KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Vyama Vya Kitume
Lejio Maria
Muhtasari wa Chama:

Lejio Maria ni Chama cha Kitume cha Wakatoliki ambao, kwa ruhusa ya Kanisa na kwa uongozi shupavu wa Maria asiye na Doa, mgawaji wa Neema zote, wameungana kwa pamoja kuwa jeshi lililoandaliwa kwa vita ambavyo Kanisa linapigana kila siku na nguvu za uovu hapa duniani

Lejio Maria iliasisiwa tarehe 7 Septemba, 1921 huko Dubline Ireland na Kaka Frank Duff (kwa sasa ni marehemu). Nchini Tanzania chama kilianzishwa 1936 kule Mbulu. Na kwa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Lejio Maria ilianzishwa 1944, mwasisi wake akiwa Edel Quinn (ambaye pia ni marehemu) Lejio Maria Dar es Salaam iliteuliwa na TEC kuwa Mratibu wa shuguli za Lejio Maria kitaifa tangu mwaka 1987. Walejio kama waamini wengine wanashiriki katika shughuli za Kanisa kwa kuhudhuria ibada mbalimbali, kuhudumu katika Kanisa mahalia, kuchangia michango mbalimbali n.k

Malengo:

1.   Nia na madhumuni ya Chama cha Wlejio Maria ni utakatifu wa wanchama wake kwa kusali na kufanya kazi za kitume na za kijamii. Pia kuwatakatifuza wengine

§        Kuongeza idadi ya wanachama

§        Kutoa semina, kufanya mafungo na hija ili kuimarika kiroho

 



Uongozi:
EMMANUEL NYAKI
MWENYEKITI
Tel : 0715117122
ALVERA KABWOGI
MAKAMU MWENYEKITI
Tel : 0784 278179
ANTHONY S. MBUNDA
KATIBU
Tel : 0654 066880
BONN LEONCE
KATIBU MSAIDIZI
Tel : 0788 266302
ANNETH H. NAISO
MTUNZA FEDHA
Tel : 0717 474748
Shughuli na Matukio
Shughuli:
  • Kuimarisha maisha ya kiroho ya wanachama kwa njia ya sala na tafakari.
  •  Kufanya kazi za kitume kama kuwatia moyo wazee na wasiojiweza Pamoja na wagonjwa hospitalini na majumbani, kushauri wasio funga ndoa, wasiobatizwa nawaliolegea kiimani. 
  • Kutembelea jumuiya ndogondogo, kufundisha Neno la Mungu na kupata wanachama wapya.
  • Kwa upande wa huduma za jamii, walejio huwasaidia kazi wasiojiweza na wagonjwa kwa mfano; kuwafulia nguo, kufanya usafi, kuwaogesha, kuwalisha wasio na uwezo Pamoja na walemavu.
  • Kwa upande wa kiuchumi; Chama cha Lejio Maria hakiruhusu mambo ya shuguhuli za kiuchumi wala kumiliki mali isipokuwa fedha kidogo zinazopatikana kupitia mfuko wa siri katika vikao vya wanachama
  • Chama hakipati misaada ya toka nje isipokuwa wanachama wenyewe huchangia kwenye mfuko wa siri wa kila mkutano wa Praesidium na Baraza husika
  •   Kuhamasisha wanachama kushiriki kikamilifu katika huduma za Kanisa
Mikutano:
  • Mikutano ya Sala: Hukutana kila wiki kwa ajili ya sala za pamoja na tafakari za kiroho.
  • Mkutano wa Mpango Kazi: Hufanyika kila mwezi kwa ajili ya kupanga na kutathmini shughuli za jumuiya.
  • Sherehe za Bikira Maria: Huandaliwa kila mwaka kwa kusherehekea sikukuu maalum za Bikira Maria.
Kuwa Mwanachama
Kuwa Mwanachama

Kuwa mshirika wa Shirika la Kimisionari ni njia ya kuridhisha ya kutumikia Kanisa na jamii yako. Iwe unahisi wito wa kuongoza, kutumikia, au kuimarisha safari yako ya kiroho, kuna nafasi kwa ajili yako katika mojawapo ya mashirika yetu. Wasiliana nasi leo ili kujua zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kujiunga.

Uanachama:
  • Jinsi ya Kujiunga:

    Kujiunga na Legio Maria, waamini wanashauriwa kuwasiliana na viongozi wa jumuiya katika parokia zao. Mafunzo ya awali yataandaliwa ili kuwasaidia wanachama wapya kuelewa misingi ya jumuiya na majukumu yao. Ada ya uanachama ni TZS 3,000 kwa mwezi. Michango hii hutumika kufanikisha shughuli za jumuiya na kusaidia wanachama wenye uhitaji.

    Kwa maswali kuhusu uanachama, tafadhali wasiliana na info@darwalei.or.tz

  • Ada ya Uanachama:
    Ada ya uanachama : TZS 3,000.
Tafadhali andika jina la taasisi yako.
Tafadhali andika jina lako la kwanza.
Tafadhali andika jina lako la mwisho.
Tafadhali andika namba yako ya simu.
Tafadhali andika barua pepe sahihi.
Tafadhali andika ujumbe wako / Maoni (ikiwa yapo).