KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Vyama Vya Kitume
Christian Professionals of Tanzania (CPT)
Muhtasari wa Chama:

Historia ya CPT iko katika vipindi vinne kwa kuzingatia vigezo vya hali ya  utume ilivyokuwa, kazi za utume zilizofanyika na njia za utekelezaji pamoja na changamoto  zilizoambatana na kipindi husika. Vipindi hivyo ni:

  1. kipindi cha kuanza na kuenea  (1980 – 1990)
  2. kipindi cha kuimarika na kutambulika na jamii ( 1990 – 1995)
  3. kipindi cha ushirikiano baina ya CPT na Tume ya Haki na Amani (1995 – 2010)
  4. kipindi cha mpito kulekea mabadiliko ( 2010 – 2018)
Malengo ya CPT:

kuwaunganisha wanataaluma wakristo wa Tanzania na kuendelea kumleta Kristo katika mazingira yao ya kazi na katika maisha ya kila siku ili waweze kuiishi imani yao  kwa;

  1. Kuendesha semina za uhamasishaji juu ya Mafundisho ya Kanisa kuhusu Jamii kwa vikundi na ngazi tofauti tofauti Jimboni
  2. Kuendesha vipindi endelevu Radio Tumaini (CPT na Mafundisho ya Kanisa Kuhusu Jamii)
  3. Kutoa Elimu ya Uraia hususan nyakati za uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu.
  4. Kuongoza vuguvugu la Uhuishaji Maadili linaloshirikisha wadau tofauti tofauti.
  5. Kuanzisha Vikundi vya kitaaluma. Kwa Jimbo la DSM, ili kila mmoja aweze kutumia taaluma yake kwaajili ya kujenga Ufalme wa Mungu
  6. Kuongeza idadi ya wanachama na vikundi (Matawi) vya CPT Maparokiani.
Uongozi:
CASMIR FAUSTINE NKUBA
MWENYEKITI
Tel : 0784 381258
SCHOLASTICA MANDWA
MAKAMU MWENYEKITI
Tel : 0783111353
CONSTANTINE KANGALAWE
KATIBU
Tel : 0764 470408
ALEX SWALEHE LIPENDELE
KATIBU MSAIDIZI
Tel : 0788 753106
TEGEMEO PATRICK
MRATIBU CPT
Tel : 0764 714293
Shughuli na Matukio
Shughuli:
  • Warsha za Taaluma: Kuandaa mafunzo na semina za maadili ya Kikristo katika kazi na uongozi.
  • Huduma za Kijamii: Kushiriki katika miradi ya kijamii kama ufadhili wa elimu kwa watoto yatima na kusaidia hospitali.
  • Kongamano la Kikristo: Wanachama hukutana mara moja kwa mwaka kwa ajili ya tafakari, ibada, na kubadilishana uzoefu wa kitaaluma.
  • Misa Maalum za Wanataaluma: Kufanya ibada za shukrani na maombi kwa ajili ya wanachama.
Mikutano:
  • Mikutano ya Mwezi: Hukutana kila mwezi kujadili maendeleo ya chama na kupanga shughuli mpya.
  • Mkutano wa Maombi: Hufanyika kila wiki kwa wanachama kushiriki maombi ya pamoja na kutafakari Neno la Mungu.
  • Kongamano la Mwaka: Tukio kubwa linalohusisha wanachama wote kujadili mafanikio na changamoto za chama.
Kuwa Mwanachama
Kuwa Mwanachama

Kuwa mshirika wa Shirika la Kimisionari ni njia ya kuridhisha ya kutumikia Kanisa na jamii yako. Iwe unahisi wito wa kuongoza, kutumikia, au kuimarisha safari yako ya kiroho, kuna nafasi kwa ajili yako katika mojawapo ya mashirika yetu. Wasiliana nasi leo ili kujua zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kujiunga.

Uanachama:
  • Jinsi ya Kujiunga:

    Wanataaluma walio na nia ya kujiunga na CPT wanashauriwa kufika kwenye ofisi za chama zilizoko katika parokia au kuwasiliana na viongozi wa chama. Fomu za usajili zitatolewa pamoja na maelekezo ya awali. Ada ya uanachama ni TZS 5,000 kwa mwezi. Michango hii inasaidia kufanikisha shughuli za chama na miradi ya kijamii inayoendeshwa na CPT.

    Kwa maswali kuhusu uanachama, tafadhali wasiliana na vyama@darwalei.or.tz

  • Ada ya Uanachama:
    Ada ya uanachama : TZS 5,000.
Tafadhali andika jina la taasisi yako.
Tafadhali andika jina lako la kwanza.
Tafadhali andika jina lako la mwisho.
Tafadhali andika namba yako ya simu.
Tafadhali andika barua pepe sahihi.
Tafadhali andika ujumbe wako / Maoni (ikiwa yapo).