DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA MBURAHATI
Somo wa Parokia ni Familia Takatifu
Kijiografia Parokia ipo Mburahati, kwa upande wa kaskazini inapakana na parokia ya manzese na parokia ya tandale, kwa upande wa kusini inapakana na parokia ya Msimbazi, kwa upande wa magharibi inapakana na parokia ya Luhanga na upande wa mashariki inapakana na parokia ya Magomeni.
Parokia ipo dekania ya Mt. Yosefu, ilizaliwa mwaka 1974
Ina jumla ya waumini 5824 hii ni kutokana na sesa ya 2017, sense nyingine inatarajiwa kufanyika 2019
Parokia haina vigango, na inatumia majina ya kanda na mitaa, mitaa na jumuiya zote zinatumia majina ya watakatifu, uongozi umekamilika kwa jumuiya ,vyama vya kitume na mitaa yote kwa chaguzi zilizofanyika 2016
Parokia ina kanda 4
Parokia ina jumla ya jumuiya 79 na inatumia majina ya watakatifu
Kila jumuiya ina wastani wa waumini 79 na kaya 15 hadi 25, kwa sasa maboresho hayahitajiki.
Sala za jumuiya ndogondogo zinafanyika siku ya jumamosi asubuhi saa 12:30 asubuhi, Jumatano na ijumaa ni saa 1;00 usiku kwa kutumia mwongozo wa wa sala ya jumuiya ndogo ndogo za kikristo.yaani Bibllia na shajara.
Mitaa husali mara moja kwa Mwezi, Kanda husali kulingana na matukio ya Kiparokia.
Mahudhurio kwa ujumla sio mabaya na yanrekodiwa.kakini kuna changamoto kwa wanaume na vijana kuhudhuria jumuiya , lakini jitihada zinafanyika katika kuwahamasisha ambazo zinafanywa na vyama vya kitume na kamati tendaji.
Upo mpango wa kuwatembelea JNNK, Kanda na mitaa.Na mpango huo ni makhsusani siku za maadhimisho ya kijumuiya , kikanda na Mitaa.
Uongozi umekamilika kwa jumuiya ,kanda na vyama vya kitume vinavyoanzia ngazi ya jumuiya
Uongozi wa halmashauri za jumuiya na mitaa hukutana kila mwezi mara moja na pia wakati wa dharura.
Huduma za kiroho zitolewazo katika JNNK/Mitaa ni kama kusaidiana wakati wa shida na raha , mfano wakati wa ugonjwa , Misiba ,harusi, Semina za Kiroho na huduma za kijamii katika pia kushirikishana mambo ya kiuchumi kwa viongozi wa jumuiya na waumini wote. Upo mkakati wa endelevu kuhusu bima ya afya kwa waumini.
Chanagamoto zilizopo katika kuzihudumia JNNK;
Baadhi ya viongozi kushindwa kutimiza majukumu yao, mfano ;Waumini kutosema sakramenti wanazozikosa.
Mahudhurio yasiyoridhisha kwa makundi kama vile Viwawa na Uwaka
Baadhi ya viongozi kutokuifahamu vizuri katiba ya Halmashauri ya walei na kuongoza Zaidi kwa mazoea.
UONGOZI
Kamati tendaji ipo na imekamilika.
Kamati tendaji hukutana mara moja kila mwezi siku ya Alhamisi au siku nyingine kwa kadiri ya mahitaji saa moja usiku.
Halmashauri ya walei ya parokia inaundwa na Kamati tendaji ya parokia, viongozi 5 kutoka kila mtaa, wenyeviti kutoka vyama vya kitume ngazi ya Parokia na kanda.
Mawasiliano ya kamati Tendaji na halmashauri ya Walei hutolewa kwa kupitia matangazo siku za Dominika.
Agenda na repoti za vikao zinapatikana kwa muda muafaka na zinatunzwa.
Parokia inayo ofisi ya Halmashauri ya Walei na ina vitendea kazi vinavyo kidhi mahitaji kwa sasa,
Njia za mawasiliano zingine zinazotumika ni mitandao ya kijamii kama vile whatsap, barua pepe, mawasiliano ya simu, na matangazo ya kwenye ubao na siku za dominika.
Email Address ya Parokia ni mburahatiwalei@gmail.com
KAMATI
Kamati za kikatiba za H/walei ni kama zifuatazo;
Kamati ya malezi na familia, Ibada na Liturjia, Haki na Amani, Elimu ya Dini, Mafundisho ya kanisa na teolojia, Kamati ya Mipango, Kamati ya Uchumi na Fedha
Na wajumbe wake wanatokana na wana halmashauri ya walei Parokia
kamati nyinginezo zisizo za kikatiba ni;Kmati ya Ujenzi, Afya, Sherehe, Ulinzi na ardhi. Kamati hizi hukutana mara kwa mara kulingana na mahitaji
kamati hizi ndogo ndogo za kikatiba na zisizo za kikatiba zinaripoti kwenye mkutano wa wa Halmashauri yay a Walei ya parokia na wakati mwingine kanisani wakati wa Ibadan a hakuna mwingiliano wowote lakini pia zina mahusiano mazuri.
Kuna Kamati ya ujenzi, afya, sherehe, ulinzi na ardhi. Kamati hizi zinaratibu shughuli za parokiani.
Dira, Malengo, Mikakati ya Parokia ipo kama ifuatavyo;
1. DIRA:Ni kitovo cha Ubora cha kushauri ipasavyo hierakia ndani ya Parokia ili kuyatakatifuza malimwengu na kupeleka wana parokia mbinguni.
2. MALENGO:Kuongoza na kuratibu utekelezaji wa maazimio na malengo yay a Halmashauri ya Walei parokia katika ngazi ya Parokia ,Kanda, Mtaa, Jumuiya na vyama vya kitume ngazi ya Parokia.
3. MIKAKATI: Kujenga uwezo kwa Viongozi wa Halmashauri wote katika kusimamaia na kutekeleza malengo yaliyowekwa katika ngazi mbalimbali.
Kuunda na kusimamaia kamati ndogo ndogo za kikatiba, na zisizo za kikatiba
4. Kuwepo kwa Taratibu za kifedha zinazokubalika na kuheshimiwa na wana halmashauri wote.
5. Kubuni na kutekeleza miundombinu bora ya kiteknologia ya mawasiliano, ulinzi na namna bora ya Kuabudu.
Ipo kalenda ya matukio ya mwaka ya Kiparokia.na imeandaliwa kwa ushirikishwaji wa waumini na kwa kufuata kalenda za dekania na Jimbo.
Njia zinazotumika kuwaarifu waamini wote kuhusu mipango ya Parokia ni kwa kupitia viongozi wanaoudhuria mikutano ya halmashuri ya walei na kwa kupitia matangazo ya kanisani siku za dominika na mitandao mbalimbali.
- Kuombea wagonjwa
- Huduma za misiba
- Kufungisha ndoa
- Sakramenti mbalimbali za kipaimara,n.k
- Semina za kiroho
- Pamoja na makongamano
VYAMA, MASHIRIKA NA JUMUIYA ZA KITUME (VMJ)
Vipo VMJ katika Parokia navyo ni;
UWAKA ,WAWATA ,VIWAWA, Utoto Mtakatifu, Wazee na wastaafu, Utume wa familia, Utume wa Fatima, Arimathea, Lejio Maria, Karesimatiki Katoliki, Wajane na wagane, Chama cha miito, Chama cha Mt. benezeti, Kwaya, Ministrant , Moyo Mt. wa Yesu, Jumuiya ya Neo-katekuminato, CPT, Kuna vikundi vingine ambavyo ni kama Scaut katoliki, marafiki wa Tumaini Media, Marafiki wa Gosple singer
Baadhi ya vikundi vina wanachama wa kutosha vingine havina kabisa.
Vyama vyote vinatimiza wito wa utume wao na vinafanya kazi kulingana na katiba ya H/walei.
Wawata wana ofisi lakini vyama vingine havina ofisi wala vifaa vya kutosha.
Vyama vyote vina lelewa na Parokia kwa usimamaizi wa baba Paroko
Kwa sasa hakuna changamoto zozote katika VMJ ambazo zinaweza kuhatarisha Imani katoliki.na ushiriki wa VMJ katika Paarokia uoo vizuri
Vyama vyote vya kitume vipo mstari wa mbele katika kufanya mambo mbalimbali ya kuboresha parokia pale ambapo kuna hitaji hilo. Mfono; wawata walifanya ukarabati wa nyumba ya Mapadre kwa kuweka madirisha ya kisasa na kununua viombo vya jikoni.Uwaka walianza ukarabati wa kanisa kwa nguvu zao, Karismatiki walitembelea nyumba kwa nyumba kujua matatizo ya kila familia na kuwakilisha taarifa kwa baba paroko.n.k
Semina mbalimbali zinatolewa kwa viongozi na Vyama vya Kitume mfano; semina za uongozi, ujasiria mali na semina za kiroho.
Hali kadhalika Uongozi wa kamati tendaji na halmashauri ya walei wameshapatiwa semina za uongozi, na mkakati huo ni endelevu katika stadi mpya.
Semina za kiroho zimepangwa kufanyika mara 15 kwa makundi tofauti kulingana na kalenda ya Parokia.
Hali ya Imani iko vizuri na inaendelezwa kwa juhudi kupitia Mafundisho mbalimbali ya Biblia na katekesi yanayofanywa na mapadre n a watawa wa kike, maketekista na vyama vya kitume
Utoaji kwa ujumla katika kanisa unaridhisha
Utoaji wa zaka kamili kama amri ya kanisa katika parokia ni mzuri, Waamini wanatumia kadi maalumu ya zaka na wengi hutoa kila siku za dominika kwa kadiri mungu alivyo wajalia.
Parokia inatoa michango kamili ya jimbo na kwa wakati.
FEDHA NA MIPANGO
Mpango wa fedha uunaotumika ni ule wa jimbo
Mapato na matumizi ya parokia yanajulikana klwa waumini na taarifa ya fedha hutolewa kila baada ya miezi sita.
Matoleo ya kila dominika yanatangazwa kwa waumini kila dominika inayofuata.
Fedha zote hupelekwa benki kwa wakati
ULINZI NA USALAMA
Hali ya ulinzi na usalama parokiani iko vizuri.
Parokia inatumia walinzi binafsi ambao ni waamini wenzetu ndani ya Parokia na hali ya ulinzi iko vizuri
Miradi inayoendeshwa na kanisa kwa sasa ni pamoja na ujenzi wa kanisa , Shule ya chekechea, mradi uliopo pembezoni mwa kanisa, na nyumba iliyo barabara ya ya kuelekea nyumba ya furaha na Amani ambazo kwa sasa zimepangishwa na waumini.
Mpango uliopo kwa sasa ni ujenzi wa kanisa kubwa la kisasa ambao unaendelea vizuri na unafanyika kwa nguvu ya waumini.
MAMBO YA JUMLA.
Hakuna mgogoro wa kimipaka katika parokia
Mpango wa kuwaendeleza waumini kiuchumi upo, zipo semina mbalimbali zinazotolewa kuhusu ujasiria mali, na mara kwa mara waumini wengi wamejiunga na vikoba. Na vikundi vya mkopo Mkombozi Benki mfano ni Wawata na shirika la wazee na wastaafu.
Idadi ya mapadre kwa sasa inatosheleza kutokana na idadi ya waumini.
Parokia ina mseminari mkubwa mmoja na waseminari wadogo kumi na moja.
Idadi ya waamini waliojiunga na utawa wa kike ni watatu na wa kiume ni saba.
Maandiko ya historia ya Parokia yapo ,hali kaadhalika picha za zamani na za sasa za mapadre na za waumini zipo.