DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA MLANDIZI
HISTORIA YA PAROKIA YA MLANDIZI
Ukatoliki mlandizi ulianza 1968 kutokana na kaya chache za waliokuwa wafanyakazi wa mtambo wa maji wa ruvu juu kwa sasa DAWASCO
Kigango kilianza tar 17/07/ 1975 kikiwa chini ya parokia ya Chalinze jimbo la morogoro.
Mwaka 1985 kigango cha mlandizi pamoja na vigango vya kikongo , zogowale na ruvu station vilihamishiwa parokia ya kibaha , jimbo kuu la dar es salaam.
August 1996 kigango cha mlandizi kilipandishwa hadhi na kuwa paarokia, kikiongozwa na baba paroko Pr Joseph Kanduta akisaidiwa na Pr Deusdedit Rugemarila ambae pia alikuwa anahudumu Seminary ya visiga .
Kwa sasa parokia inawaumini kati ya 4,343 yenye kaya 952
UONGOZI
Parokia imekuwa ikiongozwa na padre mmoja ambaye ni paroko. Pr Martin Dominic akisaidiana na kamati tendaji ya Parokia ambapo viongozi wake wake wamechaguliwa kwa mujibu wa katiba ya halmashauri ya walei, na wanafanya kazi katika kutimiza malengo ya parokia .
VIGANGO
Mpaka historia hii inaandikwa Parokia ilikuwa ina vigango 10 ambavyo ni Misugusugu, visiga, Zogowale, Ngeta, Makazi mapya, kikongo, Mwanabwito, Ruvu station, Miswe na Mbwawa.
KANDA
Parokia ya mlandizi ilikuwa na kanda 6 ambazo ni kanda ya Papa Fransis, Mt yohane Paulo wa II, Papa Benedicto XVI, Askofu Marantha, Kardinal Rugambwa na cardinal Pengo
Aidha vigango vya Misugusugu na visiga vina ngazi ya kanda baada ya jumuiya.
JUMUIYA NDOGO NDOGO
Parokia imeundwa na jumuiya ndogo ndogo 62 na 20 vigangoni na zina uongozi ulio kamilika kwa mujibu wa katiba ya halmashauri ya walei.
VYAMA VYA KITUME
Parokia ina vyama vya kitume 7, yaani wawata,Uwaka, Utoto mt, Wazee na wastaafu, Chama cha wataaluma wakatoliki ndio kina fikiriwa kuanzishwa.
VYAMA VYA KIROHO.
Vyama vingine ni kama kwaya ya Maria, Kwaya ya Kristo Mfalme, Shikwaka, Regio maria, Utume wa Fatiima, Karismatiki katliki, Moyo mt wa Yesu na chama cha miito.
KAMATI ZA KIKATIBA
Kamati hizi ni kamati ya malezi, kamati ya Liturjia , kamati ya haki na Amani , Kamati ya elimu ya dini, na kamati ya Fedha na mipango, Pia kuna kamati zilizoundwa kwa mahitaji maalumu ambazo ni ; Kamati ya mazingira , Kamati ya afya, Kamati ya ulinzi na Usalama, Kamati ya ujenzi, Kamati ya harambee na kamati ya uinjilishaji.