DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA MT MONIKA KILUNGULE
Parokia ipo kimara kilungule , kusini inapakana na parokia ya kibangu na parokia kimara baruti,kaskazini inapakana na parokia ya kimara mtoni, Mashariki inapakana na parokia ya makakoka, na magharibi inapakaana na kanisa la kkt korogwe na parokia ya kimara.
Parokia hii ipo katika dekania ya Ubungo
Idadi ya waumini ni 4,000 amayo imepatikan kwa kufanya sense mwaka 2012 na idadi inatarajiwa kuongezeka Zaidi hadi kufikia 2017-18
Kuna kigango kimoja cha mtakatifu Salome
Parokia ina kanda kumi ambazo zimegawanyika kutokana na mipaka asilia mfano Barabara, Kila kanda ina wastani wa jumuiya tano, na uongozi wake umepatikana kutokana na uchaguzi. Kanada zote zinaatumia majina ya Watakatifu.
Kuna jumuiya ndogo ndogo 51 na zinatumia majina ya watakatifu, na kila jumuiya ina kaya kati ya 15-20, na jumuiya zinakutana na kusali mara moja kila wiki siku za jumamosi
Maudhurio ni mazuri kwa akina mama na watoto lakini kwa akina baba na vijana iko changamoto kubwa katika ushiriki wa JNN
Jumiya na kanda zinaadhimisha siku ya somo wakepale wakati unapo fika kufanya hiyo
Jumuiya zinasali maramoja katika wiki siku ya jumamosi. Kwwa upande wa kanda, siku ya kusali ni jumamaosi ya mwanzo wa mwezi.
Mpango wa kuwatembelea waumini katika JNNK/Kanda na Mitaa upon a unaendelea. Viongozi wa jumuiya wanashiriki wakisaidiana na Mapadre kutembelea nyumba hadi nyumba.
Halmashauri za Jumuiya Kanda na Mitaa hukutana kama katiba inavyo elekeza baada ya Miezi mitatu.
Huduma zitolewazo ni kama ubatizo, kipaimara, Mpako wa wagonjwa, ushauri katika familia juu ya mambo mbalimbali mfano Uchumba sugu na kusuluhisha migogoro.
Uongozi
Kuna kamati tendaji na imekamilika kikatiba.
Halmashauri ya wale parokia inaundwa na viongozi wa tano kutoka katika kila kanda ,kamati tendaji ya halmashauri ya walei ya parokia na kigango, pamaja na wenyeviti wa vyama vya kitume ngazi yay a Parokia, wajume sitini na saba hukutana mara mbili kwa mwaka
Agenda za vikao zina patikana kwa wakati na zinatunzwa.Ipo pia ofisi ya Halmashaurii ya walei na inavitendea kazi vinavyo kidhi kwa kiwango chake.
Mwasiliano
Njia za mawasiliano zinazotumika ni kama zifuatazo:
- Barua pepe E mail
- Whatsaap group
- Barua
- Matangazo yanayotolewa kanisani kila dominika na pia
- Mawasiliano ya simu.
Kamati zilizoundwa zisizo za kikatiba ni kama zifuatazo:
1) Kamati ya uhamasishaji
-Kazi ya hii kamati ni kuhamasisha ulipaji wa zaka na kuhamasisha waumini kuchangia maendeleo ya parokia yao
2) Kamati ya ujenzi
-kamati hii pia inakazi ya kujishughulisha na maendeleo ya kanisa kwa ujula, ujenzi wa miundo mbinu ya kanisa n.k
Kamati za kikatiba zinaaripo shughuli zake za kiutenda kwa kamati tendaji ya halmashauri ya walei ya parokia, kwa hivyo haziingiliani kwa majukumu wala hazirudishani nyuma kiutendaji
Halmashauri ya wale parokia inaundwa na viongozi wa tano kutoka katika kila kanda ,kamati tendaji ya halmashauri ya walei ya parokia na kigango
Halmashauri ya walei parokia hukutana kutokana na mwongozo wa katiiba ya halmashauri ya walei ya parokia inavyo waelekeza
Zipo kalenda za matukio ya mwaka ya kiparokia ambazo zimepatikan kwa kushirikiana na waamini kupitia vyama vya kitume halmashauri ya walei ya parokia ambapo wajumbe wake ni wawakilishi wa waumini.
Vyama mashirika na jumuiya za kitume (VMJ)
Vyama vya mashirika jumuiya za kitume viko saba na havina wanachama wa kutosha na vinakidhi kwa asilimia ndogo
Vyama vya kikundi vya kitume vinafanya kazi kwa mujibu wa katiba ya halmashauri ya walei na vinatimiza vizuri wito wao wa kitume
Vyama hivi havina ofisi, lakini pia vina mambo ya kujivunia yaliyofanywa na VMJ za parokia-
-kuanda semina za kiroho
-Michezo na ushiriki katika maswala ya kiparokiaVyama havitoi repoti pamoja nay a fedha mara kwa mara katika uongozi wa parokia.
Ushiriki wa VMJ za Parokia katika shughuli za Dekania na Jimbo uko vizuri
Semina mbalimbali katika uendelevu wa Imani, uongozi na utegemezaji
Zipo semina na mafungo ambazo zinaandaliwa kiparokia lakini kijumuiya hakuna. Hizi ni semina zinazohusu uongozi katika kanisa na utoaji senina za ndoa
Hali ya kiimani iko wastani, na michango ya jimbo inaenda kwa wakati
-Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa jimbo
-mapato na matumizi ya parokia yanajulikana kwa waumini, nataarifa ya mapato na matumizi kwa waumini inatolewa mara nne kwa mwaka.
-Matoleo ya kila dominika hutangazwa kila baada ya juma kwa waumini na fedha kupelekwa bank
Ulinzi pia umeimarishwa kwa kutumia walinzi binafsi au kampuni
Parokia haina mradi mkubwa wowote isipokuwa shule za chekechea ambazo hazijasajiliwa
Mikakati ya baadae
-Upo mpango wa uboreshaji kanisa.
-Ujenzi wa nyumba ya mapadre kigangoni, lakini bado upembuzi yakinifu unaendelea.
-Mapadre kwa sasa hawatoshi,na hata watawa hamna kwa sasa na waanahitajika pia kuendeleza kazi za parokia.
-parokia imeweza kutoa wanafunzi kumi na mbili ambao wamejiunga na utawa.
Huduma za kiroho zitolewazo
Huduma za kiroho zitolewazo katika jumuiya na kanda ni kama zifuatazo:
- Ubatizo wa watoto wachanga
- Mpako wa wagonjwa
Zipo jumuiya zinazo saidia kulipia matibabu ya wagonjwa katika jumuia zao pale ambapo mwana jumuiya anapougua.
Changa moto zilizopo
1) Maudhurio hafifu katika jumuiya ndogo ndogo haswa kwa Wanaume na Vijana
2) Wanajumuiya wengine hawaudhurii jumuiya kabisa
3) Idadi ya Mapadre haitoshelezi, Watawa hali kadhalika hawatoshelezi.
Idadi ya wanafunzi wa seminari kutoka parokia ya kilungule ni kumi na mbili, na awaliuojiunga na utawa ni wawili.
Maandiko kuhusu Historian ya Parokia, waumini, Picha za sasa na za zamani hakuna.lakini kuna picha za mradi wa kigango cha Salome, Picha za mradi wa shule na Picha za mradi wa ujenzi wa nyumba za Mapadre.na Pia kuna picha ya mradi wa ujenzi wa ukuta.