DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA VIKINDU
KANISA KATOLIKI LA MT. VINSENT WA PAULO – VIKINDU
HISTORIA:
Inaelezwa
kuwa Parokia ya Vikindu ilianza mwaka 1960 kama Jumuiya chini ya
Parokia ya Mbagala Mission ikiongozwa na mkristu mmoja aliyeitwa kwa
jina *Katekista Joseph Namiva (alifariki Augost 2008 na kuzikwa makaburi
ya kanisa - Mmakonde kwa Kabila) ambaye akitokea Zanzibar. Mwaka 1980
muumini mmoja Capt. Joseph Mtahangarwa alitoa eneo lake la ekari 10 kwa
kanisa ili kuwezesha kuwa eneo kubwa na kupata hadhi ya kuwa Kigango.
Wakati
huo pale Parokiani Mbagala Mission*Pd. JOSEPH Bill (alifariki na
amezikwa katika kanisa la BIKIRA MARIA Entebe –Uganda) wa shirika la Mt.
Vinsent wa Paulo lenye asili yake Kerela (India) alikuja kutokea Kigoma
(Tanzania) mara kwa mara kwaajili ya mafungo.
Miongoni
mwa walioshiriki alikuwa Ndugu Joseph Mtahangarwa ambaye alikuwa akiishi
jirani na kanisa dogo la kigango hiki. Baada ya maafungo hayo
alimkaribisha Pd. Bill nyumbani na kumkabidhi sehemu ya eneo lake la
ekari 8 kama shukrani kwa Mungu lakini pia kukaribisha huduma hii ya
mafungo katika eneo la Vikindu (Soweto).
“Jina SOWETO lina asili ya
mji wa SOWETO huko Afrika ya Kusini ambapo yalitokea mauaji ya waafrika
wengi kwa sababu ya ubaguzi wa rangi (SOWETO MASACRE 1976) hivyo katika
mji huu kulikuwa na mauaji ya watu kwa sababu eneo hili kulikuwa na
mapori mengi, hata baada ya kujengwa barabara ya rami kulikuwa na ajali
nyingi zikitokea mara kwa mara hivyo kuakisi jina SOWETO kwa maana ya
mauaji” (Mzee Husein Jackson)
Historia inaonesha mwaka 1997,
Mapadre wa shirika (Pd. JAMES) kutoka Kerela (India) waliingia
Soweto-Vikindu na kuanza kazi ya kichungaji pamoja na kununua eneo
jingine ili kuongezea. Wakati wananunua maeneo kwa wenyeji; wenyeji
wengi waliwauliza mapadre;
“maeneo haya mnayonunua ni kwaajili gani?
nao walijibu “tunataka kuufanya huu mji kuwa mji wa YESU (JESUS TOWN)”
tokea hapo mji huu ulitambulika kama mji wa Yesu ingawa siku hizi za
jirani jina hili limekuwa likififia”
Kanisa dogo la
Kigango lililojengwa kwa miti na udongo na kuezekwa kwa bati liliendelea
kuchoka hali ambayo ilipelekea baadhi ya bati kuanza kuvuja. Katekista
wa kwanza kigangoni hapa Ndugu *Joseph Namiva aliendelea kutoa huduma ya
kiroho kigangoni na ujio wa mapadre hawa wa shirika la Mt. Vinsent wa
Paulo uliongeza chachu ya huduma ya kiroho katika mji wa Yesu.
(Picha zinapatikana katika albam iliyopo ofisi ya Baba Paroko)
Miaka
ya 1980 Kigango hiki kilihamishwa toka Mbagala Mission kuja Parokia ya
Mt. Xavery Mkuranga. Paroko wa wakati huo wa Parokia ya Mkuranga Pd.
Patrick akisaidiana na Mapadre wa Mt. Vinsent wa Paulo waliendelea
kuhudumu kanisa na kuendeleza uinjilishaji katika Kigango hiki cha
Vikindu.
Mwaka 1999 ujenzi wa kanisa dogo katika nyumba ya
Mapadre wa Mt. Vinsent ukawa umekamilika; kwa kuwa kanisa la Kigango
lilikuwa linavuja na baaadhi ya kuta kuwa zimeharibika; Pd. JAMES
aliwaomba waumini wa Kigango hiki wasali katika kanisa lililoko nyumba
za mapadre badala ya kanisa la kigango ambalo lilikuwa limeharibika.
Wakati huo kanisa lilikuwa na jumuiya 2 na waumini waiopungua 100 na wasiozidi 200
Kigango
hiki kilipata kuwa Parokia mwaka 21/01/2001 uzinduzi huo ulifanyika
Mwadhama Polycap Kadinali Pengo na kukabidhiwa kwa shirika la Mt.
Vinsent wa Paulo. bila jengo la kudumu la kanisa, wakati huo Parokia
ilikuwa na vigango 7.
(Picha zinapatikana katika albam iliyopo ofisi ya Baba Paroko)
Waumini walisali kwa muda katika kanisa dogo lililopo nyumba kwa mapadre kisha Pd. James alisema
“waumini hawa wakiendelea kusali katika kanisa hili hawatajenga
kanisa la parokia”
maamuzi
haya yalipelekea waumini kujenga hema katika eneo la kanisa wakati huo
eneo la kanisa liliko kando ya barabara ya kilwa badala ya lile la
zamani ambalo kanisa lilibadilishana na shirika la masista wa Bikira
Maria Mama wa Mlima Carmel. Siku moja wakati wa maandalizi ya ibada
katika hema hilo ukaja upepo mkali uliopeperusha maandalizi yote ya
ibada, wakati huo Paroko Pd. James alikwenda likizo India, ndipo Pd
Joseph akasema
“na turudi tukasali katika kanisa dogo nyumbani kwa mapadre mpaka ujenzi wa kanisa la parokia utakapo kamilika”.
jiwe
la msingi la ujenzi wa kanisa la Parokia liliwekwa na mwadhama Polycapy
Kadinali Pengo tarehe 27/09/2002. Kanisa hili la parokia lilitabarukiwa
na Mwadhama Polycapy Kadinali Pengo Askofu Mkuu wa jimbo kuu la Dar es
salaam tar. 24/09/2006
(Picha zinapatikana katika albam iliyopo ofisi ya Baba Paroko)
Pamoja
na Mapadre hawa baadae mwaka 2000 Shirika la masista wa Huruma ya Mungu
wa Mt. Vinsent wa Paulo kutoka Austria walikuja hapa Vikindu, walijenga
makazi yao, zahanati na shule ya watoto wadogo (chekechea).
Tena
Mwaka 2001 shirika lingine la masista wa Bikira Maria Mama wa Mlima
Carmel kutoka Kerela India walikuja katika Parokia ya Vikindu kwa sasa
wamekwisha kujenga nyumba ya Malezi pamoja na shule ya msingi na
sekondari
Hadi leo Parokia ina jumla ya vigango 7 kanda 9 jumuiya 74 na waumini wapatao 3,984
Huduma
ya mafungo kama ilivyo kusudiwa tokea awali rasmi ilianzishwa mwaka
2015 na aliyekuwa Paroko mwaka huo Pd. Steven Shaiju na inaendelea
Parokiani ingawaje ujenzi wa kituo rasmi cha mafungo uko katika mpango
wa vingozi wa mapadre wa shirika la Mt. Vinsent wa Paulo.
MAPAROKO WALIOKWISHA HUDUMA KATIKA PAROKIA HII
1. Pd. JOSEPH
2. Pd. JAMES
3. Pd. JINNU
4. Pd. TOMMY
5. Pd. MATAYO
6. Pd. SHAIJU
7. Pd. JINSO
MAPADRE WALIOKWISHA HUDUMU KATIKA PAROKIA HII KWA JUMLA
1. Pd. BILL
2. Pd. JAMES
3. Pd. PAUL
4. Pd. JOSEPH (MANDEVU)
5. Pd. JOSEPH
6. Pd. JOY
7. Pd. JINNU
8. Pd. TOMMY
9. Pd. MATAYO
10. Pd. BIJU
11. Pd. JIBIN
12. Pd. IBIN
13. Pd. JINSO
14. Pd. JACOB
VIONGOZI WALEI WALIOKWISHA KUHUDUMU PAROKIA (wanaokumbukwa
NO. | JINA | CHEO | MIAKA |
1. | CHRISTIAN MUSHI | MWENYEKITI | 2001- 2010 |
2. | PIUS MGAYA (2016) | KATIBU | |
3. | FAUSTIN ONYANGO | MWENYEKITI | 2010 - 2013 |
4. | SIXMUND FUSSY | KATIBU | |
5. | MARTINA MSONGO | K/MSAIDIZI | |
6. | ANNA CHARLES MWAMBUSI | MHAZINI | |
7. | ERICK MWAMBELEKO | MWENYEKITI | 2013 - |
8. | MAKARIOUS KIHAWA | M/MWENYEKITI | |
9. | ANGRIBETH NKWERA | KATIBU | |
10. | SIRILY MALLYA | M/KATIBU | |
11. | MONIKA GODFREY | MWEKAHAZINA |