KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Vyama Vya Kitume
Utume wa Fatima (UFUT)
Muhtasari wa Chama:

Jumuiya ya Utume wa Fatima ilianzishwa kwa lengo la kuendeleza ujumbe wa Bikira Maria alioutoa Fatima, Ureno, mnamo mwaka 1917. Ujumbe huu unahimiza maombi ya Rozari Takatifu, toba ya dhambi, na sala kwa ajili ya amani duniani.

Utume wa Fatima Ulimwenguni ulianzishwa na Monsinyori Horald Colgan tarehe 24, Mei 1947 huko Amerika ya Kaskazini (USA) ukijulikana kama Blue Army. Kwa sasa sehemu nyingi utume huu unajulikana kama Utume wa Fatima Ulimwenguni (UFU) na hapa kwetu unajulikana kama Utume wa Fatima Ulimwenguni Tanzania (UFUT).

Mwezi Desemba 1988, Utume wa Fatima Ulimwenguni Tanzania (UFUT) ulizinduliwa rasmi katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Hayati Monsinyori Deogratias Mbiku ambaye alikuwa Mkurugezi wa Utume wa Walei jimboni, na Paroko wa Parokia ya Chang’ombe kwa wakati huo. Uzinduzi huo ulifanyika katika parokia ya Bikira Maria wa Fatima – Msimbazi ambapo ndiyo makao makuu ya utume jimboni hadi leo

Malengo ya UFUT:
  • Kuhamasisha waamini kusali Rozari Takatifu mara kwa mara.
  • Kuimarisha sala na toba kwa ajili ya dhambi za ulimwengu.
  • Kukuza ibada kwa Bikira Maria kama Mama wa Amani.
  • Kueneza ujumbe wa Fatima katika familia na jumuiya za Wakatoliki.
  • Kujiweka Wakfu kwa Moyo Safi wa Maria ili tuwe watoto wake 
  •  Kutolea sadaka kwajili ya kufanya malipizi ya dhambi na kuwaombea wakosefu (kutakatifuza malimwengu)
Uongozi:
DAUDI MASAKA
MWENYEKITI
Tel : 0714000177
GRACE MNYANI
MAKAMU MWENYEKITI
Tel : 0754283940
ADELAIDA NUGU
KATIBU
Tel : 0688946046
GEORGE KITUPI
KATIBU MSAIDIZI
Tel : 0715582808
JUSTINA MBEPELA
MTUNZA AZINA
Tel : 0754370387
Shughuli na Matukio
Shughuli:
  • Maombi ya Rozari: Kuendesha maombi ya pamoja ya Rozari Takatifu kila Jumamosi katika parokia mbalimbali.
  • Mafunzo ya Ibada: Kuwapatia waamini mafundisho ya kina juu ya ujumbe wa Fatima na umuhimu wa toba.
  • Shughuli za Upendo: Kutembelea wagonjwa, wazee, na watoto yatima huku wakiwaombea na kuwasaidia mahitaji yao.
  • Uhamasishaji wa Amani: Kuendesha kampeni za maombi kwa ajili ya amani ulimwenguni.
Mikutano:
  • Mikutano ya Sala: Kufanyika kila wiki kwa maombi ya Rozari na tafakari ya mafundisho ya Bikira Maria.
  • Semina za Kiimani: Kufanyika mara moja kila mwezi kwa wanachama ili kujifunza zaidi kuhusu ibada ya Fatima.
  • Mkutano wa Mwaka: Wanachama hukutana kila mwaka kwa ajili ya kushirikishana mafanikio na kupanga shughuli za mwaka mpya.
Kuwa Mwanachama
Kuwa Mwanachama

Kuwa mshirika wa Shirika la Kimisionari ni njia ya kuridhisha ya kutumikia Kanisa na jamii yako. Iwe unahisi wito wa kuongoza, kutumikia, au kuimarisha safari yako ya kiroho, kuna nafasi kwa ajili yako katika mojawapo ya mashirika yetu. Wasiliana nasi leo ili kujua zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kujiunga.

Uanachama:
  • Jinsi ya Kujiunga:

    Ili kujiunga na Utume wa Fatima Ulimwenguni Tanzania (UFUT), mkristo mkatoliki atajifunza vizuri zaidi juu wa Ujumbe wa Fatima katika vipengere hivi vinne; Atajifunza maana na namna ya kutolea sadaka/ kutakatifuza malimwengu, Atajifunza namna zuri ya kusali Rozaria Takatifu kwa uchaji, Atajifunza jinsi ya kufanya ibada ya jumamosi ya kwanza ya mwezi ambayo ni ibada ya lazima sana kwa mwongofu wa wakosefu na amani

    Kwa maswali kuhusu uanachama, tafadhali wasiliana na info@darwalei.or.tz

  • Ada ya Uanachama:
    Ada ya uanachama : TZS 2,500.
Tafadhali andika jina la taasisi yako.
Tafadhali andika jina lako la kwanza.
Tafadhali andika jina lako la mwisho.
Tafadhali andika namba yako ya simu.
Tafadhali andika barua pepe sahihi.
Tafadhali andika ujumbe wako / Maoni (ikiwa yapo).