KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Rasilimali
Kupanuka kwa Shughuli za Kichungaji

Onyesho la ukuaji wa idadi ya Parokia katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwa miaka tofauti.

Tarehe 16.11.1887 itakumbukwa kama ndio siku muhimu sana katika historia ya Jimbo la Dar es salaam, ni siku ambayo Jimbo la Dar es Salaam lilizaliwa. Baba Mtakatifu Leo wa XIII ndiye aliyeongoza suala la uwekaji saini mkataba. Kanisa la Mt. Yosef lilipandishwa hadhi ya kuwa Parokia 1889 likiwa ni Kanisa pekee kabisa kuwa Parokia katika Jimbo la Dar es salaam, ujenzi wa Kanisa ulianza 1897 na kufikia 1907 ujenzi ulikuwa umekamilika. Eneo la mji wa dar es Salaam lilikuwa na parokia moja tu mpaka ilipo anzishwa parokia ya Msimbazi 1953.

Wakati anawekwa Wakfu kuwa Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam, Mhashamu Edga Aristides Maranta, alipokea Kanisa la Mtakatifu Yosefu ikiwemo Pugu na Kipatimo. Kipatimo kwa wakati huo ilikuwa ni sehemu ya Jimbo la Dar es Salaam. Kufikia 1971 tayari parokia 16 zilikuwa zimekwisha ongezeka zikiwemo Msimbazi, Chang’ombe, Oysterbay, Magomeni, Upang ana Kurasini. Kufikia 1971 mabaraza ya walei yaliundwa karibu parokia zote jimboni, wakati huo Parokia zilikuwa 16 tu 1970/71. Na kufikia mwaka 1992 parokia zilikuwa kati ya 22.

Wakati wa kusheherekea miaka (100) ya kubarikiwa Kanisa Kuu la Mt. Yosef, yaani 2003, Parokia zaidi ya arobaini zilikuwa zimeanzishwa, na kufikia 2019 parokia zilikuwa 117, na mpaka kufikia wakati huu 2025 Parokia 167 zimeanzishwa.

Tathmini katika katika eneo hili inaonyesha maendeleo makubwa ya ukuaji wa ki imani katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Na hii ni kutokana na kazi kubwa ya kichunga kupitia uongozi Hierakia, yaani Makleri kushirikiana na Waamini Walei kupitia nguvu ya Pamoja kuhakikisha Habari njema inawafikia watyu wote ili kutakatifuza malimwengu.