KOLPING

KOLPING

KOLPING NI NINI?
Kilping ni chama cha kitume chenye kubeba jina la Mwandishi aliyejulikana kama MWENYE HERI PADRE ADOLPH KOLPING.

Jumuiya ya Kolping ya kimataifa iliyoanzishwa na Padre Adolph Kolping ni jumuiya ya kikatoliki yenye kuundwa kwa mfano wa familia, jumuiya yenye kuelekeza maisha kwa njia ya kuelimisha Nyanja zote za maisha, jumuiya ya Kolping inaundwa na familia za Kolping za mahalia, Kijimbo, Kitaifa na Kimataifa.

Makao makuu ya jumuiya ya Kolping kimataifa yako Jijini KOLON – UJERUMANI

KOLPING NI NANI? Ni jina la mwanzilishi wa jumuiya hii. Adolph Kolping alizaliwa tarehe 08/12/1813 katika Mji wa KERPEN, KOLON Nchi ya UJERUMANI. Alipata daraja la upadre tarehe 13/04/1845 na akaanzisha shirika la Kolping tarehe 06/05/1849.

JUMUIYA YA KOLPING TANZANIA.
Jumuiya ya Kolping Tanzania ilianzishwa mwaka 1989 na PADRE DAVID KAMUGISHA kwa idhini ya ASKOFU NESTORY TIMANYWA Mkoani Kagera – Bukoba ndipo yalipo Makao Makuu mpaka sasa.

Jimbo la Dar es Salaam ilinzishwa mwaka 1995 na Padre Thomas Tibainuguka kwa idhini ya Askofu Mkuu wa jimbo la Dar es Salaam Mwadhama Polycup Kardinary Pengo wakianzia na familia za Kigango cha Keko ambayo mpaka sasa inaitwa Parkia ya Ekaristi Takatifu pamoja ikiwa ni kutafakari neon, kujadili miradi yao, pamoja na matendo ya huruma ikiwa kila familia hukaa kwa vikundi kama jumuiya za kanisa Katoliki.

Pia mlezi wetu ndiye aliyehakikisha kuingia katika shirikisho la vyama vya kitume “SHIVYAKI PADRE JOVIN BAKEKELA akiwa ndiye mlezi wa jimbo mpaka sasa.

Jumuiya ya Kolping Tanzania imeenea katika majimbo zaidi ya ishirini (20) nchini Tanzania ikiwa na familia za Kolping zaidi ya mia mbili hamsini (250) ikijivunia wanachama elfu kumi na moja (11,000).

UTUME.
Jumuiya ya Kolping ni chama cha kitume katika Kanisa Katoliki ambacho huelimisha na kusaidia makuzi katika Nyanja zote za maisha ya wanachama wake na jamii kwa umumla.

JUMUIYA YA KOLPING KIMATAIFA.
Muasisi ni Mwenye Heri Padre Adolph Kolping (1813 – 186)
Makao Makuu yako KOLON UJERUMANI.

JUMUIYA YA KOLPING TANZANIA – Muasisi Padre David Kamugisha, Makao Makuu BUKOBA TANZANIA.

MSINGI    -    Tunakoleza utume wetu kwa kuzingatia yafuatayo:-
-    Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo
-    Mafundisho ya Kanisa kuhusu jamii
-    Maisha ya kazi ya Mwenye Heri Adolph Kolp.

NGUZO – Tunaimarisha utume wetu kwa njia zifuatazo:-
-    Sala
-    Elimu
-    Kazi.

PROGRAMU – Tunaelekeza nguvu yetu kwenye kujenga yafuatayo:-
-    Ndoa na familia.
-    Kazi na taaluma.
-    Ushiriki katika jamii.
-    Utamaduni na burudani.

MALENGO.
Lengo kuu – kuwawezesha wanachama wake wawe chachu katika maisha yao wenyewe na washiriki kikamilifu katika kuufanya ulimwengu uwe mahali bora pa kuishi kwa wote na kumtukuza Mungu, pia kumjenga mwanachama kujiimarisha kiroho na kimwili apate kuwa mkatoliki kweli na mwananchi kweli, kuwawezesha watu wote kujijengea maisha yanayostahili hadhi na utu wa binadamu aliyeumbwa kwa sura ya MUNGU.

SEMINA.
Tunapoendelea kufungua familia mpya Parokia mbalimbali za Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Semina huwezeshwa na Ofisi kuu kila Mwaka kwa familia mpya na hasa semina ya ijue Kolping, pamoj na uanzilishwaji wa Saccos.

MAFANIKIO.
Tumepata mafanikio ya kutosha baada ya kupata semina ya muda mrefu, na kujua utume huu, hivyo waamini wanaendesha utume bila shaka kwa sehemu mbalimbali za Parokia waliko.

CHANGAMOTO.
-    Baadhi ya wanachama kutofikia jinsi utume ulivyo.

MWENYEHERI – ADOLPH KOLPING.
Padre Adolph Kolping alitangazwa kuwa mwenye heri na Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa II tarehe 27/10/1991. Hivyo familia zote duniani zilizo wanachama wa Kolping huwa na kusanyiko kuu la pamoja Kijimbo au kifamilia na shamra shamra mbalimbali siku hiyo ikiwa na matukio yafuatayo:-
-    Adhimisho la Ekaristi Takatifu.
-    Kuwa na chakula cha pamoja na burudani.
-    Kusaidia vyuo vya ufundi Kolping Tanzania.

KAULI MBIU – “Kwa moyo wa Kolping zaeni matunda endelevu”

Tumsifu Yesu Kristo.
Ndimi katika utume,

………………………………………………….
KAMATI TENDAJI KOLPING JIMBO



Kuhusu Kanisa Katoliki

Ofisi ya Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam inapatikana makao makuu ya Jimbo,
Kanisa la St. Joseph, barabara ya Sokoine na Manseld street.

P.O Box 167, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 762 024 199
Email: mawasiliano@waleijimbodaresalaam.org
            darwaleijimbo@yahoo.com
Web: www.waleijimbodaresalaam.org

Kwa Habari kemkem za Kanisa jiunge nasi

Andika email yako hapo juu, na upokee taarifa za H/walei

Copyright © 2025. All Rights reserved by H/Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam