PAROKIA YA MARIA MT. KIMARA


PAROKIA YA MARIA MTAKATIFU KIMARA
Jina la parokia ya Maria Mtakatifu haliingiliani na jina la parokia nyingine

KIJIOGRAFIA
Parokia ipo Kimara katika Dekania ya ubungo Dar es laam, Ramani ya Parokia ipo na inaeleza mipaka ipasavyo.
Idadi ya waumini ni kati ya 5200 hii ni kutokana na sense iliyo fanyika 2017 ambapo kwa mara ya mwishi imefanyika 2017

VIGANGO
Parokia ilikuwa na vigango viwili hapo awali yaani –Michungwani na Kimara mtoni. Ijapo kwamba baadae vigango hivi vilipata hadhi ya kuwa parokia.
Michungwani walikuwa parokia 2015 na kimara mtoni kupata hadhi ya kuwa parokia 2017.

KANDA
Parokia ya Maria Mt Kimara ina jumla ya kanda 7 na 4 kwenye kigango cha korogwe na majina yanayo tumika katika kanda na JNN ni majina ya watakatifu

JNNK
Jumuiya ndogo ndogo zipo 60, na kila moja inatumia jina la mtakatifu au jina la sifa mojawapo mfano: Kristo mchungaji mwema, mototo yesu, Bikira maria wa msaada wa daima n.k
Uongozi katika jumuiya umekamilika na viongozi wake wamechaguliwa kwa mujibu wa katiba

KAYA
Wastani wa kaya katika kila jumuiya ni kati ya 15-25, lakini kwa baadhi ya jumuiya kaya ni mtu mmoja haswa vijana

MAUDHURIO
Maudhurio siyo ya kuridhisha haswa kwa upande wa kina baba na kina mama mfano wakina mama wanaofanya biashara za samaki wanashindwa kuudhuria siku za jumamosi

HUDUMA ZA KIROHO
Huduma za kiroho zinatolewa kwa maombi kwa waumini walio thibitishwa, na huduma zitolewazo ni kama;
•    Kutoa sacrament mbalimbali
•    Kuombea wagonjwa
•    Kutembelea waumini katika JNN
•    Huduma za mazishi
•    Kutembelea familia zenye migogoro na kutafuta ufumbuzi
•    Kuendesha ibada za misa katika JNN has katika kipindi cha kuadhimisha somo wa jumuiya pamoja na ibada zinazoendeshwa kila siku za dominika

UONGOZI
Kamati tendaji ya parokia ipo na imekamilika.
Mikutano ya kamati tendaji hufanyika mara moja kwa mwezi ambapo ni kila jumatano ya kwanza ya mwezi.

MIKUTANO YA HALMASHAURI YA WALEI PAROKIA
Wajumbe ni viongozi watano wa JNN na kanda, kamati tendaji na wenyeviti wa vyama parokia. Zipo jumuiya 60 na kanda 9
-Mikutano inafanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu baada ya misa ya tatu
-Ajenda na kumbukumbu zinapatikana kwa wakati na zinatunzwa.
-Hakuna ofisi ya walei Parokini wala kumbi za mikutano, Bomoa bomoa ya kanisa inamaanisha hata eneo la ibada itakua ni tatizo.

NJIA ZA MAWASILIANO
Njia za mawasiliano zinazo tumika ni kama zifuatazo:
Simu , Barua pepe au E mail, Matangazo ya kila dominika, Barua na uwasilishaji wa mdomo.

KAMATI
Parokia inakamati 11, zipo za kikatiba na zisizo za kikatiba
Kamati za kikatiba ni kama zifuatazo: Familia, Liturjia,Haki na Amani, Elimu ya dini na thiolojia, Fedha na mipango na  mwisho ni afya na mazingira.
Kamati zisizo za kikatiba. Kamati ya ujenzi, Ardhi, Sherehe,Miito, Ulinzi na usalama.
Taarifa za kamaati zinaripotiwa kwa kamati tendaji na halmashauri ya walei ya kupitia kamati tendaji
-Parokia ina kalenda ya matukio ya mwaka kiparokia. Mambo yanayo bebwa ni pamoja na kanisa kuwa kigango , kubadilika kuwa parokia n.k

VYAMA MASHIRIKA NA JUMUIYA ZA KITUME (VMJ )
Viko vyama vine vya Kitume yaani UWAKA, WAWATA, VIWAWA na utoto mtakatifu. Vyama sita  ni vya hiari yaani Moyo mtakatifu wa yesu, st Vicent, SHIKWAKA, Karismatiki, Neo katekuminato na utume wa Fatima
Vyama vya waamini wote vina idadi ya kuutosha lakini vyama vingi vya hiari vinawachama wachache. Vyama vyenye wanachama wengi ni karismatiki na neo katekuminato
-Vyama vyote vinafanya kazi kwa mujibu wa katiba
Uhai ni wa kuridhisha kwa baadhi ya vyama, lanini vyama vingi vinahitaji wanachama wapya hasa vijana, waliopo wengi katika vyama kama moyo mt Yesu na utume wa Fatima ni wazee na pia wako wachache.

