PAROKIA YA BOKO


PAROKIA YA MWENYE HERI ISDORI BAKANJA BOKO

Jina la parokia na Matakatifu msimamizi wake ni Mwenyeheri Isdori Bakanja (Boko)

Mahali parokia ilipo Kijiografia inapakana na parokia za Bunju, Ununio, Mt yohana Mtume, yohane Mwinjili pamoja Na Mivumoni.

Parokia ya Boko ina waumini wapatao takribani 5600 ambapo kati ya hao 1,600 wapo vigangoni na waliobaki 4,000 wako parokiani

Idadi imepatikana kwa njia ya sense iliyofanyika kupitia JNNK

Parokia ya Boko ina vigango vitatu (3)
a.    Mt Fransis wa Asizi (Mbweni)
b.    Mt Anthony wa Padua Mbweni Mpiji na
c.    Yohane Mbatizaji.

Katika Parokia ya Boko tunatumia Zaidi majina ya kanda badala ya Mitaa.

Na parokia ina kanda 14, na kati ya hizo kanda 9 zipo parokiani na 6 zipo vigangoni.

Kanda zimegawanyika kwa kufuata ukaribu kwa urahisi wa kitawala. Kwa wastani kila kanda ina jumuiya 3-5 kulingana na jiografia mahali zilipo, zipo kanda zenye jumuiya mbili.

Uongozi
Uongozi umepatikana kwa uhaguzi kwa mujibu wa katiba.

Kanda inaundwa kutokana na viongozi watanao wa kila jumuiya pamoja na wenyeviti wa vyama vya kitume

Parokia ina JNNK 54 amabapo jumuiya 39 ziko parokiani  ana 15 zipo vigangoni

Jumuiya zote zinatumia majina ya watakatifu.

Kwa wastani kila jumuiya ndogo ndogo ina kaya kati ya 15 hadi 20, na kwa sasa hakuitajiki maboresho kwa kuwa maboresho yamefanyika hivi karibuni

Jumuiya zinasali kila siku saa 12:30 asubuhi kila siku za jumamosi. Kwa upande wa jumuiya za kikanda hukutana kila mwisho wa mwezi ambapo waumini wanasali katika kanda.

Mwongozo unaotumika ni ule wa jimbo ullioandaliwa na munsinyori Mbiku.

Maudhurio sio mabaya ila kunachangamoto kubwa kwa wanaume na vijana. Na kila jumuiya ina daftari la maudhurio

Mababa wanatembelea familia na kuhuisha familia zinazo lega lega.

Mapadre kushirikiana na viongozi jumuiya  hupanga kuwatembelea  waumini  katika familia zao

Upo utaratibu wa kanda na jumuiya kuadhimisha misa za somo wao

Kuhusu Uongozi katika jumuiya na kanda umekamilika.

Uongozi au Halmashauri wa JNNK/kanda /Mtaa huwa wanakutana mara 4 kwa mwakana vikao vya dharura huwepo pale inapobidi

HUDUMA ZA KIROHO
Semina mbali mbali za kiroho kwa waumini
Ubatizo, kuombea wagonjwa,Misa za mazishi n.k

UONGOZI
Kamati tendaji ipo na imekamilika kikatiba
Kamati tendaji hua inakutana mara moja kila mwezi ya jumapili ya kwanza ya mwezi
Na muda wa kikao utategemeana na ajenda zilizopo lakini kwa kawaida sio Zaidi ya masaa mawili.Paroko ni mshiriki mkubwa katika kikao.

Halmashauri ya walei ya parokia inaundwa na:
a.    Wenyeviti wa kutoka vyama vya kitume
b.    Wenyeviti na katibu kutoka kwenye kanda zote
c.    Wajumbe 5 kutoka kamati tendaji ya parokia
d.    Wajumbe wat ano kutoka vigangoni

Halmashauri ya walei parokia hukutana mara nne kwa mwaka vikao vya kawaida, na endapo kunadharura basi kikao cha dharura huitishwa.
Ajenda na repoti za vikao hutolewa kwa wakati na zinahifadhiwa

Halmashauri ya walei ya parokia ina ofisi na vitendea kazi kadhaa kuwezesha shughuli kufanikiwa

Njia za mawasiliano zinazotumika ni kama zifuatazo

Barua pepe, Whatsaap groups na simu ambayo ndiyo hutumika Zaidi

KAMATI
Zipo kamati za kikatiba za halmahauri ya walei ambapo pia wajumbe wake wamekamilika
Kamati zingine zisizo za kikatiba ni kama zifuatazo:
•    Kamati ya ulinzi
•    Kamti ya ardhi na afya

Kmati hizi zimeundwa hivi karibuni

Kamati hizi hutoa taarifa kwenye mikutano ya halmashaauri.

