DEKANIA YA ST.JOSEPH
DEKANIA YA UBUNGO
VIONGOZI WA DEKANIA YA KIBAHA
DEKANIA PETERS
DEKANIA YA ST. GASPAR
DEKANIA YA UKONGA
DEKANIA YA SEGEREA
DEKANIA YA KIGAMBONI
DEKANIA YA KILIMAHEWA
PAROKIA YA MIKOCHENI
PAROKIA Y MTAKATIFU MARTHA MIKOCHENI
Parokia ya mt Matha ilizaliwa 2006
Parokia hii inapatikana mikocheni katika dekania ya Mt petro
Idadi ya waumini ni kati ya 1275, na idadi hii imepatikana kutokana na sense iliyofanyika kutokana na taarifa zilizo patikana katika JNNk za mwaka 2016. Sensa nyingine imefanyika tayari 2017 kwa kila jumuiya kuleta idadi ya waumini wake kutoka katika kila jumuiya.
Parokia haina kigango kwa sasa.
Katika parokia zipo jumuiya ndogo ndogo 21 ingawa jumuiya moja inasali na kushiriki katika Parokia ya Mt petro.
Jumuiya zinatumia majina ya watakatifu.
Kwa kila jumuiya kuna wastani wa kaya 12-15.
Katika parokia kuna kanda 4, na kanda hizo ziimegawanyika kutokana na mahali zilipo, na kila kanda ina wastani wa JNNK 5, na uongozi wa kanda unapatikana kwa kupitia uchaguzi uliofanywa na viongozi wa jumuiya zake, na kanda zote zina uongozi uliokamilika. Majina ya kanda hayafuati majina ya watakatifu
JNNK na kanda/Mitaa inasali pamoja siku za juimatano jioni lakini nyingi ni siku za jumamosi (asubuhi)
Mahudhuriakwa ujumla katika jumuiya na kanda yanaridhisha na yana rekodiwa katika rejista ya kila jumuiya.
Ushiriki wa wanaume ni wakusuasua, Viongozi wanachukua hatua ya kuongea nao na kuwahamasisha ili waweze kuhudhria ipasavyo
Jumuiya zinazoonyesha kuwa na changamoto zinatembelewa ili kutatua changamoto zao.
Katika parokia ya Mt Matha, JNNK hua zinaaadhimisha misa za aina mbili
• Kubariki nyumba kila mwaka baada ya pasaka
• Kufanyika misa za somo wa jumuiya
Uongozi katika JNNK, Kanda, Mitaa na vigango umekamilika.
Pale inapoonekana kuwepo na upungufu wa kiongozi mmojawapo chaguzi za kuziba nafasi zilizoachwa wazi hufanywa.
Uongozi wa halmashauri hukutana kila baada ya miezi mitatu.
Huduma za kiroho zinazotolewa ni pamoja na ;
Kutembelea wagonjwa hospitalini, Wafungwa ,na kuwahudumia wahitaji
Ziko changamoto nyingi katika kuzihudumia JNNK ambazo ni pamoja na hizi zifuatazo;
Baadhi ya nyumba zinakuwa mbali na zingine
Badhi ya wanajumuiya hawashiriki shughuli za kanisa lakini wanataka kupata huduma.
Baadhi ya waumini kuhama na kwenda maeneo mengine.
UONGOZI
Kamati tendaji ipo na imekamilika kikatiba
Kamati tendaji hukutana mara moja kwa mwezi na muda wa kikao ni wastani wa saa limoja tokea kuanza kwa kikao, na baba paroko ni mmoja wa wajumbe wa kikao.
Halmashauri ya walei ya parokia inaundwa na viongozi watano kutoka katika kila kanda , kamati tendaji ,wenye viti wote wa vyama vya kitume ngazi ya parokia na jumla ya wajumbe ni 29. Kukutana ni mara mbili kwa mwaka au Zaidi, na kama kunadharura vikao hufanyika siku ya dominika
Agenda na riport za vikao vinapatikana kwa wakati na vinatunzwa
Ofisi Walmashauri ya Walei ya parokia imejikamilisha kuweza kufanya shughuli zake bila wasiwasi.
Njia za mawasiliano zinazo tumika ni kama vile;
I. Barua pepe E mail
II. Simu
III. Kupitia matangazo siku za dominika.
KAMATI
Zipo kamati ndogo ndogo za kikatiba ambazo wajumbe wake wametokana na kamati tendaji ya parokia
Kamaati nyingine ni zile zisizo za kikatiba yaani;
Kamati ya Ulinzi, Kamati ya Afya, Kamati ya ujenzi na kamati ya usafi. hizi kamati zinasaidiana katika utekelezaji wa shughuli za parokia lakini hazina muingiliano.
Kamati ndogo ndogo zinaleta taarifa kwa kamati tendaji kila baada ya miezi mitatu
Kuna kalenda ambayo inaeleza matukio ya mwaka kiparokia na dekania, ambazo kimsingi imeandaliwa kwa kushirikiana na waumini ili kupata taarifa mbalimbali
Njia zinazo tumika katika kuwaarifu waumini mipango ya parokia ni kwa njia ya matangazo yanayosomwa siku za dominika pamoja na matangazo yanayoweka katika mabao ya matangazo.
VYAMA, MASHIRIKA NA JUMUIYA ZA KITUME
Vyama mashirika na jumuiya za kitume viko 8.
a. WAWATA,
b. UWAKA,
c. VIWAWA,
d. SHIKWAKA,
e. Karismatiki katoliki
f. Legio Maria
g. Moyo mt wa yesu
Vyama hivi vina wanachama wachache na baadhi yake havina kabisa.
Vyama na vikundi vya kitume vinafanya kazi kulingana na katiba ya halmashauri ya walei japo bado ni wachanga.
Vyama hivi havina ofisi lakini baadhi yao wanavifaa tu vya kazi za kiofisi
VMJ havitoa taarifa pamoja na repoti ya fedha kwa uongozi wa parokia
Ushirikiano na ushiriki wa VMJ na parokia katika shughuli za kidekania na jimbo uko vizuri.
SEMINA MBALIMBALI KATIKA UENDELEVU WA IMANI, UONGOZI NA UTEGEMEZAJI
Hakuna semina na mafungo yanayoandaliwa kiparokia kwa sasa katika JNNK na kanda.
Uongozi wa parokia na, kamati tendaji na halmashauri ya walei ya parokia hawajapatiwa semina bado
Kwa upande wa semina za kiroho na tegemeza kanisa bado hazijafanyika pia
Hali ya Imani katoliki kwa ujumla katika parokia inaridhisha.
Halikadhalika swala la utoaji kwa waumini lina ridhisha kwa kiasi chake
Pia utoaji wa zaka kama amri ya kanisa unaridhisha.
Parokia inatoa michango kamili ya jimbo kama inavyo paswa na kwa wakati.
FEDHA NA MIPANGO
Mpango wa fedha unaotumika ni ule wa jimbo
Mapato na matumizi ya parokia yanajulikana kwa waumini, Taarifa ya mapato na matumizi ya kila wiki zinatolewa kila dominika na majumuisho ya mwaka mzima yanatolewa kwa halmashauri ya walei ya parokia na kusomwa kwa waumini pamoja na bajeti ya parokia kwa mwaka unaofuata.
Matoleo ya kila dominika yanatangazwa kwa waumini kila dominika inayofuata
Fedha yote inapelekwa benki kwa wakati
ULINZI NA USALAMA
Hali ya ulinzi na usalama kwa ujumla iko vizuri,na walinzi wanotumika wanatoka katika kampuni binafsi
MAENDELEO YA KIUCHUMI
Hakuna miradi yoyote kwa sasa, lakini katika swala la maendeleo ya parokia kuna ujenzi wa ukumbi wa parokia lakini baada ya hapo utaanza ujenzi wa grotto ya bikira Maria
MAMBO YA JUMLA
Katika swala la mipaka , kuna mgogoro kati ya parokia ya mt petro na parokia ya mt Matha
Idadi ya mapadre / watawa waliopo kwa sasa inatosheleza hii ni kutokana na idadi ya waumini waliopo kwa sasa