KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Vyama Vya Kitume
Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA)
Muhtasari wa Chama:

Utume wa Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA) Ulianzishwa mwaka 1924 mji wa Brussel nchini Ubelgiji na Kadinali Joseph Cardjin nakupitishwa rasmi kama Chama cha Kitume cha Vijana Kimataifa na Baraza la Kipapa Vatcan mwaka 1950.

Viwawa iliingia Tanzania mwaka 1959 katika Parokia ya Msimbazi, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, chini ya Mwanzilishi Pd. Lucas Gaemperle OFM, badaye mwaka 1960 alifika nchini kwetu Pd. Hendrikus Johannes Brinkhof maarufu kama Pd Mansuetus ambaye alimsaidia kwa karibu sana, padri Lucas kuueneza utume wa viwawa nchini kwetu, na kufuatiwa na Parokia ya St. Joseph, Kurasini, Magomeni, Chang’ombe, Kibaha. Kwa sasa utume huu umeenea nchi nzima.

VIWAWA ni chama cha kitume cha Vijana Wakatoliki Wafanyakazi wanaume na wanawake waishio mijini, vijijini na walio kwenye masomo, mafunzo ya fani mbalimbali, walio katika ajira rasmi na zisizo rasmi ambao wanatumwa na Kanisa ili kueneza habari njema ya Yesu Kristu

 

Malengo ya VIWAWA:

     kuwawezesha vijana kutambua wajibu wao katika kujielimisha na kujitegemea katika maisha yao, na pia kustawisha na kusaidia Kanisa kwa kwa kushiriki katika kazi za Kanisa kuhusu maendeleo ya kiroho, Kimwili, Kiakili na Kijamii.

Uongozi:
MACDONALD LWUAGA
MWENYEKITI
Tel : 0686 417817
NICHOLAUS ADRIANO
MAKAMU MWENYEKITI
Tel : 0767 795957
PATRICIA DAVID
KATIBU
Tel : 0718129191
DAVID PETER
KATIBU MSAIDIZI
Tel : 0787 776834
ROSE FESTO TAIRO
MTUNZA FEDHA
Tel : 0689 072528
Shughuli na Matukio
Shughuli:
  • Kuandaa semina za maadili, uongozi, na maisha ya Kikristo.
  • Vijana kushiriki katika uinjilishaji na kutoa huduma za kijamii kama ziara kwa wagonjwa na yatima.
  • Kuandaa michezo na burudani kwa lengo la kuimarisha mshikamano wa vijana.
  • Mafunzo ya kina kuhusu mafundisho ya Kanisa na Maandiko Matakatifu.
  • Makongamano: Kuandaa Makongamano kwaajili ya kupata uelewa
  • Kushiriki Hija mbalimbali ndani na nje ya nchi
  • Kushiriki majukumu mbalimbali ya Kanisa; Huduma za misa, Mapokezi ya wageni n.k
Mikutano:

Kutakuwa na Mikutano ifuatayo ya

Kamati ya Utendaji

Kamati Tendaji ngazi ya Taifa,itakutana kila baada ya miezi mitatu (mara nne kwa mwaka). Ngazi ya Jimbo kila baada ya miezi miwili (mara sita kwa mwaka) ngazi ya parokia,kigango na kanda mara moja kwa mwezi.

Kikao cha dharura cha Kamati tendaji kinaweza kuitishwa endapo kuna haja na ulazima wa kufanya hivyo.

Halmashauri ya Utekelezaji

Itakutana mara moja kwa mwaka Taifa, Jimbo mara tatu, Parokia mara nne.

Mkutano Mkuu

Ndicho kikao cha juu kuliko vyote vya VIWAWA. Utaitishwa mara moja kwa mwaka Taifa, Jimbo mara mbili, Parokia mara tatu. Kigango na kanda mara nne.

Kuwa Mwanachama
Kuwa Mwanachama

Kuwa mshirika wa Shirika la Kimisionari ni njia ya kuridhisha ya kutumikia Kanisa na jamii yako. Iwe unahisi wito wa kuongoza, kutumikia, au kuimarisha safari yako ya kiroho, kuna nafasi kwa ajili yako katika mojawapo ya mashirika yetu. Wasiliana nasi leo ili kujua zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kujiunga.

Uanachama:
  • Jinsi ya Kujiunga:

    Kuna aina tatu za uanachama. Wanachama washiriki: Awe kijana Mkatoliki mwenye umri kati ya miaka 14 hadi 17. Wanachama kamili: Kijana Mkatoliki mwenye Ubatizo. Awe na umri kati ya miaka 18 hadi 35, Mwenye akili timamu

    Kwa maswali kuhusu uanachama, tafadhali wasiliana na info@darwalei.or.tz

  • Ada ya Uanachama:
    Ada ya uanachama : TZS 3,000.
Tafadhali andika jina la taasisi yako.
Tafadhali andika jina lako la kwanza.
Tafadhali andika jina lako la mwisho.
Tafadhali andika namba yako ya simu.
Tafadhali andika barua pepe sahihi.
Tafadhali andika ujumbe wako / Maoni (ikiwa yapo).