HALMASHAURI YA WALEI
UCHANGIAJI WA MFUKO WA UINJILISHAJI
kutokana na kuwepo kwa mahitaji makubwa ya uendeshaji shughuli za Halmashauri Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam, imeonekana kuwepo haja ya kuongeza kipato kupitia vyanzio mbalimbali katika shughuli za uinjilishaji, Hivyo yamepitishwa maazimio mbalimbali ya namna ya kupata fedha kwaajili ya kutunisha mfuko. imeonekana michango ya Pentekoste pekee haitoshi kukidhi mahitaji ya shughuli za kila siku za Halmashauri Walei jimbo.
Kutokana na mahitaji hayo;
1. kila Parokia , Kuanzia Mwaka ujao, yaani 2022 Januari zitachangia shilingi 200,000
2. Kila kiongozi wa Halmashauri Walei Jimbo kuu la Dar es salaam atachangia shilingi 100,000. Fedha hizi zitatolewa kwa kwa mwaka mzima.
3. Pia , zimeandaliwa bahasha ambazo wamesambaziwa Baadhi ya wadau ambao watachangia ili kutunisha mfuko wa Uinjilishaji.
4.Pia imebuniwa miradi mbalimbali huko Kisarawe ya ufugaji ngombe wa nyama, Mbuzi na ufugaji wa nyuki
Kwa mpango huo basi Imefunguliwa Akaunti maalumu kwaajili ya kuchangia Mfuko wa uinjilishaji ijulikanayo kwa jina la UINJILISHAJI WALEI DSM, Akaunti namba ni; 00211515091101
Pia Kuna lipa kwa M- Pesa namba 5040013, Jina UINJILISHAJI HALMASHAURI WALEI JIMBO.
Kaulimbiu ya Kisinodi Inasema (Ushirika, Ushiriki na Umisionari), Sisi ndio wamisionari wa Leo. Walei ndio Nguzo ya Kanisa, na Kanisa litajengwa na sisi wenyewe.
Mungu awabariki sana.
- Matukio
- Juinge na Kanisa
- Neno kuu la mwaka 2018
- Kalenda ya matukio 2018
- Ramani ya Tovuti
- Biblia Mtandaoni na zaidi
- Liturujia ya Kanisa Katoliki
- Mkate wa siku ya LeoLorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore Ut enim ad minim magna aliqua”2 kor 2:16