Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
DIRA (VISION)
Kuwa kitovu cha ubora cha kuishauri ipasavyo Hierakia katika ngazi husika za Halmashauri kuanzia Jumuiya ndogo ndogo, Parokia, Dekania, Jimbo hadi Taifa katika safari ya kulipeleka Kanisa Mbinguni.
DHIMA (MISSION)
Kuwaunganisha Waamini Walei katika Wito na Utume wao wa kutakatifuza malimwengu kwa ajili ya Kristo katika ngazi husika kuanzia Jumuiya Ndogondogo hadi Taifa
MALENGO MAKUU (GOALS)
- Kuimarisha IMANI ya waamini Walei.
- Kuimarisha utendaji wa Halmashauri ya Walei katika ngazi zote za uongozi.
- Kubuni mipango ya kimaendeleo na kuratibisha mambo yanayohusu mipango, uchumi na fedha.
- Kuimarisha ufuatiliaji na tathimini ya malengo ya Mpango Mkakati.
KAULI YETU
Nuru yetu iangaze ili tutakatifuze malimwengu
MAADILI YA MSINGI (CORE VALUES):
- Kutenda kwa wajibu na haki;
- Kushuhudia imani kwa ujasiri na ukweli;
- Kudumu katika sala na neno la Mungu; na
- Kuimarika kiroho.