Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Muundo wa Halmashauri Walei ndani ya Jimbo, kwa mujibu wa Katiba ya Halamshauri Walei taifa ya 2019 unaanzia ngazi ya Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristu, Kanda, Vigango, Parokia, Dekania, Jimbo mpaka Taifa kama ifuatavyo;
HALMASHAURI WALEI NGAZI YA JUMUIYA
Inaundwa na Kamati Tendaji jumuiya, Wenyeiti wa vyama vya Kitume katika jumuiya husika, mwakilishi wa familia katika jumuiya husika, Makatibu wa kamati ndogo ndogo za kikatiba na zile maalum
HALMASHAURI YA WALEI NGAZI YA KANDA
Inaundwa na Kamati Tendaji ngazi ya Kanda , Kamati Tendaji za jumuiya ndani ya Kanda, Wenyeviti wa vyama vya kitume ngazi ya kanda.
HALMASHAURI YA WALEI NGAZI YA KIGANGO
Inaundwa na kamati tendaji kigango, wenyeviti wa vyama vya kitume ngazi ya Kigango na kamati tendaji zote ndani ya jumuiya za kigango.
HALMASHAURI WALEI NGAZI YA PAROKIA
Inahusisha Kamati Tendaji Parokia, Kamati Tendaji ngazi ya kigango au vigango, Wenyeviti wa kanda endapo Parokia ina kanda nyingi, wenyeviti wa vyama vya kitume ngazi ya parokia. Paroko ni mjumbe rasmi katika ngazi hii.
HALMASHAURI YA WALEI NGAZI YA DEKANIA
Inaunda na kamati Tendaji Dekania, Kamati Tendaji ngazi ya Parokia, wenyeviti wa vyama vya kitume ngazi ya Dekania.
HALMASHAURI YA WALEI JIMBO
Inajumuisha Kamati Tendaji Jimbo, Kamati Tendaji Parokia zote ndani ya Jimbo la Dar es salaam, Wenyeviti wa vyama vya Kitume Jimbo Kuu la Dar es salaam pamja na Mkurugenzi waw a Utume wa Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam.
HALMASHAURI YA WALEI TAIFA
Inajunuisha Kamati Tendaji Taifa, Wenyeviti wa Halmashauri ya Walei wa Majimbo, Wenyeviti wa vyama vya Kitume toka Majimbo yote, Askofu mwenyekiti wa Idara ya Utume wa Walei, Idara au Tume za Katekesi, Uchungaji, Liturjia, Elimu, haki na amani zaweza kualikwa pia