PAROKIA YA UBUNGO



PAROKO: FR. CASIMIRO TORRES, IMC (+255 757 245 251)
PAROKO MSAIDIZI: FR. GERVAS LYIMO, IMC (+255 759 350 036)
PAROKO MSAIDIZI: FR. ANDRÉ NZUZI (+255 746 443 442)
Website: http://parokiamsewe.or.tz/
Email: info@parokiamsewe.or.tz


HISTORIA YA PAROKIA YA MT. PAULO MTUME
UBUNGO MSEWE

Mnamo mwaka 1968 aliyekuwa Paroko wa Magomeni Padre Oswin (Cap) alianzisha Kigango cha Ubungo Msewe. Katika kipindi hicho waamini wachache walisali chini ya mti wa mkorosho, eneo ambalo kwa sasa kuna nyumba ya WAWATA hapa Ubungo Msewe. Kwa msaada wa Chifu G.P Kunambi, Balozi Richard Wambura alitoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa. Mwadhama Kardinali Lauriani Rungambwa aliwakaribisha Mapadre wa shirika la Consolata kuja kuanzisha jengo la Kanisa ambalo kwa sasa linatumika kama ukumbi mdogo wa Parokia.
Mnamo tarehe 18 Machi 1973, Ubungo Msewe ilipewa hadhi ya kuwa Parokia. Paroko wa kwanza alikuwa Padre Igino Lumetti akisaidiwa na Padre Romano Motter na Mwenyekiti wa kwanza wa HW Parokia alikuwa Chifu G.P Kunambi. Hawa walifanya kazi kubwa ya kujenga nyumba ya Mapdre. Mnamo tarehe 1 Februari 1973, Kigango cha Mavurunza walianza kupata huduma baada ya kupata Paroko mpya Mario Biestra.

Kanisa la sasa la Msewe lilianza kujengwa tarehe 9 Agosti 1976 na kutabarukiwa na Mwadhama Kardinali Laurian Rugambwa tarehe 15 Februari 1978. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa shirika la Consolata na Serikali iliwakilishwa na Mwalimu Julius K. Nyerere. Mnamo tarehe 19 Julai 1978, Padre Romano Motter aliteuliwa kuwa Paroko wa Ubungo Msewe.
Mnamo terehe 28 Desemba 1980 Kigango cha Makoka na Makabe vilibarikiwa. Na tarehe 29 Aprili 1984, Kigango cha Mbezi Luis kilibarikiwa.

Terehe 23 Februari 1983 Padre Ricardo Ossola alikuja kama Paroko Msaidizi na hapo Kigango cha Kimara kikaanza kupata huduma.

Baruti kama Kigonga kilizinduliwa tarehe 9 Septemba 2003, na Altare kutabarukiwa na Mhashamu Askofu Eusebius Nzigilwa mnamo tarehe 6 Julai 2012. Kigango cha Baruti kilitangazwa na Baba Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kuwa Parokia Teule mnamo tarehe 7 Julai 2018.

Parokia ya Ubungo Msewe kwa sasa ina Kigango kimoja tu, nacho ni Golani kilichozinduliwa tarehe 28 Agosti 2011. Kwa sasa waamini wanaendelea na ujenzi wa Kanisa.

Parokia ya Ubngo Msewe ina jumla ya Kanda tano (5) na jumla ya Jumuiya Ndogondogo sabini (40) zenye waamini wapatao 3,626 na familia 806 (kwa mujibu wa takwimu za sensa ya Wakatoliki ya 2016 – Parokia ya Ubungo Msewe).
Mnamo tarehe 12 Mei 2002, walikuja Masista wa Moyo Safi wa Maria kutoka India na kwa sasa wanaendesha huduma za Hospitali na shule ya elimu ya msingi hapa Msewe.

JE UNATAFUTA

PAROKIA?

Upate majibu yako haraka zaidi
Ramani ya Parokia
Hakuna ramani kwa sasa...
Kuhusu Kanisa Katoliki

Ofisi ya Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam inapatikana makao makuu ya Jimbo,
Kanisa la St. Joseph, barabara ya Sokoine na Manseld street.

P.O Box 167, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 762 024 199
Email: mawasiliano@waleijimbodaresalaam.org
            darwaleijimbo@yahoo.com
Web: www.waleijimbodaresalaam.org

Kwa Habari kemkem za Kanisa jiunge nasi

Andika email yako hapo juu, na upokee taarifa za H/walei

Copyright © 2025. All Rights reserved by H/Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam