PAROKIA YA BMMH MBEZI BEACH




HISTORIA YA PAROKIA  2004- 2018

1.    UTANGULIZI:

Ni vigumu sana kuandika ama kuzungumza juu ya Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma bila kuwataja Padri Dominico Arltiet, Padre Denis Masawe na Watawa wengineo,  na familia ya Emanuel Rutahindurwa ambaye alitupatia kiwanja cha kujenga Kanisa.

Maendeleo aliyofanya Padre Dominiko:-

  • Alianza ujenzi wa Kanisa Mwaka 1992- 1994.
  • Mwaka 1994 alipatikana mfadhili kutoka Italy na kuanza kujenga shule ya Chekechea  ya Mt. Yohane Merline Centre na kufunguliwa rasmi na Askofu Mkuu wa Dares Salaam tarehe 11/08/1996
  • Kuruhusu kituo cha Chekechea cha Yohane Merline Centre  kitumike kama Kanisa na pia kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha wakristo katika shughuli za ujenzi  wa Kanisa.
  • Parokia hii ilizaliwa kutokea Parokia ya Mtongani ambapo wakati kikiwa Kigango kilihudumiwa na Mapadre wa Shirika  la Mapadre Waabuduo Damu Takatifu ya Yesu.
     

Padre Denis Masawe akiwa na msaidizi wake Padre Richard  Mjigwa   watakumbukwa sana kwa kazi zoa za kiroho za kuhamasisha watu na kuamsha roho za waumini kiimani na kuwavuta watu wengi kuhudhuria misa hadi Kigango kikaonekana kufaa kuwa Parokia.

Tarehe 28/03/2004, Baba Mwadhama  Polycarp Cardinal Pengo  alitamka rasmi kwamba Bikira Maria Mama Wa Huruma itakuwa Parokia.

Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma, ni Parokia ambayo ilianzishwa mwaka 2004 mwezi wa Augusti tarehe 15, chini ya Uongozi wa Mapadre wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

2.    Uongozi:
Parokia hii ilianza na Uongozi wa Mapadri  kama ifuatavyo:-

a)     Maparoko
-    Pd. Romwald Mukandara –   2004 – 2007
-    Pd. Paul Haule – 2007-2008
-    Pd. Faustine Mlelwa – 2008 - 2010
-    Pd. Andrew Mwekibindu – 2010- 2015
-    Pd. Timothy M. Nyasulu – 2015 –
 
b)    Maparoko  Wasaidizi
-    Pd. Primo Lingamila – 2004 -2006
-    Pd. Joseph Mosha – 2006 - 2007
-    Pd. Edwin Kigomba – 2007- 2009
-    Pd. Vitalis Kassembo – 2010-2012
-    Pd. Canisius Hali – 2012- 2016
-    Pd. Jose EduardoSantos Ramos – 2017-2018
-    Pd. Meinrad Kalikawe-  2018-

c)    Kamati Tendaji:-
-    Bw Deogratias Kweka – Mwenyekiti – 2004-2010
-    Bw. Cosmas Lamosai – Makamu Mwenyekiti 2004  –2007

-    Bi. Margareth Ikongo – Mhazini Parokia – 2004-2007
-    Mr. Lucas Martin - Makamu Mwenyekiti- 2007-2009
-    Bi. Grace Mnyani – Katibu Parokia – 2004-2007
-    Bw. Deogratias Katakweba – Katibu Msaidizi Parokia 2007-2010
-    Bw. Edmund Sailale – Mhazini Parokia 2007-2010
-    Bw. Francis Msungu – Mwenyekiti Parokia – 2010-2012
-    Juliana Urio – M/mwenyekiti – 2011-2012
-    Bw. Marco Madafu – Mhazini Parokia 2010-2011
-    Bw. Onesphory Salema- Mhazini Parokia – 2011-2013
-    Bw. Philemon Felix Kelvin- Mhazini Parokia-2013-2015
-    Dr. Avemaria Semakafu – M/Mwenyekiti Parokia-2012
-    Bi. Donesta Byarugaba – Mwenyekiti Parokia- 2013-2015
-     Bw. Lucas Martin        - M/Mwenyekiti- 2013-2015
-    Bi. Grace Mnyani- Katibu Msadizi Parokia – 2013-2014
-    Bi. Anna Manchonchoryo- Katibu Parokia – 2012-2014
-    Bw. Gabriel Msangi – Mwenyekiti Parokia – 2015-
-    Bi. Basiliana Mrimi-M/Mwenyekiti P- 2015-2016- Uhamisho Kikazi
-    Bw. Alex Shayo- M/Mwenyekiti Parokia – 2016
-    Bi. Joyce Leshabari – Katibu Parokia – 2015-
-    Bw. Sixbert Msumari- K/Msaidizi – 2015-
-    Bw. Genes Kunda – Mhazini Parokia – 2015-

d)    Vigango:
Parokia ilikuwa na Vigango kama ifuatavyo:-
-    Mt. Yohana Maria Muzeyi – Tegeta A
Mwaka 2010 Kigango hiki kikawa chini ya Parokia ya Makabe

-    Bikira Maria Imakulata – Goba
Mwaka 2011 Kigango hiki kikawa chini ya Parokia ya Mbezi Mwisho kikihudumiwa na Mapadre kutoka ubungo Msewe.

