DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA TANDALE
HISTORIA YA PAROKIA YA KAROLI LWANGA
TANDALE
Parokia ya Mt. Karoli Lwanga – Tandale ipo katika Jimbo kuu la Dar es Salaam, wilaya Kinondoni, kata ya Tandale, mtaa wa Sokoni, ndipo Kanisa lilipo. Kwa upande wa kusini inapakana na Parokia ya Mashahidi wa Uganda (Magomeni), Mashariki Parokia ya Mwananyamala, Kaskazini Parokia Kijitonyama na Parokia ya Sinza, Magharibi Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu (Manzese) na Magharibi Kusini linapakana na Parokia ya Familia Takatifu (Mburahati).
Parokia yetu ilizinduliwa tarehe 17 April, mwaka 2005. Kabla ya hapo ilikuwa Kigango cha Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu (Manzese) iliyoanzishwa mwaka 1978. Kabla ya hapo ilikuwa kigango cha Parokia ya Mashahidi wa Uganda (Magomeni).
Jinsi Kigango cha Tandale ilivyoteuliwa kuwa Parokia:
Padre Helmut Revers Mafr aliyekuwa paroko ya Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu tangu mwaka 2002 hadi 2011 akiulizwa swali, Kwani nini aliomba Tandale iwe Parokia? alisema:
1. Nilizingatia idadi ya waumini walipo Tandale.
2. Niliona kuwa waamini wa Tandale wana uwezo wa kuwalisha Mapadre.
3. Mazingira ya Uislamu yanafanana na lengo la Shirika.
4. Wakristo wenyewe waliomba kwa muda mrefu Tandale iwe Parokia.
5. Ni Kigango cha kwanza Katika Parokia ya Manzese.
Ndipo jukumu la kuomba Viongozi wa Shirika ambao walikubaliana na ombi hilo kutekelezwa, na Baba Kardinali alikubali pia.
January mwaka 2005 Wamissionary wawili walioteuliwa kuja Tandale walifika Dar es Salaam. Hawa walikuwa Mbelgiji Willy Schoofs - wakati huo alikuwa na miaka 64, na Pd. Yago Abelado (33) toka Hispania. Wakati huu Pd. Willy Schoofs aliyekuwa mkurugenzi wa chuo cha Kiswahili Kipalapala, Tabora, aliteuliwa kama Paroko. Pd. Yago aliyekuwa Kipalapala akijifunza Kiswahili, ilikuwa utume wake wa kwanza. Tarehe 8 mwezi wa kwanza walipofika Tandale walipokelewa na mwumini Ndg Augustino Kashuli. Moja kwa moja walianza kutafuta chumba cha kukaa. Walikipata katika eneo la Argentina katika Jumuiya ya Mt. Anuarite kwa gharama ya Tsh 70,000 kwa mwezi. Shirika la Wamissionary wa Afrika liliwasaidia kununua vifaa vya nyumbani na walianza kuishi huko. Mwanzoni walikuwa wanajihudumia wenyewe kama kwenda sokoni, kupika, kufagia, kupiga deki, kufulia, nk. Watu waliwapokea vizuri lakini walishangaa kuona Mapadre kukubali kuishi katika mazingira ya aina hiyo.
Mwezi wa March mwaka huo hawa mapadre walianza kujenga Ofisi tatu za Parokia kwa sababu waliendesha huduma zao bila ofisi. Tarehe 3 mwezi wa March Mapadre wa Tandale waliwaalika mara ya kwanza Mapadre wa Manzese kushiriki pamoja chakula cha mchana katika nyumba yao ya uswahilini Argentina.
Misa ya uzinduzi wa Parokia ilipangwa tarehe 7 April, 2005, lakini iliahirishwa kutokana na kifo cha Baba Mtakatifu Yohane Paulo ya II. Baba Mwadhama Kardinali Pengo alienda Roma kwa Ibada ya mazishi na uteuzi wa Baba Mtakatifu mpya.Tarehe 8 May, 2005, Tandale ilizinduliwa rasmi kuwa Parokia. Baada ya Misa Baba Mwadhama alienda kubariki nyumba ya mapadre uswahilini, ambapo baada ya kushuhudia hali halisi ya mazingira, aliwaalika ofisini kwake Mapadre wote wawili kuwahimiza waweke kipaumbele kujenga nyumba rasmi ya Mapadre katika eneo la Kanisa. Parokia ilipozinduliwa ilisimikwa chini ya ulinzi wa Mt. Karoli Lwanga, mmoja wa mashahidi 24 wa Uganda walioifia imani baada ya kuinjilishwa na Wamisionary wa Afrika.
Mapadre walianza kazi zao na matembezi ya jumuiya ndogo ndogo, wagonjwa na familia, kuimarisha kiroho maisha ya waumini kupitia semina mbalimbali, na kuboresha vyama vya Kitume (Wawata, Moyo Mtakatifu wa Yesu, Msamaria Mwema, Vijana, Arimatheya, Shikwaka, Karismatiki, nk.)
Tarehe 1 mwezi wa May 2006 Severin Joseph Mhina, mzaliwa wa Kilosa Morogoro alianza kazi rasmi kama katekista wa kwanza. Alipewa makazi ndani ya eneo la Kanisa. Pamoja na kazi yake ya Ukatekesi, alikuwa pia mlinzi wa mali za Kanisa hasa usiku na mhudumu wa Sakristia.
Masista:
Tangu mwanzo Masista wa Shirika la MSOLA walikuwa wanawajibika katika kazi za parokiani. Sr. Sophie Kitoga alianza kufanya kazi kama mlezi wa Wawata na Sr. Denisse Forcier alikuwa mwalimu wa wakatekumeni watu wazima. Baada ya kuona kwamba wengi kati yao hawakujua kusoma na kuandika alianza taratibu huduma ya kuwasaidia watu wazima kujifunza kusoma na kuandika. Mwanzoni alikuwa anatoa huduma hiyo kwa wakatekumeni tu, na baadaye alikuwa anatoa huduma hiyo kwa wahitaji wengine bila kujali utofauti wa imani.
Mwezi wa October Mapadre walianza kufanya mauhusiano na PASADA ambao walikuja kutoa seminar kuhusu ukimwi. Parokia bado hakuwa na nafasi ya kuwapa ofisi lakini Mapadre waliona umuhimu wa kupanga utaratibu wa kuanzisha huduma hiyo parokiani.
Mwezi November, 2005, Jumuiya ya Mapadre iliongezeka. Pd. Deogratias Ngowi aliyekuwa anakuja mara kwa mara kuhudumia Parokiani Tandale aliteuliwa rasmi akae na kufanya kazi Tandale. Mapadre hawa walifanya kazi za utume kwa upande moja na kwa upande nyingine walilazimika kupanga shughuli za kuongeza eneo la kanisa, kupanga ujenzi wa nyumba ya mapadre na pia kumaliza ujenzi wa kanisa. Pd. Helmut alipokabidhi Kanisa kwa wanatandale alitangazia kwamba ni jukumu la waumini kukamilisha sehemu ya ujenzi wa Kanisa uliobaki.
Mwezi wa January 2006 Masista waliimarisha Jumuiya ya Masista kwa kumteua Sr. Suzy Bosuh – mzawa wa nchi ya Ghana. Sista huyo alianza kufanya kazi na wasichana wasiokwenda shuleni. Alikuwa anawafundisha kazi za mikono kama kushona, na pia alikuwa anafundisha Kiingereza na na kufundisha dini shuleni. Masista walianzisha Salome Centre – kituo cha kuwasaidia wasichana kutoka mazingira magumu. Sr. Suzy alikuwa msimamizi wa shughuli zote za kituo hicho.
Tarehe 8 mwezi wa March 2006 Pd. Willy Schoofs – Paroko wa kwanza wa Parokia Tandale alilazimika kuondoka na kurudi Ubelgiji kwa matibabu kutokana na matatizo ya kiafya. Lakini kabla ya kuondoka aliweza bado kufanya matembezi ya msalaba mara ya kwanza tangu uzinduzi wa parokia katika kipindi cha Kwaresima 2006.
Mwaka 2006 Parokia ilianzisha huduma ya Malezi na Elimu kwa yatima kwa sababu mapadre na masista waliona kwamba watoto wengi hawamalizi shule ya msingi kutokana na hali ya uchumi na mapungufu ya malezi katika familia.
Mwezi wa Mei Monsenyori Mbiku alialikwa kuja kuhamasisha moyo wa utoaji hasa Sadaka na Zaka na maendeleo ya Kanisa na alimtangaza Pd. Yago Abelado kuwa Paroko mpya wa Parokia Tandale. Aliposimikwa kuwa Paroko alikuwa kijana kuliko Maparoko wote wa Jimbo Kuu la Dar es salaam. Monsignore aliendesha Mnada ukumbini kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mapadre. Padre Yago aliandika kwatika kitabu cha kumbukumbu kwamba hapo tulitambua ugumu wa uchangiaji wa waamini wa Tandale, maana pamoja na jitihada ya Monsenyori Mbiku hatukufikia hata shilingi milioni moja. Siku hiyo ilimalizika kwa majonzi kwa vile aliyekuwa Mwenyekiti wa JNN ya Mt. Helena aliugua ghafla Kanisani na kufariki siku hiyo hiyo.
Mwaka huo Parokia ilifanyikiwa kukamilisha mambo makubwa mawili. Ya kwanza masista walipata msaada kutoka kwa Balozi wa Canada na walifanikiwa kununua nyumba ya jirani Mzee Charles Giiti iliyopakana na kanisa. Nyumba ilinunuliwa kwa ajili ya kuendesha shughuli za Salome Centre, lakini Balozi aliruhusu Mapadre kuishi katika nyumba hiyo kwa muda kwa sababu mapadre bado walikuwa wakiishi uswahilini. Mapadre walihamia rasmi katika nyumba yao Parokiani na kuyaacha makazi ya uswahilini mtaa wa Argentina tarehe 5 mwezi wa September 2006. Ya pili, mwaka huu mapadre walimaliza ujenzi wa Ukumbi wa Parokia.
Mwaka 2006 Sr. Sophie alimaliza kazi Tandale na alipata uhamisho kwenda Kongo DRC. Pia Mapadre walipata msaidizi mpya Pd. Magloire Bamali – mzaliwa wa Togo. Mwaka huo pia Frateri wa kwanza alikuja kufanya miaka miwili ya kichungaji parokiani Tandale.
Mwaka uliofuata jitihada za kuboresha huduma za maendeleo zilizaa matunda kwa kununua kiwanja cha Ndg. Omari kilichokuwa na nyumba mbili. Nyumba kubwa ilikarabatiwa na darasa la Ushonaji ambalo sasa vyumba vingine vinatumika kwa ofisi ya TASODEC (Tandale Social Development Centre) na ofisi ya ushauri.
Tarehe 4 Julai Vijana walifanya utambulisho wa vyama mbalimbali ndan ya umoja wao kikiwemo chama cha kardinali Lavigeriki ambacho kilihusika na kuamsha miito kati ya vijana wa mt Karoli Lwanga kilichokua na jukumu la kuwahamasisha vijana na kuwavutia kujiunga na Utume wa Kanisa.Siku hiyo vijana wakisaidiwa na Katekista Severine ,walicheza igizo la maisha ya watakatifu mashahida wa uganda likimwonyesha pia kardinali Lavigeria akiwatuma Pd Semeoni Lourdel na wenzake kwenda Uganda kuinjilisha. Igizo hili lilisisimua sana waumini na kuongeza ufahamu na kumjua ni nani Mt Karoli Lwanga.
Tarehe 4 agosti Palifanyika matembezi ya Askofu Methodius Kilaini , Katika nafasi hii alitembelea wagonjwwa hadi eneo la BK na uwanja wa fisi . Baada ya chakula cha mchana nyumbani kwa Mapaadre Argentina, Baba Askofu alipata nafasi ya kukutana na vikundi mbalimbali vya Parokia, upekee aliokutana nao unamfanya asisahau mazingira aliyo kutana nayo. (sielewi) Hali kadhalika alisifu moyo wa kichungaji wa Pd Willy. Uhamasishaji wa maisha ya JNNK, matembezi ya wagonjwa na familia nyumbani kwao, semina ya wanandoa na Couples for Christ, Huduma ya wakolezaji kipindi cha kwaresma . Kwa upande wa Pd Yago, Askofu alistaajabu kushuhudia padre kijana kujituma katika mazingira ya hatarishii bila kuona kinyaa wala uwoga.
Katika jitihada za kuongeza eneo la kanisa na kuboresha huduma katika kipindi hichohicho kilipatikana kiwanja kutoka kwa mzee Bundala, Shukrani nyingi kwa mzee bundala kwa kukubali kuuza eneo lake, hali kadhalika shukrani kwa Jimbo kwa kusaidia ununuzi wa eneo mkwa gharama ya shilingi ml 3, na kwa kipindi hicho kiasi hicho kilikua ni kikubwa sana.
Kipindi cha mwwezi Septemba, semina mbalimbali zilifanyika kwa mwongozo wa karismatiki katika kuwakuza waumini kiimani. Semina ya neno la Mungu ilitolewa katika kanda zote. Pia semina ya siku 16 mwezi Octoba zililifanyika kuhusu UKIMWI iitwayo KIVUKO. Pd Deograteus Ngowi alikuwa akihudumu Parokia ya Tandale akitoke atiman House.
Mwezi Desemba palikuwepo matatizo ya kichungaji, ambapo palitokea manung’uniko kwa wakristo kukosa nafasi ya kutoa maoni yao, hatimaye mwezi Aprili 2016 palifanyika mkutano wa kwanza wa Halmashauri ya Walei. Na mwwawka huohuo maafanikio yalikuwepo ya kuweka tarazo kanisani.
Katika kipindi hichohicho masista wa MSOLA walitekeleza ombi la WAWATA la kupata masista wengtine ili waweze kusaidia huduma za maendeleo kwa wasichana, walimleta SR Suzy Bosuh.
Februari 26 Pd,Helmut Paroko wa Manzese alialikwa rasmi kuongoza Misa ya kwanza siku ya jumapili tangu Tandale kuwa Parokia
KIZITO CENTRE
Mwezi Aprili Huduma za malezi na Elimu kwa yaatima na walezi wao zilianza rasmi (mwanzo wana kizito bila jengo, na wakati huo walipokelewa yatima kuanzia shule ya msingi na wale waliomaliza elimu ya msingi bila kufaulu na wakiwemo walio acha shule bila kumaliza kwa sababu mbalimbali. Kigezo ilikuwa ni kwa wale wasio na uwezo wa kiuchumi ndani ya Tandale.
Tarehe 23, Aprili Balozi wa Baba Mtakatifu Nchini Tanzania Joseph Chennoth na Katibu wake, na baada ya kuona juhudi zifanywazo alitangaza msaada kutoka MORENI FUND kwaajili ya kutengeneza mabench ya kanisa na Altare ya Heshima. Hii ilitokana na mapadre kubidiika kutafuta wafadhili katika kukamilisha mahitaji.
Tarehe 20 Mei ilikua ni uzinduzi wa JNNK Parokiani kwa kuthamini JNNK kama vyombo vya uinjilishaji. Ilifanyika misa ikitanguliwa na maandamano mpaka kanisani.
Katika kipindi hicho hicho Paarokia ya Mt Karoli Lwanga iliteuliwa kuwa kituo cha kutolea msaada wa chakula Duniani WFP kupitia Jimbo Kuu la Dar es salaam, pia cha kula cha msada kwa wanaoishi na VVU na TB kwa Dini zote, zoezi lilifanikishwa kwa ugumu mno, kwani iitegemewa kuwa ingekuwa ni njia mojawapo ya kuweka mahusiano bora na madhehebu mengine na majirani halikadha na dini nyingine. Wajumbe wa ujirani mwema awalipeleka barua ya kutambulisha mradi huo kwa kanisa na misikiti yote ya eneo la Parokia lakini ilipokelewa kwa wasiwasi mpango huo wakidhani ni kampeni kati ya serikali na Kanisa Katoliki kuvuruga imani ya wasio wakatoliki, lakini zoezi hailikuwakatisha tamaa kuendelea kutoa huduma kwa wahitaji.
Mwezi huo huo palitolewa tena msada kutoka ubalozi wa Canada kwaajili ya maendeleo ya wanawake Salome Centre Kwa juhudi za Sr Denisse. Mabaye pia alikuwa Mkanada.
Tarehe 25 Juni ilikuwa ni kuanza kwa kozi ya chuo cha maisha ya Vijana 50. Ambayo inafanyika kwa jumuiya ishirini kwa mwaka mmoja. Kozi iliwasaidia sana Vijana kujijengea stadi za maisha Life skills) Na iliandaliwa na Pd Selvam(Mkurungezi wa huduma za Vijana Don Bosco uoande wa Africa Mashariki) Na walikubali Tandale iwe ya kwanza kupata huduma hii ya Kwanza Jimboni..Kazi hii ilifadhiliwa na Shirika la Selesians (Don Bosco).
Mwezi Julai Kazi ya ujenzi wa ukumbi wa Parokia ilikamilika na kupatia jina la mwanzilishi wa Shirika la Missionary wa Africa, na Charles Lavigerie akiwa ndio Kardinal wa kwanza wa Africa.
Na mwezi jula 23, Parokia lipata bahati ya kutembelewa na Balozi wa Hispania nchini Tanzania kutokana na mwaliko wa kirafiki toka kwa Baba Paroko Yago ambaye pia alikuwa raiya wa
Hispania, na katika kipindi hicho hichoo katibu msaidizi wwa kamati tendaji ya Halmashauri ambaye alikua mwanamke peke yake aliamua kujihuzulu kwa kutokuwa na nafasi ya kushiriki katika vikao.
Mwezi Agosti Sr Birgita alikaribishwa rasmi ambapo pamoja na shughuli mbalimbali za salome Centre alihusisha sana na huduma ya malezi ya watoto katika kanda na parokia kwa ujumla.
Mwezi Septemba Mapadre walihamia rasmi katika nyumba yao na kuacha makazi ya uswahilini mtaa wa Agentina, Eneo la wachafu camp walipokuwa wamepanga na katika nyumba ya Waislamu
Tarehe 09 Septemba Uchaguzi mkuu wa Parokia ulifanyika kwa kuchagua Kamati Tendaji ya Halmashauri ya Walei ya Parokia, Viongozi watano kutoka katika kila kanda walihudhuria, Mjumbe mmoja kutoka katika kila chama cha kitume na kusimamiwa na viongozi kutoka jimboni
Mwenyekiti alikuwa Ndg Jenes Marandu, M/Kiti Ndg Wasenslaus Kente, Katibu Ndg Celestine Midauli, Katibu Msaidizi Ndg Josephine Nyamwihula, Na mwekahazina Ndg Catherine Mnga’anya.
Tarehe 11 Septemba Kilizinduliwa raasmi kituo cha maendeleo ya akinamama (Salome Centre) na kuaalika wakina mama wengine waliotaka kujifunza zaidi kusoma na kuandika.
Tarehe 17 Septemba ilikuwa ni ukamilishaji wa Altare Nzuri ya Ekaristi Takatifu na ya neno la Mungu. Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ndiye aliye kuwepo kuweka Wakfu pamoja na kubariki sakafu ya kanisa, na aliangalia pia maendeleo mengine ya Kanisa kama vile Mabenchi ya Kanisa ukumbi wa Lavigeria, Nyumba ya Mapdre na Salome centre na kuvbariki shughuli nzima kwa ujumla.
Mwezi Mei Baraza la Maaskofu la Hispania lilitoa massda kuchangia ujenzi wa nyumba ya Mapadre. Na tarehe 20 Mei vijana waliokuwa wanasoma Chuo cha maisha walihitimu, na pia walifanya Graduation na Kutunukiwa Vyeti.
Tarehe 14 Octoba, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alifika Tandale kutoa sakramenti ya Kipaimara na ndio siku hiyo aliweka jiwe la msingi la nyumba ya Mapadre na ofisi za Parokia, Mkuu wa Shirika la Wamisionary wa Afrika, Pd Don Anderson alihudhuria. Ujenzi wa nyumba ya mapadre uliuanza mwezi Novemba.
Masista wa MSOLA katika kuboresha huduma za kimaendeleo. ya wanawake walianzisha kozi maalumu ya Ushonaji na kudarizi kwa wasichana na wakina mama. Walimu wawili wwaliajiriwa.
Katika kuwajenga waumini kiroho, semina mbalimbali pia zilitolewa, ikiwa na semina ya utoaji ambayo iliendesha na Monsenyori Mbiku katika kila Misa.
Na tarehe 17 Mei Waummini walishiriki katika Jubilei iliyofanyika Bagamoyo ya Shirika la Wamisionari wa Afrika ikiwa ni kumbukumbu ya Miaka 130 tangu wamisionary hao kufika Afrika.
Tarehe 30 Mei mwakilishi wa kwanza anatumwa kuhudhuria Hija Namugongo baada ya kupokea mwaliko toka Jimboni.
Na tarehe 19 Octoba ilikuwa ni siku ya uzinduzi rasmi wa kwa sherehe ya Wazee na Wastaafu wa Parokia kwwa kuanza na semina iliyoendeshwa na Pd Geoffrey Riddle.
Maparoko waliohudumu Parokia ya Mt Karol Lwanga:
Pd. Willy Schoofs, (2005 – 2006)
Pd. Yago Abelado, (2006 – 2011)
Pd. Binu Jose, (2011 – 2013)
Pd. George Athikalam, (2013 – 2015)
Pd. Tomasz Podrazik, (2015 --........)
Maparoko wasaidizi waliofanya kazi Tandale:
Pd. Yago Abelado, Pd. Deogratias Ngowi, Pd. Magloire Bamali, Pd. Binu Jose, Pd. Jean Noel Baraka, Pd. George Athikalam, Pd. Tomasz Podrazik, Pd. John Slinger.
Kamati Tandaji:
2003 – 2005 Mti: Genes Marandu; Mti Msaidizi Thomas Paulo; Katibu Selestine Midauli; Katibu Msaidizi Grace Kobelo halafu Josephina Nyamwihula; Andrea Lubarati.
2006 – 2009: Mti Genes Marandu, Mti Msaidizi Venceslaus Kente halafu Christa Ngairo; Katibu Selestine Midauli halafu Michael Hamisi, Katibu msaidizi Josephina Nyamwihula, Mwekahazina Catherine Mnganya.
2010 – 2013: Mti Genes Marandu, Mti Msaidizi Christa Ngairo, Katibu Michael Hamisi, Katibu msaidizi Josephina Nyamwihula, Mwekahazina Catherine Mnganya.
2014 – 2016 Mti Christer Ngairo, Mti Msaidizi Arcado Nchinga, Katibu Josephina Nyamwihula, Katibu msaidizi Mark Ringia halafu Sagnus Thobias, Mwekahazina Venance Adabu.
2016 - …: Mti Arcado Nchinga, Mti Msaidizi Peter Kagabo, Katibu Maria Shukuru Ngweta, Katibu Msaidizi Silvanus Maangiri, Mwekahazina Venance Adabu.
Mpaka sasa kuna vyama vya kitume vifuatavyo;
1.Uwaka; 2. Wawata; 3.Viwawa; 4. Utoto Mtakatifu; 5. Chama cha watumikiaji; 6. Legio Maria; 7. Moyo Mt wa Yesu; 8. Arimathaya; 9. Wazee na Wastaafu; 10. Wasamaria wema; 11. Shikwaka; 12. Wakarismatiki.
Katika Parokia wanahudumia pia Masista Wamisionary wa Bikira Maria Mama wa Afrika (Missionary Sisters of Our Lady of Africa).
Shule ya Chekechea
Mpaka kufikia sasa Parokia katika shule ya chekechea inasomesha watoto Mia moja (100) walio wakatoliki na wasio wakatoliki, Waislamu na Madhehebu mengine. Walengwa zaidi ni Watoto ambao hawakumaliza shule ya Msingi kutokana na hali duni ya kiuchumi, na wengine ama wamemaliza lakini hawakufaulu kuendelea na sekondari hali kadhalika wanapatiwa msaada.
Pia wapo watoto yatima ambao hawana wazazi kabisa na wengine mzazi mmoja.(orphants na half orphants).
Wapo Pia wanafunzi wa pre form one ambao wanapatiwa mafunzo na kwa idadi wapo watoto saba(7), na wengine 47 wakisomeshwa na kulipiwa Ada katika shule mbalimbali za sekondari na baadhi yao wako VETA.
Wako vijana wawili ambao pia wamesomeshwa katika ngazi ya Chuo kikuu.
Katika miongoni mwa maazimio, kila mwaka panapokuwa na hija Namgongo, Parokia inatoa mwakilishi Mmoja (1) kutoka kila Kanda kuhudhuria Hija ambapo jumla ya wwashiriki yapata watu wanane (8) kwa kadiri ya hesabu ya kanda zilivyo.
Kwa upande mwingine VIWAWA katika namna ya uinjilishaji wanaonyesha kuwa na vipaji vya hali ya juu hasa katika kucheza na maigizo katika maeneo mbalimbali ambapo wametoa hamasa ya hali ya juu kwa vijana wenzao na waumini pia. Na hivi sasa wako mbioni kutoa filamu ya miaka150 ya Wamissionary wa Africa. Ni matumaini yetu italeta mafundisho mazuri kwa vijana na hata rika zingine.
Ziko juhudi nyingi ambazo pia zimefanyika na ambazo zinaendelea kufanyika katika kuweza kufikia makundi mbalimbali kuzunguka Parokia, katika kufikia hazma hiyo kimeundwa chama cha Wasamaria Wema ambapo kila baada ya Misa ya asubuhi wanaabudu Ekarist kwa nusu saa halafu wanaenda pamoja na Padre kutembelea wagonjwa.
Wasamaria wanamwakilishi mmoja kutoka katika kila jumuiya na hukusanyika jumamosi baada ya vikao vya jumuiya na kupeana taarifa mbalimbali kuhusu wagonjwa. Lakini pia siku ya Alhamisi haparuhusiwi kikao chochote ili kutoa nafasi kwa waumini kuabudu Ekaristi Takatifu kuanzia saa 11:00 jioni hadi saa 12:30. Hali kadhalika kila wiki chama kingine huongoza Rozali na sala mbalimbali wakati wa ibada ya kuabudu na wakati huo Mapadre wakitoa huduma ya Sakramenti ya Upatanisho. Pia kuna utaratibu kwa waumini kusali kwenye Groto mara tatu kwa wiki.
Changamoto
Parokia bado inakumbana na changamoto nyingi haswa ukizingatia asili ya maeneo yanayoizunguka parokia na jamii zilizopo.
Zipo chamgamoto katika maeneo ya parokia hasa katika mipaka na pamoja na maingiliano ya makazi ya watu, Upanuzi wa kanisa unakuwa mgumu pia.
Hali kadhalika maingiliano ya kiimani bado yanadumaza maendeleo kiroho.
PAROKIA YA, MT KAROLI LWANGA (TANDALE)
Kijiografia
Parokia ipo katika kata ya Tandale na inapakana na Manzese , sinza , kijitonyama , Mwananyamala, na magomeni.
Parokia ya mt Karoli ipo katika dekania ya Ubungo.
Parokia hii ilizaliwa mwaka 2005, ina idadi ya waumini kati ya 1800, idadi hiii imepatikana kutokana na sense iliyo fanyika 2015 kwa kuijaza fomu maaalumu zilizoandaliwa na parokia vyanzo vya taarifa vikiwa ni jumuiya ndogo ndogo.
Parokia haina kigango
Katika parokia ya mt karoli zipo kanda 9 na kila kanda ina jumuiya kati ya 4-5 kulingana na jografia iliyopo. Na uongozi wake umepatikana kwa uchaguzi kwa usimamizi wa viongozi wa parokia, na uongozi pande zote umekamilika.
Parokia ina jumla ya jumuiya 35 na zinatumia majina ya watakatifu.
Kila jumuiya ina kaya kati ya 10-25, na kusali ni siku za jumamosi kuanzia saa 12:30am
Maudhurio yanaonekana sio mazuri kwa baadhi ya makundi mfano UWAKA na vijana
Jumuiya zina utaratibu wa kuadhimisha somo wa jumuiya. Viongozi katika jumuiya na kanda hukutana mara nne katika mwaka nje na mikutano ya kawaida.
Huduma zingine zinazopatikana katika jumuiya ndogondogo ni pamoja na kutembelea wagonjwa , matembezi ya mapadre katika jumuiya na familia, chakula na tiba kwa wasio jiweza, huduma za mazishi na elimu kwa watoto, yatima na walio kaatika mazingira hatarishi
Changamoto katika JNNK
1. Maudhurio hafifu
2. Kuhamahama kwa waumini haswa walio katika upangaji
3. Miundo mbinu mibovu ha hivyo kupeleke waumini baadhi kukinbilia makanisa ya jirani kupata huduma.
4. Mafuriki ni moja katika changamoto kubwa katika parokia ya tandale.
OUNGOZI
Kamati tendaji ya parokia ndio muhimili na ipo kikatiba. Na imekamilika kiuongozi pia
Kamati tendaji inakutana mara moja kila mwezi na kila jumapili ya kwanza ya mwezi paroko akiwa miongoni mwao
Halmashauri ya walei
Halmashauri ya walei inaundwa na viongozi watano kutoka kila kanda, viongozi watatu kwa kila jumuiya na wenyeviti wa vyama vya kitume, mkutano unafanyika mara mbili kila mwakaHalmashauri haina ofisi Zaidi sana ina tumika ofisi ya baba paroko
Njia za mawasiliano
Barua pepe E mail, simu, Whatsaap group,matangazo mbali mbali yanayo tolewa kila dominika
Kuna kamaati ndogo ndogo zilizoundwa kulinganan na taaluma za watu ,kamati hizi zinzsimamiwa na kamati tendaji ya parokia isipokua kamati ya Amani.
- Kamati ya haki na Amani
- Kamati ya ulinzi, kamati ya ujenzi,
- Kamaati zinazosimamia maendeleo ya jamii kiroho, TASODEC. Kimsingi kamati hizi zinaripoti kwa wenyeviti wa kamati kwasababu wote wanatoka katika kamati tendaji ya parokia
- Zipo kamamti za katiba na zile zisiso za kikatiba
Dira kuu
1. Kutangaza ufalme wa mungu
2. Kutengeneza mahusiano kati ya parokia nan a taasisi nyingine
Ushirikishwaji katika mabo ya kanisa
Waamini wanashirikiswa kwa kupitia mikutano mbalimbali ya halmashaaauri, au kupitia jumuia ndogondogo, kanda na paarokia ba pia ushirikishwaji wa waumini kupitia matangazo siku za dominika ,barua pepe, whatsaap na ujumbe mfupi.
Vyam vya kitume
Vyama vya kitume vipo 16
- UWAKA
- WAWATA
- UTOTO MTAKATIFU
- MSAMARIA MWEMA,
- WATUMIKIAJI
- SHIKWAKA
- CHAMA CHA WITO
- SEBUGWAO,ALMATARE
- REGIO MARIA
- MOYO MTAKATIFU WA YESU
- KARISMATIKI KATOLIKI
- SEBUGWAO
Vyama hivi vinawanachama wa kutosha na vinakidhi, na baadhi ya vingine vina walezi,lakini vyama hivi havina ofisi
Fedha
Hakuna repoti ya mapato na matumizi
Semina na mafungo
Zinafanyika semina lakini hakuna mafungo, lakini kwa upande wa semina ilisha fanyika semina moja ya oungozi na maadili. Kiparokia
Semina za viongozi na maadili zimefanyika
Semina za kiparokia zimefanyika mara moja na vyama vya kitume zinafanyika kwa wakati wake
Kuhusu Imani
Inaonyesha waamini kati ya kuanzia umri wa miaka 45 wameimarika Zaidi kiimani kuliko makundi ya chini ya umri huo, Zaidi hasa kwa vijana ambao wanahitaji msukumo wa hali ya juu.
Zipo changamoto pia katika maswala ya utoaji kulingana na taarifa zilizopo. Utoaji ni mzuri lakini wenye uwezo ni wachache na walio wengi wana uwezo mdogo.
Maatoleo ya zaka kama amri ya kanisa ni hafifu pia.
Michango kwenda jimboni inatolewa lakini haifiki kwa wakati.
Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa jimbo.
Mapato na matumizi ya paarokia yanajulikana kwa waumini na taarifa inatolewa
Matoleo ya kila dominika yanatolewa na kutangazwa kwa waumini kila dominika inayofuata.
Hali kadhalika fedha za makusanyo yote hupelekwa benki kwa wakati.
Kuhusu ulinzi hali ni nzuri katika parokia.
Miradi ya kuinua kipato
-Zipo fremu za maduka na maegesho ya magari
Kuhusu ujenzi zipo shughuli za ujenzi zinazao endelea.
Parokia ina mgogoro wa kimipaka na jirani waliozunguka na barua imesha andikwa kwenda kata.
Kwa sasa hakuna mipango yeyote ya kuwaendeleza waumini ki uchumi labda matarajio ni hapo baadae.
Kwa upande wa mapadre wanatosheleza kwa sasa isipokuwa watawa.
Parokia ina wanaseminari watano wanaosoma katika seminari mbalimbali
Idadi ya waumini waliojiunga na utawa ni watatu.
Mwisho kuhusu histiria ya parokia ,waumini picha na miradi ipo.