PAROKIA YA CHANGANYIKENI



MAMBO YA JUMLA YA PAROKIA
Jina la parokia ni “UTATU MTAKATIFU” Changanyikeni
              -Msimamizi wa parokia UTATU MTAKATIFU.
             - Jina halifanani na parokia nyingine jimbo la Dar es salaam

Mahali parokia ilipo ni Changanyikeni
Kijiografia; Parokia inapakana na parokia nyingine ambazo ni parokia ya chuo kikuu cha Dar es salaam, parokia ya Msewe na parokia ya makongo
Parokia ipo katika Dekania ya Ubungo Dar es salaam.

Idadi ya waumini katika parokia ni kati ya waumini 6000 na imepatikana kwa njia ya sense iliyofanyika 2016 kwa waumini kujaza fomu maalumu.

Sensa ilifanyika kwa kupitia JNNK , na sense nyingine itafanyika 2018

Parokia haina vigango
Parokia ina kanda (3) ambazo zimegawanyika kijiografia.
a)    Kanda ya mtakatifu Paulo mtume ilioko eneo linalozunguka parokia ambapo pia kuna shule ya msingi  changanyikeni na shule ya secondary ya white lake, kanda hii ina jumuiya 9
b)    Kanda yam t maximiliani Kolbe iliyoko changanyikeni kati kanda hii ina jNNK 9
c)    Kanda yam t Fidea, iliyoko mbuyuni kanda hii inajumuiya 6

Kila jumuiya ina kaya kati ya 7-15

Jumuiya zinasali mara moja kila siku ya jumamosi kuanzia saa 12:30 kwa kufuata mwongozo wa jumuiya ndogo ndogo toka Jimboni

Kanda hua wanasali mara moja kila baada ya miezi miwili

Maudhuri kwa jumla katika JNNK ni ya wastani, na maudhurio huwekwa katika kumbukumbu.

Upo pia utaratibuwa kuzitembelea  JNNK , Kanda na pia misa zinasomwa.

Kanada, JNNK hua zinaadhimisha Misa takatifu za somo wa jumuiya na kanda kila baada ya mwaka mmoja.

Uongozi wa jumuiya umekamilika na pale ambapo inapotokea kuna mapungufu yanajazwa mara moja kwa kuitisha uchaguzi mdogo.

Halmashauri ya walei ya parokia /kanda hukutana mara chache

Huduma za kiroho na jamii hufanywa na jumuiya , hii ni pamoja na huduma za masakramenti kwa wanajumuiya  mfano;Ndoa, mpako wa wagonjwa, kipaimara, na pia matendo ya huruma kwa kutembelea wagonjwa na wenye shida mbali mbali.

Changa moto kubwa ni maudhurio ya waumini katika sala na matukio au matendo ya huruma yanapofanyika , lakini changamoto nyingine kubwa ni maudhurio duni ya wanaume na vijana

UONGOZI
Kamati tendaji ipo na imekamilika kikatiba

Kamati tendaji ya parokia hukutana mara moja kila mwezi siku za jumamosi na kikao kinachukua muda wa saa moja kujadili .Baba paroko ni mshiriki katika kikao hicho.

Halmashauri ya walei ya parokia inaundwa na viongozi watano wa kila jumuiya pamoja na wenyeviti wa vyama vya kitume na inakutana mara moja kila baada ya miezi miwili.

Agenda na taarifa za vikao zinapatikana kwa wakati na zinatunwa.

Parokia haijawa na ofisi za halmashauri ya walei ya parokia , lakini mipango ipo ya kuwa na ofisi na vitendea kazi,ofisi inaandaliwa na itakamilika hivi karibuni

Njia za mawasiliano kwa wajumbe wa kamati Tendaji pamoja na halmashauri ya walei ni :

Kwa njia ya barua pepe(yaani E mail) simu,Whats aap, lakini zaidi ya hapo ni kwa matangazo kanisani.

Anuani ya barua pepe yaani E mail ya parokia ni; changanyikeniutatumtakatifu@gmail.com

Zipo kamati ndogo ndogo za kikatiba na zimekamilika,

kamati hizo hua zinakutana mara mara.

