CHRISTIAN PROFESSIONAL TANZANIA - CPT

CHRISTIAN PROFESSIONAL TANZANIA - CPT

HISTORIA YA CPT

HISTORIA YA CHAMA CHA WANATAALUMA WAKRISTO TANZANIA (CPT)
1. Utangulizi
Wazo la kuanzisha Christian Professionals of Tanzania (CPT) lilitoka kwa wana TYCS ambao baada ya kuhitimu masomo ya elimu ya juu waliona wanahitaji chombo kitakachowaunganisha na kuendelea kumleta Kristo katika mazingira yao ya kazi. Tafakari ziliendelea kuanzia miaka ya 70 na hatimaye kufaulu kushawishi TEC kukubali na kuupokea utume huu rasmi. CPT ikatambulika rasmi kuwa miongoni mwa vyama vya kitume katika kanisa la Tanzania mwaka 1981, na kupewa msimamizi mwombezi Mt. Thomas More. Haikuchukua muda mrefu CPT ikatambulika katika chombo cha International Catholic Movement for Intellectual and Cultural Affairs (Pax Romana ICMICA). MWAKA 1983 CPT ikawa mwanachama rasmi wa ICMICA.
 
2. Vipindi vya Utume wa CPT
Historia ya CPT iko katika vipindi vinne kwa kuzingatia vigezo vya hali ya utume ilivyokuwa, kazi za utume zilizofanyika na njia za utekelezaji pamoja na changamoto zilizoambatana na kipindi husika. Vipindi hivyo ni:
i)kipindi cha kuanza na kuenea (1980 � 1990)
ii) kipindi cha kuimarika na kutambulika na jamii ( 1990 � 1995)
iii) kipindi cha ushirikiano baina ya CPT na Tume ya Haki na Amani (1995 � 2010)
iv) kipindi cha mpito kulekea mabadiliko ( 2010 � 2018)

I) KUANZA NA KUENEA UTUME WA CPT ( 1980 � 1990)
Tunashukuru Mungu kwa zawadi ya wanataaluma ambao walibuni wazo na kuhakikisha lengo lililokusudiwa linafikiwa. Hawa ni pamoja na Sr. Sandra Stich, Paulinus Irengo, Mary Mwingira, Mwanitu Kagubila, Beda Mutagahywa na Camilus Kassala,wakiongozwa na mshauri wa kwanza Pd. Marcel Mangnus.

Waasisi hao katika hatua za mwanzo walifanikiwa kuweka misingi ya utume na kufuata taratibu za kikanisa kuwezesha utume huu kupokelewa na kutambuliwa rasmi na TEC. Pia walifanya bidii kuunganisha utume wa CPT na chombo cha utume wa wanataaluma wakristo ulimwenguni ICMICA. Vile vile walifanya bidii kubwa kuhamasisha utume na ukaweza kuenea katika majimbo yote.

Mawasiliano yalikuwa murua yakiimarishwa na mikutano, semina/ warsha ngazi ya matawi, Jimbo, Kanda na Taifa pamoja na ziara za mara kwa mara. Walianzisha Machapisho endelevu mf. CPT Newsletter na Confrontation ambayo yaliandaliwa kwa njia shirikishi na kuhakikisha usambazaji wake.

Tafakari katika kila tukio ziliongozwa na dhamira maalum walau kwa kila mwaka iliyochaguliwa kutokana na Alama za Nyakati. Mada tofautitofauti ziliandaliwa kitaalam kwa kushirikisha watu wa taaluma mbalimbali na wenye uzoefu kiutendaji katika mada husika. Tafakari ziliendeshwa kwa methodolojia ya KUONA, KUAMUA na KUTENDA (RoL).

II) KIPINDI CHA KUIMARIKA NA KUTAMBULIKA ZAIDI NA JAMII (1990 � 1995)
Ni mwanzoni kabisa mwa kipindi hiki Pd. Vic Missiaen aliteuliwa na TEC kuwa mshauri wa CPT, na ameendelea na kazi hiyo hadi sasa.

Alama za nyakati zilionyesha nchi yetu kuingia katika mabadiliko makubwa kisiasa na kiuchumi. Mgawanyiko wa kijamii katika matabaka ulianza kushika kasi.

Ushirikiano na Tume ya Haki na Amani ulianza kupitia wana CPT wachache akiwemo mshauri. Hao waliteuliwa na TEC kushirikiana na Baba Askofu Paul Ruzoka aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume hadi 2016. Baadaye TEC iliweka nguvu ili kuimarisha ushirikiano wa CPT na Tume ya Haki na Amani kwa kumteua rasmi Pd. Vic kuwa Katibu wa Tume hiyo huku akiwa mshauri wa CPT.

III) KIPINDI CHA USHIRIKANO TUME NA AMANI CPT (1995 � 2010)
Mabadiliko yaliyokuwa yanaendelea nchini yalitutaka kuelekeza nguvu zaidi katika kutoa elimu ya uraia.

Mfululizo wa machapisho maalum juu ya Demokrasia shirikishi ulifanyika na usambazaji ulikuwa wa mafanikio. Hii ilikuwa njia ya kuwaandaa wananchi kushiriki uchaguzi mkuu wa kwanza katika mfumo wa vyama vingi. Na hii iliendelea katika kila uchaguzi mkuu. Mwaka 2000 chapisho lilikuwa juu ya ��Uchaguzi wa kisiasa kwa nini tujali?;�� 2005 ��Kwa nini tujali manufaa na ustawi wa wote?�� 2010 ��Ilani ya Vipaumbele vya kitaifa.��

Kazi za utume zilikwenda vizuri na wigo kuendelea kupanuka kugusa Idara ya Mahakama, Polisi na Magereza huku utume kwa wafungwa na mahabusu vikiwa sehemu ya utume wa CPT.

Kazi ya kuhamasisha utume wa CPT katika vyuo vikuu vya SAUT, na kufikiria malezi ya vijana wa TMCS juu ya mafundisho ya kanisa kuhusu jamii ni mambo yaliyopewa kipaumbele.

Vikundi vya kitaaluma vilianzishwa. Kwa Jimbo la DSM, Wanasheria walijielekeza katika Huduma ya ushauri wa kisheria, huku madaktari na wauguzi wakiendesha huduma ya afya. Vile vile jitihada zilifanyika kushirikisha wabunge utume wa CPT, hadi hatua ya kuunda kikundi cha Wabunge wana-CPT.

Utume wa CPT ulijipambanua vema katika Compendium iliyotolewa na idara ya Haki na Amani Vatikani na kuletwa Tanzania 2006 na Renato Kardinali Martino aliyekuwa Mkuu wa Idara hiyo Vatikani. Kwa ngazi ya SECAM tukio kama hilo lilifanyika Tanzania 2008.

Jitihada za kipekee zikafanyika kuhamasisha mafundisho haya katika kanisa la Tanzania kwa njia ya semina kitaifa na kikanda licha ya Compendium kutafsiriwa na kuchapishwa katika lugha ya Kiswahili na kuandika toleo la ufupisho.

IV) KIPINDI CHA MPITO KUELEKEA MABADILIKO ( 2010 � 2017)
Hali ya watu kutaka mabadiliko ilikuwa bayana. Ni katika kipindi hiki. Mchakato wa Katiba mpya ulipoanza na CPT ilitoa mchango mkubwa katika uhamasishaji.
 
Utambuzi juu ya hitaji la kujenga upya maadili likaanza kueleweka kwa wananchi wengi. Baadaye mchakato wa katiba ulipokwama, CPT ikafikia uamuzi wa kuanzisha Vuguvugu la Uhuishaji Maadili.

Upande wa TEC kumeonekana pia hitaji la mabadiliko ya muundo (restructuring) ambapo CPT imetenganishwa na iliyokuwa Tume ya Haki na Amani. Pia CPT imetambua na kuanza kufanyia kazi hitaji la kuhamasisha ushiriki wa vijana kwa mustakabali wa utume.

3. Changamoto
Historia inaonyesha mafanikio licha ya changamoto ambazo ni kushuka:
- Moyo wa uwajibikaji katika utume, na uwajibikaji wa pamoja kusudi kuhakikisha utume hautegemei mtu mmoja au wachache mno.
- Uwezo wa ofisi kiutendaji kulingana na mahitaji ya utume kwa wakati huu
- Uwezo kifedha kugharimia uendeshaji Ofisi na kazi za utume; na
- Maoni hasi juu ya Utume wa CPT ambapo baadhi huchukulia kuwa ni mambo ya kisiasa


4. Mipango ya Baadaye
- Kuendeleza Vuguvugu la Uhuishaji maadili
- Kuimarisha uwezo wa ofisi
- Kuongeza idadi ya wanachama wenye moyo wa uwajibikaji.

5. MAFANIKIO

i) Kuendesha semina za uhamasishaji juu ya Mafundisho ya Kanisa kuhusu Jamii kwa vikundi na ngazi tofauti tofauti Jimboni.
ii) Kutoa machapisho mbalimbali yenye mafundisho na uchambuzi kuhusu Mafundisho ya Kanisa kuhusu Jamii.
iii) Kuendesha vipindi endelevu Radio Tumaini (CPT na Mafundisho ya Kanisa Kuhusu Jamii)
iv) Kutoa Elimu ya Uraia hususan nyakati za uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu.
v) Kuongoza vuguvugu la Uhuishaji Maadili linaloshirikisha wadau tofauti tofauti.
vi) Kuanzisha Vikundi vya kitaaluma. Kwa Jimbo la DSM, Wanasheria wanajielekeza katika Huduma ya ushauri wa kisheria; Madaktari na Wauguzi wakitoa huduma za afya na hasa Parokia ya Upanga.
vii) Kuhamasisha utume wa CPT katika vyuo vikuu vikiwemo vya SAUT.
viii) Kutoa semina kwa vijana wa TYCS na TMCS juu ya mafundisho ya kanisa kuhusu jamii. Hii ni pamoja na kuhudhuria Mikutano yao inayofanyika kila mwaka.
ix) Kuongeza idadi ya wanachama na vikundi (Matawi) vya CPT Maparokiani.

6. VYANZO VYA MAPATO

i) Ada ya mwaka kwa kila mwanachama
ii) Michango maalum ya hiari toka CPT na washirika /marafiki kwa malengo maalum. Mfano: Thomas More Foundation; na Uimarishaji wa Ofisi
iii) Riba kutoka dhamana za Serikari (Thomas More Foundation)
iv) Uuzaji wa machapisho
v) Majitoleo ya wanachama kwa kazi za utume mf. Kuandika machapisho; kujilipia gharama mbalimbali mf. Za mafungo na tafakari.


Kuhusu Kanisa Katoliki

Ofisi ya Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam inapatikana makao makuu ya Jimbo,
Kanisa la St. Joseph, barabara ya Sokoine na Manseld street.

P.O Box 167, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 762 024 199
Email: mawasiliano@waleijimbodaresalaam.org
            darwaleijimbo@yahoo.com
Web: www.waleijimbodaresalaam.org

Kwa Habari kemkem za Kanisa jiunge nasi

Andika email yako hapo juu, na upokee taarifa za H/walei

Copyright © 2025. All Rights reserved by H/Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam