KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Vyama Vya Kitume
Vyama, Mashirika na Jumuiya za Kitume (VMJ)

Kwa mujibu wa Katiba ya Halmashauri Walei uk Viii, ni vikundi vilivyoanzisha na baadhi ya Wakatoliki, ambao ni Makleri, Walei au wale wanaoishi Maisha ya wakfu na kuidhinishwa na uongozi wa  Kanisa kwa lengo la kutekeleza  utume wa aina fulani. Baadhi ya vyama hivi vinaweza kuwa vimeanzishwa  katika Kanisa  mahalia katika ngazi ya parokia, Kijimbo na Kitaifa. Vingine vinaweza kuwa vimeanzishwa  katika maeneo fulani  lakini vikapata bahati ya kuenea katika Kanisa la Ulimwengu (Rejea Sura ya Tatu, 3,2)

Vyama Mashirika na Jumuiya za Kitume vinafanya kazi zake chini ya mwamvuli wa Halmashauri Walei katika ngazi husika.

Bila kuathiri masharti na Katiba hii, Vyama Mashirika na na Jumuiya za Kitume zitakuwa na katiba au miongozo yao kulingana na karama zao

Kiongozi Hierakia ndiye Mlezi Mkuu wa Vyama , Mashirika na Jumuiya za Kitume katika ngazi husika

Orodha ya Vyama vya Kitume
Vyama Vyetu vya Kipapostoli

Hapa chini ni baadhi ya Vyama vya Kitume vinavyofanya kazi katika Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. Bonyeza kwenye kila chama ili kujua zaidi kuhusu dhamira yao, shughuli zao, na jinsi ya kuhusika:

Christian Professionals of Tanzania (CPT)

(CPT) ni Chama cha Wanataaluma Wakristo wa Tanzania (Christian Professionals of Tanzania) kilitambulika rasmi kuwa miongoni mwa vyama vya kitume katika kanisa la Tanzania mwaka 1981, na kupewa msimamizi mwombezi Mt. Thomas More. Haikuchukua muda mrefu CPT ikatambulika katika chombo cha International Catholic Movement for Intellectual and Cultural Affairs (Pax Romana ICMICA). MWAKA 1983 CPT ikawa mwanachama rasmi wa ICMICA.

Soma Zaidi
Damu Azizi

Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ni Shirika la Kazi za Kitume la Mapadre na Mabruda lililoanzishwa na Mt. Gaspari del Bufalo tarehe 15 Agosti 1815 huko Giano Italia, katika Abasia ya Mt. Felix na kuwekwa chini ya Ulinzi wa Mama Bikira Maria wa Damu Azizi na Usimamizi wa Mt. Fransisko Ksaveri. Lengo la Gaspari kuanzisha Shirika hili lilikuwa ni kueneza Upendo wa Kristo aliouonesha alipomwaga Damu yake msalabani kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu. Ndiyo maana Gaspari alisema, 3 “Natamani niwe na ndimi elfu ili upendo huo uwafikie watu wote”.

Soma Zaidi
Familia ya Neno la Mungu

Familia ya Neno la Mungu ni chama cha Kikristo kinachojikita katika kueneza neno la Mungu na kusaidia familia katika muktadha wa kiroho na kijamii. Chama hiki kinatoa nafasi kwa wanachama wake kuungana na kujifunza Neno la Mungu, huku wakishiriki katika huduma kwa familia na jamii kwa jumla. Lengo kuu la Familia ya Neno la Mungu ni kuimarisha familia na kuendeleza maisha ya kiroho kwa kupitia mafundisho ya Biblia.

Soma Zaidi
Karismatiki Katoliki

Karismatiki Katoliki ni mwamko mmoja wapo katika Kanisa Katoliki ambao unakazia uwepo wa Roho Mtakatifu, Nguvu zake, karama zake na mahusiano naye. Ni mkondo unaolenga mabadiliko ya kiroho na kimaadili kwa mtu binafsi na Kanisa kwa ujumla. Inahusisha pia kuishi Injili katika fan izote za Maisha  kwa kutambua kuwa, kufanya hivyo ni kushirikiana na Roho Mtakatifu katika kumshuhudia Kristo

Soma Zaidi
Kolping

Kolping ni jumuiya ya waumini ambao wanajitolea kwa huduma ya kijamii na kiroho. Lengo la Kolping ni kuleta mabadiliko katika jamii kwa kuimarisha familia, kuongeza hali ya maisha, na kusaidia watu maskini. Wanachama wa Kolping wanajivunia kujitolea kwa huduma za kijamii, kusaidia watoto, vijana, na familia, na kuwa na mchango katika maendeleo ya jamii.

