Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Kuenea kwa Shirika la Utoto Mtakatifu
Mwaka 1996 Shirika la kipapa Duniani liliandaa mafunzo kwa Walezi katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na kati, mfunzo yalifanyika Entebe nchini Uganda kati ya mwezi wa Februari na Machi 1996. Kwa kupitia mpango huo, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alimwomba Padre Eusebius Nzigilwa akiungana na Masista kutoka Bukoba wakati huo wakiwa wanafanya kazi Kanisa la Mt. Yosef kwa pamoja wawe washiriki katika mafunzo hayo kwa nia ya kuja kuanzisha Shirika hilo.
Mwishoni mwa Februari na Machi 1996 kukawa na kazi ya kuanzishwa Shirika hilo hapa Jimbo la Dar es salaam, hivyo Kituo cha kwanza cha shirika la Kipapa kwa Jimbo la Dar es salaam kikawa Kunduchi Mtongani.
Kituo kingine kufunguliwa kilikuwa Kanisa Kuu la Mt. Yosefu kwasababu ya kuwepo kwa Sr. Deusdediti ambaye miongoni mwao alipokea mafunzo toka Uganda. Hivyo kazi ya uimarishwaji wa Utoto mtakatifu ndipo ulipofika katika kanisa la Mt. Yosefu na hatimae kusambaa na kwingineko.
1. Kusali Pamoja na Watoto katika jumuiya zao na majumbani.
2. Kujifunza Neno la Mungu na mafundisho ya jamii
3. Kufanya matendo ya Huruma, Mfano katika Gereza la Watoto Upanga na Wahitaji.
4. Kushiriki katika Makongamano, Warsha mbalimbali, Ziara za mafunza na Shughuli za uinjilishaji, nia kubwa ni kuwaimarisha watoto katika makuzi ya kiroho
- Ziara: Kufanya ziara mbalimbali za uinjilishaji za uenezaji injili. mfano Mafia, Utetena maeneo mbalimbali
- Mafunzo ya Kiroho: Kushiriki mafundisho ya kiroho kwa watoto familia, kujenga maisha bora ya kiroho.
- Ushirikiano wa Kijamii: Kushiriki katika kufanya shughuli za kijamii na kusaidia wahitaji katika jamii.
- Makongamano na Hija: Kushiriki makongamano na hija katika maeneo mbalimbali
- Matukio; Kushiriki matukio mbalimbali ya kiparokia , Kijimbo na Kitaifa
- Mikutano ya Kiroho: Mikutano hii ni ya kuungana kwa maombi na kujenga maisha ya kiroho ya wanachama.
- Mikutano ya Familia: Mikutano hii hufanyika mara kwa mara ili kujenga familia bora kwa kutoa mafundisho ya familia.
- Mkutano wa Mwaka: Mkutano huu unafanyika kila mwaka kwa lengo la kujadili na kupanga mikakati ya shughuli za chama.
Kuwa mshirika wa Shirika la Kimisionari ni njia ya kuridhisha ya kutumikia Kanisa na jamii yako. Iwe unahisi wito wa kuongoza, kutumikia, au kuimarisha safari yako ya kiroho, kuna nafasi kwa ajili yako katika mojawapo ya mashirika yetu. Wasiliana nasi leo ili kujua zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kujiunga.
- Jinsi ya Kujiunga:
Kujiunga na JUWAMA ni rahisi. Wanachama wanapaswa kuwasiliana na viongozi wa chama katika parokia zao na kujaza fomu za usajili. Baada ya kujiunga, wanachama watapata mafunzo ya kiroho na jamii, huku wakifanya kazi pamoja katika kusaidia familia na jamii kwa jumla. Ada ya uanachama ni TZS 2,000 kwa mwezi. Ada hii inatumika kusaidia shughuli za chama na kutoa msaada kwa familia na jamii.
Kwa maswali kuhusu uanachama, tafadhali wasiliana na info@darwalei.or.tz
- Ada ya Uanachama:
Ada ya uanachama : TZS 2,000.