Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Dekania ya Mbezi Luis ni moja kati ya dekania zinazounda Jimbo Kuu la Dar es Salaam Dekania iliundwa na Kutangazwa tarehe 18.10.2018 na Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo aliyekuwa Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar es Salaam .
Ilizaliwa kutoka Dekania ya Mt. Monika- Kibaha.
Dekano wa kwanza baada ya kutangaza Dekania alikuwa Pd. Xavery Kassase kutoka Parokia ya Mavurunza. Dekano wa sasa ni .Pd. Sylivester Msemwa.
Parokia zinazounda Dekania hii ni; Mbezi luis, Makabe, Malamba Mawili, Msumi, Pande Msakuzi, Msakuzi, Simon Stock, Tegeta A, Mshikamano, Mpiji Magohe na Mbezi Mageti
Kamati Tendaji ya Kwanza Dekania ya Mbezi Luis; Mwenyekiti -Michael Nchimbi (Mbezi Louis), Makamu M/kiti -Casmir Nkuba (Mavurunza)Katibu - Silvani Mng’anya (Mshikamano), Katibu Msaidizi: Fabian Mwakatuma (Msakuzi) Mtunza Hazina -Josephine Kolola (Tagaste)
Pd. Sylvester Msemwa, 2023-----------
Padre wa shirika la Wakarmel OCD
Pd. Vivian Menezes. 2021 - 2023
Padre wa shirika la Wakarmel OCD.
Kaimu Dekano: Pd. Fulgence Oiso - Nov. 2020 -
09.04.2021
Padre wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam
Pd. Wilfred Pais. 2019 - 2020
Padre wa shirika la Wakarmel OCD
Pd. Xavery Kassase,
OSA 2018 - 2019
Padre wa Shirika la Mt. Agustino OSA
Maelezo ya mawasiliano
Pd. Sylivester Msemwa
Mkuu wa Dekania ya Mbezi Louis
Phone : 0762 007000