Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Vuguvugu la kuanzisha Umoja wa
Wanawake Wakatoliki
Kutokana na mwaliko wa Mtaguso
Mkuu wa Vatikano wa II fursa ilitolewa kwa Walei kutokana na ubatizo wao wajue
wajibu wao na wajiweke katika utumishi wa Kristo na wa Kanisa ( Hati ya mtaguso
No. 914) Mwaka 1967 wakati wa mamlaka ya Papa Yohane wa
23 Vatikano Roma iliwashirikisha waumini Wakatoliki duniani wakiwemo maaskofu,
mapadre na walei ili kujadili juu ya hali ya kanisa.
Ndugu Joseph Mutayoba kutoka Jimbo
la Bukoba, ndugu Selestin Fidelis kutoka Jimbo la Rulenge, ndugu Linus
Kisusangi kutoka Jimbo la Iringa na Bibi Bernadete Kunambi kutoka Jimbo Kuu la
Madhumuni makuu ya WAWATA ni pamoja na kuwaunganisha wanawake Wakatoliki nchini Tanzania katika juhudi zao zinazowahusu kama Wakristo, wanawake, na raia, wakiwa katika vikundi mbalimbali ambavyo hasa lengo lao ni kustawisha kanisa na jamii. ( Katiba ya WAWATA, uk. 1 na 2). Katiba imeainisha vyema majukumu yawapasayo Wanawake katika utume wa kanisa ikiainisha pia kazi za Viongozi na taratibu zinazo wapasa kama walei ndani ya Kanisa
·
Uimarishaji
wa Jumuiya ndogo ndogo.
·
Mafungo
ya mwaka katika ngazi zote
·
Vikundi
vya sala na ushiriki katika vyama
vingine vya kitume
·
Kukuza
miito na kusaidia Seminari kwa hali na
mali
·
Kuanzisha
na kulea Utoto Mtakatifu
·
Matendo
ya Huruma kwa wahitaji
·
Tafakari
ya mafundisho ya kanisa katika matukio mbalimbali ya kanisa
- Mikutano ya Wiki: Hufanyika mara moja kila wiki kwa ajili ya kujadili masuala ya kiimani na kijamii.
- Mkutano wa Parokia: Hufanyika kila mwezi kwa lengo la kujadili maendeleo ya Umoja katika parokia.
- Mkutano Mkuu wa Wanawake: Hufanyika mara moja kwa mwaka na hujumuisha wanawake kutoka maeneo yote ya Jimbo Kuu.
Kuwa mshirika wa Shirika la Kimisionari ni njia ya kuridhisha ya kutumikia Kanisa na jamii yako. Iwe unahisi wito wa kuongoza, kutumikia, au kuimarisha safari yako ya kiroho, kuna nafasi kwa ajili yako katika mojawapo ya mashirika yetu. Wasiliana nasi leo ili kujua zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kujiunga.
- Jinsi ya Kujiunga:
Kwa maswali kuhusu uanachama, tafadhali wasiliana na vyama@darwalei.or.tz