DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA ST. JOSEPH

Intro Section


TAARIFA YA PAROKIA
Jina la Parokia ni Mt, Joseph,Jina haliingiliani nan a Parokia nyingine
Parokia ipo katika dekania ya Mt Joseph, kata ya kivukoni, mtaa wa sokoine/Manisfeld/bridge
Parokia zinazounda dekania hii ni kama zifuatazo
- Parokia ya Mt. Joseph
- Parokia ya Msimbazi
- Parokia ya Keko
- Parokia ya Upanga
- Parokia ya Chan’gombe
- Parokia ya Burahati
- Paarokia ya Mafia
- Parokia ya Muhimbili
- Parokia ya Buguruni
- Parokia ya Kurasini
- Parokia ya Mtoni na
- Parokia ya Mikoroshini
Parokia ilizaliwa 1889.
Mpaka 2016 ilikua na idadi ya waumini 1195
Parokia ya Mt Joseph ina jumuiya zipatazo 21, na zinatumia majina ya watakatifu.
kila jumuiya ina viongozi walio chaguliwa kwa mujibu wa katiba ili kuziongoza jumuiya kwa kadiri ya maelekezo.
Kuna wastani wa kaya 5 hadi 7
JNNk nyingi zinasali siku ya jumamosi asubuhi na baadhi zinasali siku za wiki jioni saa moja, na mwongozo unaotumika ni wa sala za JNNK
Maudhhurio katika JNNK ni ya wastani na kumbukumbu zinahifadhiwa
Jumuiya zinatembelewa mara mbili kwa mwaka mara moja kubariki nyumba na familia, na ya pili ni kipindi cha mavuno
JNNK /Kanda /Mitaa zinaadhimisha misa za watakatifu wao mara mbili kwa mwaka, na misa huadhimishwa katika JNNK.
HUDUMA ZA KIROHO
Huduma za kiroho zitolewazo ni kama zifuatazo:
Kuwatembelea na kuwaombea wagonjwa, na kingine ni matendo ya huruma
Vyama vya kitume ambavyo vinafanya kazi katika parokia ya Mt Joseph ni;
UWAKA, WAWATA, UTOTO MT, SHIKWAKA, LEGIO MARIA, MOYO MT WA YESU n,k
Huduma za kiroho pia zinatolewa ikiwa ni kwa kuombea wagonjwa na matendo mbalimbali ya huruma
Changamoto
Changamoto zilizopo ni kwamba waumini wengi wanatoka mbali kadiri ya hali halisi ya makazi ukizingatia parokia ipo katikati ya mji.
Uongozi
Kamati tendaji ipo na imekamilika
Halmashauri ya walei parokia inaundwa na kamati tendaji, viongozi watano kutoka JNNK pamaoja na VVK Kukutana hua ni mara mbili kwa mwaka kila inapobidi wajumbe hua ni kati ya 32
Agenda na taarifa za vikao hupatikana kwa wakati na zinatunzwa.
Bado hapajakuwepo ofisi ya Halmashauri ya Walei parokia, ofisi inayotumika ni ya waalimu
Njia kuu za mawasiliano katika kufikisha taarifa ni Barua pepe yaani (E mail),makundi ya whatsaap, simu, barua na mawasiliano ya ana kwa ana
Anuani ya barua pepe ya Parokia ni stjosephdsm@gmail.com
Zipo kamati ndogo ndogo za kikatiba za Halmashauri ya Walei kwa mujibu wa katiba na zimekamilika.
Na pia zipo kamati ndogo ndogo zisizo za kikatiba zilizoundwa katika Parokia nazo ni ; Kamati ya afya , kamati ya Ulinzi na kamati ya Mavuno.
Kamati ndogo ndogo zote zina mjumbe wa kamati tendaji na hata zile zisizo za kikatiba , mjumbe huyo ndiye anawakilisha taarifa ya kamati kwenye kamati Tendaji
Zipo pia kalenda za matukio ya mwaka kiparokia.
Waumini wanaarifiwa kuhusu mipango ya Parokia kwa ushiriki kikamilifu kwa kupitia ;Matangazo pale inapobidi, na kwa kupitia vikao.
Vyama ,Mashirika na Jumuiya za kitume
Vyama, mashirika na jumuiya za kitume ni kama vifuatavyo:
- Uwaka
- Wawata
- Viwawa
- Moyo Mtakatifu wa Yesu
- Karismatiki na
- Kwaya tano
- Utoto Mtakatifu.
Vyama na vikundi vyote vya kitume vina fanya kazi kulingana na katiba
Hivi vyama havina wanachama wa kutosha , lakini baadhi ya vyama vinawanachama wengi Zaidi
Vyama na vikundi vya kitume vinafanya kazi kulingana na katiba ya Hamashauri ya walei ijapo kwamba vingine utendaji wake ni hafifu
Vyama hivi baadhi vinaofisi parokiani mfano WAWATA, kwaya na wengine wanatumia ofisi zilizopo na vifaa wanavyo.
Vyama hivi vinasimamiwa na kamati tendaji na Paroko ndio mlezi wake, lakini pia baadhi vina wafadhili.
Taarifa na repoti ya pamoja na fedha unachangamoto katoka utolewaji wake, sio wote wanao wakilisha taarifa mara kwa mara parokiani
Moja katika mambo ya kujivuni yaliyo fanywa na VMJ ni maelewano na mshikamano ,pia kuadhimisha siku ya VMJ parokiani inasaidia kukuza vipaji mfano kuimba na uchoraji.
Semina mbalimbali katika uendelevu wa Imani, uongozi na utegemezaji.
Parokia inaendesha semina mbalimbali katika kuwezesha makuzi ya kiimani kwa waumini kupitia JNNK ikiusisha semina na mafungo mbalimbali yanayoandaliwa na vyama vya kitume ikihusisha pia makongamano mbalimbali yote hii ni katika kutengeneza makuzi ya kiroho
Uongozi wa Parokia kamati Tendaji na H/Walei Parokia wanapatiwa semina, zipo semina kadhaa ambazo zimesha tolewa baada ya uchhaguzi ikiambatana na hija na semina pamoja na zile zilizoandaliwa na jimbo.
Hali ya kiimani katika parokia inaonekana kuimarika , na hii inajionyesha katika ibada mbalimbali mfano Kuabudu Ekaristi takatifu n.k
Hali ya utoaji ni nzuri na unaonekana kukidhi mahitaji.
Hali kadhalika utoaji wa zaka kwa amri ya kanisa unaongezeka japo haujafikia kiwango kwa kadiri inavyo tarajiwa.
Parokia inatoa michango kamili ya jimbo kama ilivyo pangwa na kwa wakati.
FEDHA NA MIPANGO
Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa jimbo
Mapato na matumizi ya parokia yanajulikana na waumini, na taarifa inatolewa mara mbili kwa mwaka
Matoleo ya dominika yanatangazwa kwa waumini kila dominika inayofuata
Fedha zote zinazopatikana zinapelekwa benki kwa wakati.
ULINZI NA USALAMA
Hali ya ulinzi na usalama parokiani ni nzuri
Walinzinzi wanaotumika ni wa kampuni binafsi, na pia zipo kamera (CCTV)
Maendeleo ya kiuchumi
Katika kukuza kipato cha parokia kumeanzishwa miradi mbalimbali kama mradi wa kuegesha magari
Mradi kuuuza CD za nyimbo mbali mbali za dini na vitabu dini, Rozali Biblia n.k
Ukarabati wa majengo unaendelea, na mpango wa ujenzi wa st Joseph tower
Idadi ya mapadre inatosha ila liko pendekezo la kuongezwa padre mmoja
Waumini waliojiunga na shirika la dada wadogo ni watatu
Wanafunzi wa seminari ni watatu pia