DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA MTONI TEMEKE
Somo wa parokia ni Josephine Bakita
Parokia ilizaliwa 1996
Kijiografia parokia inapatikana maeneo ya mtoni kwa azizi ali. wilaya ya temeke
uongozi
Parokia ipo chini ya paroko Fr Anthony Mashaka akishirikia na Fr Emmanueli Morweng wote wa shhirika la Stigmatine (madonda matano ya kristo)
Parokia ina jumla ya jumuiya ndogo ndogo 34 ambaazo zimo ndani ya kanda 12.
Viongozi wake wamechaguliwa kwa mujibu wa katiba ya Halimashuri ya Walei
Sala za jumuiya ni kwa mujibu wa mwongozo wa sala za jumuiya.
Maazimio ya parokia
Maazimio ya parokia yamejikita katika Nyanja mbili
a) Ya kiroho
b) Ya kijamii,kiuchumi na maendeleo ya parokia
Ya kiroho
• Kuwa na semina mbalimbali, ubatizo wa watoto waliozaliwa nje ya ndoa, kuwa na ndoa za pamoja ,hivyo waliobatizwa kwwanzia 2016 hadi desember ni 126 wakatekumeni 20, komunio ya kwanza 82, kipaimara66 na waliofunga ndoa 25
• Vyama vya kitume kuratibu kuabudu ekarist takatifu kila alhamisi
• Kualika wahamasishaji wa ndani nan je ya parokia kuhamasisha kanisani .
• Kamati tendaji kuwa na ziara za kikanda
• Kufanya semina mbalimbali za makundi ya kitume (UWAKA, WAWAATA ,SHIKWAKA n.k
• Mafungo semina na hija, katika kipindi cha mwaka 2016 ka mfano zimeendeshwa semina mbalimbali za mafungo ukizingati ilikua ni mwaka wa huruma.
Semina mbalimbali zimesaidia kuwaimarisha waumini kiroho kwa mfano
Visiga WAWATA na Hija Pugu UWAKA, Novena kwa wanaparokia wote
• Katika kuwakuza waumini kiroho, parokia imewaandaa maketekista wawili kwa kushirikiana na mapadre katika kufanya shughuli za kiroho ikiwa kuwaandaa vijana katika mafundisho mbalimbali ya kiroho kama vile ubatizo wa wa katukomeni, komunio na hata kipaimara.
Ya kijamii , kiuchumi na kimaaaendele ya parokia
Chanzo cha mapato ya paroki kinatokana sana na:
- Sadaka za kila dominika
- Mavuno
- Shukrani
Maendeleo ni pamoja na ujenzi wa kanisa, lakini pia kijamii ina tengeneza mashirikiano.
Vyama /mashirika ya kitume na vikundi
Vyama hivyo ni kama vifuatavyo:
a) UWAKA
b) WAWATA
c) Shirika la mt Augustino la wazee na wastaafu
d) Moyo mt yesu
e) Legio maria
f) Karismatiki katoliki
g) SHIKWAKA
h) Utoto mtakatifu
i) Umoja wa vijana(VIWAWA)
j) Shirika la mt Fransis wa azizi (VIAFRA)
k) Wajane na Wagane
l) Wasoma masomo altareni
Ili kuleta umoja wa vyama vyote vya kitume parokiani , limeanzisha shirikisho la vyama vya kitume (SHIVYAKI) pamoja na uongozi wake
Mwongozo shughuki za kamati tendaji na halmashauri ya walei
Shughuli zote za Halmashauri ya walei huongozwa na katiba ya halimashauri ya walei katoliki Tanzania TEC) ya mwaka 2013 pamoja na maagizo ya babab paroko. Kamaati tendaji pia huratibu shughuli za jimbo na matukio mbalimbali
Kamati mbalimbali
Kuna kamati mabalimbali ambazo zimeundwa katika kusaidia mafanikio ya parokia katika utume nazo ni :
Kamaati ya malezi na familia
Kazi yake kuratibu changamoto zoto zinazohusiana na malezi na familia ; mfano mzuri ni swala la ndoa na familia,
Kamaati ya liturjia
Kamati hii kazi yake ni kutoa mwongozo wa kiliturjia
Kamati ya haki na Amani
kuwaelimisha waumini kuzijua haki zao mbalimbali za kuchagua na kuchaguliwa katika maswala mbalimbali ya kijamii, Pia kuijua na kuisimamia katiba ya walei n.k
Kamati ya mafundisho ya elimu na dini