OFISI ZA VMJ:
-Parokia ina majengo mawili tu, kanissa na nyumba ya mapadre. Lakini katika mkakati wa kujenga kituo cha maendeleo utajumuisha kumbi za mikutano na ofisi za ‘parokia kutokana na swa la kubomolewa sehemu ya kanisa.
-VMJ huwasilisha taarifa fupi kwenye kila mkutano wa halmashauri walei.

CHANGAMOTO
    Kesi za ardhi ambayo kimsingi ipo mahakamani kati ya kanisa na Tanganyika packers ltd
    Hati ya kubomolewa kanisa

USHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA DEKANIA/JIMBO.
Ushiriki upo wa kuridhisha katika baadhi ya vyama hususani vile vya waumini wote, lakini ushiriki kaatika vyama vya hiari ni mdogo sana na wakusuasua.

SEMINA MBALIMBALI KATIKA KUENDELEZA IMANI,UONGOZI NA UTEGEMEZAJI
-Zinaandaliwa semina na mafungo  kwaajili ya vyama vine vya waumini wote katika ngazi ya parokia na dekania mara kwa mara, Parokia inaashiriki pia katika katika maatukio yanayoandaliwa kiparokia, na kidekania.

SEMINA ZA UONGOZI WA PAAROKIA
-Viongozi wanapatiwa semina za kutosha zinazoandaliwa na parokia yenyewe na jimbo
-Semina za kiroho hua zinafanyika mara kwa mara, lakini mwakahuu hazikuweza kufanyika kutokana na matatizo yanayoikabili parokia  katika kipindi cha miezi sita.

HALI YA IMANI
Hali ya Imani imeimarika

HALI YA UTOAJI
Sadaka: hali ya utoa ni nzuri
Zaka: mwitikio ni mzuri, na  parokia inatoa  michango ya jimbo kikamilifu.


MPANGO WA FEDHA
Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa za jimbo
Waumini wanapewa taarifa za mapato na matumizi kila mwisho wa mwezi kanisani kupitia halmashauri ya walei
Matoleo ya kila dominika hutolewa na kutangazwa kila dominika inayo fuata.
Fedha zote zinapelekwa benki kwa wakati kwa utaratibu maalumu

ULINZI NA USALAMA
kuimarisha ulinzi na usalama ni ngumu na pia ni changamoto kutokana na kwamba barabara inapita katikati ya majengo ya kanisa  na nyumba ya mapadre
parokia imeajiri walinzi binafsi

MAENDELEO YA KIUCHUMI
Upo mradi wa wa ujenzi wa kituo cha maendele ambao kwa sasa umesimama kutokana na swala la ubomoaji wa sehemu ya kanisa.
lipo pia wazo la kuanzishwa mradi wa utengenezaji sabuni
Parokia imeshinda pia kesi kuhusu miliki halali ya kiwanja no- 31 kimara na zipo changamoto za utekelezaji wa amri hiyo kazi ambayo itafanyika mara baada ya kupata amri ya mahakama kwa maandishi na maamuzi ya muhadhama kama askofu mkuu wa jimbo kuu la Dar es salaam.
Parokia inamiliki viwanja viwili, Matosa na vingine Visiga.Jimbo limejulishwa viuzwe ilimradi mapato yatumike katika malengo yaliyo kusudiwa

MAPADRE/WATAWA
Parokia ina Padre mmoja  kwa takribani miezi mitano sasa tangu paroko msaidizi  Fr Chukwemeka alipohamishwa mwanza
Parokia in watawa (Masista):
     Shirika la  Mt Charles wa boromeo
     Shirika la wabenediktini st Agnes kutoka chipole Songea , kwa idadi wapo sita
     Idadi ya waumini watawa waliojiunga nan a utawa  ni Padre 1 na masista 2

Parokia ina wanafunzi 18 seminarini wanaotoke parokia ya kimara

Historia ya kanisa
Yapo maandiko ya historia ya parokia ambayo yapo katika jalada la maswala ya ardhi ambayo yanakesi mahakamani , na pia yapo maelezo katika risala maalumu za siku zilizo pita, Hali kadhalika picha za miradi zipo.  Pia utoto mt wamerekodi kanda zinazoonyesha  sura ya parokia   kwa kiasi Fulani.

JE UNATAFUTA

PAROKIA?

Upate majibu yako haraka zaidi
Ramani ya Parokia
Hakuna ramani kwa sasa...
Kuhusu Kanisa Katoliki

Ofisi ya Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam inapatikana makao makuu ya Jimbo,
Kanisa la St. Joseph, barabara ya Sokoine na Manseld street.

P.O Box 167, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 762 024 199
Email: mawasiliano@waleijimbodaresalaam.org
            darwaleijimbo@yahoo.com
Web: www.waleijimbodaresalaam.org

Kwa Habari kemkem za Kanisa jiunge nasi

Andika email yako hapo juu, na upokee taarifa za H/walei

Copyright © 2025. All Rights reserved by H/Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam