hakuna ramani kwa sasa...
Kuhusu Kanisa Katoliki

Ofisi ya Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam inapatikana makao makuu ya Jimbo,
Kanisa la St. Joseph, barabara ya Sokoine na Manseld street.

P.O Box 167, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 762 024 199
Email: mawasiliano@waleijimbodaresalaam.org
            darwaleijimbo@yahoo.com
Web: www.waleijimbodaresalaam.org

Kwa Habari kemkem za Kanisa jiunge nasi

Andika email yako hapo juu, na upokee taarifa za H/walei

Copyright © 2025. All Rights reserved by H/Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam