KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Vyama Vya Kitume
Shirika la Wazee na Wastaafu
Muhtasari wa Chama:

Wazee na Wastaafu ni kundi lililopewa nafasi maalum katika Kanisa, likizingatia umuhimu wao katika kuendeleza mafundisho ya imani na kutoa ushauri kwa vizazi vya sasa. Kupitia jumuiya hii, wanachama hupata fursa ya kushiriki ibada, mafunzo ya kiroho, na shughuli za kijamii zinazoboresha maisha yao.

Chama hiki kinalenga pia kuhakikisha mahitaji ya kiroho na kihisia ya wazee yanatimizwa kwa kuwapatia mazingira rafiki ya kuabudu na kushiriki kikamilifu katika utume wa Kanisa. Ni sehemu ya kuwapa heshima wanayostahili na nafasi ya kuchangia hekima yao kwa jamii.

Malengo:

13.     Kueneza habari njema miongoni mwao, katika JNNK na kufundisha dini shuleni. 

4.     Kushauri na kusaidia katika kukuza nidhamu na maadili ya watoto, vijana na watu wazima kutokana na mumomonyoko wa maadili..

5.     Kuwawezesha Wazee na Wastaafu kutumia karama na ushauri wao katika Kanisa na jamii.

6.     Kubuni mbinu za kiuchumi ili  kuinua  maisha ya Wazee na Wastaafu Wakatoliki katika Kanisa na  jamii

7.     Kuweka mipango na taratibu za kuhudumiana wanapokabiliwa na matatizo.

Kukuza na kudumisha mawasiliano na mshikamano wa wanachama nchini.

k

 
Uongozi:
RICHARD G. SILLO
MWENYEKITI
Tel : 0754 310443
BERNADETHA B. KHANGA
MAKAMU MWENYEKITI
Tel : 0688 328687
GERWIN K. MILLINGA
KATIBU
Tel : 0715 463710
VICTORIA D. RWEGOSHORA
KATIBU MSAIDIZI
Tel : 0712 451150
MICHAEL C. DALO
MTUNZA FEDHA
Tel : 0787 075265
Shughuli na Matukio
Shughuli:
  • Ibada Maalum za Wazee: Kuandaa misa na ibada maalum kwa ajili ya wazee na wastaafu.
  • Ziara za Upendo: Wanachama kutembelea wazee wagonjwa na wanaohitaji msaada.
  • Warsha za Afya: Mafunzo kuhusu afya ya wazee na huduma zinazowahusu.
  • Mikutano ya Ushauri: Kukutana na viongozi wa Kanisa kwa ajili ya ushauri wa kiroho na kijamii.
Mikutano:

       1  Wanachama wa ngazi ya JNNK, Kigango na Parokia watakutana kila    Alhamisi au siku nyingine ya Juma iliyokubalika kwa Misa na Sala za Shirika kufuatana na Katiba.

       2  Washirika  wa ngazi ya Kigango / Parokia watakutana kwa Misa na Sala kila Jumapili  moja katika  mwezi kama ilivyokubaliwa na Paroko.

3      Kamati Tendaji ngazi ya Kigango / Parokia zitakuwa na mikutano ya kawaida mara moja kila mwezi. Katibu ataweka kumbukumbu.

4      Kamati Tendaji za Dekania/Vikariati zitakuwa na mikutano ya kawaida mara nne kwa mwaka.

5      Kamati Tendaji ya Jimbo / Taifa zitakuwa na mikutano ya kawaida  mara nne kwa mwaka.

6      Mkutano Mkuu wa wanachama wote katika Kigango na Parokia utafanyika  mara moja kwa mwaka.

7      Mkutano Mkuu wa wanachama wote wa Jimbo utafanyika katika kipindi kisichozidi mwaka moja baada ya Uchaguzi Mkuu.

8      Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Jimbo utafanyika mara mbili kila mwaka.

9      Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Utekelezaji utafanyika mara moja kila mwaka.

Kuwa Mwanachama
Kuwa Mwanachama

Kuwa mshirika wa Shirika la Kimisionari ni njia ya kuridhisha ya kutumikia Kanisa na jamii yako. Iwe unahisi wito wa kuongoza, kutumikia, au kuimarisha safari yako ya kiroho, kuna nafasi kwa ajili yako katika mojawapo ya mashirika yetu. Wasiliana nasi leo ili kujua zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kujiunga.

Uanachama:
  • Jinsi ya Kujiunga:

    Kwa maswali kuhusu uanachama, tafadhali wasiliana na vyama@darwalei.or.tz

Tafadhali andika jina la taasisi yako.
Tafadhali andika jina lako la kwanza.
Tafadhali andika jina lako la mwisho.
Tafadhali andika namba yako ya simu.
Tafadhali andika barua pepe sahihi.
Tafadhali andika ujumbe wako / Maoni (ikiwa yapo).