Soma Zaidi
Lejio Maria

Lejio Maria ni Chama cha Kitume cha Wakatoliki ambao, kwa ruhusa ya Kanisa na kwa uongozi shupavu wa Maria asiye na Doa, mgawaji wa Neema zote, wameungana kwa pamoja kuwa jeshi lililoandaliwa kwa vita ambavyo Kanisa linapigana kila siku na nguvu za uovu hapa duniani

Soma Zaidi
Ministrant

Ministrant ni jumuiya ya waumini ambao wanajitolea katika utumishi wa kanisa kwa kufanya kazi za huduma ya madhabahuni wakati wa ibada kwa kusaidia mapadre, na kufanya shughuli nyingine zinazohusiana na ibada. Kwa njia ya huduma hii, wanachama wanajengeka kiroho na kuwa na nafasi ya kuwa sehemu ya maisha ya kiroho ya kanisa.

Soma Zaidi
Moyo Mtakatifu wa Yesu

Moyo Mtakatifu wa Yesu ni jumuiya ya waamini Wakatoliki waliotoa maisha yao kwa heshima ya Moyo Mtakatifu wa Yesu. Chama hiki kinaimarisha maisha ya kiroho ya wanachama wake kupitia sala, tafakari, na huduma za upendo kwa wahitaji.

Soma Zaidi
Mt. Anna

Mt. Anna ni chama kinachojitolea kutoa huduma za kijamii na kiroho kwa wahitaji, hasa wazee na wanawake. Chama hiki kimejikita katika kusaidia familia na jamii kwa njia ya matendo ya upendo na huduma. Wanachama wa Mt. Anna wanahamasishwa kutenda matendo mema kwa ajili ya ustawi wa jamii na kuwa mfano wa maisha ya Kikristo.

Soma Zaidi
Mt. Ritha wa Kashia

Mt. Ritha wa Kashia ni shirika linalolenga kukuza umoja, ukuaji wa kiroho, na huduma kwa jamii. Linakusudia kuleta pamoja watu waliyo tayari kutumikia jamii zao, kukuza imani, na kushiriki katika shughuli za kijamii na kitamaduni.

Soma Zaidi
Mt. Vincent wa Paulo

Mt. Vincent wa Paulo ni jumuiya ya kiroho na ya kijamii inayojitolea kutoa msaada kwa maskini, waathirika wa vita, na wale walio katika hali ya dhiki. Imetokana na wito wa Mt. Vincent wa Paulo, ambaye alijitolea kwa huduma ya watu maskini, shirika hili linafanya kazi ili kuleta mabadiliko na kuboresha hali ya maisha ya wahitaji.

Soma Zaidi
Rozari Hai

Historia ya Rozari Hai ni kama ilivyo sasa, ilianza mnamo mwaka 1826 huko Lyons Ufaransa. Mwaka huu wa 2026 inatimia miaka 200 tangu ianzishwe Duniani. Tanzania ilitufikia tarehe 8/12/1986, mwaka huu wa 2026 inatimia miaka 40 tangu iingie nchini Tanzania.Ushirika huu wa Rozari Hai ulianzishwa na msichana mmoja kwa jina Pauline Marie Jaricot binti Mfaransa ambaye kwa sasa ni Mwenye Heri(2022).).


Soma Zaidi
Shirika la Wazee na Wastaafu

Shirika la Wazee na Wastaafu Katoliki linawaunganisha Wanaume na Wanawake ambao wamefikia au wanakaribia umri wa kustaafu  yaani kuanzia miaka 50 na kuendelea, lengo ikiwa kuimarisha maisha yao ya kiroho na kijamii, kuwajali na kuwathamini hata baada ya kustaafu kwao pamoja na kutumia karama zao katika kuleta maendeleo katika Kanisa na jamii.

Soma Zaidi
UKWAKATA (UKWAKATA)

UKWAKATA ni kifupi cha neno (Utume wa Kwaya Katoliki Tanzania) Utume huu ulianzishwa mnamo mwaka 1977 wakati huo Utume huu ukijulikana kwa jina la SHIKWAKA yaani (Shirikisho la Kwaya Katoliki) Jimbo Kuu la Dar es salaam

Soma Zaidi
Upendo Group

Chama hiki kilipokelewa rasmi katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam tarehe 27/09/2020 na Askofu Mkuu Jude Thadaeus Ruwa’ichi OFM CAP, wa Jimbo Kuu la Dar es salaam.

Kabla ya hapo kilikuwa katika ngazi ya Dekania ya Ubungo kikilelewa na aliyekuwa Dekano wa Ubungo Hayati Monsinyori D. Mbiku, ambaye alikuwa pia Paroko wa Parokia ya Chuo Kikuu.

Soma Zaidi
Utoto Mtakatifu (PMS)

Utoto Mtakatifu ni mpango unaojishirikisha na malezi ya Watoto kwa kutoa Mafunzo ya Kijamii na Malezi ya Kiimani chini ya Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu (PMS). Kuna usemi unasema “Watoto ni Malezi”Parokia nyingi sasa hivi zimejikita juu ya malezi ya watoto. Kuwepo kwa shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu kumechochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa kiimani kwa watoto, 

Soma Zaidi
Utume wa Fatima (UFUT)

 Utume wa Fatima ni chama kinachojikita katika kujifunza, kutekeleza na kueneza ujumbe wa Mama Bikira Maria alioutoa kule Fatima Ureno mwaka 1917. Ujumbe huu aliwapa watoto wachungaji watatu; Lusia, Fransisko na Yasinta kwaniaba ya kanisa lote.

Soma Zaidi
Utume wa Uimarishaji wa Familia Tanzania (UFATA)

Uimarishaji wa Familia Tanzania (UFATA) ni chama kinachojihusisha na kukuza ustawi wa familia katika jamii. UFATA inalenga kutoa msaada wa kijamii na kiroho kwa familia na kuhamasisha umoja na mshikamano katika familia. Chama hiki kinahakikisha familia zinapata huduma bora zinazozingatia maadili ya Kikristo.

Soma Zaidi
Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA)

Umoja huu ulianzishwa kwa lengo la kuwawezesha wanaume Wakatoliki kuwa mstari wa mbele katika kushiriki huduma za kiroho na kijamii ndani ya Kanisa na jamii kwa ujumla. Kupitia UWAKA, wanaume wanahamasishwa kuwa viongozi wa kiroho katika familia zao, na wao pia wakiwa nguzo ya kanisa na kushiriki kutakatifuza malimwengu


Soma Zaidi
Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA)

VIWAWA ni utume wa Vijana Wakatoliki Wafanyakazi wanaume na wanawake waishio mijini, vijijini na walio kwenye masomo, mafunzo ya fani mbalimbali, walio katika ajira rasmi na zisizo rasmi ambao wanatumwa na Kanisa ili kueneza habari njema ya Yesu Kristu 

Soma Zaidi
Wajane na Wagane

Chama cha Wajane na Wagane ni jumuiya ya waumini inayoleta pamoja wanawake na wanaume waliopoteza wenzi wao kwa lengo la kutoa msaada, faraja, na ushirikiano katika kipindi cha huzuni. Jumuiya hii inatoa fursa kwa wanachama wake kujenga tena maisha yao ya kiroho na kijamii, pamoja na kusaidiana katika changamoto mbalimbali za maisha.

Soma Zaidi
Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA)

WAWATA ni chombo kinacho waunganisha Wanawake Wakatoliki Tanzania, kilianzishwa mwaka 1972 kwa lengo la kujitakatifuza na kutakatifuza malimwengu. Muundo wa WAWATA umeanzia katika Jumuiya Ndogondogo za Kikristu, Vigango, Dekania, Parokia,  Jimbo hadi Taifa kama ulivyo muundo wa Kanisa Katoliki Tanzania.

Soma Zaidi
Yusuph wa Arimathea

Yusuph wa Arimathea ni chama kinachowaleta pamoja waumini walioko katika familia za Kikatoliki na wanaohusiana na huduma ya msalaba, wakitoa msaada kwa wale wanaohitaji faraja na msaada wa kiroho. Chama hiki kinatoa huduma ya kiroho kwa wale waliopoteza wapenzi wao na kuhamasisha wanachama wake kuwa na roho ya kujitolea kama Yusuph wa Arimathea.

Soma Zaidi