PAROKIA YA MT PD. PIO WA PIETRECINA


A. MABO YA JUMLA
Jina la parokia ni Tabata kisiwani

Somo wa parokia ni PD. Pio wa pietrecina.

Mahaili parokia ilipo – Parokia inapatikana tabata kisiwani , na inapakana na Parokia ya Makuburi, Luhanga, Kimanga na tabata.

Idadi ya waumini ni kati ya 3611 na imepatikana kwa njia ya sense ngazi ya jumuiya .

Sensa ya mwisho imefanyika 2017 mwezi march kwa kupitia familia katika jumuiya na nyingine itafanyika mwaka 2019.

Parokia ya Tabata kisiwani haina kigango kwa sasa.

Katika Parokia ya tabata kisiwani zipo kanda nne (4)zenye jumuiya 21

Uongozi wa kanda umekamilika na umefuata utaratibu wa uchaguzi kama inavyo elekezwa na jimbo. Kanda zinatumia majina ya maeneo, majina ya watakatifu yamechaguliwa lakini bado hayajathibitishwa na baba paroko ijapo kwwamba mikakati kwa sasa ni kutumia majina ya watakatifu.

Kuna jumuiya 21 na zote zinatumia majina ya watakatifu.

Jumuiya zina kaya kati ya 15-20, lakini kuna baadhi ya jumuiya ambazo zina kaya Zaidi ya 20, ambapo utaratibu ni kwamba pale panapokuwa na kaya nyingi Zaidi jumuiya husika hugawanywa.

Ratiba ya sala za jumuiya ni kila jumamosi asubuhi, na kanda zinasali kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Mahudhurio ni ya wastani, lakini kundi la wanaume linachangamoto katika maudhurio hivyo uhamasishaji kuendelea ilii kuwwafanya waweze kuhudhuria kwa wingi katika sala za jumuiya.

Kuna utaratibu wa kuwatembelea waumini nyumba kwa nyumba baba paroko akiwa ndio mstari wa mbele kwa kupitia kamati ya uhamasishaji kufuatana na ratiba maalumu.

Jumuiya na kanda wanaadhimisha misa kila mwaka kwa kalenda walizojiwekea kwenye mpango kazi wa mwaka

Uongozi katika jumuiya na kanda umekamilika

Uongozi wa jumuiya na kanda una kutana kulinganan na kalenda ya kila miezi mitatu.

Huduma za kiroho
Zipo huduma za kiroho ambazo hutolewa katika parokia kwenye jumuiya na kanda kama vile kutembelea wagonjwa, ubatizo, na sakramenti nyingine mbalimbali.

Ukubwa wa jumuiya ni changamoto kubwa ambayo inapelekea waumini wengine kutoshiriki hasa pale inapotokea zile ratiba za mzunguko.

Uongozi
Kamti tendaji ya parokia ipo na imekamilika

Kamati tendaji hukutana kila jumanne ya mwisho wa mwezi saa 12:00 jioni. Vikao huchukua takribani masaa mawili kutegemeana na agenda.

Halmashauri ya walei parokia ina husisha kamati tendaji ya parokia, viongozi watono kutoka katika kanda , wenyeviti kutoka jNNK na wajumbe kutoka kamati tendaji ya parokia akiwemo baba paroko.

Taarifa zote zinatunzwa katika majalada maalumu, agenda za vikao huandaliwa mapema na zinapitishwa na kikao cha mwezi cha kamati tendaji kabla ya kikao cha halmashauri ya walei.

Ofisi Ya halmashauri ya walei parokia ipo na vifaaa vya kazi vipo ingawa havijakamilika

Njia za mawasiliano zipo: Anuani ya parokia ipo ni P.o .box 70118 DSM. Na E mail ipo ambayo ni Tabatakisiwani@gmail .com. Ipo pia what up ya halmashauri ya walei na group la kamati tendaji ya parokia ikimjumuisha paroko.

Kamati ndondogo za kikatiba zipo na uongozi wake upon na umekamilika.

Kamati zisizo za kikatiba pia zipo na wajumbe wake ni wa kitaaluma, kamati hizo ni kamati ya ulinzi na kamati ya afya

Kamati hizi huripo kwa kamati tendaji kushirikiana na paroko, na hakuna mwingiliano wowote na kamati zingine lakini zinashirikiana pale inapobidi.

Parokia inayo kalenda ya matukio na inafuatwa kama kawaida na imetengenezwa kwa kushirikiana na waumini

Njia zinazotumika kuaarifu waumini mipango ya parokia ni kwa kupitia vikao vya halmashauri ya walei ya parokia na hatimaye waumini wote kutangaziwa kanisani.

