Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Hapo awali, Parokia za Dekania Mt. Thomas More zilikuwa ni sehemu ya Dekania ya Mt. Gaspar De Buffalo. Dekano wake alikuwa Pd. Dominic Somola. Tar 07 Machi, Baba Mtakatifu Alitangaza kuunda Jimbo Jipya la Bagamoyo kwa kuligawa Jimbo la Dar es Salaam na Jimbo la Morogoro. Kufuatia kuundwa kwa Jimbo jipya, baadhi ya Parokia zinazogawanywa na mto Tegeta zilihamia upande wa Jimbo la Bagamoyo na nyingine zilibaki upande wa Jimbo la Dar es Salaam. Siku chache baada ya kuundwa Jimbo la Bagamoyo,
Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam alitangaza kuundwa kwa Dekania mpya ya Mt. Thomas More ikijumuisha Parokia za; Mt. Thomas More, Salasala, Mt. Dominiko, Mt. Gaspar De Buffalo, Kunduchi, IPTL, Goba Maria na Skanska ambazo kabla ya mgawanyo zilikuwa sehemu ya Dekania ya Gaspar. Askofu Mkuu alimteua Pd. Romwald R. Mukandara kuwa Dekano. Parokia ya Goba Mtambani, na Mt. Theresia wa mtoto Yesu -Kilimahewa juu ziliongezeka baadaye.
Tunamshukuru Mungu kwa neema na baraka zake katika Dekania ya Thomas More. Ndugu zangu, tuzidi kuwa mashuhuda wa imani yetu kwa kufuata mfano wa Mt. Thomas More, aliyesimama kwa maadili na utakatifu.
Kwa mshikamano, sala, na upendo kwa kila mmoja, tutaimarisha safari yetu ya kiroho na kuleta matumaini kwa wengine. Mungu awabariki.
Maelezo ya mawasiliano
Pd. Romuald R. Mukandara
Mkuu wa Dekania ya Mt. Thomas More
Phone : 0764 601241