Parokia ina kalenda za matukio zinazotolewa kila mwaka, na zinatengenezwa nakuandaliwa na makatibu wa kanda  zote na kusawazishwa na kamaati tendaji kabla ya kupelekwa katika mkutano wa halmashauri

Njia zinazotumika kuwaarifu waumini wote juu ya mipango ya parokia Vigango, na kwenye Kanda ni  kwa kupitia matangazo ya  dominika.

Vyama ,mashirika na jumuiya za kitume(VMJ)

Vyama mashirika ya kitume viko kama vifuatavyo:
WAWATA, UWAKA, VIWAWA, MOYO MTAKATIFU WA YESU, Karismatiki katoliki, Ministrant, Shikwaka,Utoto mtakatifu, Damu takatifu ya yesu

Vyama hivi vina wanachama wa kutosha.

Vyama hivi na vikundi vya kitume vinafanya kazi kulingana na katiba ya halmashauri ya walei, na vyote hivi vinaripoti kwa kamati tendaji ya parokia.

Kalenda ya vyama vya kitume inazingatia kalenda ya parokia

Ile iliyo kuwa ofisi ya kigango ndiyo inaandaliwa kuwa ofisi kwa sasa.

Kila chama kina msimamizi /Mlezi, lakini mlezi mkuu ni kamati tendaji kwa mwongozo wa baba Paroko

Taarifa kwa VMJ au repoti (pamoja na fedha) hufanyika kwa kuombwa na si kwa utaratibu. Vilevile hupewa nafasi wakati wa mikutano ya halmashauri.

Ushirikiano na ushiriki wa VMJ za Parokia katika shughuli za kidekania uko vizuri, lakini pale unapolegalega kamati tendaji imekuwa ikikumbusha

Mambo ya kujivunia yaliyo fanywa na VMJ za paarokia zipasavyo kuigwa na parokia nyingine ni kazi ya kuishi waumini kiroho ambayo imefanywa sana na karismatiki katoliki, moyo mtakatifu wa yesu.

Semina mbalimbali katika uendelevu wa wa Imani, uongozi na utegemezaji

Hamasa ya kukuza Imani katoliki inayofanywa na karismatiki, na moyo mtakatifu wa yesu

Uongozi wa parokia kamati tendaji na halmashauri ya walei ya parokia wamepatiwa semina mara tu baada ya uchaguzi wa viongozi, na semina zingine zinaandaliwa.

Semina za kiroho na tegemeza kanisa zimewekwa katika kalenda ya parokia .

Ukuaji wa Imani ni swala ambalo halipaswi kukoma ,hivyo mikakati iliyopo ni endelevu.

Uwepo wa karismatiki na moyo mtakatifu wa yesu unasaidia sana kutegemeza ukuaji wa Imani katika parokia.

Swala la utoaji katika parokia ni zuri si baya , lakini bado kuna changamoto kubwa ya uelewa kwa watu kati ya tofauti ya kutoa na kujitoa. Ambapo semina juu ya utoaji kuandaliwa

Utoaji zaka kama amri ya kanisa ni mzuri kwa kiasi Fulani lakini bado tunaendelea kuweka msisitizo.

Fedha na mipango
Mapato na matumizi ya parokia hutolewa na kujulikan kwa waumini, taarifa za fedha hutolewa mara mbili kwa mwaka katika mikutano wa halmashauri ambapo viongozi wa halmashauri hupeleka kwenye vigango kanda na jumuiya.

Matoleo ya kila dominika hutolewa na kutangazwa kwa waumini kila dominika inayofuata

Fedha yote hupelekwa banki kwa wakati

Ulinzi na usalama
Hali ya ulinzi na usalama parokiani ni nzuri, ipo kampuni inayolinda mchana na usiku , kwa siku za dominika  na matukio.
Kwa ujumla ulinzi unafanywa na kampuni binafsi.

Maendeleo ya kiuchumi
Miradi iliyopo ni Frame ya duka na shule ya QT
Kuna ujenzi wa vigango kwa sasa baada ya kumaliza ujenzi wa uzio.

Mambo ya jumla
Idadi ya mapadre/ watawa kwa sasa inatosheleza.
Idadi ya wanafunzi wa seminari katika parokia ni 17, na idadi ya waumini waliojiunga na utawa ni wanne(4).
Parokia haijawa na maandiko ya historia kwa sasa ila mpango huo upo.

JE UNATAFUTA

PAROKIA?

Upate majibu yako haraka zaidi
Ramani ya Parokia
Hakuna ramani kwa sasa...
Kuhusu Kanisa Katoliki

Ofisi ya Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam inapatikana makao makuu ya Jimbo,
Kanisa la St. Joseph, barabara ya Sokoine na Manseld street.

P.O Box 167, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 762 024 199
Email: mawasiliano@waleijimbodaresalaam.org
            darwaleijimbo@yahoo.com
Web: www.waleijimbodaresalaam.org

Kwa Habari kemkem za Kanisa jiunge nasi

Andika email yako hapo juu, na upokee taarifa za H/walei

Copyright © 2025. All Rights reserved by H/Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam