DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA KURASINI
Jina la Parokia ni Parokia ya Kurasini , msimamizi wake ni Mt Maurusi.
Parokia ilizaliwa 1970
Parokia ya mtakatifu Maurus kijiogrfia ipo kurasini, Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es salaam
Parokia ipo katika dekania ya mtakatifu Joseph jimbo kuu la dar es salaam.
Parokia kwa mujibu wa sensa 2016 ni waumini wapatao 3450,
Kwa ujumla parokia haina vigango
Parokia ya Mt Maurusi ina kanda saba(7)
Katika parokia ya Mt Maurus kuna jumuiya zipatazo 46 na jumuiya zote zinatumia majina ya watakatifu
Kila jumuiya ina wastani wa kaya 15 kutokana na maelekezo. hapahitajiki maboresho yeyote kwa sasa.
Jumuiya ndogondogo nyingi zinasali siku ya jumamosi
Katika Parokia ya Mt Maurus viongozi wa kamati tendaji ndio wanotembele jumuiya na kanda. Mapadre wanatembelea familia moja moja
Katika Parokia jumuiya zina utaratibu wa kuadhimisha sherehe wa somo wa jumuiya na kanda.
Viongozi wote wanachaguliwa kwa mujibu wa katiba . Pale panapotokea mapungufu ya viongozi uchaguzi huitishwa tena na kujazwa nafasi iliyo achwa wazi labda kwa sababu ya kushindwa uongozi au kuhama.
Viongozi
Katika parokia viongozi wa kamati tendaji ya parokia wanao utaratibu wa kukutanan maramoja kwa mwezi
Parokia inaandaa semina za viongozi wake kikanda na kiparokia , mfano katika kipindi cha mwaka 2017 kumekuwa na semina kwa kamati tendaji na halmashauri ya walei parokia, semina mbili zilifanyika zinazohusu uongozi
Huduma zitolewazo
Huduma zitolewazo ni pamoja na huduma za kuombea wagonjwa inayotolewa na paroko na paroko msaidizi
Pia ipo kamati ya afya ya parokia ambayo huusika moja kwa moja katika kuwatembelea wahitaji katika jumuiya na familia na kuwapa mahitaji mbali mbali
Paroko na paroko msaidizi wamekuwa pia na muda ambao wameupanga wa kuzitembelea familia zenye migogoro mbalimbali
Halmashauri ya walei parokia inaundwa na viongozi wa kamati tendaji ya kanda na wenyeviti wa vyama na vikundi vya kitume ngazi ya parokia
Mawasiliano
Njia kuu za mawasiliano ni matangazo ya kila dominika, simu, barua pepe yaani E mail ,
Kamati
Katika paarokia zipo kamati za kikatiba na zisizo za kikatiba, kamati zisizo za kikatiba ni kama zifuatazo
-kamati ya uhamasishaji wa sherehe
-kamati ya ulinzi
-Kamati ya afya
-kamaati ya ardhi na ukarabati majengo
Kamati zote hizi zina umuhimu kiparokia, na haziingiliani kimajukumu isipokua pale ambapo itaonekana kuna umuhimu wa kushirikiana.
Malengo
Kuwaimarisha wakatoliki na wasio wakatoliki kumjua kristo na Mungu kwa kukua kiimani hasa kuishi kwa sakramenti takatifu yaani Ubatizo , Komunio , Kipaimara, Ndoa na miito mitakatifu ya utawa na upadre.
Moja ya malengo mengine ya parokia ni kuifanya parokia iweze kujitegeme kwa kupitia vitega uchumi kama kumbi na miradi mingine itakayoonekana inafaa kwa sasa na nyakati zijazo baala ya kutegeme sadaka na michango kutoka kwa wa umini
Vyama na vikundi
Parokia ina vyama vya kitume vipatavyo 13,
Vyama na vikundi vipo chini ya kamati tendaji.
Taarifa za fedha na vyama vya vikundi hutolewa kila mwisho wa mwaka, na baada ya miaka mitatu hufanywa uchaguzi.
Ushiriki katika vyama vya kitume na dekania na jimbo ni mzuri na upo ushirikishwaji.
Fedha
Katika parokia mpango wa fedha unao tumika ni ule wa jimbo
Mapato na matumizi ya fedha yanajulikana kwa waumini, na yanatolewa mara nne kwa mwaka na kusomwa katika mkutano wa halmashauri ya walei parokia
Matoleo ya kila dominika husomwa kwa waumini dominika inayofuata
Michango ya jimbo inatolewa kwa utaratibu kama ambavyo maelekezo yanavyo takiwa
Changamoto
- Fedha hazipelekwi banki kwa wakati na hivyo kujikuta zinafanyiwa matumizi mengine
- Utoaji wa zaka kama amri ya kanisa ni hafifu na wa kusuasua
- Mapadri na watawa bado wanaonekana kuwa hawatoshi kutokana na mahitaji
Ulinzi na usalama
Ulinzi na usalama parokiani ni wa kuridhishisha kwa kushirikiana na kamati husika
Miradi
Hakuna mradi unaoendeshwa na parokia
Wanaafunzi ambao wanasoma seminari kutoka parokia ya maurusi ni Wawili tu mpaka kufikia 2017, na mtawa yuko mmoja kutoka shirika la masister wa usambara
Kihistoria
Hakuna mabadiliko yeyote ya kihistoria.