Vyama mashirika na jumuiya za kitume (VMJ)

Vyama vya kitume vipo kama ifuatavyo;
-Uwaka
-Wawata
-Viwawa
-Kaarismatiki katoliki
-moyo mtakatifu wa yesu
-Shikwaka
-CPT-Utoto mtakatifu
-Familia ya KOLPING

Vyama vyenye wanachama wengi ni Uwaka, Wawata na Viwawa.

Vyama vyote vinajitahidi kujiendesha kulingana na katiba ya halmashauri ya walei na kutimiza wito wake, na vyote viko hai

Kwa swala la ofisi ni viwawa tu wenye ofisi na wanavifaa na mahitaji yao ya kukidhi utume wao, vyama vingine havina ofisi kabisa

Mlezi wa vyama hivi ni baba paroko akisaidiana na kamati tendaji ya hamashauri ya walei ya parokia

Reporti za fedha zinatolewa kwa wakati japo sio mara kwa mara lakini kwa utaratibu ulio wekwa.

Hakuna vyama vya kitume vyovyote vinavyo hatarisha Imani katoliki, Amani na utulivu katika parokia

Ushirikiano wa VMJ katika shughuli za kidekani na jimbo ni mzuri.

Semina mbalimbali katika uendelevu wa Imani, uongozi na utegemezaji

Semina na mafungo mbalimbali yamefanyika kiparokia. Semina ya uongozi kwa viongozi wote imefanyika zikiwemo semina zingine kama vile semina za ujasiriamali ikijumlisha na mafungo.

Hali kadhalika kamati tendaji ya parokia imepatiwa semina ya uongozi iliyo andaliwa na jimbo na dekania, viongozi wa halmashauri ya walei parokia wameshapatiwa semina iliyoandaliwa na paroko, semina endelevu zinaendelea kuhitajika.

Semina za kiroho na tegemeza kanisa zinafanyika parokiani na zimepangwa katika nyakati tofauti kama vile wakati wa kwaresma na mavuno

Hali ya Imani ni nzuri na inapaswa kusimamiwa kwa juhudi.

Hali ya utoaji bado hairidhishi kwani kuna baadhi ya waumini wana zile hisia za kigango kigango

Toka kutangazwa kwa parokia ya tabata kisiwani ,hali ya utoaji wa zaka kama amri ya kanisa imeongezeka ukilinganisha na kipindi cha nyuma ,ingawaje watoaji wa zaka si wote ni walewale.

Parokia inatoa michango ya jimbo kikaamilifu kama inavyo paswa na kwa wakati.

Fedha na mipango
Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa jimbo

Mapato na matumizi yanajulikaana kwa waumini na hutolewa mara mbili kwa mwaka, yani mwezi juni na December

Matoleo yote ya dominika hutangazwa kila dominika inayofuata.

Fedha yote hupelekwa benki na kwa wakati.

Ulinzi na usalama
Hali ya ulinzi na usalama katika parokia ni mzuri

Ulinzi wa kampuni hutumika mchana na usiku ni ulinzi binafsi

Maendeleo ya kiuchumi.

Hakuna mradi unaoendeshwa na parokia hadi kufikia wakati huu.

Mipango ya ujenzi iliopo parokiani kwa sasa ni ukarabati wa kanisa , kuweka sakafu na kupaka rangi

Mambo ya jumla
Hakuna migogoro yeyote ya kimipaka na maeneo mengine

Mipango ya kuwaendeleza waumini kiuchumi kwa sasa haipo
Idadi ya mapadre kwa sasa haitoshelezi, na hakuna watawa.
Wanafunzi walioko seminari ni 6 na mtawa yupo mmoja
Hakuna historia iliyoandaliwa mpaka sasa lakini tupo kwenye mchakato.

JE UNATAFUTA

PAROKIA?

Upate majibu yako haraka zaidi
Ramani ya Parokia
Hakuna ramani kwa sasa...
Kuhusu Kanisa Katoliki

Ofisi ya Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam inapatikana makao makuu ya Jimbo,
Kanisa la St. Joseph, barabara ya Sokoine na Manseld street.

P.O Box 167, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 762 024 199
Email: mawasiliano@waleijimbodaresalaam.org
            darwaleijimbo@yahoo.com
Web: www.waleijimbodaresalaam.org

Kwa Habari kemkem za Kanisa jiunge nasi

Andika email yako hapo juu, na upokee taarifa za H/walei

Copyright © 2025. All Rights reserved by H/Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam