PAROKIA YA MT AMBROSE TAGASTE

n/a


A:MAMBO YA JUMLA YA PAROKIA
Jina la parokia Mt ambrose na haliingiliani na parokia nyingine za jimbo

Kijiografia
Parokia inapatikana katika mtaa wa kimara B kata ya saranga
Kaskazini-bikira maria mama wa huruma
Kusini-Temboni St Augustino
Mashariki-Bikira maria mkingiwa dhambi ya asili mavurunza
Magharibi-Teresia motto yesu mbezi

Parokia hii inapatikana katika Dekania ya Mt Monika Kibaha

Parokia inawaumini wapatao 3457 hii ni kwa mujibu wa sense ya waumini iliyofanyika feb 2017

Sensa ya mara ya mwisho inatarajiwa kufanyika tena 2019

Parokia ya mt Ambrose ina kigango kimoja ambacho ni Mt Monika Matosa.

Parokia inajumla ya kanda nne ambazo zimegawanyika kulingana na mipaka ya barabara.

kila kanda inawastani wa jumuiya (5).

Uongozi katika kanda umetokana na katiba ya halmashauri ya walei jimbo

Kanda nane zimepata majina ya watakatifu

Zipo pia jumuiya ndogo ndogo 40 na jumuiya zote zinatumia majina ya watakatifu

Kila jumuiya ina wastani wa kaya 15-20 na zinaonyesha kufanya vyema hazihitaji maboresho

Jumuiya za kikanda zinasali mara moja kwa mwezi kwa jumamosi ya mwisho ya mwezi, na muda ni saa 12:30 asubuhi.

Mwongozo unaotumika ni ule wa sala za jumuiya za asubuhi.

Maudhurio kwa jumuiya yanaridhisha lakini kwa kanda hayaridhishi. Wawumini wanahitaji kuhamasishwa zaidi

Kamati tendaji ya parokia inawajibika  kuzitembelea jumuiya za  kanda zao.

Jumuiya hufanya maadhimisho ya  misa kwaajili ya  mtakatifu wa somo wa somo wa jumuiya husika.

Uongozi katika jumuiya na kanda umekamilika bila mapungufu.

Uongozi wa halmashauri za jumuiya na kanda hukutana kila baada ya miezi mitatu.

Huduma za kiroho na kuombea wagonjwa hufanyika kila alhamisi kwa kutembelea waumini ikiwa ni pamoja na kutoa mpako wa wagonjwa.

Zipo kanda nane (8) nazo ni Mt Monika matosa, Mt monika namanga,, Mt ambrose, mt  Anna, kanda ya mbezi matosa, Mt clara, Mt caroli luhanga

B:UONGOZI
Kamati tendaji ya parokia ipo na imekamilika

Kamati tendaji hukutana mara moja kila mwezi siku ya jumapili baada ya misa ya kwanza baba paroko na msaidizi wake wakiwepo.

Halmashauri ya walei parokia huundwa na
a.    kamati tendaji ya parokia,
b.    viongozi watano kutoka kila jumuiya ,
c.    Kamati tendanji ya kigango ,
d.    wenyeviti kutoka vyama vya kitume ngazi ya parokia pamoja na
e.     wenyeviti wa ujenzi parokia na kigango

Jumla ya wajumbe wanokutana ni 34 wnaokutana mara nne kwa mwaka.

Ajenda za vikao husika hupatikana kwa wakati  na kutunzwa

Halmashauri ya walei parokia kwa sasa haina ofisi hali kadhalika vitendea kazi.

Mawasiliano kati ya kamati tendaji na wajumbe hufanyika kwa njia ya simu na mitandao ya kijamii kama vile Whatsaa groups, Barua pepe yaani E mail, na njia nyingine ni matangazo yanayotolewa kanisani.

Kamati ndondogo za kikatiba zipo na zimekamilika

Kamati zisizo za kikatiba zipo na hukutana mara kawa mara, kamati hizo ni ;
-Kamati  ya ujenzi,
-Kamati ya ardhi na - kamati ya ulinzi na usalama.

Kamati zinafanya kazi kwa mujibu wa katiba

Kamati zote za kikatiba na zisizo za kikatiba zinaripoti kwa kamati tendaji ya parokia

Kamati hizi zinafanya kazi kwa umakinifu na mawasiliano lakini hakuna maingiliano katika utendaji

Dira mikakati malengo ya parokia vipo kupitia kamati ya fedha na mipango na maazimio ya utekelezaji yanapitishwa na mikutano ya halmashauri ya walei parokia.

Kalenda ya matukio ya kiparokia ipo

Njia zinazotumika kuwaarifu waumini kuhusu mipango ya paarokia ni kwa kupitia :
a.    Matangazo ya siku za dominika
b.    Mikutano ya halmashauri ya walei ya parokia.
c.    Viongozi kuongea na waumini kanisa
d.    Viongozi kutembelea jumuiya na kueleza jamabo husika.

Vyama mashirika na jumuiya za kitume (VMJ)

Vyama mashirika na jumuiya za kitume vipo na vina fanya kazi zake za kitume kama kawaida, vyama hivi vipo 11
-wawata,uwaka,Utoto mtakatifu,Regio maria, Viwawa. Na watumishi wa altare

Baadhi ya vyama hivu havina wanachama wa kutosha , lakini baadhi vina wanachama wa kutosha ,Wastaafu,moyo mt wa yesu, Karismatiki, St vicent, mt Rita.

Vyama vya vikundi  hivi vya kitume hufanya kazi kulingana na katiba ya halmashauri ya   walei na kutimiza wito wa kitume

Uhai wa vyama hivi ni wa wastani

VMJ havina ofisi kwa sasa parokiani wala vifaa kuwwezza kukidhi mahitaji katika kufanya shughuli zake za kiofisi.

Vyama hivi hulelewa na paroko ambaye ndiye mlezi kwa sasa

VMJ hutoa taarifa au ripoti (pamaoja nay a fedha) mara kwa mara katika uongozi wa kamati tendaji

Ushirikiano na ushiriki wa VMJ katika shughuli za kidekania na jimbo uko vizuri.

SEMINA MBALIMBALI KATIKA UENDELEZI WA IMANI  UONGOZI NA UTEGEMEZAJI
Ziko semina za kijumuiya ambazo zimesha fanyika,lakini pia kwa sasa zipo semina nyingine ambazo zinzandaliwa parokia zifanyike.

Kamati tendaji ya parokia ilisha patiwa semina ya uongozi

Hali ya Imani kwwa sasa ni nzuri lakini baado juhudi Zaidi zinahitajika ili kuimarisha ustawi wa kiimani.

Swala la utoaji si zuri sana lakini lina ridhisha kwa kiasi Fulani.

Utoaji zaka kama amri ya kanisa una suasua

Parokia inatoa michango kwajimbo kikamilifu na kwa wakati jinsi inavyo paswa.

FEDHA NA MIPANGO
Parokia inatumia mpango wa fedha wa jimbo

Parokia huwajulisha waumini mapato na matumizi kwa kuwasomea taarifa ya fedha mara nne kwa mwaka.

Matoleo ya kila dominika hutangazwa kwa waumini kila dominika inayofuata

Fedha za parokia hupelekwa benki kwa wakati

ULINZI NA USALAMA.
Hali ya ulinzi na usalama katika parokia ni nzuri.

Walinzi wanaotumika ni kutoka kampuni binafsi.

MAENDELEO YA KIUCHUMI
Hakuna shughuli za miradi.

Kwa sasa kuna maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya mapadre na kanisa la kudumu kigangoni.

MAMBO YA JUMLA
Parokia kwa sasa haina migogoro ya mipaka yake.

Kwa sasa parokia haina mpango makhususi wa kuwaendeleza waumini wake kiuchumi isipokuwa kadiri parokia inavyoendelea kukua itafanya juu chini mipango hiyo iwepo.

Idadi ya mapaadre /watawa haitoshelezi.

Ipo historia ya parokia pale itakapo hitajika.


JE UNATAFUTA

PAROKIA?

Upate majibu yako haraka zaidi
Ramani ya Parokia
Hakuna ramani kwa sasa...
Kuhusu Kanisa Katoliki

Ofisi ya Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam inapatikana makao makuu ya Jimbo,
Kanisa la St. Joseph, barabara ya Sokoine na Manseld street.

P.O Box 167, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 762 024 199
Email: mawasiliano@waleijimbodaresalaam.org
            darwaleijimbo@yahoo.com
Web: www.waleijimbodaresalaam.org

Kwa Habari kemkem za Kanisa jiunge nasi

Andika email yako hapo juu, na upokee taarifa za H/walei

Copyright © 2025. All Rights reserved by H/Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam