DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA OYSTERBAY
Parokia ya mtakatifu petro (Ostabay), Imezaliwa 1958
KIJIOGRAFIA.
Parokia ipo mashariki mwa mji wa Dar es salaam, Upande wa masharikiki imepakana na bahari ya Hindi, na kusini mashariki ni Upanga daraja la salenda, na kusini magharibi ni Mt Anna, (Hananasifu), Magharibi ni Mt Martini De pores (mwananyamala), kaskazini magharibi ni Mt Martha (Mikocheni).
Parokia ipo Dekani ya mt Petro
Idadi ya waumini ni kati ya 4000 kwa taarifa ambazo zimepatikana kutokana na sense ya mwaka 2013
Katika parokia ya Mt petro kuna kigango kimoja na kinatumia jina la Mt.
Kigango kinaidadi ya jumuiya 12, na Uongozi wake upo na umekamilika, Majina yanayo tumika ni ya watakatifu
Kiujumla JNNK zipo 60 pamoja na zile 12 za kigango, na zote zinatumia majina ya watakatifu
Jumuiya za kanda zinasali pamoja kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, na baadhi ya jumuiya zinasali siku ya jumanne jumatano na ijumaa saa 12 :00 jioni. Na jumuiya zote zinatumia mwongozo wa jimbo
Maudhurio katika jumuiya na kanda ni ya wastani na vikundi vyote vinaonyesha kushiriki ipasavyo
JNNK pia huadhimisha misa wa somo wa jumuiya kila mwaka
Viongozi katika halmaashauri ya walei ya parokia hukutana kila baada ya miezi mitatu kulingana na katiiba inavyo elekeza
HUDUMA ZA KIROHO
Mapadre hutumia muda wao kuwatembelea waumini katika JNNK na kanda na wakati mwingine nyumba kwa nyumba
Kutembelea wagonjwa na kuwaombea wale wenye shida mbalimbali, kuwafariji ili kuwati moyo, kuwafundisha neno ili watu wamjue Mungu
UONGOZI
Kamati tendaji ipo na imekamilika
Kamati tendaji hukutana maramoja kwa mwezi saa moja jioni kwa masaa mawili hadi matatu kufuatana na agenda, baba paroko anahudhuria katika kikao hicho
Halmashauri ya walei inaundwa na viongozi watano kutoka JNNK na vyama vya kitume.
Halmashauri ya walei parokia hukutana mara moja kila baada ya miezi mine lakini wanaweza kukutana mapema Zaidi iwapo kama kutatokea dharura
Ajenda na taarifa za vikao zinapatikana kwa wakati na vinatunzwa katika ofisi ya halmashauri ya walei ya parokia.
Njia za mawasiliano kwa wajumbe wa kamati tendaji pamoja na halmashauri ya walei ya parokia ni kama ifuatavyo:
a) Barua pepe yaani e mail
b) Whatsaap groups
c) Matangazo yanayo tolewa kanisani siku za dominika
d) Barua na simu,
E-mail au barua pepe ya Parokia ni; stpetersparish@yahoo.com
KAMATI
Zipo kamati za kikatiba na zisizo za kikatiba kama ifuatavyo;
Kamati za kikatiba
Hizi ni zile kamamti ambao wajumbe wake wanatokana na viongozi watano kutoka JNNK na vyama vya kitume, Viongozi wake wanatoka kamati tendaji.
Kamati zisizo za kikatiba
1. Kamati ya ardhi; hii hushughulika Zaidi na mipaka ya kanisa ,kujua ukubwa wa eneo la kanisa na ndio huusika kusuluisha migogoro n.k
2. Kamati ya afya; Kamati hii inashughulikia mambo ya dharura kiafya katika matukio mbalimbali.
3. Ulinzi; Kusimamai masuala yote yahusuyo usalama kuanzia maeneo ya parokia na maneo waabuduyo waumini.
4. Tegemeza kanisa;Kushughhulilkia maswala yote yanayohusu mavuno parokia na jimbo
Kamati zote hizi za kikatiba na zisizo za kikatiba zote zinaripoti kwa kamati tendaji kila baada ya miezi miitatu, au kabla ya hapo kama watatakiwa kufanya hivyo.kamati hizi huingilia wakati Fulani haswa wakati wa matukio.
DIRA
Dira yetu ni kuwa parokia yenye ustawi wa juu kiroho, kutoa huduma za kiroho na za kijamii, na pia kuona waumini wote wanashiriki ibada mafungo na semina za kiroho
Parokia imeandaa pia kalenda ya matukio ya mwaka ya kiparokia kwa kushirikisha waumini kupitia kamati ya liturjia na vyama vya kitume ili kuweza kutoa maoni.
Waumini wanaarifiwa mipango ya parokia kwa kupitia mikutano ya halmashauri na JNNK.
VYAMA, MASHIRIKA NA JUMUIYA ZA KITUME
Vyama ,mashirika na jumuiya za kitume zipo kama ifuatavyo;
Legio maria, Neokatekuminato, Moyo mt wa yesu, Kwaya, Vijana, Uwaka, Wawata, Watumishi wa altare, Utoto mtakatifu ,Utume wa Fatima, Miito na karismatiki katoliki Kwa ujumla vipo 11
Vyama hivi baadhi vina wanachama wa kutosha, lakini vingine wanachama wake ni wa kusuasua
Vyama na vikundi vya kitume vinafanya kazi kulingana katiba ya halmashauri ya walei na vinatimiza wito wake ipasavyo.
Uhai wa vyama, Mashirika na jumuiya za kitume unaridhisha, ijapokwamba kuna changamoto katikia sehemu ya ofisi kwaajili ya kutunzia vifaa na zana za kufanyia kazi.
VMJ vina walezi ambao ni mapadre
VMJ vina toa taarifa ya au report ikiwa pamoja na ile report ya fedha mara kwa mara katika uongozi wa parokia
Ushirikiano na ushiriki wa vyama vya kitume na jumuiya katika shughuli za kidekania na jimbo sio mbaya isipokuwa baadhi ya vyama vya kitume. Uwaka Wawata ushiriki wao unaonekana.
Baadhi ya VMJ katika Parokia vyaweza kuwa mfano wa kuigwa na parokia nyingine kwa kuwa na miradi katika parokia mfano; Miradi ya duka kwa WAWATA na Vijana
SEMINA MBALIMBALI KATIKA UENDELEVU WA IMANI, UONGOZI NA UTEGEMEZAJI
Zipo semina za mafungo mbali mbali ambazo zimeandaliwa katika JNNK kanda au kiparokia hasa wakati wa kwaresma na sikukuu wa somo
Uongozi wa parokia kamati tendaji na halmashauri ya walei ya parokia wameshapatiwa semina ya uongozi ambayo iliandaliwa na jimbo kisha kuletwa parokiani.
Semina za kiroho na tegemeza kanisa zinafanyika parokiani na ambazo zinafanyika walau mara tatu hadi nne kila mwaka
Hali ya kiimani kwa ujumla inaridhisha , na hata utoaji ni mzuri na unaridhisha.
Utoaji zaka kwa amri ya kanisa pia sio mbaya waumini wanajitahidi kiasi chake.
Michango ya jimbo inatolewa kama ipasavyo na ni kwa wakati
FEDHA NA MIPANGO
Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa jimbo
Mapato na matumizi yanajulikana kwa waumini , na taarifa hutolewa katika mikutano miwili ya halmashauri
Matoleo ya kila dominika hutangazwa kwa waumini kila dominika iinayofuata na fedha zote kupelekwa benki
ULINZI NA USALAMA
Hali ya ulinzi na usalama katika parokia ni mzuri na unaridhisha, na pia walinzi wanaotumika ni kutoka katika kampuni binafsi
MAENDELEO YA KIUCHUMI
Miradi ambayo inaendeshwa parokiani kwa wakati huu ni kama ifuatayo;
-Kituo cha kijamii cha cardinal Rugambwa chenye ofisi ,mgahawa na ukumbi
-Ipo pia mipango ya kuboresha Grotto ramani inafanyiwa masahahisho ili kazi iweze kuendelea
MAMBO YA JUMLA
Ipo mipango ya kuwaendeleza waumini wake kiuchumi kwa ujumla kupitia chuo cha VETA katika mabo ya Ushonaji, Mapishi , na Mapambo
Idadi ya mapadre haitoshelezi hii ni kutokana na mahitaji kuwa ni makubwa.
Idadi ya waumini waliojiunga na utawa kutoka parokia ya Mt petro ni watatu tu, wawili wapo shirika la wadada wadogo mbagala, mmoja yupo Neo katekumenato.