Zipo kamati zingine Ambazo sio za kikatiba na zinaripoti kwa kamati tendaji ya parokia, kamati hizi ni kama zifuatazo:
a)    Kamati ya ujenzi
b)    Kamati ya ulinzi na usalama
Ipo kalenda ya matukio ya mwaka ya kiparokia amabayo imetengenezwa kwa ushirikishwaji waumini
Waamini wanaarifiwa mipango ya parokia kwa kupitia maatangazo kanisani , pia kupitia JNNK kupita halmashauri ya walei ya parokia
VYAMA MASHIRIKA NA JUMUIYA ZA KITUME (VMJ)
Vipo vyama vya kitume 8 kama ifuatavyo
1.    WAWATA,
2.    UWAKA
3.    VIWAWA,
4.    Utoto mtakatifu
5.    Shikwaka
6.    Watumishi wa altare
7.    Regio Maria
8.    Moyo Mtakatifu wa yesu

Vyama hivi havina watumishi wa kutosha na havikidhi mahitaji ya parokia

Vyama na vikundi vya kitume vinafanya kazi kulingana na katiba ya halmashauri ya walei ya jimbo.na vyama vyote hivi viko hai

Vyama hivi havina ofisi parokiani, lakini vinalelewa na vipo chini ya uongozi wa parokia

VMJ vinatoa taarifa na repoti pamoja na ya fedha  mara kwa mara kwa uongozi wa parokia

Na pia vinajitegemea na viko chini ya uangalizi wa parokia

Vyama vina ushirikiano mzuri katika dekania na katika ngazi ya jimbo

VMJ havijafanya mambo maalumu ambayo yanaweza kuigwa na parokia nyingine

SEMINA MBALIMBALI KATIKA UENDELEVU WA IMANI, UONGOZI NA UTEGEMEZAJI
Kuna semina za kijumuiya ambazo zimeshafanyika ,lakini kwa sasa mipango inaandaliwa ili semina nyingine ziweze kufanyika

Kamati ya walei parokia ilishapatiwa semina ya uongozi na mkurugenzi wa utume wa walei jimbo , lakini bado semina zingine zinahitajika kwaajili ya jumuiya.

Semina za kiroho hazijaanza kufanyika bado

Hali ya Imani kwa ujumla inaridhisha, na inatakiwa kuendelezwa kwa nguvu

Kimsingi hali ya utoaji parokiani pia si nzuri bali inaridhisha.

Hali kadhalika utoaji wa zaka kama amri ya kanisa haziridhishi.

Parikia inatoa michango ya jimbo kamili kama inavyo paswa

FEDHA NA MIPANGO
Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa jimbo

Mapato na matumizi ya parokia yanajulikana kwa waumini na yanatolewa taarifa mara nne kwa mwaka

Matoleo ya kila dominika yanatangazwa kwa waumini kila dominika inayofuata

Fedha zote zinazokusanywa hupelekwa benki kwa wakati

ULINZI NA USALAMA
Hali ya ulinzi na usalama parokiani ni ya kuridhisha, na ulinzi unafanywa na kampuni binafsi

MAENDELEO YA KIUCHUMI
Parokia haijawa na miradi yake kwa sasa
Kwa sasa kuna mipango ya uendelezaji wa ujenzi  wa kanisa ambao unaendelea vizuri

MAMBO YA JUMLA
Parokia haina mgogoro wowote wa kimipaka

Kwa sasa parokia haina mipango yeyote ya kuwaendeleza waumini wake kiuchumi isipokuwa kwa kadiri parokia inavyokuwa  itafanya juu chini mipango hiyo iwepo

Idadi ya mapadre na watawa hawatoshelezi

Parokia haina wanasemiari kwa ujumla

Ipo pia historia ya parokia pindi itakapohitajika





JE UNATAFUTA

PAROKIA?

Upate majibu yako haraka zaidi
Ramani ya Parokia
Hakuna ramani kwa sasa...
Kuhusu Kanisa Katoliki

Ofisi ya Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam inapatikana makao makuu ya Jimbo,
Kanisa la St. Joseph, barabara ya Sokoine na Manseld street.

P.O Box 167, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 762 024 199
Email: mawasiliano@waleijimbodaresalaam.org
            darwaleijimbo@yahoo.com
Web: www.waleijimbodaresalaam.org

Kwa Habari kemkem za Kanisa jiunge nasi

Andika email yako hapo juu, na upokee taarifa za H/walei

Copyright © 2025. All Rights reserved by H/Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam