Parokia
DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA THERESIA WA MTOTO YESU
PAROKIA YA MAFIA
Parokia ya mafia msimamizi wake ni Mt teresia wa mototo Yesu
Parokia hii ilizaliwa 1997
Kijiografia Parokia hii inapatikana katika mipaka ya kisiwa cha mafia
Ipo katika Dekania ya Mt joseph
Parokia ina idadi ya waumini 985 wanaume na wanawake 537, hii ni kutokana na sense iliyofanyika 2017, Sensa nyingine inatarajiwa kufanyika 2018.
Parokia ina vigango nane (8)Parokia haina kanda wala mitaa.
Jumuiya ndogo ndogo zipo 29 na zina tumia majina ya watakatifu, na viongozi wake wamechaguliwa kwa mujibu wa katiba Upo pia utaratibu wa jumuiya kusali pamoja siku ya jumamosi
Kuna jumla ya jumuiya 7 , Jumuiya 1 inasali jumanne, na jumuiya sita (6) zilizobaki zinasali siku ya jumamosi.saa moja kimili na sa 11 jioni.
Maudhurio kwa jumla kwa jumuiya JNNK na kanda sio mazuri haswa kwa wanaume na vijana lakina juhudi zinafanyika ili kuhamasisha waweze kushiriki.
Pia upo mpango wa kuwwatembelea waumini katika JNNK na kanda na umeanza kutekelezwa ngazi ya Parokia.
Jumuiya Kanda na mitaa huadhimisha siku ya watakatifu na wsimamizi.
Halikadhali uongozi katika JNNK Kanda na mitaa umekamilika.
Uongozi katika halmashauri JNNK ,Kanda na Mitaa hua hawakutani.
Huduma za kiroho /Kijamii zinazotolewa katika JNNK ni kama zifuatazo; Ibada za Mazaishi , Mpako wa wagonjwa, Ekarist Takatifu kw wagonjwa na wazee pamoja na misa wa somo wa jumuiya.
Lakini changamoto zilizopo ni maudhurio dhaifu.
UONGOZI
Kamati Tendaji ipo na imekamilika, Kwa kawaida hukutana mara moja kwa mwezi na muda ni saa kumi na moja jioni. Vikao huchukua muda wa saa moja. Paroko ni mmoja wa wahusika katika kikao.
Halmashauri ya Walei inaundwa na wajumbe wafuatao;
Kamati Tendaji ya Parokia na Vigango, Wenyeviti wa vyama vya kitume ngaazi ya Parokia ,
Hlmashuri ya walei parokia inaundwa na wajumbe kutoka kamati tendaji , na vigango, Wenyeviti wa vyama vya kitume, Wenyeviti kutoka JNNK na Baba paroko akiwemo. Mikutano inayofanyika ni miwili kwa mwaka na hufanyika siku ya jumamosi.
Agenda na taarifa za vikao hupatikana kwa wakati na vinanatunzwa.
PArokia imeweza kuwwa na ofisi ,vitendea kazi vipo na vinakidhi kwa kiasi chake.
Mawasiliano yanayo tumika kwa wajumbe wa Kamati Tendaji katika kufikishiana taarifa ni kama zifuatazo; Barua pepe (E mail), Whats aap groups, Simu, Barua na Matangazo ya kanisani siku ya Dominika.
Zipo pia kamati ndogondogo za kikatiba zilizokamilika, na viongozi wake wamekamilika ambazo zinajumuisha viongozi watano.
Kamati isiyo ya kikatiba iliyoundwa na Parokia ni moja ambayo ni Kamati ya uhamasishaji.
Kamati zote hizi zinaripoti kwa kamati Tendaji ya Parokia. Kamati hizi hazikutani inavyo stahili isipo kuwa tu kamti ya Liturujia ndio inaonekana kuwa Aactive. Na ndio kamati pekee inayoto mrejesho kwa kamati Tendaji ya Parokia kuhusu majukumu yake.
Miongoni mwwa dira na mikakati ya Parokiia ni kuondoa utegemezi na kuwa parokia mojawwapo bora katika Dekania.na mikakati ni kama ifuatavyo;
Kuboresha vyanzo vya mapato,Kubainaisha na kurasimisha Rasilimali za kanisa.Kusomesha makatekista, Kujenga majengo ya Kanisa na Nyumba za makatekista Vigangoni, kukarabati majengo ya kanisa.
Parokia haijawa bado na kalenda yay a mwaka ya matukio ya kiparokia.
Njia zinazotumika kuwaarifu waumini juu ya mipango ya Parokia ni kwa kupitia vikao na matangazo mbalimbali Kanisani.
Vyama , mashiriika na jumuiya za kitume(VMJ)
Vipo vyama vya kitume sita (6) navyo ni: UWAKA, WAWATA, VIWAWA,Utoto mtakatifu, Legio Maria na Kwaya.
Vina wanachama wa kukidhi haswa kwa upande wa Parokiani lakini kwa upande wa kigango.
Vyama na vikundi vya kitume vinafanya kazi kulingana na katiba ya Halmashauri ya Walei na vinatimiza vizuri wajibu wake.uhai wa VMJ ni wa wastani na havijaweza kuwa na ofisi Parokiani kwa wakati huu, lakini baaadhi vina vifaa kwwaajili ya kufanya kazi za kiofisi.
VMJ vinatoa taarifa ya (pamoja nay a fedha )mara kwa mara katika Parokia.
Ushiriki wa VMJ za Parokia katika shughli za Dekania na Jimbo uko vizuri.
Semina mbalimbali katika uendelevu wa Imani,uongozi na utengenezaji.
Kamati Tendaji Ya Parokia wamepatiwa semina inayohusu wenyeviti na makatibu. Zipo pia semina nyingine za Kiroho ambazo zimekuwa zikitolewa kwa kwa viongozi wa kamati Tendaji ya Parokia.
Hali ya iimani kwa waumini ni ya wastani , na swala la utoaji kwa waumini sio zuri sana, na hali ya utoaji wwa zaka kama amri ya kanisa nao pia hairidhishi.Michango inayopaswa kutolewa Jimboni inatolewa inavyopaswa na kwa wakati.
Fedha na mipango
Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa Jimbo, na mapato na matumizi ya Parokia yanajulikana kwa wwaumini mara moja kwa mwaka.
Matoleo ya kila dominika hutangazwa kwa waumini kila domiinika inayofuata. Na fedha hupelekwa benki kwa wakati.
Ulinzi na usalama
Hali ya ulinzi na usalama katika parokia ni nzuri na ya kuridhisha.na walinzi wanaotumika ni wa binafsiMaendeleo ya kiuchumi
Parokia ina mradi wa vibanda 21 vya biashara , mashamba ya minazi na mashamba ya mikorosho ambayoo hayajaanza kuzaa bado.
Mambo ya jumla
Parokia haina mgogoro wowote wa kimipaka changamoto iliyopo ni maaeneo yaliyo wazunguka hayajapimwa.
Parokia inayo mpango wa kuwaendeleza waummini wake kiuchumi kwa kupitia SACCOS.
Idadi ya wanafunzi wa seminari kutoka Parokia ya mafia mpaka sasa ni wanne(Wasichana 3, na Kijana mmoja.
Yapo pia maandiko ya parokia ikiwemo historia ya Parokia , Mapadre, waumini na picha za sasa na za zamani.
JE UNATAFUTA
PAROKIA?
Upate majibu yako haraka zaidi
Ramani ya Parokia