DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA MSIMBAZI
Jina la Parokia ni msimbaziSomo wa parokia ni Bikira Maria mama wa huruma
Mahali parokia ilipo kijiografia ni kawawa road, Wilaya ya ilala katika, Dekania ya St Joseph.
Idadi ya waumini mpaka 2013 inaonyesha kuwa ni 8770 hii ni kutokana na sense ya mwaka 2013.
Parokia ilizaliwa 1952
Mpaka sasa parokia ina kigango kimoja kariakoo
Parokia ina JNNK 59 yenye kaya 20 kwa jumuiya , Viongozi wake wamechaguliwa kwa kura kwa mujibu wa katiba.
Huduma za kirohosiku za jumamosi kwa kushirikishana neno-Huduma zingine zitolewazo ni pamoja na kutembelea wagonjwa , ekaristi na mafuta ya misa.
Parokia inaandaa semina mbalimbali pamoja na makongamano ili kukuza imani na makuzi ya kiroho ikisaidiana na vyama vya kitume Huduma za kiroho hutolewa kupitia JNNK kwa kukutana pamoja
Parokia imetaa wanafunzi ambao wameenda kimasomo katika seminari mbali mbali.
- Visiga wanafunzi wawili (2)
- Maua seminary wawili (2) na
- Kihonda wanafunzi 4
Padre Mkude na sister Agnes ni moja ya matunda ya Parokia ya msimbazi
UongoziParokia ina kamati tendaji ambayo hukutana kila mwezi na kupanga malengo mbalimbali ya Parokia.
Halmashauri ya walei Parokia imeundwa na wajumbe 295 ambao umetokanan na kamati tendaji yenyewe, vyama vya kitume kama UWAKA WAWATA SHIKWAKA, UTOTO MTAKATIFU MOYO MT WA YESU N.K
Taarifa mbalimbali kuhusu Parokia zinapatikana kwa kupitia Barua pepe yaani E mail, Whatsaap group, Simu, Barua na hata taarifa za mdomo.
Njia nyingine zinazotumika kuwafikishia waumini taarifa juu ya mipango ya parokia ni kupita matangazo baada ya ibada na kupitia mbao za matangazo.
Parokia imeunda pia kamati ndogo ndogo kama zifuatazo;
- Kamati ya ulinzi
- Skauti
- Kamati ya ardhi
Zipo pia kalenda ambazo zinaonyesha matukio mbalimbali ya mwaka kiparokia
Vyama ,mashirika na jumuiya za kitume(VMJ)
Kwa idadi vipo 11 navyo ni
- UWAKA
- WAWATA
- VIWAWA
- Legio Maria
- Moyo Mt wa Yesu
- Shirikisho la kwaya.
- Utoto Mtakatifu n.k
Taarifa za zedhaParokia ina wajibu wa kuandaa bajeti kila mwaka wa fedha na mapato na matumizi kusomwa mara moja kila mwaka kila mwaka wa bajeti.
Matoleo yote ya kila dominika yanatangazwa kwa waumini kila dominika inayofuata
Kwa kadiri ya utaratibu, fedha zote hupelekwa benki.
MiradiParokia ina mradi wa duka, vitu vinavyo uzwa ni pamoja na Biblia, Mishumaa, tasbii, n.k
Changamoto
Moja ya changamoto kubwa iliyo jitokeza ni mgogoro wa mipaka na petro station iliyo karibu.