-    Bikira Maria Mama wa Rozari
Kigango kimetangazwa kuwa Parokia Teule 2018 na kuitwa Bikira Maria Mama wa Kanisa.

-    Thomas Moore
Kigango hiki kilihamishiwa Parokia ya Mt Gaspary.

-    Mt. Rita
Kigango hiki bado kipo chini ya Parokia ya BMMH

e)    Vyama vya Kitume vilivyopo na idadi ya Wanachama wao
-    WAWATA             - 210
-    UWAKA                - 680
-    Vijana                   - 200
-    Shikwaka             - 160
-    Moyo Mt. wa Yesu        - 25
-    Couples for Christ           - 6
-    Karismatiki                     - 60
-    Utume wa Fatima           -30
-    Legio Maria                     - 26

-    Utoto Mtakatifu            - 302
-    Wazee na Wastafu        - 46

f)    Idadi ya Jumuiya zilizopo Parokiani
-    Parokia Jumuiya              34
-    Parokia Teule BMMK       16
-    Kigango cha Mt. Rita        23

                 Jumla         73


g)    Idadi ya Kanda zilizopo Parokiani na vigangoni – 13
h)    Idadi ya Waamini waliopo
-    Parokiani                         3009
-    Parokia Teule BMMK     1337
-    Kigango cha Mt. Rita     1300
                             
                      Jumla  ya Waamini        5646

3. WATAWA
Kuanzia mwaka 2004 tumehudumiwa na Watawa wafuatao:-
-    Sr. Scolastica Nyongo
-    Sr. Flaviana  Alfred
-    Sr. Magdalena Pantaleo
-    Sr. Honoratha Vitalis – 2010- 2013
-    Sr. Rose Priva – 2013- 2014
-    Sr. Venosa Joseph     – 2014-
-    Sr. Fransiska Thomas- 2016-2017
-    Sr. Plasidia Ponsiani  - 2017-

Tunayo Convent moja ya Masista Waabuduo Damu Takatifu ya Yesu ambao wanahudumia Parokia.

4. MAKATEKISTA
Kuanzia mwaka 2004 tumehudumiwa na Makatekista wafuatayo:-
-    Katekista Elias Kayange – 2004-2012
-    Katekista Didas Kachele – 2004
-    Katekista Evanjelist Elias – 2012
-    Katekista John Kobero      – 2004-2011
-    Katekista Joseph Msimbe – 2004-2010
-    Katekista Bruno Ngoma     – 2012-2015 ( Marehemu)

5. HUDUMA ZA KIROHO
Parokia imekuwa ikishiriki katika matukio mbalimbali ya Jimbo (hija, semina, kongamano nk) katika kuimarisha Imani kwa waamini wake.
Aidha waamini wamepokea huduma mbalimbali za kiroho tangu kuanzishwa Parokia hii zikiwamo Ubatizo, Komunio, Kipaimara, Ndoa na Mazishi wakati wote zilipohitajika baada ya kukamilisha matakwa yote kulingana na taratibu za Kanisa.

6. MAENDELEO
Kuanzia mwaka 2004  mpaka sasa, tumeweza kujenga ofisi ya Parokia hapa Parokiani,   kununua   viwanja na kujenga Makanisa ya kudumu na nyumba za Mapadre vigangoni  na kujenga shule ya Chekechea ya Mt. Rita iliyoko Goba.

MATUKIO MENGINE NI KAMA IFUATAVYO;

  1. Uzinduzi wa Jengo la ofisi ya Parokia ni tarehe 19/12/2015, Lilijengwa kwa nguvu ya waamini, makisio yake ni Tshs 541,205 128/=
  2. Kanisa lilitabarukiwa mwaka 2005 na Baba Mwadhama Kardinali Pengo.
  3. Vyama vya kitume vilivyokuwepo: Vijana, WAWATA, Moyo Mt. wa Yesu, Utume wa Damu Azizi, na Utoto Mtakatifu
  4. Idadi ya waamini kipindi hicho ni 2630
  5. Nyumba wanapoishi Mapadre ilinunuliwa  kutoka kwa Bw/ Bi Peter Rutahindurwa kwa Gharama ya Tshs 55,000,000/=  Title no 55758 Plot no.858.
     

MWISHO
Tunawaombea kwa Mungu waamini wote ambao walishirikiana na Paroko kuhakikisha  Mapadre wanapata mahali pa kulala  tangu kuanzishwa kwa Parokia yetu. Mungu mwenyezi awabariki sana.


JE UNATAFUTA

PAROKIA?

Upate majibu yako haraka zaidi
Ramani ya Parokia
Hakuna ramani kwa sasa...
Kuhusu Kanisa Katoliki

Ofisi ya Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam inapatikana makao makuu ya Jimbo,
Kanisa la St. Joseph, barabara ya Sokoine na Manseld street.

P.O Box 167, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 762 024 199
Email: mawasiliano@waleijimbodaresalaam.org
            darwaleijimbo@yahoo.com
Web: www.waleijimbodaresalaam.org

Kwa Habari kemkem za Kanisa jiunge nasi

Andika email yako hapo juu, na upokee taarifa za H/walei

Copyright © 2025. All Rights reserved by H/Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam