SHIRIKA LA WAZEE NA WASTAAFU
HISTORIA YA SHIRIKA LA WAZEE NA WASTAAFU WA MT AGUSTINO
JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM
1. MWANZO WA SHIRIKA LA WAZEE TANZANIA
Shirika la wazee na wastaafu lilianzishwa hapa nchini miaka ishirini iliyopita Jimbo la Moshi.
mnamo mwaka 1970 waalimu wastaafu wa Parokia ya kilema Jimbo kuu katoliki la Moshi walijiunga na kuanza umoja wao kwa lengo la kusaidiana wakati wa matatizo mbalimbali na hasa kuzikana .Wastaafu kutoka sekta binafsi na serikalini walianza kushirikiana nao kwani matatizo yao yalifanana, na maranyingi walikutana kanisani baada ya misa . Mwaka 1987 kikundi hiki kikiongozwa na padre Gregory Mashtaki kama padre muhudumu wa parokia hiyo kilipewa jina la wazee wastaaafu wa mt Agustino baada ya kuandaa katiba na kupata kibali cha Muhashamu askofu wa jimbo, Askofu amedeus Msarike, mnamo 1988 shirika lilikubalika rasmi kuwa ni la WAZEE WASTAAFU yaani watu waliojiajiri wenyewe katika sekta mballimbali kama wakulima , wafanya biashara, wafugaji yaani watu waliokuwa wameajiriwa serikalini au sekta binafsi na sasa wamestaafu. Na hatua iliyofuata ilikuwa ni ya kuandaa kitabu cha shirika nembo na bendera ambayo ilikamilika 1989, na kukubaliwa na jimbo kwa lengo lililo kusudiwa
Shirika llilizinduliwa rasmina muhashamu baba Askofu Amedeus Msarikie tar 05 oct 1989 Parokiani Kilema. Shirika liliendelea kuenea sehemu mbalimbali na hadi kufikia taarifa hii inaandikwa ,jimboni moshi pekee Parokia zenye washiriki zilikuwa 53 zenye jumla ya washiriki Zaidi ya 700.
Kkwa Jimbo kuu la Dar es salaam, mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama ili mradi awe na sifa zifuatazo;
Awe ni mwanamke au mwanume Mzee katika eneo lake
Awe amestafu katika kazi za kuajiriwa
Awe ni mkatoliki
Na awe na umri usiopungua miaka hamsini.
2. MWANZO WA CHAMA JIMBO KUUU LA DAR ES SALAAMU
Uhamasishaji ulianza kufanyika mwaka 2003 kwa kuwaita viongozi wa parokia mbalimbali n a kuwaeleza kuhusu chama , Pd mashtaki aliyekuwa mwanzilishi wa chama jimbo la moshi alikuja kuwahamasisha wazee na wastaafu n abaadae jimbo kuu la Dar es salaamu liliandaa taratibu za kuanzisha chama ikiwa ni pamoja na kutengeneza katiba ya chama .ambapo utaratibu ni kwamba , Paroko au Paroko Msaidizi ndio atakaekuwa mlezi parokiani, lakini katika Jimbo ni Padre atakae teuliwa jimboni na Baba Askofu akishauriana nan a idara ya utume wa walei jimbo. Kwa sasa askofu mkuu amemteua Mkurugenzi wa utume wa walei Jimbo kuwa ndio mlezi wwa chama cha wastaafu.
3. MANTIKI YA KUWA NA CHAMA CHA WAZEE NA WASTAAFU
Jimbo limekuwa na vyama vingi vya kitume vikiwa vikitofautiana kwa kwa mfumo wa aina ya wanachama wake, kitu ambacha hakivitofautishi vyama vyote na chama cha wazee ni kushiriki Zaidi katika ibada na kuyaishi maisha ya kikristo vizuri Zaidi.
Waze ni kundi mojawapo katika maisha ya binadamu . kuna watoto, vijana , na watu wazima pia .Makundi yote haya yanaishi kwa wakati mmoja na yanajitegemea , wakati makundi ya kwanza yanategemea malezi kutoka kwenye makundi mawili , aidha kundi la watu wazima lina majukumu sana kuhusu ustawi wa jamii hasa kwenye uzalishaji na uchmi, WAZEE WASTAAFU WAMEYAPITIA MAKUNDI YOTE MATATU KWAHIYO WANAYO NAFASI NZURI WALIOJALIWA KUWA VIONGOZI WAZURI.
4. UENDESHAJI WA CHAMA.
Utaratibu wa uendeshaji wa chama hauna tofauti na vyama vingine vya kitume hususani uundaji wa halmashauri na kamati tendaji.
Kamati tendaji kwajili ya ufanisi kwa kupitia Halmashauri imeunda kamati ndogo ndogo kufuatana na mahitaji.
5. KALENDA YA SHIRIKA
Shughuli za chama zimeainishwa na shughuli za matukio ya kijimbo matukio ambayo shirika huadhimisha kila mwaka ni kama ifuatavyo;
- Mikutano ya kawaidha nay a dharura ya kamati tendajina halmashauri
- Hija ya wazee Pugu
- Sherehe yam t Agustinoambayo hufanyika tarehe 28.08 kila mwaka
- Kushiriki kwenye sala siku za alhamisi baada ya misa
- Kushiriki kwenye maswala ya shirikisho ya vyama vya kitume
- Kushiriki kwenye ibada na kongamano zinazopangwa na jimbo
6. MAPATO KWAAJILI YA UENDESHAJI WA CHAMA
• Michango ya wanachama
1. Kila parokia yenye wanachama huchangia kila mwezi 5000=
2. Kila mwanachama mzee anapaswa kuchangia 1000 na fedha kuwekwa kwenye akaunt maalum kwaajili ya fungu la maendeleo ya wazee.
3. Kila mwanachama anachangi sherehe yam t Agustino na hija.
• Michango kutoka kwa wafadhili.
• Michango kutoka kwenye miradi iliyo buniwa na shirika kama ASEC
• Shirika lina akaunti katika benki ya post, lakini pia mkombozi banki
• Shirika limeweza kujipatia hekari kumi za ardhi sehemu ya mvuti kupitia chanika na kuikabidhi ardhi hiyo jimboni kwaajili ya kuwajengea makazi mapadre wazee na wastaafu ambao hawana walezi.
• Shirika linaendelea kujiimarisha jimboni
• Shirika lipo pia kwenye mchakato wa kukifanya chama kiwe cha kitaifa.
7. MADHUMUNI YA SHIRIKA.
a. Kuunganisha pamoja wazee na wastaafu wa katoliki katika ngazi mbalimbali tangu Parokia hadi taifa.
b. Kueneza na kuimarisha habari njema miongoni mwao na pia katika familia,Jumuiya , mashule na jamii kwa ujumla ili kuuleta ujumbe wa injili kwenye mioyo ya jamii , kuwaongoza kumwona Mungu. Kusoma na kutafakari neno la Mungu Kuta wawezesha kuwa na mizizi ya kina katika kristo na kutoa huduma zao kama wahudumu wa upatanisho, haki na Amani.
c. Kusaidi na kukuza nidhamu ya waatoto .vijana na watu wazima katika Nyanja mbalimbali ..Dhamira za watu zimekufa na maadili kutoweka , Kuna umuhimu wa kuamsha tena dhamira hizi kwa ushauri nasaha.
d. Kuwawezesha wazee kuwa na sauti ya pamoja ili waweze kutambulikana na Kanisa na serikali. Kanisa linawahitaji wazee , na jamii ina wahitaji wazee hii ni kutokana na hekima na weledi (experience) uzoefu na karama mblimbali walizojipati kwa gharama kubwa . Wazee ni hazina ya kanisa na katika maisha ya jamii , Pia wanaushawishi wa namna mbailimbaili ili kuwatajirisha wanafamilia wa Mungu na jamii kwa ujumla kwa maisha na sala zao za Imani.
e. Kubuni mbinu mbalimbali za kuinua hali za kiuchumi wa wazee wastaafu katika jamii.
f. Kuweka mipango na mbinu mblimbali za kudumisha mshikamano kati yao wanapokabiliwa na matatizo miongoni mwao pia katika furaha na mafanikio ya kimaisha.
g. Kudumisha mawasiliano kati yao na jimbo, taifa na kimataifa.
8. DIRA YA SHIRIKA(Tazama utaratibu wa kueneza shirika)
9. SABABU ZA KUWA CHINI YA MT AGUSTINO (Tazama utaratibu wa kueneza shirika)
10. SHIRIKA KIMATAIFA
Baada ya vita vya pili vya dunia 1945 nchi nyingi za Ulaya zilikumbwa na njaa, Ukosefu wa ajira, mmomonyoko wa maadili , magonjwa na shida nyingi za kijamii. Vikundi vingi vya wazee wakatoliki wanye hekima walijiunga na kutafakari namna ya kukabiliana nan a changamoto za maisha ya uzee na jamii kwa ujumla , 1945-1962 Wazee hao walikutana ufaransa na kutambuliwa kama shirika la wazeee na wastaafu (vie montante International ua ( Ascendinding Life Movement) Walianzisha mafungamano na wazee kwa ukombozi wa dunia (a general mobilization of the aged and retered for salvation of the world) kutoka kwenye shida na maangamizi , shirika lilienea ulaya , Amerika , Kanada , Afrika kaskazini na Magharibi.
Tarehe 4 oct 1982 Baba mt yohane Paulo wa II alihutubia wazee na wastaafu wapatao 8000 waliokutana katika makao yake huko Roma. Hotuba hii iliingizwa katika kitabu cha shirika . Makao makuu ya Baba mtakatifu yalitambua rasmi shirika hili Tarehe 25march 1996 na kulitaja kama shirika la kipekee la wazee walei wakatoliki. Mwaka 1999 katika sherhe ya haki za binadamu Umoja wa mataifa kama “NGO”ya wazee kimataifa .Shirika la wazee na wastaafu linatambuliwa na shirika hili la kimataifa na lina mawasiliano ya karibu.
Tarehe 19-29 agost 2004 mlezi wa shirika alitembelea Jimbo kuu la Blantyre Nchini Malawi kwa mwaliko wa ndg Agustino Kengere na kuanzisha shirika katika parokia mbili . Mawasiliano ya uhai wao yapo hadi wakati huu.
Tarehe 22-30 oct 2004 Melzi aliitembelea Uganda kwa mwaliko wa Pd Agustino Mwanga katibu Mtendaji wa baraza la maaaskofu katokliki Uganda n na waliweza kuanzisha shirika katika majimbo y kmpala , masaka na mitiyane.Kutembelea maeneo hayo ilikua ngumu kutokana na mtume wa mlezi parokiani lakini kwa sasa mawasiliano ymeongezeka.
Tarehe 23-30 juni 2006 kwa mwaliko wa katibu mtendaji wa idara ya utume wa walei KFCalihuduria mkutano wa kitaifa wa idara hiyo huko Nakuru Kenya ili kuhamasisha Shirika . Kulikua na majimbo Zaidi ya 10 yaliyokuwa na nia ya kuanzisha shirika katika majimbo yao , Miongoni mwao yakiwa majimbo ya Nairobi, Mombasa, Nakuru , kakamega, Meru, Nyeri, Marsabi,Lodwar, Kericho na nyahururu,
Pia kuna mawasiliano na Nchi za Zambia, Namibia, Afrika kusini, Zimbabwe na Angola kutokana na mawaasiliano na makao mkuu huko Ufaransa.
11. MAENEO AMBAYO SHIRIKA LA WAZEE NA WASTAAFU LILIPO ENEA KATIKA BARA LA AFRIKA
Ni katika Nchi za Guinea, Burkina Faso, Moroko, Senego, Ivory coast, Cameroon, Mali, Afrika ya kati , Jamuhuri ya watu wa kongo, Rwanda, Burundi, Mauritius, Uganda, Malawi, Kenya , na Tanzania
12. BARA LA ULAYA
Shirika limeenea katika mabara yote ya ulaya , Marekani ya kaskazini na kusini, kanada na Bara la Asia.
13. MAKONGAMANO YA KIMATAIFA.
- Mwaka 1982 Roma ana kuhutubiwa na mwenye heri Baba yohane Paulo II
- Mwaka 1994 Miami marekani ,Mlezi wetu aliwakilisha nchi zinazozungumza kiingereza
Bara la Afrika. - Mwaka 1998 Burkina Faso Afrika Magharibi.
- Mwaka 2002 Bangkok Thailand ambapo mlezi alikua Mratibu wa Afrika hadi 2006
- Mwaka 2006 Ufaransa akiwakilisha bara la Afrika na Mjumbe wa Afrika magharibi
kuchukua nafasi yake mwaka 2010, Kongamano lilifanyika Kanada.
14. MATARAJIO YA SHIRIKA.
- Viongozi wa majimbo hapa Tanzania kufahamiana na kuendelea kuwasiliana ili kuimarisha shirika
- Kuimarisha shirika katika parokia na majimbo yaliyo na wanachama na kueneza katika majimbo yaliyo salia, Mshikamano kuanzia jumuiya hadi parokiani ni muhimu.
- Kuunda kamati za kanda ili kuwezesha uenezaji wa shirika kuwa mwepesi . Kuhimiza washiriki kuwezesha shirika kitaifa kwa michango yao na moyo wao wa ukarimu.
- Kupata kibali cha kutambuliwa na TEC kwa maelekezo na ushauri wa mwenyekiti wa idara ya utume wa walei TEC.
- Kudumisha uhusiano mzuri kati ya kamati ya taifa nay a kimataifa.
- Kuhimiza na kuwezesha washiriki kuwa na moyo na nia ya kuweka katika
maandiko mambo ya kumbukumbu katika maneno , makabila na mila zao kwa
vizazi vijavyo.
15. CHANGAMOTO
-Shirika bado halija kubalika katika parokia zote za jimbo la Dar es salaam
-Uwezo mdogo wa kifedha ulifanya shirika lishindwe kufanya mambo yale ya kimsingi kam mikutano na maendeleo mengine
- Matukio
- Juinge na Kanisa
- Neno kuu la mwaka 2018
- Kalenda ya matukio 2018
- Ramani ya Tovuti
- Biblia Mtandaoni na zaidi
- Liturujia ya Kanisa Katoliki
- Mkate wa siku ya LeoLorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore Ut enim ad minim magna aliquaâ€2 kor 2:16